Roma alishangazwa na mke wake kumpendekeza kwenda Japani na Doris kwa ajili ya kusaini mkataba huo , lakini sio kwake tu alieshanga , kila mmoa hapo ndani alishangaa isipokuwa Dorisi.
“Naona mmeshangaa , lakini nimemchagua mume wangu kuniwakilisha kwakua anafahamu vizuri kuzungumza kijapani , itakuwa msaada mkubwa kwa Doris pia”Aliongea Edna na na alionekana maamuzi yake ni ya mwisho na hakukuwa na wakupinga , ila Roma bado alikuwa akiwaza kwanini mke wake anafanya hayo pasipo kumuambia kwanza kama anataka kwenda Japani au la.
Kikao kiliisha na Edna aliwaambia waondoke kwani alikuwa na mazungumzo na mume wake na hakukuna aliekuwa akipinga wote walikuwa ndani ya ofisi ya mwenye kampuni na pia Edna na Roma ni mume na mke hivyo ni haki yao kuongea hata kama hawapendi.
“Mke wangu kuna ulazima mimi wa kwenda Japani ,Doris anaweza kufanya vizuri tu kwani anajua kingereza”.
“Mimi ndio bosi wako na nishafanya maamuzi hivyo, Kwanza inuka kwenye kiti changu”Aliongea na Roma hakuleta ubishi alinyanyuka.
“Lakini hata kama, kwanini haukuniambia mapema , tokea nyumbani , jana tumeshinda wote hausemi”Edna alinyamaza hakujua aseme nini , ukweli Edna alitaka kumwambia Roma jana yake usiku lakini Roma aliondoka kwenda kwa mahawala wake hivyo alikosa nafasi.
“Kama hutaki kwenda nitaenda mimi mwenyewe”
Roma alijikuta akianza kufkiria , aliwaza kama Edna akienda wale mamluki lazima wangetumia nafasi hio kuweka mazoea na mke wake , lakini pia aliamini huenda Edna hakutaka kwenda kutokana na kuwakwepa Abu na Elvice , aliona huenda ni maamuzi sahihi mke wake ameyafanya.
“Okey mke wangu nitaenda kukuwakilisha vyema na kuhakikisha dili lako linafanikiwa”.Edna alitingisha kichwa.
Na Roma aliona asiendeleea kukaa hapo ndani na aliusogelea mlango kwa ajili ya kutoka.
“Roma..! “Aliita Edna na kumfanya Roma ageuke amwangalie
“Nini mke wangu?”.
“Najua siku tuliosaini mkataba haukuusoma licha ya kwamba nilikuambia uusome”
“Ndio , lakini mkataba unaingiaje hapa Edna?”Edna alifikiria kidogo kwa kukaa kimya na kumwangalia Roma .
“Basi unaweza kwenda tutaonana nyumbani”Aliongea na Roma alitingisha kichwa na kisha akatoka.
“Ningemwambia mkataba wetu unakipengele cha kutoingiliana kwenye maswala ya kikazi huenda angekasirika nadhani nimefanya jambo zuri kutoongea , ningezidi kujiweka mbali na yeye na ushauri wa Bi Wema pia ni wa maana lakini pia nataka kujua kwanini macho yake yanabadilika”Aliwaza Edna.
“Miss Airport kazi njema” Aliongea Roma huku akimpita Monica ambaye aliishia kubenua midomo, hakupendezwa na Roma lakini pia alijiuliza kwanini anamwita “Miss Aiport’ .
Roma baada ya kutoka moja kwa moja alienda kwenye ofisi ya Doris, alitaka kwenda kumpetipeti mwanamke huyo kwani alijua alikuwa na hasira nae , kwani macho yake wakati wakiwa ndani ya ofisi yalikuwa yakionyesha kabisa , hali iliokuwa ikiendelea kwenye kichwa cha mrembo huyo .
Aliingia na kumkuta akiwa bize kama kawaida akiwa na miwani ya kuzuia mwanga wa Bluu wakati wa kutumia tarakishi,licha ya kumuona Roma ameingia lakini hakutaka kumuongelesha Roma , bado alikuwa na chuki nae.
“Bebi Doris , acha kujifanya haujaniona”.
