SEHEMU YA 33
2010 -KIGALI STATE HOUSE
Ni mwaka 2010 muda wa saa tano za Asubuhi mheshimiwa Jeremy alionekana ndani ya ofisi yake akifanya kazi kama kawaida, katika kuwatumikia wananchi wa Rwanda, lakini siku hii kwa mheshimiwa huyu hali yake ilionekana kuwa sio ya kawaida , kwani alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi sana kuliko siku zote hali ambayo ilimfanya kukosa utulivu , kila saa alionekana kuangalia saa ya ukutani kama mtu ambae alikuwa na jambo ambalo alikuwa akilisubiria.Ilivyofika saa sita na nusu aliingia Linda mlinzi wa karibu wa Mheshimiwa Jeremy.
“Mheshimiwa Ashafika”Aliongea Linda na kumfanya mheshimiwa Jeremy avute pumzi .
“Mruhusu aingie”Aliongea mheshimiwa na kisha akatoka kwenye meza yake na kwenda kwenye masofa na hapo hapo mlango ulifunguliwa na aliingia mwanaume mmoja wa kizungu alievalia shati la Blue bahari na suruali ya kadeti , muonekano wa huyu jamaa ni kama vile hakuwa akiingia kuonana na mheshimiwa , kwani alivaa kikawaida sana kama muhuni flani hivi.
“Welcome Mr Viladkov”Aliongea mheshimiwa kwa kingereza.
“Asante sana mheshimiwa”Aliongea na kisha alitoa karamu nyeusi flani hivi pana kidogo lakini ya kawaida , kama zile za rangi na kisha alianza kuifungua kama mtu ambae anatoa ule mrija wa wino, na akatoa kifaa Fulani hivi kama kile kichwa cha kuchomekea kwenye Earphone lakini hiki kwa juu mwisho kina kitu kama kigoroli.
“Hili ndio faili mheshimiwa”Aliongea na kisha alimpatia Jeremy kile kidude na mheshimiwa alishangaa m inakuwaje kadude kama hako kawe ndio faili ambalo alikuwa akilisubiria kwa hamu.
‘”Usishangae mheshimiwa Hata Urusi sasa imeendelea kwenye teknolojia , na hio ni mbinu yetu mpya kuficha taarifa wakati wa kuzisafirisha” ’Mheshimiwa Jeremy hapa alishangaa na akachukua Tablet iliokuwa kwenye meza yake na kuchomeka kale kadude na baada ya tablet ile kusoma kama Earphone ilisoma kama memori , alishangaa na Viladkov akatabasamu.
“Ni taarifa nyeti sana hio , na serikali ya Urusi imelipa kiasi kikubwa kuinunua kwa mtu aliekuwa akiuza”Aliongea bwana huyu na mheshimiwa Jeremy aliifungua na ajabu ni kwamba alikutana na picha.
“Mbona ni picha sio kama faili nilivyokuwa nikitegemea?”
“Angalia kwanza hizo picha mheshimiwa kwa umakini na uniambie umegundua nini?”
Alianza kuangalia hizo picha kwa kuzizoom na katika picha hizo kulionekana meli kubwa ya mizigo ikiwa inashusha mavyuma , lakini baada ya mheshimiwa kuangalia kwa ukaribu Zaidi aligundua ni bawa la Ndege.
“Linaonekana kama bawa la Ndege”
“Angalia na hio nyingine” Aliangalia na pia yenyewe ilionekana kama baadhi ya vipandevvipande vya mabaki ya ndege.
“Hio meli inamilikiwa na kampuni Neptune , kampuni ambayo ni sehemu ya kampuni kubwa ya kuzalisha ndege ya kimarekani inayofahamika kwa jina la Ngebo Aeronautical”Mheshimiwa alionekana kushangaa , lakini pia alizidi kuongeza umakini.
“Hizo picha zilipigwa Tarehe saba March 1998”Aliongea na mheshimiwa huyu alishangaa sana.
“Unataka kumaanisha kwamba ni siku moja kabla ya ndege ya Malaysia kupotea?”
