Kila mmoja alishangaa kwanini mzee huyu alipandwa na jaza ghafla namna hio mara baada ya kunong`onezwa jambo na muhudumu wa nyumba.
Tikayi aliekuwa amekaa pembeni na baba yake alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa ni kama mtu ambaye alikuwa akijua ni taarifa gani baba yake ameambiwa.
Na wakati wakiendelea kujiuliza ni kwanini mzee Yamamoto kapandwa na Jazba mara aliingia bwana mmoja mkumkukuku , bwana ambaye alikuwa amevalia shati lake rangi ya maua maua na suruali ya Jeans.
Bwana huyu ukimwangalia mara moja tu utagundua kuwa Tikayi na huyu bwana ni ndugu kimuonekano, jamaa huyu baada ya kuingia alijikokota na kudondoka kwenye miguu ya Yamammoto na kisha akaanza kulia kwa sauti na alionekana kulewa pia , jambo ambalo lilifanya hali ya hewa kuwa mbaya.
“Wu.. baba .. ninafanya nini mimi.. aaaaaah Dina kaniacha baba ..iiii .. Dina..weeee… aaaa”
Jamaa alikuwa akilia mpaka anatema mate kitendo kilichozidi kumkasiriasha mzee Yamamoto na alichokifanya ni kumpiga teke na akadondokea upande mwingine , lakini huyu bwana aliamka tena na kukamata mguu wa baba yake na kuanza kulia tena huku akiwa anamtaja mwanamkie anaeitwa Dina akilalamika ameachwa , na kila mmoja aliekuwa hapa ndani alikuwa ashajua ni nini kinaendelea kwa huyu bwana, walijua yote hayo ni sababu ya kimapenzi. Na bwana huyo alikuwa ameachwa.
“Jamani naomba mniwie radhi kwa jambo hili , huyu ni mwanangu mkubwa Tikayeshi , lakini licha ya kuwa mkubwa katika familia , ndio mpumbavu kuliko wanangu wote”Aliongea mzee huyu wa kijapani huku macho yake yakiwa mekundu kwa hasira.
“Hakuna shida mzee ni jambo la kawaida kwa vijana” Aliongea moja ya wafanya kazi wa kampuni na mzee huyu aliwapa ishara walinzi wamtoe eneo hilo na bwana huyu alikokotwa na kutolewa huku akiendelea kulia kwa sauti kama toto jinga , na kwa kumuangalia tu ungejua kuwa ni sahihi kwa mzee Yamamoto kumuitwa Tikayeshi mtoto mpumbavu kuliko Watoto wake wote.
Tikayi alionekana kutabasamu na kufurahishwaa na tukio hilo , ali mwangalia baba yake alivyokuwa na hasira na kuridhishwa na hali hio.
Basi baada ya chakula wageni wale walitawanyika na hata kwa Mzee Yamamoto waliagana na Roma na kuwatakia usiku mwema huku wakiwaahidi kuonana keshi kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara.
Roma aliingia kwenye chumba chake na hata kwa Dorisi hivyo na wale wawakilishi wa JR pia kila mmoja aliingia kwenye chumba chake .
Roma baada ya kuingia alipunguza nguo na kisha akajilaza kitandani kuutafuta usingizi kwani muda hio ilikuwa yapata saa nne usiku.
Roma alitumia nusu saa tu kujipumzisha mara mlango uligongwa na kujikuta akishangaa nani anagonga, kwani walikuwa washaagana na hata na Dorisi pia , akiwa na singlendi yake pamoa na pensi , alisogelea mlango na kufungua na mbele yake alikuwa mhudumu wa kiume ambaye alikuwa ameshikilia sahani ambayo ilikuwa imefunikwa na kitambaa cheupe na Roma akamwagalia huyu mhudumu pasipo kumsemesha chaohcaote na kushangaa ameleta nini kwani hakuwa amegiza aina yoyote ya huduma , lakini ghafla tu muhudumu huyu wa alievalia sare za hili jumba alitoa kile kitambaa kwa kasi na kwenye ile sahani kulikuwa na kisu na alikishika haraka sana kwa ustadi na kumrushia Roma kwa madhumuni ya kumdhuru , lakini Roma ni kama vile alitegemea , kwani ile kisu kinarushwa alihepa kushoto na kisu kikapita nusu inch na umbali wa kidevu chake kiasi kwamba hata ndevu ziliguswa kiana na Roma hapo hapo akajua huyu ni mhudumu feki na ametumwa kwa ajili ya kuua.
