Reader Settings

Dorisi na Roma walizidi kushangaa kwa hali iliokuwa hapa ndani , kilichowafanya washangae zaidi ni uwepo wa  Tikayeshi na Abuu.

Wakati huuTikayeshi hakuwa tena yule toto jinga aliekuwa akililia mapenzi kama alivyokuwa  dakika kadhaa nyuma  ,pia hakuonekana kama mpumbavu kama baba yake Yamamoto alivyokuwa ana muita , Dorisi na Roma walimuona Tikayeshi kama mtu anaejiamini.

Upande wa kulia alikuwepo Tikayi akiwa na begi lake vilevile  kama alivyotoka Twillght Villa huku upande wa Tikayeshi alikuwa amesimama na   Abuu ,Yoshida yule mlinzi ambae Roma alimtambua kwa uwezo wake wa kimapigano kwa kumuangalia tu , lakini pia  walikuwepo baadhi ya walinzi wa Mzee Yamamoto ambao wote walionekana wapo tayari kupambana kwa ajili ya Tikayeshi..

Kwa hii hali ya hapa ndan Roma na Dorisi waligundua  Abuu yuko upande wa Tikayeshi  ,lakini swala walilojiuliza ni vipi akawa upande wa Tikayeshi na ni sababu gani kaamua kufanya hivyo kwani Abuu alikuwa na kiasi kikubwa cha pesa  tu hivyo hawezi kutega mabomu ndani ha Twillight Villa kwa ajili ya kupata kiasi cha Yen Bilioni kumi.

"Tikayi umekuwa wa kujifanya mjanja sana na leo ndio utakuwa mwisho wako"Aliongea Tikayeshi huku akiwapotezea  Dorisi na Roma kama vile hajawona , walionekana kujiamini kutokana na Sitaha walizokuwa nazo ,lakini  pia walionekana kujiamini kutokana  na wingi wao na pia waligundua kuwa Dorisi Na Roma wako peke yao baada ga Mlinzi mmoja kutoka na kukagua eneo la nje kujihakikishia  kama kuna watu wengine waliokuja nao.

"Tikayeshi nimekufanya nini mpaka unichukie namna  hii ya kunipangia njama kwa ajili ya kunidhuru mimi mdogo wako  wa damu"

"Tulia acha kuongea unafiki Tikayi , unajua sana  nini umefanya kwenye Maisha  yangu mpaka ukanifanya kuchukua haya maamuzi magumu , siku zote baba alikuwa ni mwenye kukupendelea na kukuona una akili sana kuliko mimi  na akaniita mtoto mjinga bila ya kuutafuta ukweli wote,umekuwa ukinizunguka kwa kila kazi ambayo  baba alikuwa akinipatia  na kuhakikisha inafeli , ili tu  nionekane mjinga na uchukue nafasi yangu ndani ya urithi  katika famlia"

Tikayeshi aliongea  kwa uchungu sana na  jambo ambalo alikuwa akiongea lilionekana kuwa kweli  na  kwa jinsi hali ilivyo, ilionesha Tikayeshi hakuwa mjinga kama Baba yake alivyokuwa akimuona , ila  ilionekana pale ambapo Tikayeshi alikuwa akipewa Jukumu ndani ya kampuni ,Tikayi alikuwa akihakikisha jukumu hilo linafeli , alifanya hivyo ili Tikayeshi aonekane hana akili  na hayuco ‘competent’  katika kuongoza kampuni.

Dorisi na Roma walionekana kushangaa , ila walikaa kimya kuangalia Drama hio ya kifamilia  waone nini muisho wake ,Katika mapambano hayo ya kugombea urithi.

Kwa Roma hakuonekana kushangaa sana , alionekana kuzoea  kuona mambo hayo yakitokea mara kwa mara ndani ya familia za kitajiri  ,watoto kugombana mpaka kuana kisa tu  kupata urithi , kwake ni mambo ambayo hayakuanza leo wala juzi ni  , ni mambo ambayo yalikuwepo tokea enzi za kale na  yataendelea kuwepo.

"Hahahahaha.... Tikayeshi wewe ni mjinga na siku zote utakuwa mjinga  .. na nikuambie tu mimi  mdogo wako nimekuzidi kila kitu"

"Acha kuongea ujinga  Tikayi , leo ndio mwisho wako na kauli zako za majigambo nakuua hapa na kampuni itakuwa yangu"

"Huna uwezo huo Tikayeshi .. hauko smart  kichwani kama mimi na haitokuja siku  ukanizidi akili .. masikini kaka yangu , jaribu kuniua kama una uwezo huo"

Roma na Dorisi walishangaa namna Tikayi alivyoanza kujiamini , lakini pia hata kwa Tikayeshi alishangaa  na kupandwa na jaziba maradufu  na kupandwa na hasira, yeye alitaka amuone Tikayi akipiga magoti  na aombe  asimuue lakini hali imekuwa tofauti , kwanini asishangae.

