Ni ndanni ya dakika chache tu Roma alikuwa ashafika Mbutu akiwa na wageni wake , aliingiza gari na kuegesha na kisha akawakaribisha ndani , Wageni hawa walipendezwa sana na nyumba , hio licha kwamba ilikuwa usiku , lakini ilionekana kuwa nyumba nzuri kwao yenye mazingira ya kuvutia.
“Guys here is now your home , all your missions will be operated here , feel free and welcome again in Tanzania”.
“Thank you! ,Your Majest Pluto , it`s has been our dream working with you personally and we ready for any instructions”
Aliongea kijana mmoja kibongea ambaye ndio alionekana kuwa kiongozi katika hili kundi la wazungu na Roma alitabasamu.
Kwanza kabisa aliwanza kuwakagua mmoja mmoja kwa dakika kama nne hivi , akiwazunguka nyuma na mbele na kisha akatabasamu baada ya kuona ya kuridhishwa nao , lakini bado vijana hawa wa kizungu walionesha hali ya wasiwasi , walionekana kukosa kujiamini.
“Okey nimeridhishwa na uwezo wenu, tuingie ndani kwanza”Aliongea Roma kwa kingereza Safi na wakatabasamu na kisha wakamfautisha kwa nyuma na wote wakaingia ndani na kuweka mizigo yao chini kwenye sebule hii kubwa ambayo ilikuwa na furniture za bei kubwa , mabwana hawa waliangaliana na kisha wakatabasamu.
“Kwanza kabisa nataka niwatambue majina yenu mmoja mmoja na kila mmoja kwa uwezo wake cheo ndani ya The Eagles”
Aliongea na wakaanza kuangaliana ni kama kila mmoa alitaka mwenzake aanze huku wakiwa wamesimama na Roma akiwa amekaa huku amekunja nne , alikuwa ni kama bosi hapa ndani kwa muonekano wake na waliokuwa mbele yake walikuwa vijakazi wake.
“My name is Bram Garcia, I am an expert in computer , with various records in hacking issues, in 2016 I managed to hack the communication system of the international space station, also.....”( jina langu Bram Garcia ni mtaalamu katika maswala ya Computer , nikiwa na rekodi mbalimbali katika maswala ya Hacking , mwaka 2016 nilifanikiwa kuhack mfumo wa mawasiliano wa international space station, na pia ..) Roma alimwambia asiendelee kwani asharidhika na kuashiria mwingine aendelee
Baada ya dakika chache Roma aliridhika na utambulisho wa kila mmoja na kusimama na kuwaangalia mmoja mmoja.
“Okey Liutenant Diego utakuwa kiongozi wa kundi hili na utapokea maelekezo yote kutoka kwangu .. kuna mwenye pingamizi?” Wote walipiga Salute.
“Chiara na John mtakuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa mke wangu popote pale anapoenda na iwe kwa siri sana , akiwagundua mnalinda kazi hamna” Walipiga wote saluti.
“Wote nane mliobaki kwanzia leo hii kazi yenu ni kuhakikisha mnajua kila kinachoendelea kwa watu ninaoneda kuwatajia… “alisimama kuongea na akawaangalia wote na wanajeshi hawa walianza kujishuku .Na Diego alijua kwanini Pluto anawaangalia na alimpa ishara Chiara mwanadada ambaye alikuwa ndio aliekuwa amefunga shati kiunoni na Chiara alielewa ishara hio na haraka haraka akatoa notebook na kalamu.
“Nataka muanze kumfatilia mtu anaejiita kwa jina la The Don kwanzia nani anaongea nae , ratiba zake za kila siku na mtandao wake wote wa kibiashara ndani na nje ya nchi , wa pili nataka taarifa za mheshimiwa Senga watu wote ambao anawasiliana nao kwa siri na kila kitu kinachoendelea Ikulu ambacho kina muunganiko na mimi, naomba taarifa hio ipewe kipaumbele na kuchambuliwa vyema , nikija kwenu nitahitaji ripoti tu , kazi ya tatu ambayo nadhani wote mnamfahamu Seventeen nafasi yake ndani ya kikosi na sehemu yake katikamaisha yangu? , nataka mchimbe na mnipatie muunganiko wote uliopo kati ya mke wangu na Seventeen”Walishangaa na Roma akatabasamu.
