Ni siku nyingine kabisa , siku ambayo Roma alikuwa akielekea nchini Japani kwa ajili ya kumuwakilisha mke wake katika dili nono kati ya kampuni ya Yamakuza , Vexto na JR , ni muda wa asubuhi kabisa saa mbili kamili Roma alikuwa ashajiandaa kwa kila kitu na kilichobaki ilikuwa ni kuelekea nchini Japan.
Edna alishuka kutoka kwenye chumba chake akiwa tayari ashajiandaa kwa ajili ya kumsindikiza Roma mpaka uwanja wa ndege, baada ya wawili hao kuungana huku Edna akionesha ukauzu wake kama kawaida mbele ya Roma ,alitangulia na kuingia kwenye gari yake ya Mercedenz aliokuwa akipendelea,na Roma na yeye akaingia na Edna kama dereva alitoa gari hio taratibu na wakatoka nje ya Geti na kuingia barabarani.
Muda mchache tu walikuwa washafika ndani ya uwanja huu wa ndege wa JNIA ,Doris alionekana kuwahi , kwani alikuwa ashafika tayari na alionekana alikuwa akiwasubiria , alikuwa amependeza kama kawaida kuzidi wanawake karibia wote walikuwa ndani ya uwanja huu wa ndege na kufanya baadhi ya wanaume wamkodolee macho.
Wakati wanaendelea kuongea , mara walisogelewa na watu wawili , mmoja akiwa ni mwanaume na mwingine alikuwa ni msichana mrembo hivi alievaaa akapendeza na hata kwa mwanaume alikuwa amependeza pia.
“Naitwa Isack Bathomayo ,Assistant CEO kutoka JR Group na huyu ni Sasha sekretari wangu na mpenzi wangu ”Aliongea bwana huyu kwa kujitambulisha na kuwafanya Dorisi , Edna na Roma kushangaa na Roma alijikuta akitukana matusi ndani kwa ndani Abuu , alikumbuka ile siku ambavyo Abuu alivyokuwa aking`ang`ania Edna aende huku akisema ni masharti kutoka kwa Yamakuza , lakini leo hii alikuwa ametuma muwakilishi alijua yote yale yalikuwa ni mipango yao na anashukuru aliifahamu mapema .
Edna alimwangalia Roma kwa kuibiaibia na Dorisi pia alimwangalia Roma na hawakutaka kuongea mengi ,Edna aliwapa maelekezo ya kuwa makinni katika kusaini mkataba huo na kisha wakaagana na ndani ya madakika kadhaa tu ndege ya Emirates iliapaa kuelekea Japan.
Kwenye ndege hakukuwa na maongezi mengi sana , kwani Dorisi alilala mapema sana , aliekuwa macho alikuwa ni Roma ambaye alikuwa akiwakagua wahudumu wa ndege kila aliekuwa akija kumhudumia ndani ya daraja la Kwanza la wafanyabiashara.
****
KANSAI -INTERNATIONAL AIRPORT,JAPAN
Saa kumi na moja kamili za Asubuhi Ndege ya shirika la Fly Emirates iligusisha taili zake ndani ya uwanja wa kimataifa wa Kansai ndani ya jiji hili la Osaka.
Osaka ni moja ya miji mikubwa sana ndani ya Japani ni mji ambao ni mzuri sana kutokana na uwepo wa safu za milima ndani ya jimbo lote la Honshu, na ni sehemu pekee ambayo watu wengi wanaosafiri kwa ajili ya kutalii hupendelea sana kufika.
Osaka ni maarufu sana kwa raia wake kuishi watakayo , lakini pia upatikanaji wa aina nyingi ya vyakula na hili lilivutia sana watu na kwa kwa kiasi Fulani unaweza kuufananisha mji huu na Los Angels Marekani. Kutokana na mazingira yake na pia namna watu wanavyokula bata ndani ya hili jiji.
Muda huu wa Saa kumi na moja Roma , Dorisi pamoja na wafanyakazi wawili wa JR Grupu walikuwa washakamilisha taratibu zote na sasa walikuwa wakitoka nje ya jengo hili la kufikia wageni , baada ya kutembea na kufika nje sehemu maalumu kwa ajili ya kupokelea wageni , hatimae waliweza kumpata mwenyeji wao ambao alikuwa amekuja kwa ajili ya kuwapokea baada ya kuona bango la JR na Vexto likiwa limeshikiliwa na kijana mmoja wa Kijapani ambaye alikuwa amesimama na bwana mmoja ambaye alionekana kibosibosi kutokana na aina ya mavazi yake, alikuwa amevalia Navyblack suti ambayo ilionekana kuwa ya bei kubwa , pamoja na saa kampuni ya Brand ya Radeon.
“We’ve been expecting you, friends of Vexto and JR Group . I’m Yamakuza Corporation’s Vice-CEO, Tikayi . My father, Yamamoto was unable to make the trip down due to sickness, so I am welcoming you on his behalf, and also express his apologies.”
