Tikayi kwenye Maisha yake hakuwahi kuwaza kama anaweza kukutana na mtu anaebadilika kama ilivyokuwa kwa Roma , alijiambia katika akili yake kwamba katika siku zote alikuwa amefanya makosa na kumgusa mtu ambae hakupaswa kuguswa basi ni bwana aliekuwa mbele yake, aliamini ana asilimia ndogo sana za kutoka hapo ndani akiwa salama , akili yake ilikuwa ikifanya kazi kama mashine , alimwangalia Roma ambaye awamu hii alikuwa anaonekana kawaida na nikama alikuwa haamini kama mtu aliekuwa mbele yake dakika kadhaa zilizopita alikuwa kiumbe cha kutisha kilichojaa ukatili.
“Utachukua asilimia sitini za faida ndani ya mkataba wa kibiashara tutakaofanya”Aliropoka Tikayi na kumfanya Dorisi ashangae , kwani katika mkataba huo wa kibiashara walikuwa wakichukua asilimia therathini tu na JR asilimia ishirini huku Yamakuza wakichukua asilimia hamsini, hivyo Dorisi kusikia hivyo moyo waka ulipiga kite na kuona dili hilo litakuwa nono kama tu wangelikubali
“Unadhani ninaweza kukuacha hai kwa asilimia sitini?”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida na Tikayi akamwangalia Roma kwa wasiwasi.
“Asilimia hizo ni nyingi sana ndani ya kampuni yenu kutokana na uthamani wa Material”
“Umefanya makosa mangapi , isije ukawa unapendekeza asilimia sitini lakini hata makosa yako huyajui”
Tikayi alinyanyuka na kupiga magoti , huku akianza kufikiria ni makosa mangapi alikuwa amefanya na kisha akamwangalia Dorisi aliekuwa akimwangalia kwa wasiwasi na Tikayi ni kama alikuwa akitaka kuomba msaada kwa Dorisi.
“Nimefanya makosa matatu”
“Yataje niyasikie”
“Kwanza kabisa nilipanga kuwaua wewe na Dorisi kule nyumbani , pili nikataka kukuaa hapa ndani ,tatu….”Alianza kujikuna kichwa akifikiria ni kosa gani tena ambalo alikuwa amelifanya , lakini hakuelewa alikumbuka katika makosa yote alitaka tu kumuua Roma.
“Umenikosea halafu hukumbuki makosa yako , sasa nasema hivi mimi Roma Ramoni siwezi kukuacha hai leo na nakupa dakika moja tu unishawishi nisikuue na kama unajiona huwezi kunishawishi niambie niivunje shingo mapema tu nisipoteze muda wangu, mimi kuua kwangu ni jambo jepesi sana”
Aliongea Roma huku akionekana kuwa siriasi na Tikayi alijikuta akikumbuka macho ya Roma dakika kadhaa zilizopita na mwili wake ukahisi ubaridi wa hali ya juu sana wa woga.
Dorisi alishindwa kuongea chochote , alitamani kumwambia Roma wakubaliane na asilimia Sitini alizotaja Tikayi lakini alishindwa kuongea , hakuelewa kwasababu gani, lakini alikosa hali ya kujiamini kuongea na Roma.
“Bado Sekunde kumi”aliongea Roma huku akiendelea kumuangalia na Tikai hakujua ni namna gani anaweza kumshawishi Roma asimue.
“Tatuuu ….mbiliii ….”
“Kosa lingine tulitaka kuwasainisha mkataba feki”Aliongea Tikayi kwa kukurupuka na kumfanya Roma atabasamu na Dorisi macho yalimtoka , hakuelewa alichozungumza Tikayi kina ukweli ndani yake.
“Wewe na nani mlitaka kutusainisha mkataba feki, nataka maelezo yalionyooka la sivyo nitakunyonga hapahapa na Japani yote hii hakuna atakae kuwa na uwezo wa kunigusa”Roma alionyesha hasira zake waziwazi na kumfanya Tikayi kuanza kuogopa.
“Black Mamba kupitia muwakilishi wao Abubakar”Dorisi alizidi kushangaa na hakuelewa Black Mamba ni mtu gani , lakini kwa Roma alikuwa ashasikia sana hili kundi na pia alikumnbuka Karimu ndio aliekuwa kiongozi wa kundi hilo na baada ya kusikia maneno haya kutoka kwa Tikayi alijua Black Mamba walikuwa wakitafuta namna ya kulipiza kisasi kupitia kampuni ya mke wake , alijikuta akikasirika na kujilaumu kwanini alimuachia Abu akimbiena hakumua , lakini alijiambia katika nafsi yake atamkamata tu na kifo kitamuhusu.