“Roma niko bize kwasasa naomba kama hauna jambo la maana usinisumbue”Roma alitabasamu na kisha akasogea mpaka kwenye kiti cha Doris na kukigeuza na kikazunguka na wakaangaliana.
“Roma nimekuambia nina kazi naomba utoke ofisini kwangu , jaribu kuwa muele..” Kabla hajamaliza Roma alikuwa ashanasisha mdomo wake kwa Dorisi na kumfanya mwanamke huyu atoe macho na kuanza kumsukuma Roma , lakini alishindwa kwani Roma alikuwa amembana haswa , na alishitukia mkono umetua kwenye suruali yake, kwenye kitumbua chake na alihisi shoti ikisambaa mwili mzima na Roma aliendelea kufokonyoa.
Dakika mbili mbele Doris hisia zilimzidia na alishindwa kujizuia , akili ilikuwa inamwambia unachofanya sio sahihi na hapo ni ofisini lakini mwili haukuwa tayari kuacha na Roma alitumia udhaifu huo haswa kwani aliongeza mashambulizi na kuendelea kufokonyoa.
Dakika tano mbele Doris alimvua surali Roma mwenyewe na kutoa Mchi wa Roma , huku akisimama kabisa na waliendelea kunyonyana midomo , hakuna aliewaza kabisa hapo ni ofisini , akili zao zilikuwa mbali kabisa , baada ya Roma kuona jaribio lake limefanikia alifyatua suruali ya Doris na kuishusha akikusanya na nguo ya ndani kwa wakati mmoja na Dorisi alielewa somo kwani alishikilia kiti na kubinuka kimbuzi mbuzi na Roma akauzamisha mpini na kilichosikika hapo ni miguno ya kuzidiwa kutoka kwa Dorisi.
“Romaa..Arrgh..”
Doris hakuamini kama amefanya uzinzi kwenye ofisi yake , siku zote alikuwa ni mwenye kujiambia kwamba hata iweje hawezi kupanajisi sehemu yake anayofanyia kazi , lakini siku hii ya leoalikuwa amefanya kile alichokuwa hataki kitokee.
“Naomba utoke niendelee na kazi”Aliongea Doris huku akimwangalia Roma.
“Seme bebi cha ofisini ni kitamu balaa”.
“Roma naomba utoke”Alitumia kauli ya kibabe na Roma hakuwa na ubishi alitoka zake na kurudi kwenye ofisi yake anayofanyia kazi kuendelea na kucheza gemu.
Ile anakaa na kutulia tu simu yake ilianza kuita na alipoangalia anaepiga alikuwa ni Najma , alijikuta akijilaumu kwa wakati mmoja kumsahau Najma kwani tokea amuache hospitalini hakuwa amemtafuta hata kidogo.
Alipokea na Najma alionekana kumlalamikia Roma kwamba kamdanganya , kwani alimuahidi kwamba atarudi na Roma nae hakuwa nyuma alimpa habari za kiuongo uongo na mwanadada huyo alikubari japo kishingo upande.
Ki ufupi ndani ya moyo wa Roma alikuwa akimpenda Najma lakini alikuwa mzito sana kuuanzisha mahusiano nae , hakujua ni kwanini lakini aliona kukaa mbali na Najma ni heri Zaidi kuwa nae na ndio maana hakuaka sana kuonekana mbele ya Najma.
****
Ilikuwa ni muda wa usiku saa nne hivi kwenda saa tano , ndani ya jiji la Mwanza ,alionekana mwanamke ambaye alikuwa akikimbia huku akiwa ameshikilia tumbo kwa mkono mmoja , huku mkono mwingine ukimsaidia kumpa sapoti ya kutembea katikati ya chochoro zilizokuwa ndani ya eneo la Mabatini.
Mwanamke huyu alionekana kupitia maumivu mengi , kwani damu nyingi zilikuwa zimeganda kwenye nguo zake hasa upande wa tumbon na kwenye kifua , alikuwa amevalia suruali ya jeans rangi nyeusi na viatu vikubwa kama Mabuti vyeusi , huku akiwa na blazia ya rangi nyeupe ambayo ilimfanya damu iliokuwa imemtoka na kusambaa na kuonekana vyema.