“Ndio kutoka sehemu ambayo meli hio ilipo na sehemu ambavyo ndege ya shirika M ilipotea ni umbali wa kilomita ishirini tu , kwa maana hio hayo ni mahesabu ambayo yamepigwa kabisa na hio meli ilitupa mabaki hayo unayoyaona kwenye hizo picha eneo hilo”Mheshimiwa Raisi alijikuta akitetemeka maana anacho ambiwa hapo ni taarifa nzito sana , tena nzito kweli kweli.
“Mheshimiwa hii ni siri ninayokupatia ambayo ni siri kubwa ndani ya taifa la Urusi na ni kama Asset kwetu , hivyo taarifa hii inapaswa kuwa siri , mheshimiwa Raisi Viladmn karuhusu upatiwe taarifa hio ili kwa ajili ya kushawishi mataifa ya Afrika kuingia kwenye Mpango TASAC”Mheshimiwa alishangaa Zaidi.
:Mheshimiwa chomoa hio flash na uichomeke tena” aliongea Viladkov na mheshimiwa alichomoa na kuichomeka tena na ikasoma tena kama memori , aligusa ten ana zile picha zikawa zimefutika ils sasa kulionekana faili lililokuwa kwa mfumo wa ‘Xml’ , mheshimiwa alilifungua na kuanza kusoma na hapa ndipo aliposhangaa.
“Hio ni barua ya wito iliotumwa kwa mashirika ya kijasusi makubwa yote duniani na katika hio barua inaonesha kulikuwa na makubaliano ambayo yalikuwa yanatakiwa kufanyika juu ya mpango ambao ulipewa jina la LADO ambapo sisi tulishindwa kung`amua kirefu cha neno hilo , na shirika letu pekee ndiio halikutuma muwakilishi kwenda kuhudhuria kikao hiko ambacho kilifanyikia nchini Italy”Mheshimiwa jasho lilimtoka maana kadiri anavyoambiwa ndio anavyoona siri hii kuzidi kuwa nzito na kuhofia Maisha yake.
“Kwa hio unamaanisha kwamba LADO na kupotea kwa ndege ya shirika la M ni swala ambalo lina muunganiko na limeratibiwa kwa makubaliano ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani?” Aliuliza na jamaa alitingisha kichwa kukubaliana nae.
“Kwanini mmeamua kunipa hii taarifa?”
“Mpango TASAC ni mpango ambao unahusisha serikali ya Urusi kurudisha umoja wa Kisoviet , lakini hili ili liweze kufanikiwa , tunahitaji sapoti kutoka Afrika , tunahitaji udhaifu kutoka kwa mataifa makubwa ambao utatusaidia pale itakapobidi serikali yetu kuingia vitani , mataifa haya hayatoi msaada , lakini nyie wa mataifa ya Afrika mnapaswa kutuunga mkono kwa kukaa kimya.”
“Na ili swala hili lifanikiwe unapaswa kuhakikisha asiliamia sabini ya mataifa ya Afrika yanakuwa kwenye huu mpango TASAC na mheshimiwa Raisi wa Urusi amekuchagua wewe kutokana na uzoefu wako katika uongozi, ukifanikisha mpango huu basi serikali ya Urusi itafanya juu chini kubaini ni nini kipo ndani ya operesheni iliopewa jina la LADO”.
“Natakiwa kukubali swala hili hapa hapa?”
“Hapana mheshimiwa , swala hili lina umuhimu sana kwa nchi yetu na mheshimiwa Raisi atakupigia simu na mimi nipo hapa kwa ajili ya kukueleza haya , kwani tunajua kuwa wewe ni mmoja ya wahanga wa AJali ya ndege na unataka kulipiza kisasi , lakini kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe na udogo wa taifa lako, hautoweza kupata hio nafasi ya kuujua ukweli”Aliongea bwana huyu na heshimiwa Jeremy alikubali kuwa kiongozi wa juu wa mpango TASAC.
****
“Sauron habari za muda huu?”
“Salama kabisa mfalme Pluto, habari za Tanzania?”
“Hapa ni kwema kabisa Sauron , nimekupigia kupata ripori ya yale tilioongea jana”
“Mfalme Pluto , nimeshayakamilisha yote na nimepanga vijana kumi wenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kuja nchini Tanzania, lakini kuna jambo moja nimeona nitoe pendekezo”
“Edelea kuongea Sauron nakusikiliza”
“Nimeona makomandoo hawa wakiingia nchini kama watalii hawatapata kibali cha muda mrefu cha kukaa hapo Tanzania , hivyo nimejaribu kuwasiliana na balozi ya Sweeden nchini Tanzania na kuwaomba watufanyie mpango wa kuwaingiza wanajeshi wetu kama wafanya kazi wao”Roma Alitabasamu.
