Edna ile anataka kugeuka kukimbilia ndani kufuata simu ili apigie polisi mara muda huohuo, bila ya kueleweka imetokeaje , waliingia wazungu wawili mmoja mwanamke na mmoja mwanaume walitokea hewani na wakatua kitaalamu kabisa ndani ya eneo hili la ndani , wale majambazi yaliokuwa yamevalia maski yaligeuka na kushangaa uwepo wa watu waliongia ghafla na kujiandaa kwa mapigano , lakini mabwana hawa walionekana kukosa spidi , kwani ile wananyanyua bastora zao zilizokuwa mikonni walifikiwa kwa spidi ya hali ya juu kabisa na siraha zile zikaenda pembeni na haikuishia hapo tu, walipigwa kitaalamu tumboni na shingoni kwa mapigo ambayo hayakueleweka ni Karate au ni Kungfu kwani walijikuta wote wakiona nyotanyota na kudondoka chini.
Kwa namna walivyodhibitiwa na wazungu hawa ilikuwa ni ya kushngaza kwani spidi iliotumika haikuwa ya kawaida kabisa maana wazungu walikuwa ni wawili lakini wao walikuwa ni wanne na licha ya wingi wao walidhibitiwa ndani ya sekunde mbili tu.
Baada ya wazungu wale kuona wamefanikiwa kuwadhibiti majambazi walibeba wale majambazi mmoja mmoja na kufunfua geti na kutoka nayo nje na hali ikawa imetulia kama kawaida kama hakuna kilichokuwa kimetokea Zaidi ya Derick na walinzi wenzake kuwa katika hali ya kuzimia.
Lakini sasa wakati yote hayo yanatendeka Edna aliekuwa juu ya Balconi aliweza kushuhudia kila kitu , kilichokuwa kimetokea , hakuelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea kwa wakati mmoja , alichokifanya ni kukimbilia ndani na kuchukua simu yake na kupigia polisi.
Na wakati huo huo akashuka mpaka sebuleni na kumkuta Bi Wema ambaye hakujua hata nini kilitokea getini kwani alionekana kunogewa na tamthilia ya kimexico ilikuwa ikonyeshwa ITV.
“Miss kuna nini?”Aliuliza baada ya kumuona Edna anashuka mbio mbio.
“Bi Wema kuna majambazi yameingia ila nimeshindwa kuelewa kilichotokea”
“Yako wapi hayo majambazi?” Aliongea kwa kupaniki lakini Edna alishindwa kuongea , woga ulikuwa umemvaa na muda huo huo gari ya polisi iliingia , na ilikuwa imewahi kweli kuliko ilivyokuwa mategemeo ya Edna, baada ya Edna kuona polisi wamefika alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.
“Nini kimetokea hapa?”Aliuliza afande aliejitambulisha kama Koplo Juma aliekuwa ameambatana na polisi wenzake watano na Edna alielezea kilichotokea na polisi hawa walishangaa lakini pia waliweza kuamini kwani Derick na wenzake bado walikuwa ndio wanaanza kurejewa na fahamu baada ya kupulizwa na maji ya ubaridi huku wakionekana kuwa na maumivu shingoni.
Kitendo cha Edna kumaliza kuongea namna ya tukio lenyewe lilivyotokea Bi Wema alipata kujua sasa tukio zima na akili yake ikasimama kwenye neno ‘Mzungu’.
Polisi wale baada ya kuona hawakuwa na cha ziada hapo ndani na hakuta uharibifu wowote uliotokea waliaga na kuondoka huku wakiahidi wataendelea kulifanyia kazi swala hilo na kuwatoa hofu.
“Itakuwa ni walinzi wa Roma”Aliongea Bi wema na kumfanya Edna kushangaa.
“Walinzi gani Bi wema Roma kaleta?”
“Jana wakati anaenda kazini aliniambia kama kuna wazungu watakuja hapa niwaruhusu kufanya mambo yao kwani ni maswala ya kiulinzi na akaniambia hakuna haja ya kukuambia lakini nilisahau na pia hawakutokea kama alivyosema”
Aliongea bi wema na kumfanya Edna ashangae Zaidi na kutoka tena nje na kumfuata Derick na kumuuliza kama Roma jana aliacha maagizo yoyote kuhusu kuja kwa wazungu na Derick alisema ndio alitoa maagizo hayo na hapo ndipo sasa akili ya Edna ilianza kufunguka na alijua sasa wale waliowadhibiti majambazi huenda ni Wazungu ambao Roma alileta , lakini swali likabaki kwenye kichwa chake , Roma kawezaje kuleta wazungu.
