Reader Settings

Roma hakujua sababu  ya Edna  kumwambia abaki nyumbani ,lakini kwake  yeye alikuwa na jambo muhimu sana la kufanya usiku huo  na kwa vyovyote vile asingeweza kukubaliana na mke wake.

“Mke wangu ninatoka ila nitarudi”Aliongea  Roma na akanawa mikono na kuchukua ufunguo wa Gari yake na kuondoka.

Edna aliishia kusikilizia tu mngurumo wa gari  ukifubaa kwenye masikio yake ,  Bi wema hata yeye alijisikia vibaya , alitamani Roma abaki nyumbani kama Edna alivyopendekeza lakini hakubaki , aliwaza ni jambo gani la muhimu ambalo Roma anaenda kulifanya nje kuliko kubaki na mke wake  , hakujua lakini hakutaka kuwaza Zaidi , kwani Roma alikuwa ni mwanaume na pia hakutaka kuangilia katika mahusiano yake yeye na Edna.

Edna alirudi chumbani kwake , huku akijisikia mnyonge sana lakini pia akiwa na hasira nyingi , katika akili yake alijua kabisa Roma alikuwa akienda kuonana na wanawake wake.

“Mimi sio muhimu  kwake , wanawake  wake  ndio muhimu ..Damn you Roma .. nimejipanga vyote hivyo leo  kwa ajili yako halafu unaniona  sina thamani… shenz kabisa , nakuambia hivi Roma utanisikia kwenye bomba ,Kwanza  nini kilinipata mpaka nikawa  na mawazo ya kijinga ya kumpa mwili wangu …Aaah Edna wewe mjinga kweli, Roma sio wa kumpa  mwili wako  ni Malaya  yule mwanaume”Ungemuona  Edna anavyoongea na mto usingemdhania ni yule CEO mwenye heshima zake , alikuwa akiongea mweyewe huku akiangalia mto uliokuwa kitandani kwake.

“Ila mimi mjinga sana hadi aibu ..Aaa nisingemwambia abaki nimejidharirisha leo  …Edna usie ukarudia tena”Aliendelea kuongea mwenywe na kisha akachukua shuka na kujifunika gubigubi.

Upande wa Roma alifika  Uwanja wa ndege kama kawaida  muda ulikuwa ni saa tatu  hivi kama na nusu , baada ya kusimama nje ya jingo la Terminal 3 akisubiria wageni wake , alikuja mwanaume mmoja wa kizungu  alievalia suti bila tai huku  akiacha vifungo viwili vya shati lake kuwa wazi na kumfanya nywele za kifuani kuonekana, aligonga gari la Roma   mara mbili kwenye kioo cha mbele.

“You are Mister  Roma ??”Aliuliza  yule mzungu na Roma alitingisha kichwa   kukubali kuwa ni yeye , yule mzungu  alitoa  ufunguo mfukoni na kumpatia na Roma alitabasamu na kisha  akauchukua ule ufunguo huku bwana yule wa kizungu akiondoka mbele ya gari la Roma , alionekana kazi ambayo ilikuwa imemleta mahali hapo alikuwa ashaimaliza.

Baada ya dakika kama mbili hivi kupita ,Roma alitoka kwenye gari yake  akiwa ameshikilia ile funguo ya  gari na kisha alianza kubonyeza bonyeza kitufe cha  rimoti iliokuwa imeambatana   na ufunguo na gari lilitweak na kuwahsa taa  za mbele na Roma alitabasamu na kuisogelea.

Ilikuwa ni gari  kubwa kutoka kampuni ya Toyota , iliokuwa na uwezo wa kubeba Zaidi ya watu kumi na tano na ilikuwa imeletwa hapo na Ubalozi  kwa ajili ya  kuwasafirisha wageni kutoka  uwanja wa ndege kwenda kwenye makazi yao.

Roma baada ya kuikagua na kuridhika , alitoka nje  na ndani ya dakika chache tu , alishuhudia ndege kubwa  kampuni ya KLM  ikiiambaambaa kwa kushuka ndani ya uwanja huu wa Dar  es salaam, aliendelea kusubiri kwa takribani  dakika kumi na tano na hatimae   alianza kuona wageni wake wakitoka  nje kabisa ya mlango wa ‘Arrivals’.

Wa kwanza kabisa alikuwa ni mwanamke mzungu  aina ya Cauccasian aliekuwa amevalia surali ya jeans rangi ya bluu n araba nyeupe  huku akiwa amefunga kiunoni shati moja ya draft  akiwa amevalia miwani , alionekana mrembo.

Wasichana wengine watatu walitoka huku nyuma yao  wakifuatiwa na wanaume sita wote walionekana kuwa katika lika moja la ujana kati ya miaka  25 kwenda 30 , Roma aliwaona wazungu hao na kutabasamu , kwa namna ambavyo walikuwa wamebaba mabegi yao walionekana kama watalii , karibia wote  walikuwa wakitafuna  bublish.

“Your Majest Pluto”Aliongea yule mwanamke kwa mshangao , huku akionesha heshima ya hali ya juu kwa Roma  lakini Roma alimpa ishara na mzungu yule alielewa na wenzake walielewa na kutulia .

“Welcome in Tanzania guys”

“Thank you” waliitikia wote kwa pamoja na Roma alitabasamu na kumrushia kijana mmoja funguo ambaye alikuwa mwembaba.

“You will drive  along with me”Aliongea Roma na kuwaonyesha gari iliokuwa upande wao wa kushoto na wote wakatabasamu na kuisogelea  na wote wakaingia  ndani , lakini wakati  Roma ashaanza kulisogeza gari lake kuingia barabara kuu , mara zilikuja gari tatu   diffenda  na kusimama barabarani na   palepale walionekana wanajeshi wakiruka kwa ustadi mkubwa kwenye gari wakiwa na siraha na kisha kulizunguka gari  lile walilopanda wazungu  , walionekana walikuwa wamejipanga kweli.