“Tulikuwa tukiwasubiria ndugu zetu kutoka Vexto grupu na JR grupu , mimi ni CEO msaidizi wa Kampuni ya Yamakuza naitwa Tikayi , baba yangu ameshindwa kuja kuwapokea kutokana na maradhi yake na nipo hapa kuwakaribisha kwa niaba yake , na niombe Radhi kwa kutokuwepo kwake”:Aliongea Tikayi kwa kingereza safi.
“I never expected to be received so warmly, sorry to make you wait”(Sikutarajia mapokezi haya ya kikarimu tusamehe kwa kukufanya usubiri kwa muda mrefu” aliongea Doris .
“Tunafurahi kukufahamu bwana Tikayi , Niite Roma ni mkalimani kutoka kampuni ya Vexto”Aliongea Roma na kumpa mkono Tikayi na bwana huyu akatabasamu
“Nilikuwa nikisikia taarifa Tanzania kuna wanawake warembo nadhani leo ninaamini fununu hizo ni za kweli”Aliongea na Dorisi alitabasamu , ila Roma hakupendezwa na namna ambavyo Tikayi alikuwa akimwangalia Doris.
“Ni kweli kabisa bwana Tikayi ,Tanzania imebarikiwa na kuwa na wanawake warembo ila wanapendelea wanaume wenye mashine kubwa sio kama wajapani na vipenseli vyenu”Aliongea Roma kwa Kijapani na kumfanya Tikayi akunje sura , kwa dakika na kisha akatabasamu , huku Dorisi na wenzake wakishangaa ni nini Roma alimwambia mkaka wa watu mpaka akakunja sura.
Basi waliongozana na kuingia kwenye magari mawili yote yakiwa ni Caddillac limousine ambayo yalikuwa yameandaliwa kwa ajili yao na kisha wakatoka nje kabisa ya uwanja huu wa Ndege.
Jiji lilionekana kuwavutia sana Doris na wafanyakazi wa JR kweli , kwani walikuwa wakishangaa miundombinu na kujikuta kutabasamu bila kupenda, majengo ya Japani hayakuwa yameenda hewani sana , lakini yalikuwa yakipendezesha mji kutokana na mpangilio.
Ndani ya dakika chache walifika ndani ya eneo moja lililokuwa likifahamika kwa jina la Ashiya , hii ni sehemu ambayo inaishi matajiri wengi ndani ya Osaka na ni sehemu ghari sana kupata nyumba ya kuishi ndani ya eneo hilo ni kama hapa Tanzania useme Osterbay ndio ilivyokuwa kwa Ashiya.
Sehemu hii ilikuwa katikati ya Kobe na Osaka , na upande wa kushoto kulikuwa na fukwe ambayo ilizidi kupendezesha eneo hili.
Doris alionekana kupenda sana hili eneo na alishindwa kuzuia furaha yake na kumwangalia Roma aliekuwa pembeni yake na kutabasamu.
Upande wa Roma hakuonekana kushangaa sana , ila alionekana kama ni mtu ambaye alikuwa akikumbuka mambo mengi sana ya nyuma akiangalia maeneo haya.
Dakika chache mbele gari zote mbili zilikuja kuingia ndani ya kizuizi kilichokuwa kikipakana na barabara upande wa kushoto.
“Imekuwa heshima kwetu sana kufanya kazi na Kampuni kutoka Tanzania na kwasababu ya hilo tumeona ni vyema mkiishi kwa muda wote mtakaokuwepo hapa japani ndani ya Twillight Villa ya kifamilia”Aliongea Tikayi kwa kingereza na Dorisi alitabasamu na kisha akasema ‘Thank you’.
Hii sehemu ilikuwa nzuri mno na ilikuwa ikiendana na sifa ya eneo hili kuitwa sehemu wanayoishi matajiri , licha ya ukubwa wa eneo hili lakini pia unadhifu wake ulifanya kuvutia sana , bustani zilikuwa zimejengewa kwa ustadi mkubwa na miti yake mirefu ya wastani aina ya Italian Cypress Tree ilizidi kupendezesha macho.
“Karibuni Sana”
“Asante” Alijibu Doris huku akivuta pumzi ya hewa iliokuwa ikinukia ndani ya eneo hili , na mbele yao kulikuwa na jengo ambalo lilikuwa limejengwa kwa muundo wa Nyota , lilikuwa ni jengo kubwa na la kuvutia sana , kwa mbele kulikuwa sanamu la Samurai lililokuwa limejengwa na kunakishiwa kwa madini ya Dhahabu na kufanya sehemu hii kupendeza Zaidi.
Wakati wakiendelea kushangaa , uzuri wa hili eneo ziliingia gari mbili za kifahari MBW 7 na kwenda kusimama mita kadhaa kutoka walipokuwa wamesimama na akashuka mzee mmoja hivi makadirio ya miaka sabini hivi akiwa na fimbo ya kutembelea na akawasogelea huku akiwa ameweka tabasamu pana usoni.
Aliwasalimia kwa ukarimu sana na kuwakaribisha Japani ,Mzee alikuwa akiongea vizuri kingereza kwa rafudhi nzuri tofauti na Tikayi , huyu mzee ndio anafahamika kwa jina la maarufu la Yamamoto na ndio alikuwa mmiliki wa kampuni ya Yamakuza na pia alikuwa Tajiri mkubwa ndani ya jiji hili.
