Dorisi alimuuliza Roma wanatokaje baada ya kutulia, Roma alimwambia amfuate na Dorisi hakubisha alfuatisha nyuma nyuma mpaka wakatokea eneo la mbele sehemu ambayo kwa kushoto kulikuwa na magari yaliokuwa yameegeshwa, na uzuri ni kwamba eneo hili, taa mwanga wake ulikuwa ni mdogo san ana wa rangi ya kijani kiasi kwamba hawakuwwa wakionekana , kwani watu wote ndani ya hili jumba walikuwa wapo upande mmoja.
“Sasa tumekuja kufanya nini kwenye haya magari?” Aliuliza Dorisi kwamshangao.
“Inabidi tuondoke na gari moja”
“Tutawezaje kuondoka bila kushitukiwa nadhani umesikia mwenyewejambazi lilisema linaona kila kinachoendelea hapa ndani tukiwasha gari atajua” Aliongea kwa wasiwasi na Roma alimwangalia na kisha akatabasamu.
“Sikia Dorisi tutatoka na gari bila kuliwasha” Aliongea Roma na kumfanya Dorisi ajiulize inawezekana vipi.
“Roma hakutaka kuendelea kupoteza muda alizunguka upande wa kulia na kuchagua gari ya bei rahisi na akaipata na Roma alijua tu huenda hio gari itakuwa ni ya moja ya wafanyakazi kazi hapa ndani kwani ilikuwa ndio gari ya kawaida, na ilikuwa bahati kwake kwani kioo cha upande wa kulia kilikuwa hakijafungwa vizuri mpaka kufiti juu , na uwazi ulioachwa ulikuwa ukiingiza vidole viwili na Roma hapa alitabasamu na kisha aliingiza vidole viwili kwenye ile sehemu na kuminya kwa nguvu kwenda chini na kioo kile kilianza kushuka kwa mbinde na ndani ya dakika moja tu Roma alikuwa ashafanikisha zoezi hilo la kwanza , na Dorisi alishangzwa na uwezo wa nguvu za Roma.
Roma aliingiza mkono na kufungua mlango kwa ndani na kumwambia Dorisi aingie.
“Utaendesha mimi nitalisukuma mpaka tutoke eneo la nje sawa”
Dorisi alizidi kushangaa , na kujiuliza mtu mmoja anawezaje Kusuma gari , lakini hakutaka kuuliza sana aliingia ndani ya gari na kushika usukani na Roma akaanza kulisikuma kwa nyuma na kweli gari lile lilianza kusogea taratibu na Dorisi alizungusha usukukani na gari ikakaa sawa kwenye barabara na Roma alizidi kusukuma kwenye barabara hio ya Tambarare na gari ilikuwa ikijongea utadhani imewaka na Dorisi licha ya kuwa makini na usukukani kwani kulikuwa na giza na taa hawakuwa wamewasha kutokana na gari kuwa imezima. Aliendelea kuwaza na kujiuliza Roma ananguvu za aina gani.
Baada ya dakika kama tano hivi kupita wlaikuwa washatoka kabisa nje ya uzio na kuingiza gari barabarani na Roma aliacha kusukuma na kuingia kwenye gari , lakini wakati wote Dorisi akiwa anamshangaaa , alikuwa akishangazwa na uwezo wa Roma kusukumba gari peke yake .
Roma alivuta nyaya chini ya usukani na kisha akachomoa nyaya tatu , nyekundu ,Blu una nyeusi , aliunganisha ule mweusi na wa blue na kisha akagusanisha na wa rangi nyekundu gari ikawaka , kitendo ambacho kilimfanya Dorisi aone kama anaangalia muvi kwani mambo kama hayo hakuwahi kuyashuhudia , lakini pia hakuwahi kuwaza kama atakuja kuona mambo hayo yakitendeka laivu.
“Umejifunzia wapi haya Roma?”Aliuliza Dorisi na Roma alitabasamu pasipo kuongea lolote
Baada ya kwenda mita kadhaa mbele Roma alikunja kushoto na kuchukua barabara ya Rami lakini iliokuwa nyembamba kiliko waliokuwa wametoka .
“”Tunaelekewa wapi?”.
“Tunamfuata Tikayi”
“Unajua alikoelekea?”
