Reader Settings

Sikuweza hata kujitingisha, kichwa kilikuwa kinaniuma sana nikiona kama damu yote ya mwilini inajaa kichwani kwa like pozi la kuinama. Minyororo ya chuma kizito ilikuwa imefunga miguu yangu kwa kukazwa mpaka miguu ikafa gazi kwani hata damu ilikuwa inatembea kwa shida. Sikuweza kumwona mama yangu wakati huo kwa sababu hata kugeuka nilikuwa siwezi, lakini nilijua yuko karibu, kwa sababu nilisikia sauti yake, iliyokuwa ya chini sana, lakini imara. "Mwambie hakimu niko tayari kukiri na kuungama makosa yote niliyoshitakiwa," alisema. "Ikiwa tu atamwachilia binti yangu kuwa huru. Hajui lolote kuhusu jambo hili. Hafahamu chochote kinachoendelea hata kidogo. Tafadhali naomba umfikishie ujumbe huu."

Mwanaume aliepewa ujumbe huo na mama hakujibu chochote alinguruma na kuguna kana kwamba ndio jibu lake. Kisha wanakijiji wote wakaondoka kurudi majumbani mwao kama waliambiwa na hakimu kwamba wasubiri mpka asubuhi ndio kesi ingeendelea. Pale katikati ya uwanja, tukiwa tumepinda migongo na kushikiliwa kwa nguvu na minyororo na bawaba zile za mbao shingoni na mikononi, tulisubiri kupambazuke ili ujue hatima ya maisha yetu. Upepo wa baridi kali ulitufyatua na kuchana ngozi zetu kama wembe, na barafu ilioambatana na upepo iliendelea kutupiga kwa nguvu. Miguu ilikuwa ikitetemeka kwa ajili lile pozi la kuinama lilikuwa la kikatili sana, macho yalikuwa yamevimba na kuwa mekundu kwa kulia huku lips za midomo zikiwa zimepauka na kuchanika kwa baridi kali. Nilitetemeka na kuanza kulia kwa uchungu nikiwa siamini kama shangazi yangu wa damu, ndugu ya baba yangu leo ametusaliti.., uso wangu ukiungua kwa baridi, mikono yangu ikiwa ganzi, na miguu yangu ikiwaka moto kwa maumivu na uvimbe.

Kisha nikasikia sauti ya mama yangu, laini na ya upole, ikiimba taratibu,

"Upepo mtakatifu wa Kaskazini, usituletee madhara.

Upepo wa Kale wa Kusini, njoo, utupe joto."

Aliyarudia maneno hayo tena na tena, na nikajitahidi kufunga mdomo ili meno yangu yasitetemeke na kujiunga naye, nikifumba macho yangu na kuita upepo utusaidie. Uchawi wa mama yangu haukuweza kuyeyusha minyororo ya chuma, lakini aliweza kuvuta nguvu za asili na kututii.

Ndani ya dakika chache upepo mkali ulitulia, na theluji ikakoma kunyesha. Upepo laini na wa joto ulichukua nafasi ya baridi kali, na kutetemeka kwangu kukapungua. Bado sikuwa huru na maumivu, lakini nilijua mama yangu alikuwa akiteseka zaidi kuliko mimi, kwani mwili wake ulikuwa umezeeka zaidi. Lakini hakulalamika. Nilipata nguvu ya ujasiri kutoka kwake, na nikaapa kushikilia uchungu wangu mwenyewe ndani kwa ndani.

"Nyakati ngumu zinatungoja, binti yangu," aliniambia.

"Lakini chochote kitakachotokea kesho, Yolanda, lazima ukumbuke ninachokuambia sasa. Niahidi uta—"

"Naahidi," nilinong’ona. "Lakini, Mama, usikubali kukiri lolote kwao. Hata kama ni kuniokoa mimi. Siwezi kuishi ikiwa utakufa." Mawazo hayo yalinipa hofu, na nikajaribu kuvuta mikono yangu dhidi ya mbao ngumu zilizoniweka kifungoni, ingawa sikuwa na matumaini ya kujinasua. Yeye ndiye kila kitu nilichokuwa nacho ulimwenguni. Yeye pekee.

"Labda hii ndiyo hatima yangu," alisema kwa upole. "Lakini si yako."

"Unajuaje?"

"Najua," alininong’oneza.

"Nilijua tangu siku uliyokuwepo duniani, mwanangu. Kwa alama ya kuzaliwa uliyonayo kwenye nyonga yako ya kulia. Nusu mwezi."

Machozi yalinichoma macho. Lakini mama yangu aliendelea.

"Wewe ni mchawi mwenye nguvu saana zaidi kuliko nilivyowahi kuwa, Yolanda."

