Reader Settings

Roma alisubirisha gemu lake na kisha akainuka kwenye meza na kujivuta na kuianza safari , huku nyuma akiwaacha Recho ,Tina  na warembo wengine wakimwangalia kwa nyuma mpaka pale kisogo chake kilipotokomea nje , walitingisha vichwa vyao na kuendelea na majukumu yao.

Roma  baada ya kutoka kwenye lift  alitembea  kuelekea ofisi ya CEO  lakini njiani alikutana na watu wawili , wa kwanza alikuwa ni Dorisi ambaye alikuwa ametangulia kwa  mbele mita kadhaa akimuacha Nadia nyuma ,Doris baada ya kukumfikia Roma alimkonyesha na kumpa busu la hewani na kisha akampita , lakini kitendo hiko kilishuhudiwa na Nadia aliekuwa nyuma na hakufurahishwa na jambo lile , alimwangalia  Roma kwa hasira na kisha akampita na Roma aligeuka na kumwangalia  Nadia na kutabasamu na kuendelea mbele  , mpaka kuingia kwenye ofisi ya mke wake.

“Bebi Nishafika”Aliongea  Roma mara baada ya kuingia na kumshuhudia  mke wake kama kawaida akiwa bize na tarakishi yake , licha ya kwamba Edna alionekana kauzu lakini muonekano wa yeye kuwa bize na kazi ulikuwa ni wa kipekee kabisa  na Roma alitaman kuwa na picha ya mke wake akiwa anafanya kazi ilia awe anaikodolea macho.

Edna hakujibu mara moja aliendelea na kazi na Roma alikaa kwenye sofa akimsubiria  mke wake amwangalie , baaada ya  kuwa bize kwa dakika mbili Edna aliinua macho yake  na kumwangalia Roma ambae  amepandisha miguu kwenye sofa  akiegemea  sehemu ya kuwekea mkono na miguu kuning`inia upande mwingine, Roma hakuwa na tofauti na mtoto kwa mambo ambayo alikuwa akifanya ,  Edna alitingisha kichwa kwa kusikitika na kisha aliangalia pembeni kwenye kitrei flani  hivi cha chuma kinachong`aa na kutoa karatasi.Alinyanyuka kwenye kiti chake na kisha  akamsogogelea Roma.

“Angalia hizo karatasi  , naomba uzisome zote  na uelewe , ni sehemu ya vipendelea vya mkataba ambao mtakwenda kusaini  huko Japani”.Aliongea Edna huku akiwa Siriasi na Roma aliinua uso wake na kumwangalia Edna.

“Mke wangu , unaonaje kwanza ukinitengenezea kahawa uniletee niwe na kunywa  taratibu wakati nikiendelea kusoma hizo karatasi”

“Huo muda sina , katengeneze mwenywe na karatasi  hizi utazisoma  mpaka uzimalize ndio uondoke”.

“Bila kahawa  nakwambia hivi , sizisomi na nalala hapa  mpaka muda wa chakula cha mchana na sitaki kahawa iliotengenezwa na  Monica nataka  uliotengeneza  na wewe mke wangu” Aliongea  Roma na kisha akarudia staili yake  ile ile na kufumba macho , Edna alijikuta akichemka kwa hasira , alimwangalia Roma namna ambavyo amelala , huku akishindwa kuelewa ni kitu gani akifanye. , aliinua karatasi alizoshikilia mkononi na kuziangalia  kwa  sekunde na kisha  akakunja ngumi kwa hasira  na kuziweka kwenye meza na  kutembea kihasira hasira na kutoka nje  ya ofisi yake.

“Boss unahitaji nini?” Aliongea Monica akiwa amekakamaa  kwa heshima.

“Unaweza kuendelea na kazi Monicca natengeneza kahawa”Aliongea  Edna na  kupita kushoto huku akimuacha Monnica ambaye alikuwa kwenye mshangao ,   maana kwa mara ya kwanza tokea aanze kazi yeye ndio aliekuwa akimtengenezea Edna kahawa , inakuwaje leo , alitingisha kichwa na kisha alikaa chini na kuendelea na  kazi.

Roma na yeye baada ya kusikia mlango ukifunguliwa  na Edna kutoka nje , aligeuka na kuangalia  na kujikuta akitabasamu na kujisemea moyoni kwamba amemuweza leo.

“Nimemuweza na asipoleta kahawa hapa nzuri sizisomi karatasi zake” Alijiwazia na kisha aliendelea kukaa  vile vile akisikilizia kaubaridi  kakiyoyozi pamoja na harufu nzuri  ya ofisi hii ya mke wake.

