RWANDA -KIGALI 2014
Ni ndani ya hoteli kubwa iliokuwa ndani ya jiji hili la Kigali , hoteli iliokuwa ikifahamika kwa jina la The Aquad alionekana mwanamke na mwanaume wakiwa ndani ya chumba kikubwa cha hoteli hii , katika floor ambayo ilikuwa ikihudumia VIP , huku nje ya Floor hii wakiwa walinzi wengi waliokuwa wamevalia suti.
Ndani ya chumba hiki mwanaume alionekana akiwa amepiga magoti chini , huku mwanamke mmmoja mrembo wa mweupe wa kabila la wanawake wa Babati yaani Wairaq akiwa amesimama huku akiwa na machozi mengi usoni , alionekana kulia mfululizo huku akiwa ameshikilia moyo wake.
“Nisamehe sana Raheli, naomba unisamehe mpenzi ,,, sikudhania haya yote yatatokea”
“Jeremy acha kuomba msamaha wako wa kipuuzi mbele yangu , unazidi kuniumiza , kwanini ulinificha muda wote kama Lorraine alikufa , kwanini Jeremy haukuniambia hii.. hiii…kwanini Jeremiiii…..”Mwanamke alionekana kulia kilio ambacho hakikiwa cha kawaida huku akimshutmu Jeremiii.
“Sikuwa na jinsi Rahel , sikutaka upitie maumivu niliopitia mimi”.
“Hata kama Jeremy , Lorraine ni mwanangu nilipaswa kujua haya yote ,hivi unajua ni siku ngapi nilitumia kuchukua maamuzi ya kukukabidhi Lorraine na kubaki na Edna eeh , unajua ni uchungu gani niliopitia kuwa mbali na mwanangu , hayo yote nilifanya kwasababu nakupenda Jeremy .. lakini kwanini ulishindwa kumlinda…..”Kilio kilikuwa ni cha aina yake kwa mwanamama huyu alionekana kumlaumu Jeremy kwa yale ambayo yamemtokea Lorraine , lakini pia anamlalamikia Jremy kwa kutompa taarifa ya kifo cha mwanae ,
“Rahel naomba unisamehe , najua ni maumivu gani unapitia baada ya taarifa hii , najua ulitarajia kumuona Lorraine akiwa na furaha ndani ya mikono yangu , lakini mimi pia kama baba yeke nilikuwa nikimpenda sana Lorraine na nilipanga kumpa Maisha mazuri , lakini haya makafir.. ya Dunia yamenichukulia mwanangu”.
“Unamaanisha nini Jeremy?”Aliuliza mwanamama huyu huku akisimama , hakumuelewa Jeremy baada ya kusema makafir alitaka kujua anamaanisha nini, Na kwa Jeremy alijikuta akijilaumu kwa kuropoka.
“Unamaanisha nini Jeremy ukisema Makafir ndio waliomchukua Lorraine?”
“Sijamaanisna hivyo Lorraine.. ni …”Kabla hajamaliza kuongea alikuwa ashashikwa tai na Raheli , mwanamama huyu alionekana kuzingatia kila neno mtu analoongea na ndio maana aliweza kumsikia vyema Jeremy alipo sema Makafir .
“Rahel namaanisha ,,”
“Usipo nipa maelezo ya kutosha leo Jeremy nakwambia hapa hutoki …”Jeremy alikuwa akimjua sana Rahel akiamua lake jambo lazima litimie , lakini hakutaka kumwambia Rahel juu ya kile anachokijua na anachoendela kukitafutia ukweli wake.
Jeremy aliamini kwa asilimia mia moja Ndege ile haikuanguka , bali kuna mpango wa siri ambao ulikuwa ukiratibiwa na mataifa yenye nguvu duniani , mpango ambao ulihusisha ndege hio kupotea, aliogopa kumwambia Rahel ukweli.
“Jeremy umenificha kwa miaka kumi na sita juu ya kifo cha mtoto wangu .. ukinificha jambo lolote na nikagundua jua sitokuja kukusamehe mpaka naingia kaburini”Aliongea mwanamama huyu huku akionesha hasira zake waziwazi.
Jeremy hakuwa na jinsi aliona Rahel anapaswa kuujua ukweli ule ambaye yeye alikuwa akiufahamu , aliona haina maana ya kumficha.
“Rahel tokea siku ambayo ndege ile ilipotea moyo wangu haukuwa na Amani kabisa , niliona kabisa kuna jambo ambalo halikuwa sawa , sikuwa na amani nilikuwa nikiota kila siku Lorraine yupo hai lakini sehemu aliokuwepo anateseka..”Alitulia kwanza na kufuta machozi na kisha akasimama huku akiwa anaangalia dirisha kama mtu aliekuwa akitafuta kitu.
“Kupotea kwa ndege ya shirika la M ilikuwa ni mpango wa wazungu”Rahel ni kama hakuwa amemsikia vizuri , kwani alinyanyuka na kwenda mpaka mbele ya Mheshimiwa Jeremy na kumwangalia vizuri usoni.