"Hapana. Si kweli. Siwezi hata kutengeneza mduara wa uchawi kwa usahihi."

Alitabasamu, kwa sauti laini, na sauti yake ilinigusa moyo. Kwamba aliweza kucheka katika hali kama hii na kunifanya nizidi kumpenda na kumheshimu hata zaidi ya hapo awali, ingawa sikuwa nadhani ingewezekana.

"Sizungumzii kuhusu mbinu, bali nguvu, Yolanda. Nguvu hiyo ni kubwa ndani yako. Na utaihitaji sana siku zijazo. Baada ya haya kuisha, mwanangu, lazima uondoke hapa. Nenda kwenye Dunia Mpya. Shangazi yako, Mayasa, yupo huko, katika mji mdogo uitwao Shira, katika koloni la Kilema Kyaro" (dwelling place of Ngai, the Supreme Being). Yeye si mchawi, na hajui lolote kuhusu mila zetu. Alizaliwa kutokana na usaliti wa baba yangu na kulelewa na mama yake, na si katika nyumba yetu. Lakini ni mwema na ana upendo sana. Hawezi kukutenga."

"Labda ni kweli atakuwa mwema kwangu," nilisema. "Lakini mama siwezi kukuacha hapa, sioni maisha yoyote mbele yangu bila wewe mama."

“I fear ‘tis I who will leave you behind, my darling. ‘Tis the night of the dark moon, when our powers ebb low. But even were our lady of the moon shining her full light down upon us, I doubt I could save myself. Do not cry for me, Yolanda. Dying is part of living, a birth into a new life. You know this.” Aliongea mama kwa uchungu akimanisha….

"Nina hofu kwamba ni mimi ndie nitakayekuacha, mpenzi wangu. Huu ni usiku wa mwezi mweusi, unaosababisha nguvu zetu kupungua. Lakini hata kama mama wa mwezi angekuwa aking’aa juu yetu, sidhani kama ningeweza kujinusuru. Usilie kwa ajili yangu, Yolanda. Kifo ni sehemu ya maisha, ni kuzaliwa katika uhai mwingine mpya. Unajua hili."

"Oh, Mama, tafadhali acha kutamka maneno hayo!" nililia kwa sauti, nikibubujikwa na machozi hadi kushindwa kupumua sawasawa.

Aliponena tena, nilisikia machozi pia katika sauti yake. "Yolanda, nisikilize. Lazima unisikilize kwa umakini."

Nilijaribu kujituliza, na kufanya vile alivyotaka, lakini pia niliapa kwamba hatokufa kesho. Kwa njia yoyote ile nitafanya kumuokoa mama yangu kipenzi.

"Baada ya haya yote kuisha," aliniambia,

"Lazima uhakikishe umerudi kwenye nyumba yetu kijijini. Lakini fanya hivyo usiku, na uwe mwangalifu sana. Usionekane. Usingoje kwa muda mrefu, mwanangu ukachelewa, nahofia wanaweza kuichoma nyumbayetu moto kwa hasira zao au kuikabidhi kwa familia ya shangazi yako Njinga kama zawadi kwa ushahidi wake dhidi yetu. Lazima urudi kwa siri. Chukua tu unachohitaji kwa safari yako. Kisha nenda kwenye mahali pa moto(fire place). Kuna jiwe lililokuwa limelegea pale. Lisogeze pembeni halafu chukua utakachokiona kimefichwa nyuma yake..."

"Lakini, Mama—"

"Na uchukue farasi, kama bado yupo. Unaweza kumuuza katika kijiji kingine ukiwa una safiri. Lakini kuwa mwangalifu. Ukikutana na mtu yeyote, usimwambie jina lako halisi. Na mara tu utakavyoweza, tafuta nafasi kwenye treni inayoelekea Ulimwengu Mpya. Sasa nipe ahadi kuwa utafanya kama nilivokuelekeza."

"Siwezi kukubali wakuue, Mama."

"Huwezi kufanya chochote kuzuia hilo, mwanangu. Lakini niahidi utafanya vile nimesema, nami nitakufa kwa amani kwa sababu ya hilo. Niahidi, Yolanda."

Macho yangu yakiwa yamejaa machozi, nilinong’ona, "Naahidi."

"Vizuri." Alihema kwa kina kana kwamba mzigo mzito ulikuwa umeondolewa mabegani mwake. "Vizuri," alinirudia kwa sauti ya kunong’ona, kisha akapumzika. Labda alilala. Sikuweza kuwa na uhakika. Nililia kimyakimya tangu hapo, nisiwe kero kwa Mama yangu kwa machozi yangu. Lakini nahisi alikuwa akijua.

Previoua Next