Dakika  tano mbele Edna alirudi akiwa ameshikilia kikombe na kwenda kusimama mbele ya sofa  akiwa anamwangalia Roma kwa hasira  na Roma aliinua uso wake   na kumwangalia Edna na kisha alitabasau na kupokea kikombe.

“Asante  mke wangu kipenzi”aliongea Roma huku akitabsamu na kunywa kidogo  na kisha  akafumba macho  akifurahia burudanni ya utamu wa kahawa.

‘kumbe ni mtaalamu kwenye utengenezaji wa kahawa nitakuwanakuja uwe unanitengenezea mumeo mara kwa mara”Edna hakujibu kitu  alilirudi kwenye meza yake kuendelea na kazi  na Roma alichukua karatasi na kuanza kuzisoma.

Baada ya dakika kumi kupita Edna aliinua shingo yake  na kumwangalia Roma na kumuona yupo bize akisoma karatasi hizo kwa umakini mkubwa na  alijikuta  moyo wake  ukipata joto na  alishindwa kujizuia na kutabasamu.

“Anaonekana mwanaume aliekamilika akiwa siriasi”Aliwaza Edna na kuendelea na kazi.

Baada kama ya dakika arobaini na tano hivi za mara ya kwanza kwa Roma kuwa siriasi tokea aanze kuingia kwenye hii kampuni , simu yake ilipata uhai  , na simu hii ilikuwa na kelele maana ilikuwa ni simu ya Tecno batani  kitochi   aliotoka nayo Mbagala, na kama unavyojua simu hizi kwa makele .

Roma alitoa simu yake mfukoni na kuangalia nani anapiga na  namba ilikuwa mpya , alimwangalia mke wake ambaye alijua anajifanya kuwa siriasi na kisha akapokea.

“Mr Roma Ramoni , unaongea na Meja Generali Maeda Mkwizu  , tulionana jana  Uwanja wa ndege  , nimepiga  tuonane  ofisini kwangu saa sita kamili Lugalo”Ilisikika sauti nzito upande wa pilili.

“Sawa Mr Maeda nitakuwa hapo ndani ya muda”

Baada ya kukata simu  , Roma aliangalia muda na kuona ni saa  tano na dakika iishirini na saba ,aliangalia karatasi  zilizokuwa kwenye meza na kisha akainua macho yake  na kumwangalia Edna.

“My Wife utakuja nazo nyumbani hizi karatasi nizimalizie , kuna sehemu naenda”Aliongea Roma na kisha alinyanyuka na kupiga hatua kuelekea nje.

“Romaa.. !, kwanini usizimalizie kabisa”.

“See you at home babe , uje nazo”Aliongea Roma Nakisha akafungua mlango  na kutoka , akimuacha Edna alikuwa amekodolea macho mlango.

****

Roma aliendesha Gari yake  huku akiwa anasikiliza mziki  mdogo mdogo , alitaka atumie muda   mwingi mpaka  kufika Lugalo , alichukua barabara ya Morogoro na kuendesha mpaka  Ubungo na kuchukua barabara ya Mawasiliano ,Sam Nujoma  na akaja kutokezea Mwenge na kuingia kwenye barabara ya  Bagamoyo , aliendesha kwa utaratibu  huku akiendelea kula mziki  na pia alifurahishwa na madhani ya jiji.

Dakika chache mbele alikunja kushoto na  kusimamaisha gari yake   na kisha aliangalia saa na kuona alikuwa na dakika kumi kabla ya muda , alitulia kwa dakika kadhaa na  zikiwa zimebaki dakika  mbili aliingiza gari yake ndani  ya eneo la Brigade  baada  ya kujitambulisha getini.

Ndani ya ofisi ya uongozi wa juu wa jeshi  alionekana Meja General  Maeda akiwa kwenye mavazi yake ya Gwanda iliokuwa imechafuka na manyota manyota na mwenge na alama  ya x iliokuwa na visu, huku mbele yake akiwa  Kanal Augustin Tobwe  akiwa ameketi kwa heshima ndani ya ofisi hii

Ilikuwa ni ofisi kubwa iliokuwa na kiyoyozi   na harufu nzuri na kufanya eneo hili kuzidi kupendeza , ukiongezea na fanicha za hapa ndani pamoja na kapeti la unyoya lililotandazwa chini , palikuwa  panavutia na kuonyesha hadhi  ya ofisi ya  cheo cha mkuu  huyu wa jeshi.