“Nieleze vizuri nielewe Jeremy .. mpango wa Wazungu ,, unanichanganya hebu eleza nielewe”
“Siwezi kukueleza mengi Rahel lakini naamini Lorraine yupo hai .. hakuna ushahidi wowote wa ile ndege kuanguka Rahel , yote ni mipango na mahesanu ya wazungu juu ya mpango ambao mpaka sasa hatuujui , mpango ambao umeratibiwa na mataifa makubwa yenye nguvu.. hii ni siri kubwa Rahel na sitaki kukuambia Zaidi ila naomba uelewe nitahakikisha naujua ukweli wote , nitatumia nguvu zangu zote kuhakikisha naupata ukweli wote na kama Lorraine yupo hai nitamrudisha “.
Taarifa hio ilionekana kuwa nzito sana kwa mwanamama Rahel , alikuwa akimjua Jeremy kwa muda mrefu tokea walivyokutana miaka kadhaa nyuma na kuanzisha mahusiano yao , alikuwa akimjua kuwa hawezi kuongea jambo ambalo hana uhakika nalo , alijikuta nguvu zikimuishia na kurudi kukaa kwenye sofa huku machozi yakiendelea kumbubujika.
Ukweli ni kwamba mwanamama huyu sababu ambayo ilimfanya asigundue kuwa Lorraine amekufa ni kutokana na kwamba Jeremy alitumia Mchezo wa kumuigizia kuwa anamchukia , kipindi chote ambacho Rahel alijaribu kuwasiliana na Jeremy , mheshimiwa huyo alionyesha kumchukia sana Rahel na hakutaka mazungumzo, na hata pale ambapo aliomba kuonana na Lorraine mheshimiwa alimtishia Rahel kukaa mbali na Lorraine la sivyo ataongea ukweli wote na dunia ijue kuwa Edna ni mwanae.
Kwa upande wa Rahel hakuwa tayari kwa watu kujua kuwa Edna sio mtoto wa Adebayo kwani kulikuwa kuna mkataba wa siri ambao alisaini na familia ya Adebayo , mkataba ambao Raheli alisainishwa na mama yake Adebayo.
“Jeremy una uhakika ndege ile haikudondoka na yote uliosema juu ya mpango ya wazungu ni kweli?”Aliuliza kwa sauti ndogo iliokuwa dhaifu na Jeremy alimuonea huruma sana Rahel , alijua ni afadhali kwake maumivu ya kumpoteza Lorraine yamezoeleka kwani tukio lilikuwa ni la muda mrefu tarkribani Zaidi ya miaka kumi na sita , alimsogelea Rahel na kisha akamkumbatia na walianza kuambizana kulia.
Kwa namna ambavyo Jeremy alikuwa akillia usingedhania ni kiongozi mkubwa wa taifa , kiongozi ambaye wananchi wa Rwanda wanamtegemea sana kuwafikisha katika nchi ya Ahadi.
“Ni kweli Rahel nina amini kwa asilimia kubwa Lorraine yupo hai na ninaompango wa kuhakikisha namrudisha”.
Rahel alifuta machozi na kisha alijitoa kwenye mikono ya Jeremy na akaweka sura ya usiriasi .
“Jeremy kama haya unayoyasema ni ya kweli hakikisha unaujua ukweli la sivyo sitokusamehe kwa kumpoteza mwanangu Lorraine”Aliongea mwanamama huyu na akafuta machozi na kuchukua mkoba wake na kutoka ndani ya chumba hiko.
****
Ilikuwa ni muda wa saa sita kamili za mchana alionekana Roma akiingiaa maeneo ya Club B , alikuwa na muda mrefu hajaingia ndani ya hii club , kwani tokea apate mke mara nyingi alikuwa akienda moja kwa moja nyumbani kwa Rose , lakini leo alikuwa amewahi sana kuja haya maeneo na alijua kabisa Rose hakuwa kwake na atakuwa ofisini na mawazo yake yalikuwa sahihi kwani alimkuta mwanada huyo akiwa kazini kama ilivyokuwa kawaida yake na kwa Rose alishangaa ujio wa Roma muda huo wa mchana.
“Hubby karibu” Aliiongea Rose huku akitoka kwenye meza na kuja kukaa kwenye masofa , huku akimwangalia Roma kwa kumsanifu , aliwaza Roma kaja muda huo kwasababu gani.
“Bebi Rose nimekuja leo nina shida”Aliongea Roma mara baada ya kuketi.
“Shida gani mpenzi , ongea tu nipo tayari kukusaidia”
“Unamiliki nyumba ngapi?”
“Bebi kwanini unauliza hivyo nina nyumba nne mbili hapa Dar na nyingine zipo nje kidogo ya Dar , kuna ambayo ipo Kisarawe na Bagamoyo “
“Kwa hapa Dar ukiachana na unayoishi hio nyingine ipo maeneo gani?”
