Reader Settings

Roma alishindwa kuvumilia  , alikuwa akishindana na hali iliokuwa ikiendelea kwenye mwili wake , alifumba macho yake haraka sana , ili Mama Issa asimuone akibadilika na kisha akageuka, Uzuri ni kwamba mwanamama huyu  alikuwa amempa mgongo  Roma na hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea kwenye kichwa chake.

Roma alikimbilia nje , lakini ile anatoka kwenye ofisi alijikuta akikumbana na Edna  ambaye aliona hali yake   ya macho Alitaka kumwepa lakini Edna  hakufanya hivyo , alimshika mkono.

“Roma Calm Down”Aliongea  Edna na  Roma ni kama ameshituka  kwani macho yake yaligeuka na kurudi katika hali yake ya kawaida  na kumwangalia Edna.

“Am Sorry Edna”.

“Sorry ya nini?”

“Sijui …”Kabla Roma hajaibu  walishitushwa na sauti ya Bi Tabea.

“Nilishangaa umeenda wapi kumbe umemfata mkeo”Aliongea  Bi Tabea  na Edna alitabasamu.

“Edna niseme tu hongera sana kwa kupata mume , Roma anaonekana kuwa kijana mzuri  naamini  mama yako na bibi yako watakuwa na furaha na wanaweza kupumzika kwa  amani maana wewe..”

“Mama Issa Maana nini…”aliongea huku akicheka.

“Umekuwa mgumu sana , nakumbuka yule nani yule .. ee Elvice alikuwa akitoka jeshini lazima aje hapa kulalamika..”Mama huyu alijikuta akiishia njiani kuongea na kujiona ameropoka ila kwa Roma alikuwa amesikia kila kitu na akajiuliza  kuna  historia gani kati ya Elvice na Edna ambayo hakuwa akiijua , ila hakutaka kuuliza.

Saa moja kamili za jioni ndio muda ambao wawili hawa walitoka ndani ya kituo hiki kurudi nyumbani  , Edna alionekana kuchoka kweli  kutokana na  kucheza na Watoto , kwa upande wa Roma yeye hakuwa amechoka , kwanza hakucheza kabisa na Watoto kwani sio mtu wakupenda sana kama ilivyokuwa kwa Edna.

Alimwangalia mke wake aliekuwa amesinzia pembeni na kujikuta  moyo wake ukiwa wa moto  , alitamani Maisha  yake yawe kama hivyo kila siku  ,awe anapendana  na mke wake , watembee hapa na pale  kurefresh mind, alitamani kufurahi na kuendeleza Maisha ya ukawaida , lakini Roma Maisha ya aina hio yalikuwa kwake ni ndoto.

“Hapana lazima nifanye  juu chini nina kamilisha yote yalionileta Tanzania , nikishachimba swala hili kwa undani  na kujua kwanini nilikuwa kwenye kile kisiwa cha  mateso mimi na Seventeen na  kuifahamu familia yangu nadhani nitatulia na mke wangu, Edna licha ya kwamba  hatujaoana kimapenzi , lakini sidhani kama itakuja siku nitakuacha  hata pale mkataba utakapoisha”Roma aliwaza mawazo hayo mchanganyiko huku akizidi kukanyaga pedeli kuelekea jijini Dar es salaam.

Wakati akiendelea kuendesha gari alikumbuka kauli ya Bi Issa kumuuliza hali ya kimaendeleao ya Nasra , alijiuliza kwanini mwanamama yule kauliza  juu ya maendeleo ya Nasra ila alikosa majibu kwa wakati mmoja , alijiambia kuwa  atafahamu kadri atakavyokuwa karibu na Nasra.

****

Doris  alijikuta ni mwenye hasira sana , baada ya kujua kuwa Edna  na Roma ni  mume na mke  , alikasirika sana , lakini na kuumizwa kwa wakati mmoja.

Alianza kukumbuka tukio ambalo Roma alimuomba hela ya nauli wakati akiwa anarudi nyumbani na kumpatia , alikumbuka usiku wao waliotumia  na kufanya mapenzi na mwanadada huyu alizidi kutokwa na  machozi ,alihisi moyo wake ulikuwa ukimuuma sana  kiasi cha kwamba mwenyewe alishindwa kuelewa kwamba moyo wake ulikuwa ukimuuma kutokana na kwamba Edna  na Roma walimficha na kumuona mjinga siku zote , au  ni kwasababu alijua  kuwa Roma  mke wake ni Edna mwanamke mrembo na kilichokuwa kikimliza ni wivu wa kimapenzi.

Alisimama kukodolea maji  ya baharini muda huu wa jioni   huku machozi yakiwa yanamtoka ,  lakini kila alipokuwa  akiangalia baadhi ya  wapenzi waliokwa ndani ya fukwe hii  ya Coco walivyokuwa wakifurahi na kuonyesheana   mapenzi , aliijikuta akizidi kutoa machozi.