“Mr Vice ni muda gani mazungumzo yetu ya kibiashara yataanza?”Aliuliza Doris na alionekana alikuwa akitaka mazungumzo ya kibiashara yaanze wamalize ili wajue mambo mengine
“Miss Doris , please rest assured, you’re all fatigued from the flight today, so please rest at our Villa for hours My father and the others would also relax, and we will only begin the talks Tomorrow. Then, there will be two days of visits to the research facility, and exchanges with the researchers. Then, we will draft up a collaboration document.”
Hapo akimaanisha kwamba wapumzike kwanza ndani ya nyumba hio kwa masaa kadhaa kuondoa uchomvu unaotokana na safari na kesho wataanza maongezi ya kibiashara halafu baada ya hapo watatembelea taasisi ambazo zinahusika na utafiti wa Material hayo mapya na pia mabadilishano ya watafiti halafu watakaa mezani kwa ajili ya kujadiliana juu ya makubaliano ya pande zote .
Kwa mtiririko mzima wa kikazi itawachuku jumla ya siku tatu kukaa ndani ya nchi hii ya Japani na Doris alitabasamu , aliona atapata wasaa mwingi wa kukaa na Roma na kufurahia Maisha.
“Roma ushawahi kufika Japan?” Aliuliza mzee Yamakuza na Roma alimwangalia na kutabasamu na kisha akasema hakuwahi kufika , ila ukweli Roma kwenye moyo wake alikuwa amekuja ndani ya Japani mara kibao na mara zote alizoingia ndani ya hili taifa ilikuwa ni kwa kazi maalumu.
“Waheshimiwa mnaonaje kwanza tukiachana na maongezi na mkafanya mpango wa chakula maana nahisi njaa sio ya kawaida” Aliongea Roma mara baada ya kuona mzee huyu alikuwa bize kuongea na Dorisi juu ya umaarufu wa Japani na mambo yake ya kipekee yanayopatikana na Roma mambo hayo yalimchosha maana kwake hayakuwa na maana.
Msosi uliandaliwa baada ya mzee huyu kuwapa ishara wafanyakazi wa hapa ndani na ndani ya madakika kadhaa tu Meza ilichafuka kwa aina mbalimbali ya mapishi . jambo ambalo lilimfurahisha sana Roma.
Baada ya kupata chakula ambacho haikueleweka ni chakula cha asubuhii au cha mchana , Roma na Doris na wale wapenzi kutoka JR grupu walionyeshwa sehemu zao za mapumziko.
Dorisi na Roma kama kawaida walipewa chumba kila mmoja cha kwake , lakini waliishia kuwa ndani ya chumba kimoja na kuanzia asubuhi mpaka muda wa jioni ilikuwa ni kukiamsha na hata chakula cha mchana walikula humohumo.
Saa mbili kamili za jioni Roma , Dorisi na wale wapenzi kutoka JR walitoka kwenye vyumba vyao mara baada ya kuitwa na wahudumu kwa ajili nya chakula cha usiku , na walijikuta wakishanngaa mara baada ya kukuta watu wengi waliokuwa kwenye meza tofauti na ilivyokuwa asubuhi.
Baada ya kuketi kwenye nafasi ambazo walionyeshwa na wahudumu , Mzee Yamamoto alianza kuwatambulisha kwa wageni hao waliokuwa wanaonekana kuvaa mavazi ya suti na hapo Roma na Dorisi ndipo walipowatambua kuwa hao ni moja ya wafanyakazi wakubwa wa kampuni ya Yamakuza na wamealikwa kwa ajili ya chakula cha jioni kama sehemu ya kujipongeza katika mafanikio ya kuelekea kusaini mkataba kati ya Yamakuza na Kampuni mbili kutoka Afrika.
Msosi wa nguvu uliandaliwa , jambo ambalo lilimfurahisha sana Roma kiasi cha kutoa tabasamu, wageni hawa walitoa mshangao mara baada ya Roma kuanza kula bila habari , kwani wote walikuwa hawajaanza na ni kama walikuwa wakisubiria kukaribishwa na mzee Yamamoto , ila wakati wao wanasubiria Roma yeye alikuwa tayari ashaanza yake na hata Dorisi alimshangaa Roma ila aliishia kutabasamu na hata kwa mzee Yamamoto aliishia kutabasamu na ilibidi wote waanze kula.
Wakati wanaendelea kula mara aliingia bwana mmoja ambaye alikuwa amevaa suti lakini kwenye mfuko wa suti yake kukiwa na kibango kidogo kilivhokuwa kikionesha nafasi yake ya kazi ndani ya nyumba hii yaani ‘House’ Meneja na kumsogelea mzee Yamamoto na kumnong`oneza jambo na mzee huyu aliweka vijiti(chopstick) vyake alivyokuwa anatumia kula.
“Huu ni ujinga” Aliongea kwa sauti na kwa hasira na kufanya waliopo hapa ndani washangae.
Comments