Baada ya mhudumu huyu feki kuona Jaribio lake limefeli , alirusha ngumi lakini kwa Roma alimuona kama mtoto anaejifunza kurusha ngumi kwani aliushika mkono na kuuzungusha na kilichosikika ni mlio wa mifupa kukatika , na Mhudumu feki akaachia mguno wa maumivu , lakini Roma hakuishia hapo tu , alimpiga kwenye koo kwa mkono , kama vile alikuwa akimchinja , kwnai pigo hilo lilikuwa ni la Karate na mhudumu feki aliregea na kudondoka chini.
“Shi*t watakuwa wengi hawa ,Dorisi atakuwa kwenye matatizo”
Aliongea Roma na kuchomoka kwa spidi kuwahi kwenye chumba cha Dorisi na ile anafika tu alimuona mhudumu akiingia ndani ya chumba cha Dorisi huku akiwa na sahani kama ile ile ya mhudumu aliemuua ikiwa imefunikwa na kitambaa cheupe.
Roma alikimbia kwa kasi na kuzama na ile anafika mhhudumu alikuwa tayari ashashika kisu na kumlenga nacho Dorisi kooni na Dorisi aliishia kufumba macho huku akiwa anatetemeka mwili mzima akisubiria kifo , lakini mhudumu baada ya kufikisha sentimita mbili karibu na koo la Dorisi alidakwa mkono na kuzungushwa kwa nguvu ambayo hakuwa ameitegemea , na baada ya kugeuka tu, aliopigwa na mikono miwili kwa wakati mmoja na Roma kwenye mbavu na mhudumu yule wa kijapani aliishia kuachama na kukosa pumzi na kisha akadondoka chini kwani mbavu zilikuwa zishakatika.
Dorisi alihikuta akimkimnbilia Roma na kumkumbatia huku akianza kulia kama mtoto na Roma alimtuliza na walati huo huo aliingia ndani ya chumba cha Dorisi Tikayi.
“Mko salama?” ndio swali la kwanza kutoka kwa Tikayi huku akimwangalia Roma kwa macho ya kumsanifu.
“Naona mmetuleta Japani kwa ajili ya kutua”Aliongea Roma kwa hasira na Tikayi alianza kuomba msamaha kwa tukio hilo na wakasema kwamba hawahusiki nalo.
“Mr Roma hili swala halituhusu hata kidogo na tutahakikisha tunawakamata wahusika , kwani tunaamini ni watu ambao wametumwa”:
Aliongea Tikayi na muda huo huo aliingia bwana mmoja alievalia Robes za kitamaduni za Japani huku akiwa ameshika upanga kwenye mkono wake na Roma kwa kumuangalia tu aliuona huyo jamaa anajua mapigano.
“Yoshida hakikisheni mnamkamata aliehusika na hili jambo haraka , naamini ana watu wake humu ndani na bado wapo, kagua wahudumu wote mmoa mmoja” aliongea Tikayi na bwana huyu aliamrisha walinzi waliokuwa wamevalia mavazi ya majoho meusi kama yeye na kuanza kutawanyika kumtafuta muhalifu.
Dorisi na Roma walitolewa na kupelekwa kwenye chumba maalumu cha usalama Zaidi na wakati huo huo mzee Yamamoto na yeye aliingia kwa spidi na kuanza kuasihi Roma, Dorisi na wawakilishi wa JR grupu watulie mpaka pale mtuhudumiwa atakapo kamatwa huku akiomba msamaha kw akujitetea jambo hilo hawakuwa wakihusika nalo.
Wote walikusanyika na kukaa kwenye masofa haya , akiwemo Tikayi ,Yamamoto Roma ,Dorisi pamoja na wawakilishi wa JR Group , wakati wakiendelea kuongea juu ya tukio hilo ambalo halijawahi kutokea ndani ya hii nyumba kutokana na ulinzi wake , mara aliingia meneja wa nyumba , yule ambaye alimnong`oneza Yamamloto kuhusu ujio wa kilevi wa Tikayeshi.
