Reader Settings

Roma aliendelea kumshangaa  Mage mpaka pale alipowafikia, huku akiendelea kujiuliza maswali ni jambo gani limemleta Mage makao makuu ya jeshi  , baada ya   Mage kuwafiikia , alisimama wima kama mwanajeshi na kisha akakakamaa mwili  maarufu kama kubana ta*ko.

“Jambo Afande , jambo afande ,Ajenti Flamingo  kutoka kikosi cha wachawi naripoti”

“Karibu tena  Tanzania Ajenti Flamingo”

“Asante sana Afande” Huku akilegeza , huku  upande wa Roma akishangazwa na kitendo hiko  inakuwaje Mage akawa mwanajeshi ghafla tena ndani ya kikosi cha wachawi.

“Meja naomba niulize kwanza”Aliongea Roma na kuwafanya maafande  hawa wamwangalie na kumpa ruhusa .

“Huyu si Mage  , polisi  namba moja kwa  kunichukia hapa Tanzania , mbona ni mwanajeshi?”Aliuliza Roma na Afande Maeda alitabasamu   baada ya kuona Mage na Roma washakutana na kisha akamwangalia  Afande Tobwe.

“Magreth ni polisi ndio , huyu ni pacha wake anaitwa Magdalena Tobwe ni Special Ajenti kutoka  kitengo maalumu  cha kupambana na   maadui wanaotumia nguvu za  giza na  alikuwa nchini China kwa miaka minne akisomea mafunzo ya  uchawi wa kachina na  kijapan”.

“Kwa hio Afande Meada Mage na huyu Magadalena baba yao ni  Kanali Tobo?”

“Kijana kuwa na Adabu  nishakwambia naitwa afande Tobwe sio Tobo “Kitendo kile cha  Roma kumuita baba yake Magdalena Tobo  kilimuuzi.

Roma alimwangalia mwanadada huyu ambaye alikuwa akifanana kwa kila kitu na Mage   na kisha  akatabasamu na kisha akaagana na  maafande na kuingia kwenye gari yake  kuondoka.

Baada ya Roma kuondoka  Afande Maeda alimwangalia Ajenti Flamingo na kisha akamgeukia kanali.

“Ajenti Flamingo wewe ni invicible Solder  na kwanzia sasa  utakuwa unafanya kazi  kwa ukaribu na  Pluto”.

“Afande  unamzungumzia Pluto gani?”Aliongea Flamingo kwa  mshangao  na Afande Maeda alitabasamu

“Unaonakena kuwa na habari za kutosha kuhusu Pluto  ulipokuwa kwenye mafunzo si ndio?”

“Ndio Afande , nimesikia sana habari zinazomuhusu  Mrithi wa Mfalme Pluto Hades , hakuna mwanajeshi yoyote wa  kitengo cha uchawi ndani ya China asiemfahamu Hades”Aliongea Ajenti Flamingo  huku wakiwa wanaingia ndani ya ofisi.

Na baada ya mkuu wa  Afande Maeda  kukaa kwenye kiti chake , huku kanali Tobwe alikuwa asharudi kwenye ofisi yake kuendelea na majukumu.

“Okey Ajenti Flamingo , ninachokuambia hapa ni siri za jeshi na wewe kama mwanaeshi unapaswa kutotoa siri hii , hata Raisi amiri mkuu wa jeshi hajui hili ninalokuambia niswala linalojulikana na watu wachache sana  ndani  jeshi”Alitulia kidogo na kuvuta pumzi.

“Kijana tuliekuwa tumesimama nae hapo nje ni Pluto mwenyewe  , ambaye umezisikia sana  habari zake”Ajenti flamingo alijikuta akishangaa mno na alionekana kutokuamini maneno ya Mkuu wake.

Naona umeshangaa , lakini pia utakuwa unajiuliza kwanini na kuambia siri hii ,  nimekuambia kutokana na kujua uwezo wako  wa kimapigano , wewe ni komandoo , lakini pia unajua mbinu zote za kichawi  na uwezo wako  unakufanya kuwa mtu sahihi wa kufanya kazi na Pluto”Ajenti Flamingo alizidi kushangaa .