“Haina haja ya kushangaa maafande , mkishamuona mke wangu mtajua kwnini nawapa hio kazi ,na yangu kwa leo ni hayo tu nasisitiza ulinzi kwa mke wangu lazima upewe kipaumbele naelewa The Eagles tuna teknolojia kubwa , hivyo teknolojia hio nataka itumike katika kumpa ulinzi Edna tumeelewana”
Wote waliitikia kwa kupiga saluti na Roma alinyanyuka na akamwangalia Diego.
“Utawasiliana na Sauron kwa mahitaji yote mtakayohitaji mkiwa hapa nchini , lakini pia mishahara yenu itaongezeka kwa asilimia ishirini kutokana na kazi hii , niwatakie usiku mwema na maukumu mema”Wote walitabasamu kwa shangwe .
Baada ya kusema hayo Roma alitoka na kuwaacha na kugeuza kwenda nyumbani kwake , na muda ulikuwa umeenda kweli , lakini kutoka Mbutu na Sunlight Villa palikuwa ni umbali mdogo sana.
Kama kawaida alikuta walinzi wako macho na kikama walikuwa wanamsubiria kwani ile anafika tu alifunguliwa geti na kuingia ,taa za ndani zilikuwa zimezimwa kuonesha Bi Wema na ,mke wake walikuwa washalala kitambo , na hakujali sana , alijirusha kitandani baada ya kupunguza nguo na kuangalia gypsum.
“Kazi yangu ilionirudisha hapa nchini imeanza na nitaujua ukweli wote kwanini Seventeen na Edna wanafanana na kwanini mimi na Seventeen tukawa peke yetu kwenye kile kisiwa”Alijiongelesha Roma na kisha akalala.
****
Ratiba za asubuhi zilikuwa kama kawaida kwa Roma , alianza kwenda kufanya mazoezi ya kuuweka mwili sawa na baada ya hapo alirudi chumbani kwake baada ya kusalimianan a na Bi Wema ambaye alikuwa bize na usafi pamoja na kuandaa kifungua kinywa.
Baada ya kujiweka sawa kwa ajili ya kuelekea kazini alishuka na ufunguo wake chini kwa ajili ya kifungua kinywa , leo alikuwa amechelewa kidogo kufika mezani kwani Edna alionekana kwenye meza akiwa amenuna , na hakutaka kabisa hata kumwangalia usoni Roma na hata pale Roma alipomsalimia aliishia kutingisa kichwa tu kama salamu na Roma hakujali sana , alikua akijua kwanini Edna amenuna na hakuwa na namna ya kujitetea mbele yake , alichokifanya ni kunywa chai ilioandaliwa.
Wa kwanza kumaliza alikuwa ni Edna alimuanga Bi Wema na mama huyo kumtakia siku njema na kisha kuondoka na ni mgurumo wa gari pekee uliokuwa ukisikika ukifubaa kwenye masikio ya Roma na Bi wema.
Bi wema alimwangalia Roma aliekuwa akimalizia mayai yakukaanga yaliokuwa kwenye sahani , mwanamama huyu alitamani kumuuliza Roma jana kulikuwa na umuhimu gani wa kutoka , kwanini asingebaki nyumbani kama Edna alivyo omba kama Edna , lakini ile anataka kuinua mdomo…
“Bi Wema Asante kwa chai na usiwaze sana kuhusu Edna..”Aliongea Roma na kumfanya mwnamama huyu amuangalie na kujiuliza amejuaje kama alikuwa akiwaza kuhusu Edna , ila Roma hakujali mshangao wa Bi Wema Zaidi ya kufungua mlango… lakini alikumbuka jambo na kusimama.
“Bi Wema kama kuna mtu yoyote akifika hapa wa kizungu naomba umpe nafasi ya kufanya kazi yake , ni maswala ya kiulinzi hivyo haina haja ya kumwambia Edna”.
“Sawa mr Roma kazi njema”Roma alitabasamu na kisha akaondoka na kuchukua gari yake aliodhurumu kule PANZ security Aud Q7 rangi ya Silver , ilikuwa gari nzuri kweli ambayo Roma alikuwa akiendesha , kwa muonekano wa Roma wa sasa usingemdhania kama alikuwa akibeba mizigo siku kadhaa nyuma ndani ya soko la Mbagala , licha ya sasa kuonekana kawaida kimtindo lakinni alikuwa na utofauti mkubwa , uso ulikuwa unang`aa.
Baada ya kufika getini alisimamisha gari na kushusha kioo na kumwangalia Derick aliekuwa ameshikilia gati , licha ya kwamba geti hili lilikuwa likitumia umeme lakini bwana huyu alikuwa akilifungua kwa kulisukuma ili kuonyesha juhudi yake kazini kwa mabosi wake.