“Sauron wewe unakili sana , hili sikulifikiria , ni kweli watapaswa kukaa nchini muda mrefu kidogo kwani pia nataka wamlinde mke wangu”Sauron alishangaa.
“Mfalme Pluto usiniambie umepata mke?”
“Ndio Sauron , sio muda mrefu sana nimefanikiwa kupata mke”
“Hongera sana mfalme Pluto , ila kwa hatua hio sidhani kama utarudi huku kisiwani”
“Yanayotokea kesho hatuyajui Sauonoi hivyo siwezi kuongea lolote juu ya hili”.
“Ni kweli Mheshimiwa Pluto , ila nitatamani kumuona malkia wetu”Roma alitabasamu
“Utamuona Sauron nitakuja nae siku moja , Sauron kuna jipya lolote kutoka The Zeros?”
“Mfalme Pluto vijana bado wanaendelea kufuatilia na naamini muda si mrefu watatupatia taarifa “
“Sawa Sauron , nadhani tutawasiliana baada ya vijana kufika Tanzania”Baada ya hapo waliagana na Roma akakata simu .
Muda huu Roma anawasiliana na Sauron ilikuwa ni saa moja kwenda saa mbili hivi , hivyo baada ya kumaliza tu aliitwa na Bi wema kwa ajili ya chakula cha usiku.
Baada ya kufika tu chini na Edna alikuwa akishuka alievalia kigauni kilichokuwa kikipeperuka kiasi kwamba kilimfanya Roma aliekuwa chini ya ngazi aone mapaja ya malaini ya Edna na alijikuta hisia za mapenzi zikimuandama.
“Kukaa na mwanamke kama Edna halafu hupati kitumbua chake ni swala ambalo nina uhakika madaktari wataniambia ni sumu kwa Afya yangu , nikimaliza hapa nduki kwa Rose nikapunguze kichupa”Aliwaza Roma huku akivuta kiti na kuketi.
Edna na yeye alijikuta akitabasamu baada ya kumuona Roma leo hajatoka kabakia nyumbani , kwani mara nyingi hakuwa akipenda sana Roma a tabia yake ya kutoka na kurudi asubuhi yeye kama mke aliona sio vizuri.
Wanafamilia hawa walikula wakashiba na baada ya hapo Edna aliungana na Bi wema kusafisha vyombo , lakini wakati Edna akiwa bize na vyombo upande wa jikoni Roma alimchungulia kwenye mlango.
“Bebi ndio natoka hivyo , hapa hadi kesho”Aliongea Roma na Edna ambaye alikuwa ameweka mikono yake kwenye Sink alijikuta akikunja ngumi kwenye maji na kung`ata meno , kwani kila ambacho kilikuwa kikimfurahisha dakika chache nyuma kimegeuka ndivyo sivyo,Edna aliishia kutingisha kichwa na Roma hakujali aliondoka.
“Yaani huyu mwanaume hatulii nyumbani”Aliongea Edna kwasauti pasipo kujua nyuma yake kasimama jasusi mbobezi wa mapenzi Bi Wema.
“Miss ulifikiri sasa atafanyaje , mmeoana lakini hamlali chumba kimoja , yule ni mwanaume na wanaume tendo la nndoa ni kama hitaji lao la msingi hawezi kukaa na mtoto mrembo kama wewe halafu akuangalie kama picha ya ukutani”Edna alifikiria kidogo.
“Bi Wema nitafanyaje , bado sina hisia nae na wewe unaelewa tumeoana kimkataba”.
“Naelewa ndio , lakini miss angalau jaribu kuufungua moyo kwa Roma , huenda ukampenda na mkawa Mume na mke kimapenzi sio kimkataba”Edna alitingisha kichwa kuelewa
Baada ya kufika chumbani kwake alionekana kuwaza maneno ya Bi Wema na kuona kidogo yana maana.
“Au nijaribu kumpa?”Aliwaza Edna akimaanisha ajaribu kumpa Roma kitumbua.
Comments