Ukweli ni kwamba  tokea  aende kwenye  mafunzo  kichawi (Cultivation training) nchini china alikuwa akiskia habari nyingi zilizokuwa zinamuhusu  Hades au pluto kama moja ya macultivator wakubwa waliovuka  steji za juu kabisa  za kucultivate.

Pluto  na Hades ni majina sawa , Pluto ni jina ambalo  miaka  ya nyuma mtoto Venetia Burney aliekuwa mpenzi wa kusoma hadithi za  Ugiriki alipenda kumuita Hades kama Pluto na kuanzia kipindi hiko  jina la Pluto  likawa maarufu Zaidi kuliko hades.

Licha ya mshangao wa   Ajenti Flamingo na kukubali kazi  hio , hakuwa akiamini kwamba mtu aliekuwa akisifika  kwa ulozi  wa kachina na Japani  Mfalme Pluto kutoka jeshi la The Eagles ndio  Yule mwanaume aliekuwa hapo nje , akili yake ilikataa kabisa , lakini akajiambia kwenye nafsi yake  kwamba ataendelea kulithibitisha hilo kwa kumfatilia Roma kwa kila atakachokuwa anafanya

Ni muda wa saa nane nane hivi ,  wakati Roma akiwa ameshusha kiti cha gari yake na kuuchapa usingizi  ufukweni   kilomita chache  kutoka lilipokuwa  Daraja kubwa la Tanzanite , simu yake ilitoa mlio na aliinua na kuangalia na kujikuta akitabasamu.

“Hehe.. kwa mata ya kwanza Edna kanipigia” aliiongelesha Roma  huku akipokea simu baada ya kuona jina la ‘My Wife’ kwenye kioo.

“Ndio wife , usiniambie umenimiss mume wako?”.

“Uko wapi?”

“Ufukweni bebi”.

“Njoo  tukutane  My World Fashion Mall pale”Na simu ikakatwa, Roma alitabasamu  huku akifikiria ubabe wa mke wake , ila hakujali sana aliwasha gari na kisha alielekea  lilipo jengo refu sana ndani ya Posta lililokuwa likifahamika kwa jina la My World Fashion Mall

Roma ndani ya madakika kadhaa tu alikuwa ashafika na nikama walikuwa wameambizana , kwani wakati Edna  anaegesha gari na Roma alikuwa akiingiza gari maegeshoni, alisimamisha na kufungua mlango na kisha akamrushia ufunguo Valet(mtu uanaehusika na kupaki magari) na kumsogelea Edna.

“Bebi  hapa tumekuja kufanya nini?”Edna hakujibu Zaidi ya kutangulia  na Roma  alimsogelea na wakaingia kwa pamoja na kama kawaida watu wengi wlaikuwa wakimshangaa Edna kwa uzuri aliokuwa nao , kuna waliokuwa wakimjua kama mfanyabiashara mkubwa , lakini pia kuna  ambao hawakuwa wakimjua.

Edna hakuwa mtu wa kupenda sana  kunyionyesha kwenye mitandano na vyombo vya habari , hakuwa hata  na akaunti yoyote katika mtandao wa kijamii  na ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu na hata mara nyingi kama tu atasaini mkataba ambao utahusisha  waandishi wa habari mara nyingi Dorisi ndie aliekuwa akimuwakilisha , hivyo ndani ya Tanzania imemfanya kutotambulika sana licha ya kuwa mwanamke ndani ya taifa mwenye pesa nyingi kuliko  mtu yoyote.

Baada  ya kuingia kwenye  duka moja kubwa ambalo lilikuwa limesheheni nguo za kiume  , Edna alianza kupita  taratibu upande wa suti na alionekana alikuwa akichagua , huku wafanyakazi hapa ndani wakionekana kutoa heshima kubwa kwa  Edna.