Baada ya dakika chache tu aliingia  mwanajeshi cheo cha luteni  kwa nyota zake mbili na  kutoa saluti  kwa wakuu wake .

“Mr Roma amefika”

“Okey! Mruhusu aingie”.

Roma aliingia ndani hapa  kama kawaida yake  ,sura kutokuwa na wasiwasi na kujiamini ndio ilikuwa imemvaa , alikuwa ni Roma yule yule ambaye hakuw akibadilisha na mazingira,  watu walokuwa ndani ya hii ofisi wote  alikuwa akiwajua , wa kwanza aliekuwa amekaa upande wa kulia  , alikuwa ni  mzee aliekutana  nae jana na kumpiga biti la kutaka kuondoka nae kwenda kambini pamoja na wageni  kwa mahojiano na aliekuwa kwenye meza alikuwa ni Meja jenerali  mwenyewe Maeda Mkwizu.

“Karibu Mr Roma , naitwa kanali Augustin Tobwe”Aliongea mzee wa jana aliempiga biti na Roma alitabasamu na kupokea mkono wake.

“Unaitwa Tobo au Tobwe”Mzee yule aling`ata meno kwa hasira  na kisha akatabasamu .

“Naitwa Augustin Tobwe  sio Tobo tafadhari”

“Sawa Afande Tobo nishalinakiri jina lako hivyo ili iwe rahisi kukumbuka”Aliongea Roma na kumfanya  Afande Maeda atabasamu na kuona  Roma alikuwa akilipiza kisasi cha jana na hakutaka kutia neno na mzee alietwa Tobo  alikuwa ni mwenye bisara hakutaka kuonesha hasira zake waziwazi.

“Karibu sana mr Roma  , nadhani sina haja ya kujitambulisha  kwani nishafanya hivyo kwenye simu”Roma alitingisha kichwa na wote wakaketi kwenye masofa yaliopo hapo ndani.

“Mr Roma nadhani niende moja kwa moja  kwenye jambo  ambalo limefanya tuonane ,   na kabla ya kuendelea naomba tusahau ya jana”.

“Meja nishasahau   yote mimi  na Afande Tobo hatuna shida kabisa  , yaliotokea na ni sehemu ya majukumu yake ya kikazi”

Aliongea Roma huku akitabasamu , lakini bado alikuwa akishangazwa na namna Meja alivyokuwa akiongea  hakuwa akifanannia na cheo chake ,  kwani aliongea kama mwanasiasa.

“Mheshimiwa Afande twende sasa moja kwa moja kwenye maongezi , tusiwe kama wanasiasa , nimeondoka bila ruhusa ya mke wangu nataka nirudi nikampet peti” Aliongea Roma na Meja jenerali alitabasamu  na kisha aligundua alikuwa anaongea na mtu wa aina gani , kwani alionekana kujiamini mno.

Baada ya Roma kuongea hivyo Afande Maeda alimpa ishara  Kanali na  akaibua fomu iliokuwa pembeni yake  na kisha akatoa karatasi na kumkabidhi Roma ambaye alizichukua na kuanza kuzipitia.

“Hio ni katatasi  ya kikosi chetu maalumu  kinachoendelea na mafumbo ndani ya kambi ya Mirambo”

“ Mr Meja ndio ni kikosi , lakini sijaelewa kwanini umenipa majina yao?”alitabasamu.

“Mr Roma  miezi miwili iliopita tuliomba msaada wa wakufunzi kutoka jeshi la Urusi kwa ajili ya kuwafundisha  wanajeshi wetu  mbinu maalumu za kivita  kupitia ofisi ya CDF  lakini   ombi letu lilikataliwa  kwa pendekezo”

“Unamaanisha nini kwa Pendekezo”

“Uongozi wa Jeshi la urusi walipendekeza  tukuombe wewe usaidie katika kufundisha  wanajeshi wetu  baada ya kutupitishia taarifa  ya ujuzi wako wa kimapigano , lakini pia uongozi wako wa juu ndani ya Kikosi cha The Eagles na nadhani dunia nzima inajua umahili wa kikosi cha The Eagles , hivyo hata sisi tulishangaa baada ya kusikia kuwa wewe ni sehemu ya  wanajeshi kikosi hiko”Alitulia  na kisha akamwangalia Roma , ila Roma hakuonesha mshangao , wala hakuonyesha  mabadiliko yoyote.