“Kwa hio unamaanisha swala lote la Mkataba kati ya Yamakuza na kampuni yetu , yote yalikuwa ni uongo na hakukupaswa kuwa na mazungumzo ya aina yoyote yale ya kibiashara baina yetu?”Aliuliza Dorisi na hio ni baada ya Roma kumueleza kinachoendelea kwa kutafsiri maneno ya Tikayi.
“Kuhusu Material Mapya ni biashara ya kweli , lakini kuhusu material hayo kusambazwa na kampuni ya Vexto hakuna kitu kama hiko, kampuni ambazo tulichagua kufanya nayo kazi kwa Tanzania ni Maple Group na JR Group na mkataba halisi ulipangwa kusainiwa siku tatu mbele baada ya kusaini na nyie mkataba feki a kuhakikisha mmetupa kiasi cha pesa ambacho kipo kwenye mkataba”
Aliongea Tikayi na kumfanya Dorisi kushangaa mno , lakini sio kushangaa tu aliogopa kwa wakati mmoja , kwani kama angesaini huo mkataba na kisha wakaruhusu kiasi kikubwa cha pesa kikatoka kwenye kampuni na baada ya hapo wakagundua kuwa mkataba ulikuwa ni feki huenda Vexto Grupu ingefilisika rasmi,Dorisi alimwangalia Roma na kuzidi kushangaa na aliamini hata kama angekuja Edna mwenyewe Japani huenda asingegundua jambo hilo.
“Sasa Bwana Tikayi nyie na hawa Black Mamba mna uhusiano gani na kwanini mkubaliane nao kwa ajili ya kusaini mkataba feki na kampuni yetu , ilihali swala hili huenda lingewaletea matatizo mbeleni?”
Tikayi alifikiria kidogo na kisha akakaa chini kabisa kwani alionekana kuchoka kwa kutumia magoti na hakujali uchafu uliokuwa chini na kisha akamwangalia Roma kwa wasiwasi ,Tikayi hakuwa na namna , aliona bila ya kusema ukweli asingeweza kutoka kwenye mikono ya Roma.
“Black Mamba ndio wasambazaji wakubwa wa madawa yetu ya kulevya kwa Afrika Mashariki yote kwa Zaidi ya miaka kumi , lakini miaka mitatu nyuma kulitokea tatizo baada ya raisi mpya kuchukua madaraka”
“Tatizo gani?”
“Njia ambayo tulikuwa tukitumia kuingiza madawa ya kulevya ndani ya Tanzania Raisi Senga aliigundua na kuizuia , lakini pia sharia zake mpya na ukaguzi mkali bandarini na njia zote za usafirishaji tulishindwa kupata Njia salama ya kupitisha madawa na kwa Afrika mashariki soko kubwa la madawa lipo Tanzania , hivyo uongozi wa senga ulifanya mapato ya biashara kushuka kwa kiasi kikubwa san ana hapo ndipo tulipokuja na wazo la kutengeneza njia mbdala ya kuingiza madawa Tanzania”.
“Hio njia yenu inahusiana vipi na kampuni ya Vexto?”
“Vexto ndio kampuni pekee ambayo imepewa mkataba wa kudumu wa kuingiza mafuta ya petroli Tanzania kutoka India na huo mkataba unaifanya Vexto kuwa na nguvu ndani ya taifa la Tanzania”Aliongea Tikayi na kumfanya Roma ashangae kwani hilo hakuwa akilifahamu na alimgeukia Dorisi na Dorisi alitingisha kichwa kuashiria ni kweli.
“Saa kama ndio wanamkataba wa kudumu wa kuingiza Mafuta inahusiana vipi na madawa yenu ya kulevya?”
“Njia salama ya kusafirisha madawa ya kulevya duniani kwasasa ni kwa njia ya Shehena ya Mafuta”Dorisi alishangaa lakini Roma hakushangaa.
“Kwa hio mlitaka muitumie Vexto kuingiza madawa Tanzania kupitia shehena ya Mafuta wanayoingiza?”Alitingisha kichwa kuashiria ni kweli.
“Black Mamba mkuu wake ndani ya Tanzania ni nani?”
“Mkuu wa Black Mamba Tanzania simfahamu ila ninachojua ni kwamba anafahamika kwa jina la The Doni , ila muwakilishi wake mkuu ambaye mara nyingi ndie anaemuakilisha katika mazungumzo ya kibiashara ni Abubakari Juma”
Roma alijikuta akishangaa na kuwaza huyu The Doni ni nani , kwanini kila mtu hakuwa akimjua na ana nguvu gani ndani ya taifa la Tanzania , ila alijiambia atayajua yote hayo taratibu huku akijipiza moyonni akimpata lazima amvunje shingo.
“Baada ya kutusainisha mkataba feki ni kipi kingefuara baada ya hapo?”