“Ninaonekana kutokuwa na bahati katika Maisha yangu , Edna nifanye nini mimi nahisi kumpenda sana mumeo , najiona kabisa siwezi kumuacha hata kidogo , kwanini iwe wewe rafiki yangu”Aliwaza mwanadada huyu na kuwazua  huku akionekana ni mwenye kukosa jibu , alionekana alikuwa akishindana na hisia zake.

Doris licha ya kwamba  alikuwa sio mwenye kuonyesha waziwazi mapenzi yake kwa Roma alikuwa  ashampenda tokea siku ya kwanza wanaonana  ,Roma alivyomuomba kiasi cha pesa  , tokea siku ile alikuwa  alikuwa ni mwenye kumkumbuka Roma , hakujua ni kwanini alikuwa akimkiumbuka mwanaume huyo , lakini picha yake haikuwa ni yenye kutoka kwenye kichwa chake.

Siku ambayo anamuona Roma kwa mara nyingine ndani ya kampuni yake , akija  kufanya usaili , alijiambia kabisa ni Mungu ndie aliekuwa amewakutanisha  kwa mara nyingine  na hivyo hapaswi kuzarau kile Mungu alichompatia na ndio maana siku  ile ile aliona atumie nafasi ile kumtambulisha  Roma kwa mwanaume mzee aliekuwa akimsumbua , mwanaume aliekuwa akimfahamu kama Mr Kijembe .

Hakujali kabisa katika moyo wake kwamba Roma ameoa , alichokuwa akiamini ni Kwamba Roma alikuwa amepangiwa kuwa nae katika Maisha  yao yote na mke aliemua ni makosa ambayo Roma alikuwa amefanya , hayo ndio yalikuwa mawazo ya mwanadada huyu mrembo , aliamini mke wa Roma sio mtu sahihi kwa  Roma na yeye ndio alikuwa sahihi , kwani matukio yao ya kukutana ni kama  Mungu aliwakutanisha.

Hata pale alipopata taarifa ya Roma kulala na mwanamke Neema  Luwazo Mwanamke ambaye alikuwa akimjua sana tu, kwa kuwa na mahusiano na Raisi mstaafu , alijiambia kuwa ni  mihemko tu ya Roma  ya kukosa mtu sahihi wa kumtuliza na kama atampata  basi  Roma angetulia kwake na kuachana na mambo ya wanawake , kwani angempa kile kitu ambacho anakitafuta nje , kitu ambacho aliamini ni kwamba alikuwa akikikosa kwa mke wake.

Siku ya Jumapili ndio siku ambayo alipanga  kutimiza jambo lake la kuanza kuweka ukaribu na Roma , aliamini anapaswa kufanikisha swala la yeye kuwa karibu kabla ya kwenda safari ya kikazi Japani , alitaka katika safari hio waitumie kama  sehemu yao ya matembezi kama wapenzi ,  na ili kukamilisha swala hilo anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha Roma anakuwa karibu yake anamzoea  na hatimae kumpenda.

Baada ya kuwaza hayo , hatua ya kwanza aliofikiria ni kwenda kutafuta zawadi yoyote ambayo aliamini  itamfurahisha Roma  na eneo pekee alipoona panafaa kupata zawadi hio kwa siko hio ya jumapili ni  Mlimani City.

Nwanadada huyu alijiandaa , alichukua kadi yake ya benki  aina ya ‘Black Card’ kadi ambayo ilikuwa ikimruhusu  kutoa kiasi chochote kile cha  pesa na kuiweka katika mkoba wake , na kisha akachukua ufunguo wa gari yake   na  kutoka ndani ya jumba hili la kifahari alilokuwa akiishi mwenywe   na wafanya kazi.,Jumba ambalo alikuwa amenunuliwa kama zawaidi na baba  yake .

Lakini baada ya kufanya safari yake  na kufika Mlimani anajikuta akishuhudia kitu ambacho moyo wake haukutarajia kukiona , alimuona mwanamke ambaye aliamini sio sahihi kwa Roma akiwa ni Edna , Rafiki yake kipenzi ,  bosi wake  kazini, moyo wake ulipigwa na ganzi.

“Doris!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanaume iliosikika nyuma yake na kumfanya mwanadada huyu ageuke ni nani anamuita , lakini ile anageika alikutana na uso wa Abu.

“Abu vipi , kwanini uko hapa ?”Aliuliza  Doris kwa  namna ya kushangaa.

“Nimekuja kupunga upepo kama wengine Doris , wewe vipi , kwanini uko hapa?”.

“Namini nipo kwa ajili ya kupunga upepo  “Abu alijikuta akitabasamu .

“Doris najua  unaonekana kuwa katika  hali ya mawazo , lakini  nimekuwa nikisubiria sana  jibu lako”

Doris alishangaa na kuanza kuvuta pumzi kwa nguvu  na kumgeukia Abuu….

Ni jibu gani ??

Previoua Next