“Lakini swala hili hatukuombi ulifanye bure , sisi kama jeshi tumekaa tukaridhia wanajeshi wako kuendelea kukaa hapa nchini  lakini wewe utatusaidia  kuwafundisha vijana wetu mbinu mpya ambazo sisi jeshi la Tanzania hatuna , ikiwemo   baadhi ya siri mnazotumia ndani ya  jeshi la The Eagles”Aliongea Afande Maeda na kumwangalia Roma.

“Kwa hio Afande milikuwa mnasubiri mpate  Collateral ili uandae haya mazungumzo na mimi?”

“Ndio hivyo Mr Ramon licha sisi ya kuwa wanajeshi ila tunaelewa kanununi za kuwa katika nafasi nzuri katika mazungumzo”

Roma alifkiria kwa dakika kadhaa na kuona jambo hilo sio baya , kama ni kuwafundisha tu anaweza kawapa kazi hio wanajeshi wake , na asiende yeye   lakini pia alikuwa akihitaji sana wanajeshi wake kuwa ndani ya taifa la Tanzania kwa kazi yake  iliomleta.

“Sawa meja , lakini kabla ya kukubaliana na ombi lenu  nina masharti makuu mawili , kwanza kabisa nataka nijue , ilikuwaje mpaka afande Tobo hapa  kupata taarifa zangu na kuintercept wanajeshi wangu , kwani kwa maelezo yako  na kwa tukio lile inaonekana kabisa hakukuwa na muunganiko wa taarifa kati yenu”

“Ni kweli Mr Roma , kilichotokea  ni Misunderstanding kati yetu , Project ya kikosi kinachoendelea na mafunzo huko Mirambo  haikuwa imemfikia  kanali hapa na niseme tu kuwa kanali ni moja ya wanajeshi wenye weledi  mkubwa ndani ya jeshi letu na ndio maana licha ya kukosa  taarifa kamili kutoka kwetu aliweza kunusa harufu ya wanajeshi  wanaozamia ndani ya Tanzania”.Roma alikubali maelezo

“Sharti langu la pili  ni hili  Afande Meja jenerali , nataka unihakikishie  jambo lolote kutonikuta  nikiwa hapa Tanzania , ikiwa nitafanya maauzi ya kuua mtu , hapa naomba usinielewe vibaya ila ni kwamba kuna watu ni wachokozi sana ndani ya taifa hili na  mimi sipendi mtu anaenichokoza , hivyo afande ikitokea nimeua you have to  clean  up the mess for me”Aliongea Roma na Mzee huyu alitoa macho , kwani aliona sharti hilo kuwa kubwa na Roma aliona kusitasita kwa  Meja.

“Meja ombi langu ni hilo  , kama haliwezekani  sinabudi pia kukataa ombi lako na kuhusu wanajeshi wangu nitatafuta namna ya kuwabakisha Tanzania  maana hilo lipo ndani ya uwezo wangu”Aliongea Roma na  Afande Maeda alifikiria ombi hilo kwa dakika kadhaa.

“Okey Deal  Mr Ramoni , utafundisha jeshi letu mafunzo ya hali ya juu na mbinu zote zinazomilikuwa na jeshi la The Eagles  na mimi nitahakikisha na ‘Clean up the Mess’ lakini licha ya hivyo Mr Roma nataka kukuambia kuwa hii nchi inaendeshwa kwa sheria , hivyo  hatutakuwa tayari kuona unavunja sharia kwa namna ambavyo unapenda”Roma alitabasamu na kisha alipeana mkono na Meja Generali Maeda.

“Kanali hapa atakuwa na wewe bega kwa bega katika zoezi hilo , na tunatarajia  mafunzo hayo yaanze mwenzi ujao  yaani baada ya wiki tatu kuisha kutoka leo”

“Hakuna shida Meja”Aliongea  Roma na kisha  wakaagana  huku akisindikizwa mpaka nje eneo la kuegesha Magali  ,   jambo ambalo kwa wanajeshi walikuwepo eneo hili kushangaa.

Wakati wanapeana mikono mara iliingia pikipiki  na kwenda kusimama mita kadhaa   umbali  walipokuwa wamesimama  Roma.

Na  dereva wa pikipiki alitoa helmeti na hapo ndipo Roma alipomshuhudia  Mage  mwanadada mrembo ambaye  kila siku wanapokutana  ni kwa shari., alijiuliza mrembo huyu kaja hapa ndani kufanya nini maana kwa kumbukummbu zake alikuwa anaelewa kuwa Mage alikuwa ni  polisi  na hapa ndani hapakuwa pakimuhusu.

Previoua Next