****
Yoshida alionekana kuwa tayari kupigana na Roma na alichokuwa akisikiliza ni oda ya bosi wake tu , lakini licha ya kuonesha kutaka kupigana kwa Roma hakuonesha mabadilio yoyote na aliishia kutabasamu baada ya kuangalia mwili wa kimazoezi wa Yoshida.
Tikayi hakuwa na wasiwasi na Roma kabisa ,alijua kabisa ataweza kumdhibiti na ndio maana alimpa ishara Abu waondoke na kazi wataimaliza vijana wake.
“Nani kasema mnaweza kuondok?a”Aliongea Roma kwa sauti na kumfanya Tikayi pamoja na Abu wasimame huku Tikayi hakuwa hata na wasiwasi lakini kwa Abu alionekana kuwa na wasiwasi , licha ya kwamba alishawahi kukutana na mziki w a Roma lakini hakuwa akijua uwezo wake halisi.
“Unaonekana kujiamini sana Bwana Roma , lakini ni bahati mbaya kwamba leo hauwezi kutoka mahali hapa pamoja na huyu mwanamke , mmeona mambo ambayo hamkupaswa kuona”
Aliongea Tikayi na ile anamaliza kuongea haikueleweka Roma alimpita vipi Yoshida , kwani tayari alikuwa mbele ya Tikayi , lakini tofauti ni kwamba leo hii macho yake yalikuwa kawaida tu.
“Umekosea sana kutujumlisha kwenye mpango wako , kwanza kabisa nikwambie tu nilikuwa nishafahamu kuna drama iliokuwa ikiendlea kati yako na kaka yako , lakini jambo lililoniuzi ni kuagiza watu waje kutudhuru”
Aliongea Roma huku akiwa siriasi na Tikayi alishangazwa utambuzi wa Roma mapema , lakini muda huo huo kabla hajaongea chochote Yoshida huyu hapa na panga lake linalowakawaka likiwa hewani kama vile kwenye muvi za wakorea akiwa na dhamira ya kumdhuru.
“Romaa.. angalia”
Ilikuwa ni sauti ya Doris akiongea kwa kupaniki baada ya kuona Yoshida anataka kumfyeka Roma na panga lake , lakini ile panga linamkaribia Roma karibu na Tumbo alilishika kwa mkono wa kulia bila ya kujali kama ameshika upande ambao ulikuwa na makali na kisha akalipindisha kwa nguvu kwa spidi ya hali ya juu na palepale panga likakatika vipande viwiwili na kumfanya Yoshida ashangae huku damu zikiwa zinatoka kwenye mikono ya Roma , lakini pia Yoshida hakuwa mzembe kwa kutumia kipande kilichobaki kwa spidi kabisa alizungusha na kupeleka usawa wa shingo ya Roma huku akiwa hewani na ile anafikisha sentimita kama kumi na tano kutoka kwenye shingo ya Roma alijikuta kile kipande kingine kikizama kwenye koo lake na kutokezea upande mwingine , jambo ambalo lilimfanya Dorisi mwili kuwa wabaridi na huo ukawa mwisho wa Yoshida.
Baada ya wale walinzi wengine waliokuwa wamesimama mita kadhaa kutoka mlangoni kuona Yoshida mkuu wao kashakufa waliinua bastoa zao na kuanza kumlenga Roma na hapa ndipo kila mmoja alijikuta akipatwa na kiwewe kwani Roma ni kama alikuwa akijua ni nani anavuta triga na kuachia risasi kwani alikwepa risasi nne kwa ustadi mkubwa sana kiasi kwamba Tikayi hakuamini.
“Nachukia sana bunduki”Aliongea Roma kwa sauti nzito sana kama Roboti huku akiwa ameinamisha uso wake chini na hio ni mara baada ya kukwepa risasi ya tano , lakini sasa sauti yake ya awamu hii haikuwa ya kawaida na kumfanya Dorisi atoe mshangao na kumwangalia Roma , na haikuwa kwake tu hata Abu na wengine wote walikuwa kwenye mshangao.
Roma bado alikuwa ameinama chini vilevile huku mwili wake ukianza kutingishika kama mtu anaepandisha mashetani na hakuna aliekuwa akielewa Roma alikuwa akifanya nini na walianza kushangaa Nguo alizovaa Roma zikianza kuloana huku mwili wake ukitoa mvuke mwingi kama sufuria iliokuwa ipo jikoni.