Aliangalia baadhi ya suti karibia zote za Brand tofauti tofauti   za ndani ya nchi na nje ya nchi  na kila aliokuwa akivutiwa nayo aliinyoshea kidole na  mfanyakazi wa hapa ndani alichomoa na kuishika mkononi.

Wakati huo Roma hakuwa na habari kwani alikuwa amekaa kwenye masofa ,  akimwangalia  mke wake na kutabasamu , baada ya  dakika kadhaa Edna alikuja akiwa amebeba suti na mashati mpaka alipokaa Roma.

“Kajaribu hizi nione zinakaaje kwenye mwili wako”Aliongea Edna kama kawaida na sura yake ya usiriasi.

“Bebi kwakua umezichagua wewe zitanipendeza haina haja ya kujaribu”

“Nimekuambia kajaribu”

Roma aliinuka huku akiangalia baadhi ya watu waliokuwa na wapenzi wao  wakiwaangalia ,  na Roma alijua tu kuwa walikuwa wakimwangalia  mke wake alivyokuwa mzuri.

“Kaka una mke mzuri , ukimsaliti utaonekana kichaa kaka , mchunge sana”Aliongea  jamaa mmoja  ambaye na yeye alikuwa  akibadilisha.

“Jua mambo yako braza”Aliongea Roma huku akimpita na kwenda kubadilisha.

Walitumia takribani nusu saa ya kununua nguo viatu na saa .

“Bebi hivi vyote vya nini sasa?”

“Ni vya kwako na kesho utavaa hii na hii nyingine tukienda kwenye kusanyiko la wafanya biashara”Alionyesha moja  moja.

“Kusanyiko la wafanyabiashara , mbona sijui kama tuna ratiba ya kwenda kwenye kusanyiko la wafanya biashara”

“Ndio nakuambia , ukisharudi inabidi nikakutambulishe kwa wafanyabiashara wenzangu”

Lakini wakati wakiwa wanaendelea kuongea , mara aliingia mwanadada mwingine hapo ndani akiwa ameongozana na mabaunsa kama manne  hivi na kufanya hali ya hewa kubadilika kwani watu wote waliwakodolea macho.

“Donyi Donyi”Aliita Roma mara baada ya kumuona mwanamke aliekuwa  mbele yake ni  yule aliekutana nae siku kadhaa nyuma  ufukwen, sasa Roma alimwita huyu mwanadada lakini huyu mwanadada ni kama hakuwa amemuona vizuri  Roma na ile anageuka vizuri kumwangalia  Roma alijikuta akipatwa na mshangao na kumkimbilia Roma na kumvaa mzima mzima  mwilini na kumkumbatia , kitendo ambacho kilimfanya Edna na baadhi ya watu waliokuwa  hapa ndani  washangae , ikiwemo  yule bwana aliempa ushauri Roma dakika chache nyuma.

Roma mwenywe  ni kama tukio hilo kwake lilikuwa ghafla sana kwani alishindw akulizuia  na aliona Donyi kaharibu Zaidi alivyoanza kumbusu mashavuni.,Roma alimwangalia mke wakena kumuona akianza kukunja sura kwa hasira na Edna alichukua  mkoba wake  na kupiga hatua kuelekea nje , huku akiona aibu , kwani aliona kitendo kile kimemdharirisha   mbele ya watea waliopo  hapo ndani kwani ni dakika chache nyuma  tu walionekana kama mume na mke  kweli lakini dakika kadhaa mbele kila kitu kimebadilika na mchepuko kwa Roma amemvaa.

“Sema   wanaume hawajahi kuridhika , kwa  jinsi yule mrembo alivyomkumbatia yule kaka ni lazima ni wapenzi”Aliongea mwanadada mmoja aliekuwa pembeni akilipia nguo alizonunua

“Tokea tulivyoachana nilishindwa kulala , kabisa nimekuwa nikikufikiria kila dakika kila sekunde kila saa , niliilaumu sana kwa kusahau kuchukua namba yako”Aliongea Donyi na  kuzidi kumchangaynya Roma , alimtoa kwenye kifua chake na kisha akamwangalia.