Roma alishuhudia kitendo kile  akiwa ndani ya gari yake na kujikuta misuli ya uso ikisimama , kwa namna wanajeshi hao walivyokuwa wanaonekana mahali hapo ilionesha kabisa walikuwa na  taarifa za kutosha na ndio maana walionekana kujipanga.

Baada ya kuona  gari lile limezingirwa  Roma alishuka kwenye gari yake na kusogea upande wa wale wanajeshi walipo , lakini kabla hajawafikia  gari iliokuwa mbele yake  mita kadhaa , gari ambayo ilikuwepo hapo muda mrefu kidogo  kwani aliiona , ilifunguliwa na akatoka mzee mmoja hivi mwenye mwili mkubwa wenye afya  alievalia miwani pamoja na suti  ,Roma hakumjua mzee huyu.

Yule mzee alimsogelea Roma  huku  wanajeshi watatu wakimzingira upande wa kulia na kushoto na nyuma wakionesha kumlinda ,Roma aliendelea kujiuliza mtu huyu ni nani na kwanini amewazingira wageni wake , kwani swala la wageni wake kuja ndani ya taifa la Tanzania lilikuwa ni siri sana na waliokuwa wakijua ni watu wachache sana ndani ya ubalozi wa Sweden.

“Tunaomba mshuke kwenye gari”Aliongea kwa kingereza moja ya wanajeshi ambae alikuwa na  nyota tatu begani na wale wazungu waliangaliana na jamaa mmoja mwenye mwili mkubwa  aliwapa ishara  wenzake washuke na wakashuka huku wakiwa wamenyoosha mikono  juu kuonesha kwamba hawapo kishari.

“Tupo hapa baada ya kupata taarifa   ya nyie kuwa wanajeshi  mnaokusudia kuingia  ndani ya nchi yetu bila ruhusa”Aliongea yule Mwanajeshi  alieonekana  kuwa kiongozi na wakati huu Roma alikuwa ashafika upande aliosimama mzee ambaye alikuwa amevalia suti  na yule mzee alimwangalia Roma na kisha wakasogeleana.

“Habari yako mzee , unaonakana wewe ndio kiongozi mkuu hapa , nini kinaendelea mbona wageni wangu wanazuiwa”.

“Nadhani mpaka sasa ushajua kwanini wanazuiwa Mr Roma Ramoni , Sisi ndio walinzi wa mipaka ya taifa hili na tunajua kinachoendelea nje na ndani ya mipaka yetu  na hatupo tayari kuona  wanajeshi wanaingia ndani ya taifa hili bila kuwa na kibali maalumu”

“Una Ushahidi gani kama  wakujitosheleza kama hawa ni wanajeshi?”Mzee huyu alitabasamu.

“Hawa ni wanajeshi kutoka  kundi la The Eagles na taarifa za ujio wao tulizipata kutoka kwa watu wetu ndani ya ubalozi”.Aliongea mzee huyu na Roma alimwangalia na kuwageukia wanajeshi wake waliokuwa katika hali ya  wasiwasi.

“Mr Roma  tunajua wanajeshi hawa wanauwezo mkubwa wa kimapigano  , lakini leo lazima sheria za nchi  zifuatwe hatuwezi  kuwaachia wakaingia uraiani pasipo kujua ni sababu zipi zimewafanya kuingia hapa nchini , hivyo tutaenda nao pamoja na wewe kambini  kwa ajili ya mahojiano”

“Hapana,naondoka na wageni wangu”Aliongea Roma na kumfanya mzee huyu amshangae  na kisha akatabasamu

“Hauna uamuzi katika hili”: aliongea na kisha aliwapa ishara  wanajeshi wafanye kazi , lakini  ile wanataka kuwasogelea wale  wanajeshi wa kizungu walishusha mikono chini  na wanajeshi wa kitanzania walikuwa fasta sana kwani walikuwa ashakoki siraha zao tayari kwa mashambulizi.

 

Wanajesh wale wa kuzngu walimwangalia Roma  huku wakionesha wanataka  Ruhusa kutoka kwake , ila Roma aliwaangalia na kisha akamgeukia huyu mzee   huku akiwaza  jambo la kufanya , lakini kabla  hajaongea  ziliingia ndani ya eneo hili gari nyingine  mbili moja Range Vx na moja difenda na baada ya  gari hizi kusimama alishuka mzee mwingine  alievalia  gwanda  huku mabega yake yakiwa yamechafuka kwa vyeo vingi, wale wanajeshi baada ya kuona  mtu huyo ametoka kweye gari na  na kumtambua walijikuta wakitoa heshima na kushangaa kwa wakati mmoja kwanini mkuu wao yupo hapo.

Upande wa  huyu mzee aliekuwa akiongea na Roma pia alishangazwa  na ujio  wa mkuu wake , ghafla tu alikakamaa mwili.

“Jambo Afande”  lakini Mzee huyu hakuongea chochote Zaidi ya kuinua mkono ya kumwambia alegeze  na  kumsogelea Roma.

“Mr Roma unaweza kuondoka na wageni wako , mengine tuongee siku ya kesho baada ya kuwasiliana ”Aliongea  huyu mzee mwenye manyota mengi na Roma alitingisha kichwa pasipo kusema  lolote na kisha akawapa ishara wanajeshi wa kizungu na wote wakaingia kwenye gari na kuondoka eneo hili Roma akiwa ametangulia.

Previoua Next