Watu waliokuwa kwenye hili eneo walionekana kumshangaa mwanamke , licha ya kwamba alionekana kutaka msaada kutoka kwao kutokana na hali yake ila hakukuwa na mtu mwenye ujasili wa kumsaidia na pia kwa mwanamke hakuonekana kuwa tayari kuomba msaada kwa watu waliokuwa ndani ya hili eneo ,ni kama mtu ambaye hakutaka kumbebesha mtu mzigo juu ya mazira yake.
Baada ya mwanamke kutembea kwa umbali mrefu , akikaribia kutoka ndani ya sehemu hii iliokuwa ikifahamika kwa jina la Mabatini kuingia mtaa mwingine upande wa kushoto , alijikuta akidondoka pembeni ya bababara , sehemu ambayo ilikuwa na nyasi ndefu kidogo zilizomfanya kumzibia kwa mbele asipate kuonekana kwa wale wanaopita , lakini sehemu hii pia kulikuwa na mti mkubwa ambao ulifanya hili eneo liwe na kivuli kilichofanya giza kuwa kubwa kuliko maeneo mengine .
“Atakuwa ameelekea wapi?” Aliuliza kijana mmoja kati ya watatu walikuwa barabarani mita kadhaa kutoka alipodondokea Mwanamke , walionekana walikuwa wakimfafuta , wanaume hawa walikuwa wameshikilia siraha mkononi na walionekana walikuwa wakimtafuta mwnamke kwa ajili ya kumfanyia shari.
“Ngalu ana jeraha la risasi , hawezi kwenda mbali maana amepoteza damu nyingi “Aliongea lakini moja ya wale wanaume aliona majani yaliokuwa upande wake yakitingishika , huku akiwa ameona kivuli cha mtu lakini ni kama hakuwa na uhakika.
“Oya pale” Aliongea na wenzake wote wakageuza macho kuangalia na hawakutaka tu kuangalia kwa umbali , walianza kusogea ndani ya eneo hilo , ili kuhakiki kile wanachodhania.
Walijongea kwa tahadhari kubwa sana , lakini kabla hata hawajaafika ile sehemu , mmoja aliangalia chini na kuona kitu .
“Oya Kishoka angalia hiki”Aliongea bwana huyu mfupi kuliko wenzake wote huku akiwa ameshikilia kitambaa aina ya Bandama , walianza kukikagua.
“Ndio ni damu hii , hayuko mbali “ waliongea huku wakianza kutawanyika , kwani waliona mtu ambaye walikuwa wakimtafuta alikuwa maeneo hayo .
Upande mwingine , wakati vijana hawa wakiendelea kutafuta , Mwanamke alikuwa mita kadhaa kutoka walipokuwa wamesimama na alionekana kuvumilia kutoa kelele kwani maumivu yalikuwa makali , ni kweli alikuwa amedondosha kitambaa alichokuwa akitumia kuzuia sehemu ya jeraha la risasi na kufanya kidonda kizidi kuvuja damu huku maumivu yakiwa ya hali ya juu.
“Hatimae nimekupata” Aliongea bwana huyu aliekuwa anaitwa Kishoka na kuwaita wenzake , Mwanamke hakutaraia kukamatwa mapema hivyo licha ya kuvumilia sana maumivu alitamani kuongea neno , ila nguvu zilimuishia kabisa.
“Oya kishoka mpige risasi tuondoke”
“Unaonaje tukimpeleka kwa boss kwanza akafanya maamuzi, huenda akawa na maamuzi mengine kuliko aliotoa mwanzo”
“Kishoka boss alituambia tukimkamata tumpige risasi , tumpeleke wa nini sasa mtu mwenyewe anakaribia kufa , wewe mmalizie , kama unashindwa lete nifanye mimi”
“Okey Ngalu wewe mmalize” Aliongea na kisha akampatia siraha alioshika mkononi kijana mnene kidogo alieenda hewani ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Ngalu na alionekana kutokuwa muoga na kuwa katili kuliko wenzake , alinyoosha bastora kwa ajili ya kumpiga mwanamke aliekuwa chini akiwaangalia kwa tabu , Mwanamke alionekana kuwa nusu mfu hakuweza kujitetea hata kwa kuongea.