“Kuna nini meneja?”
“Boss kuna simu yako hapa kutoka kwa mtu ambaye hatumjui na anadai humu ndani ametegesha mabomu”
“Mabomu!”Aliongea kwa kupaniki huku akichukua ile simu na kusikiliza.
“Mr Yamamoto , nyumba yako yote imejaa mabomu ambayo yataripuka baada ya nusu saa , na hata ujifanye kuyatafuta hautoweza” ilisikika sauti hio ya kijapani kwenye simu na Roma aliisikia vyema kwani na yeye alikuwa akijua kijapani.
“Unataka nini katika familia yangu”Aliongea Yamamoto kwa hasira kwa kijapani.
“Kwanza kabisa nikwambie tu kwamba mabomu yatalipuka baada ya nusu saa na hata kama ulete wataalamu wa uwezo wa juu hatoweza kufanikisha hilo ndani ya nusu saa , na mabomu hayo ni ya sumu kwa maana hio nikibonyeza kitufe ambacho nimeshikilia hapa , itawachukua dakika tano kwa kila kiumbe ndani ya nyumba kufariki”
“Sema unataka nini acha maneno mengi”
“Ni jambo rahisti tu nahitaji Yen Bilioni kumi zinifikie mahali ambapo nitawaambia na nataka Cash….” Aliongea bwana huyo , lakini muda huo huo aliingia Tikayeshi huku akilia.
“Baba .. mabomu … mabomu baba… tunakufa .. Mama wee.. babab niokoe sitaki kufa sitomuaona tena Dina mimi ,,,,aaaaaa” Alilia bwana huyu kama chizi kiasi kwamba Yamamoto alikasirishwa Zaidi na kujisemea moyoni boar ahata abadilishane na mt una gunia la Pumba heanda akapunguza hasara ya kuwa na toto jinga.
“Mtoeni huyu mpuuzi hapa” Aliongea Yamamoto na Tikayeshi alitolewa huku akiendelea kulia kwa sauti akitaja mabom na baada ya Tikayeshi kuondoka Yamamoto aliendele akusikiliza simu.
“Endelea na masharti yako nakusikiliza”
“Nishasema mzee kiasi ninachotaka , shariti la pili mtu atakae leta hizo pesa lazima awe wewe au Tikayi” mzee alitoa macho.
“Kwanini mimi au Tikayi , shida yako ni pesa na tutakupatia haina haja ya mimi kuja au Tikayi kuja”.
“Mzee nadhani haulewi nishasema nahitaj wewe uje ulete pesa hizo au Tikayi ndio alete na niwaambie tu naona kila kitu mnachokifanya hapo ndani na ikitokea mtu atatoka ama kuingia ndani ya hio nyumba bila ruhusa yangu nabonyeza kitufe na Maisha yenu yatakuwa yamefika mwisho na kama haumini mlangoni hapo kuna mtu aliesimama kama kaegeshwa” Wote waliangalia mlangoni na kuona kweli kulikuwa na mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa Yamamoto na wakaini ni kweli bwana huyu alikuwa akiwaona.
Mzee yamamoto jasho lilianza kumtoka , licha ya kwamba kulikuwa na baridi kali lakini jasho lilionekana kwenye uso wake , hakuwa tayari kumuachia Tikayi aende kwani alikuwa ndio mrithi pekee na ndio mtoto ambaye alikuwa na akili , kwani kaka yake alikuwa ni kama chizi.
“Okey tupe dakika kumi na tano tukuandalie Cash”
“Dakika kumi zinatosha hakuna maongezi na narudia , naona kila kitu kinachoendelea hapo ndani mpaka panya wanaoingia na kutoka, hivyo nikiona mtu anatoka ambaye sio wewe au Tikayi nabonyeza kutufe na kuwalipua”.