“Donyi naomba nimuwahi mke wangu  kwanza na naomba  Mungu asije kutukutanisha tena”Aliongea Roma na kujitoa kwenye mwili wa  mrembo huyu na kisha  akachukua nguo walizonunua na kuwahi nje , lakini alikuwa amechelewa kwani ile anatoka aliona gari ya Edna ikitokomea  nje kabisa ikiingia barabara kuu.

****

 NEW YORK

Ni ndani ya chumba cha hoteli  katika floor inayohudumia VVIP alionekana The First Black akiwa  ameketi kwenye masofa ndani ya chumba hiki , huku mbele yake kukiwa na mwanaume mwingiene wa kizungu  mwenye umri kimakadirio kama miaka arobaini hivi , aliekuwa amevalia suti na shati la blue na tai nyeupe .

Bwana huyu alifungua mkoba wake mweusi aliokuwa ameuweka pembeni na kisha akatoa picha na kumpatia  mheshimiwa Mstaafu  na Mheshimiwa  alizipokea zile picha na kuanza kuangalia moja moja pasipo kubadili muonekanao wake , baada ya kuridhika na picha zile aliziweka kwenye meza  ya kioo na  kuinua macho nyake kumwangalia huyu bwana.

“Futeni Ushahidi wote  , ambao unaweza kumfanya  akafahamu ukweli , hakikisheni anajua kile ambacho tunataka sisi akijue  na sio Zaidi ya hapo”Aliongea  The first black huku akiangalia picha iliopo mezani , ni picha ambazo zilikuwa zikimuonesha Roma  akiwa na Edna na picha hizi kwa haraka haraka zilionekana  zilipigwa siku ambayo Roma na Edna walienda kusajili ndoa yao Bomani.

“Sawa mheshimiwa  ila Mr President anataka  nyaraka zote ambazo zinahusiana na Project LADO , maana kwa taarifa tulizonazo mpaka sasa  inaonesha Urusi  inataka imshawishi Agent !3 kujiunga  nao , jambo ambalo kama litafanikiwa itakuwa hatari kwa upande wetu”.

“Kuhusu mikataba ile , nitakaa nayo , naelewa ni mali ya taifa , lakini mpaka sasa sina ninaemuamini nitaongea na Mr President mimi mwenyewe  na kumuelewesha juu ya hilo , kuhusu  Agent 13  acheni shaka kabisa , hawezi kujiunga na upande wowote, kabla ya kwenda Tanzania alisaini ‘The Gods Treaty’  na huu mkataba unamtaka kuwa Neutral , ninachowaasa ninyi kama CIA hakikisheni hamfanyi jambo lolote  la kijinga na  akafahamu kama mnafuatilia , itakuwa hatari kwenu na kwa taifa”Yule mzee alishangaa kidogo , lakini hakuweza kuongea chochote.

“Rogani  Project LADO  ilitugharimu kiasi  kikubwa sana  cha pesa  na mpaka sasa mimi ndio mkuu wa Project  hio , hivyo Raisi kusema kuwa anataka nyaraka ni swala ambalo haliwezekani , licha ya kwamba nchi yetu iliwekeza sehemu kubwa  kuliko taifa lolote , lakini bado Project LADO  ni ya kimuungano”

“Nimeelewa mheshimiwa na sisi kama CIA tutakaa mbali na Hades”The First Black  alitabasamu na kisha alinyanyua  glass ya wine na kunywa kidogo.

“Itakuwa vyema sana kama utawaweka vijana wako  under Control , labda nikudokezee tu Project LADO inaendelea na sasa tupo kwenye Testing Phase(Hatua ya majaribio)

Rogani  alionekana kumuelewa vizuri mheshimiwa na hakutaka kuongea neno lolote kumpinga The First Black.

Previoua Next