"Mpigeni risasi acheni kuzubaa muda unaenda"

Aliongea Tokayeshi lakini ajabu ni kwamba vijana wake  hawakuonekana  kusogea wala kunyanyua siraha zao na alishangaa na wakati akiendelea kuwa katika hali yake ya mshangao Yoshida  , Abuu na vijana wake wakatoka upande waliokuwa wamesimama na  Tikayeshi na  kusimama  upande wa Tikayi na jambo hilo likawashangaza Dorisi na Tikayeshi lakini Roma akatabasamu.

"Hahaha.. brazaaa.. umejiona sasa ulivyokuwa mjinga , siku zote nimekuwa wakukuambia kuwa hauwezi kunishinda kiakili , angalia sasa ulivyoanguka kwenye mtego wangu .. hahahaha"

 Tikayi alicheka kifedhuli na hapa hakuonekana mpole kama baba yake alivyokuwa akimtambua  bali alionekana kama  muuaji na mtu mwenye roho mbaya sana .

"Yoshida wewe sio wa kunisaliti mimi , Abuu hapana  .. hii haiwezekani "

Aliongea  Tikayeshi huku akionekana kuchanganyikiwa , alijikuta akiwa peke yake wale ambao alikuwa akiwaamini kama wako upande mmoja walikuwa wamemgeuka ,tena wamemgeuka kwenye wakati ambao alikuwa akiwahitaji sana , alijiona kama mtoto alieachwa katikati ya msitu mnene peke yake ,Bwana Tikayeshi chozi lilimtoka.

"Usijali sana broo .. leo nitakuondoa duniani ili kumpunguzia baba kichwa kuuma mara kwa mara ,maana siku zote umekuwa mzigo  kwake"

"Hapana Tikayi naomba usiniue .. tafadhari mdogo wangu naomba usiniue  .. nimekosa kuanzia sasa nitaendelea kuwa mjinga naomba usiniue"Aliongea Tikayi akiwa amepiga magoti na kupasha viganja vyake baada ya kuona hali ya hewa imebadilika na  chaguo pekee ambalo aliona kwa muda huo ni kupiga magoti na kuomba kusamehewa , ungemuona usingedhania ni yule aliekuwa akiongea kwa kujigamba dakika chache zilizopita , Tikayi alionekana kumzidi mbinu na akili.

"Broo pole sana kwa kuzaliwa mjinga , unawaona hawa wote  walikuwa  wangu kabla ya kuja kwako na nilichokifanya nikuwapa maneno ambayo yatakurubuni na hata huu mpango niliupanga mwenyewe na nikamtumia Yoshida akuambie huu mpango na ulivyokuwa mjinga ukaufuata  alichokuwa anakuambia ,huo ndio ujinga wako na usinilaumu mimi kwa kukuua ,familia yetu haiwezi kuwa na mjinga  kama wewe"

Baada ya kuongea hivyo, Tikayi  bila ya kumsikiliza kaka yake aliekuwa akiomba msamaha kwa kumkosea, wala kumhurumia  alivuta upanga uliokuwa kwenye kiuno cha Yoshida na kisha akamsogelea kaka yake huku akiwa na macho yaliojaa roho ya kinyama na akamfyeka kaka yake kwenye shingo na damu pekee ndio zilizosambaa kwa kuruka  na kutapakaa mahali hapa na kila mmoja alishangazwa na roho ya kikatili  ya Tikayi.

"PAAA...PAAA ... PAPAPA .."

Roma alinyanyuka kutoka alipoketi na kuanza kupiga makofi  huku akisogelea upande waliokuwa wamesimama Tikayi , Abuu na Yoshida  na Tikayi aligeuza shingo na kumwangalia huku akionekana hakuwa na hatia hata kidogo ya kumuua kaka yake kifo cha kikatili .

Dorisi alijikuta akijuta kuja na Roma ndani ya hili eneo kwani alikuwa akitetemeka mno , kwa mara yake ya kwanza alikuwa akishuhudia laivu mtu akikatwa kichwa kikatili kwa namna hio , kwake alijiambia tukio hilo ndio la kwanza na ambalo halitakuja kufutuka katika akili yake ,alishindwa hata kuendelea kuangalia maiti ya Tikayeshi na kugeuzia shingo yake pembeni .