“Sawa tupe dakika kumi tukuandalie Cash”
“Nitapiga baada ya dakika kumi , muwe na Cash na ndipo nitawapa eneo mnalotakiwa kuja”
Baada ya simu kukatwa Yamamoto alimuuliza Tikayi kama wanashilingi ngapi hapa ndani na Tikayi alisema wana Yen bilioni kumi na nusu, mzee baada ya jibu hilo alipata ahueni na kumuagiza Tikayi akaziweke kwenye begi na baada ya dakika kama saba hivi Tikayi alirudi akiwa ameshikilia begi zito likiwa na vibunda vya hela .
“Nitaenda mimi baba”Aliongea Tikayi na kufanya watu wote hapo ndani washangae.
“Hapana Tikayi , hao majambazi siwaamini kabisa wanaweza wakakufanya kitu , kibaya na wewe ndio mrithi pekee ambaye napanga kukuachia kuiongoza Yamakuza , hapana siwezi kukuruhusu kwenda”
Aliongea Yamamoto lakini Tikayi aling`ang`ania kwenda na baada ya malumbanio ya dakika mbili Mzee huyu alikubali Tikayi aende lakini akimsihi kuwa makini.
Baada ya dakika kumi Jambazi lilipiga simu na kutoa maelekezo ya sehemu ambayo alitakiwa kwenda , ni sehemu moja iliokuw aikifahamika kwa JPN.
Jambazi aliendelea kuwapiga mkwara kwamba hakuna mtu kutoka Zaidi ya Tikayi, na mzee Yamamoto licha ya kwamba alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa , alikubaliana na Jambazi , kwani hakuwa akitaka kuona watu wote waliokuwa humu ndani wanakufa kisa pesa,
Baada ya Tikayi kutoka akielekea mahali ambapo majambazi hayo ndio walisema wapo , Roma hakubaki hapo kwenye chumba cha usalama , alitoka na kuelekea kwenye chumba chake na baada tu ya kufika , aliangalia nje kwa kutumia dirishani kwa sekunde kadhaa na kisha akatabasamu na kufungua dirisha , alirudi na kuvaa shati na suruali na kisha akarudia dirisha na alionekana alikuwa akijiandaa kuruka.
“Unataka kuniacha sio?, ndani ya hii nyumba unajiokoa mwenywe ”Ilikuwa ni sauti ya Dorisi iliomfanya Roma aliekuwa amepandisha mguu kwenye dirisha ageuke na kumwangalia Doris.
“Doris narudi ,baki hapa naamini hakuna kitakacho kutokea” Aliongea Roma
“Hapana tunaenda wote na sipo tayari kubaki”Aliongea huku akionekana yupo siriasi na Roma alifikiria kwa sekunde na kisha akamgeukia.
“Utaweza kuruka hapa?”
“Hapana”
“Sasa utaendaje na mimi kama hapa huuezi kuruka” Dorisi hakuwa na jibu na Roma alifkiria jambo na kisha akamwangalia.
“ Natangulia kwenda chini , utajirusha na mimi nitakudaka”Aliongea lakini Dorisi alitoa mshangao , kwani alipochungulia umbali kutoka walipo mpaka chini aliogopa.
“Kama huwezi mimi nitaondoka mwenyewe”
“Okey nitajirusha kama kweli utanidaka”.
“Usijali nitakudaka”Aliongea Roma na kumwnaglaia tena Dorisi.
“Nitahesabu mpaka nne usipojirusha naondoka”.
Baada ya kuongea Roma alijirusha chini na kwenda kutua kwenye bustani bila ya kupiga kelele ya aina yoyote ile , alionekana kuwa mtaalamu kweli na baada ya kutua aligeuka na kuangalia juu huku akimpa ishara Dorisi ajirushe , ila Dorisi alikuwa akitetemeka ,Roma baada ya kuona Dorisi anatetemeka na hayuko tayari kujirusha , alimuonesha vidole kwa ishara na kuanza kuhesabu , na ile anafika tatu Dorisi alimpa ishara ya kujirusha na hakuwa na jinsi alikuwa akiogopa kufa mabomu na hakutaka kubaki mwenyewe hapo ndani na ndio maana alitaka kuondoka na Roma , alifumba macho na kujiachia kwa ujasiri na ile anafika chini alikuwa kwenye mikono ya Roma , huku akihema kwa kasi sana na Roma alimtuliza na kumwambia apunguze presha.
Comments