Reader Settings

Ni jumatatu  asubuhi   iliokuwa imekucha na makucha yake , wengi huwa hawaipendi hii siku kutokana  na mambo mengi ambayo huwa yanatokea wikiend , sio wanafunzi , sio waajiriwa  kila mtu anasababu yake ya kutokuipenda hii siku , lakini kwa mwanadada Edna alikuwa  na motisha  , kwake jumatatu aliichukulia kama safari ya wiki ya kimafanikio.

Mwanadada huyu alikuwa na jambo kubwa sana mbeleni ambalo alikuwa akilipanga kulifanikisha , dili ambalo kama likienda kama alivyokuwa amepanga , lingezidi kumfanya kuwa mwanamke Tajiri  Zaidi , lakIni pia kampuni yake ingezidi kuchanja mbuga na kufahamika duniani kote na ndio maana hakutana ‘glitches’ za aina yoyote katika mkataba  anaokwenda kusaini na kampuni ya Yamakuza , kampuni kubwa ndani ya taifa la Japani.

Kwake  uwekezaji huo ndio mkubwa Zaidi kuwahi kuutekeleza tokea aichukue kampuni hio kutoka kwenye mikono ya mama yake na kama dili hilo pia litafanikiwa ndio dili ambalo litaifanya  kampuni yake kuwa na mafanikio makubwa ndani ya mwaka huo.

Asubuhi ya leo alikuwa ameketi kwenye kiti akipata ;Breakfast’ , huku Roma akiwa mbele yake , upande wa kushoto kwake kulikuwa  na Bi Wema ambaye muda wote alikuwa akimwangalia Roma kwa tabasamu akiwa ni mwenye kufurahishwa na uwezo wa kula wa Roma.

“Siku zote nyumba ikiwa na mwanaume inaonekana kuwa hai”Aliwaza  mwanamama huyu  Mzungu wa Roho.

Upande wa Edna  , macho yake yalikuwa kwa Roma , aliwaza Roma ni mwanaume wa aina gani , kwanza amerudi asubuhi  hio akitoka kwa wanawake  wake , lakini alionesha  kutokuwa na hatia hata kidogo , ndio ndoa yao ni ya  mkataba lakini angalau aonyeshe  ile heshima ambayo ambayo ipo ndani ya neno  ‘Ndoa’ lakini kwa Roma  hakuwa ni mwenye kujali.

Edna aliendelea kutafakari  , kwanini Roma yupo kama alivyo Roma , kwanini  hakuwa siriasi na Maisha   , haoneshi kuwa na mipango ya kimaisha ya baadae , yeye anafikiria  kufanya mageuzi katika biashara lakini mume wake wa mkataba yeye anafurahia chakula  na wanawake  pasipo mpango wowote  alikuwa akishangaa na kujiuliza maswali lakini alikosa majibu.

“Mke wangu , itoshe kusema najivunia sana kuwa mumeo ,maana hii ‘breakfast’ ni nzito , wakati nabeba mizigo kwenye soko la Mbagala  kuna siku nilikuwa nashindia mihogo”Aliongea Roma na kisha alibeba bakuli iliokuwa na mchuzi na  kupeleka mchuzi wote tumboni.

“Roma unaonaje kwanzia sasa ukiwa siriasi na kazi?”Aliongea  Edna aliekuwa akimwangalia  ,Roma kabla ya kujibu alichukua yai la kuchemsha  na kuligonga mezani na kisha akaanza kulibandua  na kisha akalipeleka  mdomoni lote , akavuta  kikombe cha chai na kushushia..

“Aargh … mke wangu  umeng`ang`ania na mimi kuwa siriasi na Maisha , lakini mimi najiona niko siriasi”.

“Uko siriasi kivipi Roma , kila siku naletewa ripoti ya wewe kucheza magemu tu kazini na kwenda kula , huo usiriasi unaozungumzia   ni upi, haya ukirudi nyumbani badala ya kukaa kutulia na kuwaza siku ya kesho ,ila wewe unawaza wanawake na unaenda huko unalala na unarudi asubuhi kweli Roma”Edna leo hii asubuhi alionekana  kuwa na nongwa sana  , kiasi ambacho kilimfanya Roma kushangaa nini kimempata mke wake mpaka kuanza kulalamika.

“Mke wangu wewe piga kazi , mimi nitaishi kama mtoto wa Tajiri , nitafute mapesa mengi ya nini wakati hizi hatutazimaliza …Bebi Edna labda tukipata mtoto na nikiitwa baba naweza kuishi kama baba”.