Baada ya Derikc kumuona boss wake kasimamamisha gari alimsogelea kwa heshima, huku akipanga ayajenge na Roma kwani tokea siku ambayo alimwita kichaa msafi hawakuwahi kuongea nae tena, kwani muda wote Roma akitoka alikuwa ndani ya gari na hakuwa na ruhusa ya kuingia ndani ya Jumba hilo kwa ajili ya kuongea nae , lakini leo hii bosi wake amesimamisha gari , aliona hio ndio nafasi nzuri.
“Hivi unaitwa nani vile” Aliuliza Roma na ni kweli alikuwa amemsahau jina kwani siku ile alimsikia Edna akimuita ila hakulishika vizuri.
“Naitwa Derick Bosi”.
“Sawa Derick , hebu acha kukakamaa mwili kwa namna hio unaweza ukajamba , kuwa kawaida tu , haina haja ya kuniogopa”
“Sawa bosi” aliongea Derick huku akijiweka sawa kwa kufunga suti yake vizuri .
“Okey kuna watu watakuja hapa wazungu , wakiomba kufanya mambo yao hapa waruhusu nni maswala ya kiulinzi sawa”
“Sawa bosi”
Roma alifika kazini akiwa ni wa mwisho kuliko wafanyakazi wote , lakini leo kulikuwa na mabadiliko kidogo , wafanyakazi walionekana kumuangalia sana kiasi cha kuiuliza kuna nini kwanini wenzake wanamwangalia.
“Recho mambo?”
“Poa Vipi Roma”
“Gudi , kuna nini mbona mnaniangalia sana , au nimezidi kuwa handsome”
“Hongera , tumesikia unaenda Japan kesho kikazi , tumeshangazwa na taarifa hio na kila mmoja anashangaa kwanin umechaguliwa , maana tokea ufike haukuwahi kufanya kazi zaidi ya kucheza gemu , na isitoshe hauna uzoefu wa kutosha na Kampuni , lakini wote hapa ndani hatujawahi kupewa hata kazi ya kwenda nje ya mkoa lakini wewe huna hata mwezi umepata nafasi hio , lazima tukuangalie kwa mshangao”
“Sasa mnachoshangaa nini hapo , ushasahu mimi ndio mwanaume peke yangu ndani ya hii idara, hehe ukute CEO mwenyewe kapagawa na uwepo wangu anataka kuniweka karibu , kwahio msiwaze sana pigeni kazi”Recho alibetua midomp na Roma akageukia tarakishi yake , alitoa headohone kwenye droo ya meza na Pad za kuchezea gemu ,haikueleweka ni lini alizinunua, alichomeka na kuanza kucheza gemu la Mpira PES 2021 , huku wafanya kazi wenzake wakizidi kushangaa, maana mtu kazi yake ni kucheza gemu , lakini kapewa kazi ya kwenda Japani kumwakilisha bosi wa kampuni , jambo hilo kwao liliwashangaza na kuona kuna walakini na uongozi wa kamouni.
Licha ya kujua Roma ni mhitimu wa chuo kikuu cha Harvard lakini bado hawakukubali , kwani ndani ya kampuni hio kulikuwa na wasomi wakubwa tu akiwemo Nasra ambaye alisomea masomo yake yote Cambridge Marekani.
Wakati Roma anaendelea kucheza gemu alikuja Miss Airport na kwenda kusimama kwenye meza yake na kumwangalia Roma kwa sekunde namna ananyofurahia gemu , huku baadhi ya wafanya kazi wakishangazwa na uwepo wa Monica hapo ndani , kwani ni mara chache sana kwa Monica kuja kwenye ofisi yao.
Miss Aiport alionekana kutompenda kweli Roma , na alikasirika Zaidi baada ya kuona Roma anacheza gemu wakati wenzake wote wako bize kufanya kazi , alitamani awe na cheo kisha amfukuze. Alimsogelea Roma na kisha akamvua Headphone na kumfanya Roma ageuke.
“Miss Airport!”Alishangaa roma mara baada ya kugundua mtu aliekuwa amesimama nyuma yake ni Monicca.
“Unaitwa na CEO”aliongea Monica na kisha akageuza na kuondoka kwa maringo , huku viatu vyake vikitoa sauti ya ‘kwaa.. kwaaa.. huku sehemu katikati ya mapaja yake ikionekana kutokana na pasua ya sketi nyeusi aliovalia , alionekana kujisikia kweli kwa mnafasi yake alionayo kwenye kampuni.
Comments