Mwanamke , alionekana kukata tamaa kabisa , alianza kuona picha picha wakati akiwa mtoto akicheza na mama yake huku akiwa na furaha sana , alianza kuona kumbukiumbu nzuri ambazo kwake zilionekana kuwa ndio nyakati aliopokuwa na furaha sana katika Maisha yake alipokuwa na mama yake ,alijikuta akilazimisha tabasamu hakutaka kufa akiwa na sononeko moyoni , tabasamu la mwanamke huyu liliashiria hali ya kufuta yote na yupo tayari kupokea kile ambacho Mungu amemuamulia.
“Nisamehe mama , sijafanikiwa kulipiza kisasi”
Aliwaza mwanadada huyu na kisha akafumba macho kusubiria saa yake ya mwisho , aliendelea kufumba macho kwa takribani dakika mbili , lakini bado alijiona mzima , alifungua macho huku akiwa anadhania labda wanaume hao wameghairi kumuua kama ambavyo wametumwa na bosi wao , lakini ile anafungua macho anakutana na sura nyingine kabisa , licha ya kwamba macho yake yalikuwa na ukungu , lakini aliweza kutambua kuwa mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni mwanaume ambaye hakuwahi kumuona mahali kutokana na mavazi yake, aliangalia pembeni na kushangaa Zaidi baada ya kuona wale watu waliokuwa wakitaka kumuua dakika chache nyuma wanatapatapa huku miili yao ikishindana na kifo , lakini licha ya mapambano hayo ya kimwili ,kifo kilionekana kuwa na nguvu Zaidi na wakatulia tuli.
Mwanaume yule alichuchumaa na kisha alishika mkono wa mwanamke na kisha akatoa mkono aliouweka katika jeraha lake , na kitendo cha kutoa tu mkono damu zilianza kutoka mfululizo.
“Inaonekana umeumia sana , inashangaza mwanamke kama wewe kuwa na uwezo mkubwa wa kuvumilia maumivu” Aliongea mwanaume huyu huku mwanamke akiendelea kumwangalia kwa mshangao ,alishindwa kuongea lolote kutokana na hali yake ya kimwili kukosa nguvu hata ya kutamka neno , alichofanya ni kumwangalia tu pasipo kusema lolote.
Yule mwanamke nguvu zilizidi kumuishia na alijikuta macho yakijifumba yenyewe pasipo yeye kuyaruhusu na mpaka hapo hakuelewa nini kiliendelea.
Baada ya kufumba macho muda mrefu huku akishindwa kuelewa nini kiliendela , hatimae aliweza kuyafumbua , aliangaza eneo alilokuwepo na kujiona yupo ndani ya chumba chenye harufu nzuri , sehemu ambayo hakuwa akiijua kabisa.
Wakati akiendelea kuangalia mandhari ya hili eneo , huku akijihisi kuwa na nguvu kuliko alivyokuwa mwanzo , alizidi kushangaa , chumba kilikuwa kizuri lakini alikuwa pake yake na hakujua ni kwa namna gani alifika mahali hapo , alinyanyuka na kukaa kitako huku akianza kukumbuka matukio yaliomtokea na picha mbalimbali zilianza kumtokea , alikumbuka alivyokuwa akipambana na mpaka kupigwa na Risasi tumboni, namna ambavyo alikuwa akikimbia huku akivuja damu na kusikia maumivu makali na watu walioagizwa kummaliza wakiwa nyuma yake wanamfukuzia , alikumbuka yote hayo lakini mwisho kabisa alikumbuka alipokuwa amekamatwa tena na wanaume ambao walikuwa wanataka kummaliza na akafumba macho kwa mara ya mwisho kusubiria kifo chake , aliendelea kukumbuka alipofungua macho yake na kumuona mwnaume ambaye hakuwa akimtambua na baada ya hapo hakuelewa ni nini kiliendelea .
Baada ya mwanamke kukumbuka hayo , alijikuta akijiangalia tumboni na kujiona akiwa msafi huku akiwa na mavazi mengine kabisa , alitoa blazia ya rangi ya pink aliokuwa amevalia na kuangalia eneo la tumboni , lakini kilichomshangaza huyu mwanamke ni kwamba sehemu yake ya tumbo ilikuwa ikifanana na sehemu nyingine za mwili , kwa maana kwamba hakukuwa na jeraha la aina yoyote.
“Imekuwaje? Ni swali la kwanza la mwanamke huyu kujiuliza , kwani alikuwa akikumbuka kabisa kuwa alikuwa na jeraha tumboni.