“Ipo Kigamboni Mbutu huko”
“Hio ndio shida yangu , nahitaji nyumba nina marafiki zaku kutoka nje ya nchi ambao wanaingia leo nchini nataka niwahifadhi kwa muda , ila sina nyumba kwa sasa”Aliongea Roma na Rose alitabasamu.
“Hubby chukua ya Kigamboni itakufaa , pia ni sehemu nzuri kwani ipo ufukweni na isitose ni mpya na nilikuwa nikipanga kuipangisha lakini sikupata mtu”Aliongea Rose na Roma alitabasamu na kumkiss Rose.
“Nataka nikaione leo maana marafiki zangu wakifika nchini moja kwa moja nataka niwapeleke na wanaingia leo usiku”Aliongea Roma na Rose hakukataa , kwanza alijisikia fahari kwa Roma kumuomba msaada yeye, msaada ambao Roma ameomba kwake ulikuwa na maana kubwa.
Ni ndani ya dakika chache tu walikuwa washafika Mbutu , hii sehemu ilikuwa nzuri licha ya kwamba haikuwa na nyumba nyingi , lakini mazingira yake yalikuwa safi sana kiasi cha Roma kupapenda na kuona wanajeshi wake kukaa hapo ni chaguzi sahihi.
Waliona jumba hili ambalo lilikuwa kubwa sana kiasi kwamba hata Roma mwenyewe alishangaa , licha ya kwamba alikuwa akijua Rose ni Tajiri kwa kufanya biashara yake ya kuuza madawa ya kulevya , lakini hakujua kama anapesa kiasi hiko cha kumiliki mjengo kama huo. Walikabidhiana nyumba hio na Roma akamrudisha Rose nyumbani.
Saa mbili kamili Roma alikuwa nyumbani kwa ajili ya chakula , sebuleni alimkuta Bi Wema pamoja na Edna kama kawaida na walikuwa washaanza kula, alimsalimia Bi Wema na kisha akamgeukia mke wake na kumwangalia anavyokula kimapozi , Edna alikuwa bize na chakula chake , lakini ile anapeleka kijiko mdomoni alimwangalia Roma na kukuta Roma anamwangalia.
“Mbona unaniangalia hivyo?”
“Bebi unajua hata staili yako ya kula inakufanya uwe mrembo kuliko wanawake wote duniani”Edna alijikuta akimwangalia Bi Wema na kuona aibu kiasi kwamba mwili wake ulipata uwekundu.
“Kaa pakua chakula kula”Aliongea Edna na kumfanya Bi wema aliekuwa pembeni atabasamu kwa kushuhudia aibu za Edna.
Roma alipakua chakula chote kilichokuwa kwenye mabakuli na kujaza kwenye sahani kama mlima Kilimanjaro na kuanza kula , bila habari .
“Roma..!”Aliita Edna huku akimwangalia Roma na sahani yake na Roma alimwangalia Edna bila kuongea.
“Kesho kutwa ndio siku ya kwenda Japan , ujiandae basi nitakupatia baadhi ya karatasi za mkataba uzisome”.
“Mke wangu mimi naenda kama mkalimani kuna haja gani ya kuzisoma?”
“Ndio najua lakini huu mkataba ni muhimu sana kwa kampuni na kukitokea tatizo lolote ninaweza kufirisika moja kwa moja , ni vizuri ukijua nini kinaendelea ili kama ikitokea tatizo iwe rahisi ya wewe kuligundua kuliko kumwachia kila kitu Doris”.
“Sawa nitazipitia mke wangu”.
Baada ya Roma kushiba , aliangalia saa yake na kuona ni muda muafaka wa kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kupokea wageni wake , kwani mchana alikuwa ashawasiliana na Sauroni na kumpa taarifa kuwa wataingia Tanzania saa nne usiku.
“Wife ninatoka kidogo”
“Leo naomba usiende”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae na sio Edna tu hata Bi Wema alishangaa , lakini alitabasamu moyoni .
Ukweli ni kwamba Edna mchana yote alikuwa akifikiria swala la kujaribu kumpa Roma kitumbua na alishinda kwa kutafuta mitandaoni jinsi ya kumuanza mume wake maana alikuwa na aibu sana , alitamani kumuuliza Bi Wema ampe mbinu lakini aliona aibu na msaada pekee aliona ni kuingia mtandaoni na kutafuta namna ya kumuanza Roma.
“kama nitakuwa nampa maramoja moja anaweza kutulia nyumbani”Aliwaza wakati akiendelea kusoma mbinu mtandaoni.
Na alijikuta akipata mpango kabambe wa kumpagawisha Roma huku akiamini kama atafanikiwa katika mpango huo basi anaweza kumtuliza Roma nyumbani.
Na alipanga mpango wenyewe ili ukamilike lazima Roma alale nyumbani na ndio maana baada ya Roma kumwambia anataka kutoka aliona mpango wake hautofanikiwa na alitaka kuukamilisha kabla ya Roma na Dorisi kwenda Japani.
Comments