Edna  hakutaka kuongea  maana aliona  kuongea na Roma hakuna heri yoyote  , alichukua mkoba wake na kumuaga Bi Wema na  kisha akatoka.

“Sijui ninamfanya nini angalau awe siriasi na Maisha?”Aliwaza Edna wakati akiwasha gari yake .

Roma alifika kazini kama kawaida , na kuingia kwenye jengo hili ambalo kwake kila siku sehemu hii ilizidi kumvutia kutokana na harufu nzuri za pafumu za warembo.

“Romaa..”Ilikuwa ni sauti iliomwita Roma   akiwa anaingia kwenye Lift  na mwanadada aliekuwa akimwita alikuwa ni Benadetha.

Benadetha kwenye macho ya Roma alikuwa mrembo sana ambaye alitamani pia  angalau apate wasaa mzuri wa kumjua nje na ndani , hayo ndio yalikuwa mawazo yake  , lakini mwanadada huyu alionekana kuwa bize sana na kazi , muda mwingi hakuwa   akipenda sana kupiga Stori  kama ilivyokuwa marafiki zake.

“Niambie mrembo, za wikiend?”

“Nzuri vipi wewe?”

“Njema kabisa”Alijibu Roma  wakati wakiwa wamesimama wakisubiria Lift ifunguke waingie , lakini mara nyuma yao wakasimama wanaume wawili na wanaume hawa hawakuwa wengine bali alikuwa  ni Abu na Elvice .

Elvice baada ya kumuona Roma alijikuta akikumbuka  tukio ambalo alifanyiwa na Roma na alijikuta  hofu ikianza kumjaa,Benadetha alisalimiana  na  Abu pamoja na  Elvice , ila Roma alionyesha hali ya kutofurahia uwepo wa mabwana hawa.

“Mmekuja kufanya nini  hapa?”Aliuliza Roma pasipo  kusalimia , huku Benadetha yeye akitangulia akiwaacha Abu na Elvice  wanamwangalia.

“Mr Roma nadhani  uwepo wetu hapa haukuhusu , kwanza nasikia una nafasi ndogo sana kwenye hii kampuni kwanini tuongee na  wewe juu ya swala lililotuleta hapa?”Aliongea Abu kwa kejeli  na Roma kwanza alitabasamu.

“Ni kweli sipaswi kujua nini kimekuleta hapa , lakini naamini unakumbuka  onyo nililokupa mara ya mwisho , hivyo kuwa makini”Aliongea Roma na muda huo huo Lift ilifunguka  na Roma aliingia huku Abu na Elvice wakiwa wamesimama wakiangalia Lift hio  inajifunga taratibu na Roma akamwangalia Elvice na kumkonyeza.

“Hawa mafala  wote wamekuja kufanya nini hapa?”Alijiuliza Roma wakati akiingia ndani ya  ofisi aliokuwa akifanyia kazi na aliiendeea meza yake , huku akisalimiana na baadhi ya wafanya kazi wenzake ambao walikuwa bize , isipokuwa tu Recho pekee ambaye hakuonekana  kwenye meza yake na alijiuliza ni kwannini mwanadada huyo hakuwa amefika kazini , lakini alipotezea.

“Hapa nicheze EuroTrack simulator  nipoteze poteze  muda , hii kazi siipendi , sema ndio hivyo kuna warembo  wanaonipa motisha lakini pia nataka kumridhisha mke wangu”Aliwaza Roma  na kuwasha gemu na kuanza kucheza , lakini bado akili yae ilionekana kutofarahia gemu hilo , ni kama  moyo wake haukuwa na amani , baada ya kuona hafurahii  aliinuka kwenye meza yake na kutoka  nje ya ofisi, huku wafanyakazi  wenzake wakimshangaa , aliingia moja kwa moja kwenye Lift na kwenda juu.

“ Miss Airport nahitaji kuonana na CEO”Aliongea Roma mara baada ya kumfikia Monica mwanamke ambaye alikuwa sekretari wa Edna , kwa Roma mwanadada huyu alimuona kama mbaya kuliko wanawake wote wa hii kampuni , kwanza  kabisa  alimuona kuwa na kifua  ambacho hakikuwa na manyonyo na   kilikuwa Flati kama vile  barabara za Airport.

Kwa huyu Monica na yeye hakuwa akipendezwa kabisa na Roma , alionekana kutompenda  kwenye hii kampuni na alitamanni awe na uwezo amfukuze , lakini licha ya kutokumpenda hakuwa akijua kuwa Roma ni  mume wa Boss wake.