“Ndio maana naendesha wewe tulia lazima tuwafikie” Aliongea Roma huku akiendesha gari kama mwehu na alionekana haya maeneo kwake ni kama chochocho za mbagala Rangi Tatu , kwani hakuwa na wasiwasi kabisa na Dorisi alikuwa akimshangaa sana na kujiuliza huenda hamfahamu Roma vizuri , inawezekanae mtu kafika leo kwa mara ya kwanza Japani ila anaonekana kama kaishi Japani miaka mingi , ila hakutaka kuuliza Zaidi alitaka kujua mwisho wake.
Baada ya Roma kukata kulia na kushoto hatimae waliingia kwenye kajimsitu na kupita baadhi ya nyumba chache ndani ya eneo lililokuwa likifahamika kwa jina la JPN na kisha akasimamaisha gari na akashuka na hata Dorisi pia.
“Hapa tutatembea , si umali mrefu kutoka hapa na majambazi yalipo?”
“Wewe umejuaje au unafamiana na majambazi”
“Ningejuana nayo nisingekuja huku Dorisi hilo swali ni la kijinga”
Roma aliongoza njia kuelekea mbele , hakutaka kuendelea na gari kwani aliamini lingepiga makelele na kuwashitua maadui.
Baada ya kutembea kwa dakika kadhaa hatimae walikuwa mbele ya jengo kama kiwanda na Roma alimwambia Dorisi kuwa ni hapo na akae nyuma yake amfuate , na ni kweli ile wanasogea mbele waliweza kuonga gari ambayo Roma aliamini kabisa itakuwa ni gari la Tikayi lakini pia kukiwa na magari matatu kampuni tofauti tofauti maawili yakiwa Rangi yeusi yote na moja Rangi nyeupe.
“Vua viatu halafu tembea na vidole”Aliongea Roma akimwamlisha hivyo Dorisi , ili wasipige makele na Dorisi hakutaka kubisha na pia hakuwa muoga , aliamini alikuwa na mwanaume hivyo hapaswi kuogopa kabisa.
Hapa ndani upande wa kulia kulikuwa na manguo nguo yaliokuwa yamerundikwa upande mmoja kwa mbele kulikuwa na dude kama tanki hivi , na kushoto kulikuwa na nyumba ambayo mlango wake ulikuwa ukionekana kwa mbele , taa za mwanga zilikuwa hafifu kidogo , ila zenye mwanga , palikuwa pametulia kimya kiasi kwamba usingedhania hapo ndani kuna watu.
Roma alimwangalia Dorisi nyuma yake na kuanza kumpa ishara za kijeshi lakini mwanamke akawa haelewi , ilibidi Roma aongee nae kwa kuinua mdomo ili Dorisi aweze kusoma lipsi zake na alielewa na Roma alikuwa akimwambia kwamba watumie vidole na watakimbia haraka na kujibanza kwenye ukuta wa kushoto karibu na mlango , baada ya kuhesabu mpaka tatu.
Dorisi alimwangalia Roma na kujikuta akitabasamu na haikueleweka alikuwa akitabasamu nini , ila alijiona kama mwanajeshi wakati huo na hapo wapo kwenye misheni ya kijeshi(Rescue Mission) ya kiuokozi , alijihisi shujaa na kapata kitu cha kwenda kupiga nacho umbea, alipanga kuwaambia marafiki zake namna ambavyo yeye na mpenzi wake Roma Ramoni walivyamua kufanya misheni ya kiokozi kwa ai kumuokoa mtoto wa Tajiri mkubwa ndani ya jiji la Japani… Dorisi alimwangalia Roma na kujiona anafikiria ujinga.
Baada ya kwenda kujibanza kwenye ukuta kushoto , hatimae walikuwa hatua chache kutoka ulipo mlango na hapo Roma alimpa ishara Dorisi na kumwambia atembee usawa wake kwa nyuma na Dorisi alionyesha kidole gumba kuonesha kuwa wako pamoja.
Kitendo cha kuzama ndani tu walikutana na watu waliokuwa wamenyoosheana Bastola lakini jambo ambalo Lilimshangaza ni baada ya kumuona Abuu pia ndani ya eneo hilo na hata kwa Dorisi pia alishangaa…..
Comments