“Mnashangaa nini mpigeni Risasi”Aliongea Tikayi kwa kijapani huku akianza kupiga hatua kuelekea mlangoni baada ya kuona hapa ndani hapakaliki , lakini kitendo cha kufumba na kufumbua Roma kama jini vile alipotea na kuibukia mlangoni.
“Nani kasema unaweza kuondoka”
Ilikuwa ni sauti nzito sana ambayo ilisababisha mwangwi , yaani Roma aliongea mara moja lakini sauti ilisikika mara mbili katika masikio ya watu wote waliokuwa hapa ndani ,Tikayi ile anainua macho na kumwangalia Roma alijikuta akidondosha begi la hela alilokuwa ameshikilia na hakuelewa mkojo ulitokea wapi kwani alihisi majimaji ya moto yakishuka kwenye mapaja yake na hio ni mara baada ya kushuhudia macho ya Roma yaliokuwa ya kijani huku yakiwa na michirizi ya damu iliokuwa ikionekana kabisa na sio kwa Roma , kila mtu alianza kutetemeka huku mwili wa Roma ukiendelea kutoa mvuke ambao ulisababisha aina flani hivi ya Harufu kama nailoni inachomwa jikoni kwenye moto.
“Paaa.. paaa , khaaa...”
Ilikuwa ni milio ya risasi zilizokuwa zikirushwa kuelekea alipokuwa amesimama Roma , lakini ni kama walikuwa wakipiga hewa kwani hakukuwa na risasi hata moja iliompata Roma zikaishia kwenye mlango na ni kama walikuwa wamepandisha mashetani ya Roma kwani palepale ni kama muvi iliokuwa ikipelekwa mbele Roma alionekana akiwaadhibu wale walinzi kwa spidi sana huku akiwavunja shingo na alitumia sekunde therathini tu walinzi wote walikuwa wapo chini wakiwa hawana uhai.
Dorisi hakuwa akiamini kama mtu aliekuwa mbele yake ni Roma aliekuwa akimjua , mwanaume ambaye alimsababishia hata kudiriki kufanya nae mapenzi ndani ya ofisi , alionekana hakuwa ni mwenye kuamini kile alichokuwa akikiona mbele yake na haikuwa kwake tu Abu na Tikayi walikuwa wamebaki na Bumbuwazi huku suruali zao zikiwa zimeloa kwa mbele walikuwa kwenye woga usiokuwa na kifani na kuzidiwa hat ana Dorisi ambaye hakuonesha woga mwingi ila alikuwa na wasiwasi huku machozi yakiwa yanatiririka kwenye mboni za macho yake.
Roma aligeuka kama Roboti baada ya kumaliza kudili na walinzi na sasa alisogea taratibu kumuendea Tikayi , Roma alikuwa akipiga hatua moja mbele na Tikayi alikuwa akipiga hatua mbili kinyume nyume na ile Roma anaongeza hatua Tikayi aligeuka na kuanza kukimbia , lakini sasa ni kama alikuwa amesahau mlango kwani kule alikokimbia ndio ukuta ulipokuwepo na kufika ukingoni.
Kwa upande wa Abu ni kama alipata upenyo kwani alichomoka kama mshale kuelekea nje na Roma aligeuka na kumwangalia akitokomea lakini hakuwa na habari nae.
“Romaaa…!!”Ni sauti ya Dorisi iliojirudia rudia kama mwangwi kwenye masikio ya Roma na kumfanya ageuke na Dorisi alimwangalia kwa woga na kutingisha kichwa akimuoneshea ishara ya kwamba asifanye anachotaka kufanya na Roma aliongekana kumuelewa na hapohapo mwili wake ulipoa ghafla na mvuke kukauka lakini kiini cha macho yake kilikuwa hakijabadilika.
Roma alimwangalia Tikayi aliekuwa amedondoka chini akitetemeka miguu kwa woga.
“Naomba unisamehe?”
“Ulifikiri ni rahisi hivyo mimi kusamehe”.
“Hapana naomba unisamehe , nitafanya chochote unachotaka”Aliongea kwa pupa huku akipiga magoti kama ilivyokuwa kwa kaka yake.
Roma sasa alionekana kurejewa na fahamu zake za kawainda ,kwani licha ya kwamba rangi ya macho yake ilionekana kuwa ya kijani bado , lakini ilikuwa imefubaa.
“Siwezi kukusamehe kirahisi hivyo , napaswa kukuua hapahapa kwa kuvuka mipaka , sipendi kutishiwa kwenye Maisha yangu
Comments