“Mpango uliokuwepo ni kwamba kama mkataba huo ungesainiwa na ikajulikana kwamba ni feki ,Edna angekosa vigezo vya kuwa CEO , lakini wakati huo huo kampuni ingefirisika na JR Group ingeinunua kampuni ya Vexto na JR ni sehemu ya Black Mamba na mpango ungekuwa umefanikiwa kirahisi”
Dorisi alijikuta akivuta pumzi , hakuwa akijua kuwa kampuni ya Vexto ilikuwa ikikodolewa macho kwa namna hio na wafanya biashara wa madawa ya kulevya , sasa alianza kuhisi ile michakato yote ya Abu kutaka kumuoa Edna ni kwasababu ya hilo swala la uingizaji wa Madawa nchini , hakika alishangaa na kuona siku hio amejua mengi lakini pia alishukuru moyoni kwamba swala hilo la kusaini mkataba feki halikuwa limefanikiwa, maana kila alipokuwa akikumbuka nguvu na juhudi za Rafiki yake Edna kuifikisha Vexto ilipofikia aliogopa na aliona huenda Edna angechukua maamuzi magumu hata ya kujinyonga.
“Mpaka hapo bwana Tikayi umenishawishi japo bado kidogo sana , nadhani mpaka sasa unafahamu kuwa mimi na Dorisi ndio tunajua kuwa wewe ndio umemuaa Tikayeshi ndugu yako , lakini pia mpaka sasa unajua fika kwamba ulitaka kutuua , lakini pia mlitaka kutusainisha mkataba feki , Sasa wewe mwenyewe hebu kaa chini tena fikiria unadhani utanipatia kitu gani cha thamani nikusamehe?”Aliongea Roma na kumfanya Tikayi afikirie,
“Kwakua biashara ya Material mapya ni halali nitaiota JR Group kwenye mkataba na kuiingiza Vexto , lakini katika mkataba huu Vexto mtapata asilimia sitinni na Tano ya faida yote ya mauzo kwa bara la Afrika nadhani hilo sio dili baya kwa kampuni ya Vexto”
Dorisi macho yalimtoka , alitamani aseme ndio hapo hapo lakini alikumbuka dakika chache nyuma kuwa kama sio Roma wangesainishwa mkataba feki bila wao kujua. Akaona atulie na Roma amalize kila kitu.
Basi Roma alikubaliana na Tikayi kwa kusainishana mkataba mpya kati ya Maple Group na Vexto Group huku kampuni ya JR ikitolewa kwenye mkataba huo.
Roma kama kawaida yake alimpiga mkwara wa kutosha Tikayi kwa kumtishia kama tu angefanya ujinga mwingine wa kufanya janjajanja ya kumzunguka , basi angeimaliza familia nzima ya Yamamoto na kuchukua na kampuni yao na Tikayi kutokana na mziki wa Roma aliokuwa ameushuhudia kwa macho yake , alijikuta akiapia kwa majina yote hatokuja kumuuzi Roma tena na atafanya kama ambavyo wamekubaliana.
Siku iliofuata Roma na Dorisi hawakulala ndani ya Twillight villa kutokana na mambo yaliotokea kati ya Tikayi na Roma , lakini pia familia hio ilikuwa kwenye maombolezo ya msiba wa Tikayeshi ambaye alikuwa ameuliwa na mdogo wake Tikayeshi na kuhusu Tikayi kumuua kaka yake lilimalizwa kifamilia na hakukuwa na taarifa yoyote iliotolewa Zaidi ya kutangaza kuwa ni ajali ambayo ilitokea na kumuua Tikayeshi.
Dorisi aliwasiliana na Edna na kumpa taarifa ya kile kilichokuwa kimetokea na Edna alifurahishwa sana na taarifa hio huku akiahidi zawadi kwa wawili hao watakaporudi nchini.
Mkataba ulikuwa ukisainiwa siku mbili mbele lakini kabla ya kusainishana mkataba huo viongozi wa Maple Group walitakiwa kufika nchini Japani kwa ajili ya mazungumzo hayo ya kibiashara lakini pia kukagua miundo mbinu ya kiwanda ambacho kitakuwa kikitumika kutengenezea material hayo mapya.
Ni saa Moja za jioni ndani ya uwanja wa Kansai Tikayi alikuwa eneo la mapokezi la kufikia wageni akimsubiria mgeni atakaeiwakilisha Maple Group katika kusainishana mkataba mpya.
Baada ya kusubiria kwa takribani nusu saa akiwa na walinzi wake , hatimae eneo la kutokea wageni alionekana mwanamke mrembo akiwa anatoka huku akiwa amependeza sana , mwanamke huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Naibu waziri wa Sanaa , mheshimiwa Neema Luwazo.
Comments