“Yupo ila ana wageni huwezi kuingia”Aliongea Miss Airport .

“Miss Airport haujui kujibu maswali , darasani ulikuwa unapata  ngapi mimi nimeuliza swali moja ila wewe umajibu mawili”Aliongea Roma na kuuendea mlango wa CEO na kuufungua  na kuzama ndani na Monica alipandwa na Jazba na kumfuata Roma.

Roma baada ya kuingia alikutana na Sura tano , ya kwanza ilikuwa nni ya Mke wake ambaye yuko ‘Composed’ kama ilivyokuwa kawaida yake ya kujiamini  akiwa amekunja nne   na suti yake  ya rangi nyeupe , wa pili alikuwa ni Nadia mwanasheria  Mpya wa kampuni na Roma hakumtaraia  ndani hapo na watatu alikuwa ni Doris  ambaye  alikuwa amependeza kama kawaida , lakini  alikuwa na uso wa  usiriasi, wawili wa mwisho ni wanaume ambao Roma  hakuwa akiwapenda hasa wakiwa karibu  na mke wake yaani  Abubakari Hamadi na Elvice Temba.

Kwanza wote watano  walijikuta wakimwangalia Roma ambaye aliingia bila hodi  na muda huo huo na Monica aliingia.

“Boss nisamehe nimejaribu kumzuia lakini  hakunielewa”Aliongea Monica kwa wasiwasi  mno , aliogopa kumkasirisha bosi wake.

“Unaweza kwenda kuendelea na kazi Monica”Aliongea  Edna ambaye  alionekana kuwa kawaida , lakini alikasirishwa na kitendo cha Roma kuingia  hapo ndani moyoni  kwani alikuwa na kikao muhimu sana  na wageni wake, baada ya Monicca kutoka  Roma  alijongea mpaka upande wa kiti anachokaa mke wake na kisha akaketi  huku akizunguka zunguka , hakuwa na wasiwasi hata kidogo, Abuu alikuwa na hasira alitamani afanye shambulizi palepale  kwa Roma , kwani alikuwa akimchukia sana bwana huyo , lakini hakuwa na ujasiri wa kupambana na Roma ana kwa ana , alijua sio saizi yake , kwa upande wa Elvice na  yeye alikuwa hampendi kabisa Roma , hasa akikumbuka bwana huyo  ni mume wa Edna alijikuta  akitaka kuonyesha uwezo wake wa kimapigano aliokuwa ameupata akiwa jeshini , lakini alivyokumbuka namna ambavyo Roma macho yake yalibadilika   na kutaka kunyongwa na mkono mmoja aliogopa na kuona atulize mshono

Upande wa Doris na Nadia haikuelewaka walikuwa na mawazo gani ila walimwangalia Roma kwa macho ambayo yalikuwa na maswali mengi , upande wa  Edna alikuwa akimwangalia kila mmoja aliekuwa hapa  muonekano wake , na kisha akamgeukia Roma.

“Mke wangu kipenzi , Endelea na kikao chako sijaja kukuvuruga”Aliongea Roma na kisha aligeuza kiti chake na kuangalia upande wa nje kwa kutumia Dirisha akiangalia  upande wa bandari hii ya Dar es salaam ilivyokuwa bize.

Edna hakuwa na chakumfanya Roma , kwanza angeonekana sio mke bora kama angemfukuza , lakini pia  lilikuwa ni jukumu lake kumlindia heshima Roma kama mume wake , walikuwa wameoana kwa mkataba lakini  alikuwa akiheshimu sheria za ndoa , hivyo aliwasihi wenzake waendelee na kikao.

“Tunaweza kuendelea , Roma ni mume wangu hivyo hakuna kinachoharibika akiwepo hapa , labda kama kuna mwenye shida na uwepo wake”Aliongea Edna  na kuwaangalia  wenzake na Nadia ndio  aliekuwa wa kwanza kutingisha kichwa chake  kuonyesha anakubaliana na Edna , na  wengine wote wakaonyesha sura za kwamba hakuna tatizo , ila  ukweli kila mmoja hapo ndani hakufurahishwa na kauli ya Edna , kila mtu  aliona kauli hio kama  Risasi  iliozama moja kwa moja moyoni na kutibua  chemba za moyo.

Kikao kiliendelea na Roma  aligeuka na kuanza kutumia Computer ya mke wake , kama kawaida alikutana na gemu la nyoka na kuanza kucheza huku akila  Karanga zilizokuwa kwenye  kibakuli.