“Au nimepona , inamaana nimelala muda mrefu kiasi kwamba hata jeraha langu limepona na kutokuacha kovu?”Aliendelea kujiuliza maswali kedekede yaliokosa majibu.
“Hapana hata kama nimepona , lazima kuwe na alama au kovu siwezi kupona haraka sana kwa namna hii”Aliendelea kujiuliza mwanamke maswali meengi , lakini yasio kuwa na majibu , wakati akiendelea kuwaza mara mlango ulifunguliwa na akaingia mwanamke mwingine.
“Habari yako dada, umeamka?”
“Hapa ni wapi na nimelala kwa miezi mingapi?” Mwanadada yule alievalia sketi ya rangi ya bluu na tisheti ambayo kwa kumwangalia mara mmoja tu ungejua ni muhudumu wa hoteli.
“Upo Iringa dada , hapa ni Camp Nine Motel , umeletwa jana na mwanaume alietambulisha kwa jina la Roa Ramoni”
“Roma Ramoni , jana???!!!”Mwanamke alishangaa yaani kama ni kweli aliletwa jana , inamaana ni jana yake alipigwa risasi na kuokolewa lakini pia ni jana yake ameletwa hapa Moteli na mtu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni akiwa na jeraha tumboni.
“Dada leo ni tarhe ngapi na ni siku gani?”Mwanadada muhudumu alishangaa.
“Leo ni Jumanne na ni tarehe ishirini mwezi wa kumi mwaka 2021”Alizidi kushagaa Zaidi na Zaidi , aliinua tena blazia aliokuwa amevaa na kuangalia sehemu ambayo anakumbuka kabisa amepigwa risasi lakini bado ni vilevile.
“Dada hebu kwanza naomba unieleze , wakati naletwa hapa nilikuwaje kuwaje yaani sikuwa nimeumia?”Mwanadada muhudumu bado aliendelea kushangaa , kwanini mteja wake ana maswali mengi , kwani alichokuwa akikumbuka kwenye akili yake ni kwamba mwanaume aliemleta alimuachia tu maagizo kwamba mtu wake anapaswa kupewa huduma kwa uangalizi mpaka pale atakapo amka lakini hakuwa na shida yoyote Zaidi ya kuwa usingizini.
“Uliletwa kama ulivyo tofauti ni kwamba ulikuwa tu umelala , mbona maswali mengi dada kwani aliekuleta sio mpenzi wako?”
Mwanamke bado alishangaa maswali ya mhudumu na kuzidi kuchanganyikiwa Zaidi , alitaka kuthitbitisha kile ambacho anawaza , hakuamini kwamba yupo ndotoni na kupigwa kwake risasi kulikuwa ni ndoto.
“Jana nimeletwa hapa saa ngapi ?”Aliuliza mwanamke na mhudumu akafikiria kuonekana alikuwa akikumbuka.
“Umeletwa hapa kati ya saa tano na nusu hivi”Mshangao mwingine ulimpata mwanamke .
“Kama nililetwa saa tano na nusu na nilikuwa Mwanza wakati napigwa risasi amenisafirisha vipi mpaka kunileta Iringa ndani ya nusu saa” mwanamke aliwaza .
“Dada mini nina wateja wengine wa kuwahudumia , hizi ni pesa ambazo mpenzi wako kakuachia kaniambia ni kukabidhi baada ya kuamka , alisema zitakusadia katika matumizi”Aliongea mwanadada yule huku akitoa kibunda cha pesa zilizokuwa kwenye mfumo wa Euro na kumkabidhi mwanamke na mwanamke alizidi kushangaa maradufu.
Baada ya mhudumu kutoka , mwanamke alijiramba kofi moja zito ili aamke katika ndoto , lakini haikuwa ndoto , bado alihisi maumivu na kujiona kinachotendeka kwa wakati huo ni uhalisia.
“Rose amka kwenye usingizi , Rose unaota amka” Mwanamke alijiambia kwa kujiita jina lake , ili aamke katika ndoto , lakini bado mwanamke hakua akiota kila kitu kilikuwa ni uhalisia na mwanamke katika kichwa chake likabaki jina la Roma Ramoni .
Naam mwanamke ndio Rose wa Club B ilikuwaje inaendelea
Kiliendelea nini baada ya hapo .. tunaendelea…
Comments