"Nishamalizana na Tikayeshi na sasa nimalizane na nyie wawili ,licha ya kwamba sikutaka yafikie hapa yalipofikia lakini sina budi , kutokana na umbea wenu  wa kufatilia mambo yasio wahusu leo mmeweza kushudia jambo ambalo hakumpaswa kushuhudia  na hio ni tiketi yenu ya kunifanya nisiwaache hai , mngebaki kule Twillght Villa kesho tungesaini mkataba na kumalizana"

“Hongera bwana Tikayi  kwa kumuua ndugu yako , sio watu wote wanaweza kufanya hivi”Aliongea Roma na kama kawaida yake hakuwa akitishika na meneno ya Tikati , alifika aliposimama na kisha akampita na kuchuchutama huku akiangalia  maiti ya Tikayeshi ,  aliingiza kidole sehemu ambayo panga lilipita na kama kawaida yake alitoa kidole na kukipeleka puani  na kumfanya Abuu  na wengine kushangazwa na ujasiri wa Roma.

Baada ua Roma kufanya kitendo chake  kiilichowashangaza hawa watu  , alinyanyuka na kumuangalia Tikayi lakini  ghafla tu Yoshida aliekuwa mita kadhaa kutoka aliposimama Tikayi  kwa spidi ya hali ya juu alikuwa ashafika  aliposimama Roma na kumzibia Tikayi kwa mbele , huku bwana huyu akionekana kuwa tayari kimapigano.

****

Ni ndani ya  mji wa kigamboni saa tatu kamili za usiku Edna leo hii alionekana kusimama nje ya Balconi  akiwa ni kisweta chake  cha Rangi nyekudu  pamoja na  pensi  huku  mkononi akiwa ameshikilia  glasi ya kinywaji cha Wine.

Wakati Edna   akifurahia upepo wa baharini , upande wa nje ya ukuta ilisimama gari aina ya Noah mita kadhaa kutoka lilipokuwa geti la Nyumba hii anayoishi mrembo  Edna , baada ya gari hio kusimama , walishuka watu wanne waliokuwa wamevalia kofia nyeusi aina ya boshori ambazo zilikuwa zimewaziba uso mzima na kubakiza uso  tu , watu hawa wanne pia  walikuwa na siraha kwenye mikono yao.

Mmoja ya wale watu   aliwapa ishara kwa kuwaonyeshea ishara ya Vidole  viwili na kuonyesha upande wa kushoto , akimaanisha kuwa wawili wazunguke nyuma ya  ukuta upande wa kushoto , eneo hili lilikuwa limetulia kama  ilivyokuwa kawaida ya utulivu wa hili eneo , basi mabwana hawa walionekana kutumia nafasi hio vyema.

Wawili waliobaki wakazunguka upande wa kulia mita chache  kutoka lilipokuwa geti na kisha walirusha  kifaa flani ambacho hakikuonekana vizuri mfano wa chuma kinene na kutua kwenye nyaya za juu za ukuta  na kuning`inia  na  baada ya kufanya hivyo jamaa alimpa ishara mwenzake na  wote kwa pamoja wakaruka juu na kutua kwa ndani bila ya kupigisha kelele ya aina yoyote ile na walionekana kuwa wataalamu.

Edna wakati akiendelea kuangalia mandhari ya usiku ya bahari  , alijikuta akigeuza  shingo na kuangalia upande wa getini na hapo ndipo alipoona watu wakiruka ukuta na moyo wake kupiga paa.

Wakati akiendelea kuwa katika hali yake ya mshangao , majambazi yale yaliinama kwa ustadi mkubwa na kunyata  kuelekea upande  ilipokuwa nyumba ya walinzi  na kwa eneo ambalo Edna alikuwa amesimama , alikuwa akiona vyema kilichokuwa kikiendelea licha ya kwamba taa za eneo la getini zilikuwa zikitoa mwanga hafifu, walinzi waliokuwa eneo la getini ni kama walikuwa wamezubaa kwani ile wanataka kufanya shambulizi walikuwa washafikiwa kitaalamu kabisa na kugongwa shingoni na kulazwa chini na  yote hayo yalikuwa yamefanyika kwa wakati mmoja kati ya mabwana wale wawili waliozunguka upande wa kulia na wale waliokuwa wamezunguka upande wa kushoto na wote wakawa wamekutana  getini  na walikuwa washakamilisha kuwaweka chini walinzi wote  wanne waliokuwa wakilinda nyumba ya Edna.

Upande wa Edna ni kama sasa akili yake imerudi na kuanza kufanya kazi kwani alijikuka akijisema.

“Majambazi!!!”Aliongea Edna kwa mshituko.

Previoua Next