“Kutokana na ukubwa  wa uwekezaji huu naamini  viongozi wote wa  juu  tunapaswa  kwenda Japan kusaini huu mkataba na hayo pia ni mapendekezo ya Viongozi wa Yamakuza”Aliongea Abubakari.

“Kuna ulazima  wa CEO wote kusafiri mpaka Japan ?”Aliuliza Edna.

“Ndio Edna” Maagizo niliopewa na Yamakuza  ni kwamba CEO Abubakari  na wewe lazima muwepo , hili ni dili kubwa sana  ambalo kampuni ya Yamakuza  inafanya kwa mara ya kwanza na kampuni za Afrika ,tusilichukulie  kwa wepesi”Aliongea  Elvice na alionekana yupo hapo ofisini kuwakilisha kampuni ya Yamakuza.

“Kuna ulazima gani wa  mke wangu kwenda?”Aliuliza Roma kwa sauti na alionekana kukerwa sana na Elvice kwani aliona hakukuwa na sababu  ya Edna kwenda kama tu  anataka kuwakilishwa na mtu mwingine.

“Mr Roma hili ni swala ambalo linahusu   uongozi wa  juu wa kampuni  , hivyo  unatakiwa ukae kimpya  mabosi wako tukiongea”Aliongea Abubakari na Roma kwanza alitabasamu.

“Kwanza nikurekebishe  , unaonekana hauko profesheno na kazi yako , mimi sio boss wako  , pili   sioni haja ya Edna kwenda  kama anataka kuwakilishwa na mtu kutoka kwenye kampuni , sioni utofauti  mtu mwingine akienda  , kwani mazungumzo ya kibiashara  yashafanyika kupitia mkataba na kule ni kitendo cha kutia sahihi , kuna tatizo gani hapo , au shida tu uende na mke wangu”

Abu na Elvice walionekana kukasirishwa sana na Roma , ni kweli hakukuwa na shida ya Edna kwenda ila Elvice alitaka atumie nafasi  ya kwenda Japan na Edna ili akajiweke karibu  na angalie namna ya kumpata mrembo huyo, na mpango wa Elvice na wa Abuu hakukuwa na utofauti na  kila mtu  aliona hio ndio nafasi ya kuongeza ukaribu na Edna , lakini waliona mipango yao  Roma anaingilia , kwanini wafurahi.

“Alichongea Roma ni sahihi , hakuna haja ya CEO kwenda  kama anataka kutuma mwakilishi naweza kwenda mimi au Doris na hata Nasra ambaye ni mhasibu mkuu wa kampuni”Aliongea  Nadia na Roma alikumbuka  kwanini Nasra hakuwa kwenye kikao hicho kwani na yeye pia swala hili la mkataba lilikuwa likimhusu.

“Swala hili sio  nani kwenda , swala ni kwamba kampuni ya Yamakuza wamotoia ombi hilo kama Sharti”Aliongea Elvice  na alimfanya Roma akasirike Zaidi , jambo ambalo kwa Nadia na Doris hawakulipenda , kwani Roma alikuwa akionyesha wivu waziwazi.

“Mimi Roma Ramoni .. Edna ni mke wangu  licha ya kwamba ni kiongozi mkubwa wa kampuni hii  lakini  pia lazima apate baraka zote kutoka kwangu  hilo ni la kwanza , la pili  naomba nimuulize mke wangu ..” huku akimwangalia Edna

“Mke wangu kwenye huo mkataba kuna kipengele chochote ambacho kinakulazimisha wewe kwenda Japan??”Edna alitingisha kichwa kama hakuna na Roma alitabasamu.

“Sasa nasema hivi  nisikie  mtu anaongea tena kuhusu Mke wangu kwenda kusaini huo mkataba uone ..”

Aliongea Roma na  kurudi kwenye kiti na kuendelea kucheza gemu baada ya kutoa biti ambalo  lilimkasirisha kila mmoja Abu na Elvice walikasirishwa na kitendo cha Roma kuharibu mipango yao na  Doris na Nadia walionekana kuwa na wivu  wa Roma kumlinda Edna , walitamani nafasi hio iwe ya kwao.

Elvice na  Abuu japo  ya kukasirika  walipiga kimya , hakutaka tena  kuongea swala hilo, kwani waliogopa.

“Okey kwa upande wangu ataniwakilisha Doris pamoja na Mume wangu”Aliongea Edna na kufanya  hali ya hewa ibadilike.

Previoua Next