Reader Settings

Neema Luwazo waziri wa Sanaa kutoka Tanzania alionekana kufurahia ukaribisho kutoka kwa Tikayi kwani muda wote alionekana kuwa na uso uliokuwa umepambwa na tabasamu.

“Licha ya kwamba  swala hili la kibiashara   lilikuwa ghafla kwangu baada ya kuvuta tarehe nyuma  , lakini nafurahi sana kufanya kazi na kampuni yenu”Aliongea Neema  baada ya kuingia kwenye gari ile ile iliowapokea Dorisi  na Roma Caddillac Limuosine

“Hata sisi pia kama kampuni  tunafuraha kubwa sana kufanya kazi na Maple grupu , karibu tena Japani kwa mara nyingine”

“Nashurkuru sana , sio mara yangu ya kwanza kufika Japani  lakini ni mara yangu ya kwanza kufika hapa Osaka , unaonekana kuwa mji mzuri sana , nimezoea kufika Tokyo mara kwa mara katika  safari zangu zote za kibiashara”

“Ndio Osaka ni mji mzuri sana  na  una utulivu wa hali ya juu”Alijibu Tikayi kwa kingereza safi na safari iliishia  katikati ya mji huu kwenye hoteli iliokuwa ikifahamika kwa jina la W Osaka Luxury one  ni moja ya hoteli nzuri sana na ya bei ghali ndani ya jiji hili la Osaka usiku mmoja tu ni milioni nne za kitanzania.

“Wow! Its so amaizing hereTikayi”Aliongea Neema huku akifurahishwa na mandhari mazuri yaliokuwa ndani ya hili eneo na alishindwa kuzuia furaha yake na Tikayi alitabasamu na kumuongoza  ndani.

Ni Siku nyingine ndani ya makao makuu ya kampuni ya Yamakuza  kwenye ukumbi  mkubwa wa mikutano ,  walionekana viongozi wa juu kabisa wa kampuni wakiwa wameizunguka meza  , lakini pia kwenye meza hio  alionekana mwanadada Neema luwazo alievalia vazi lake la suti akiwa ameketi kwenye nafasi yake , huku pembeni yake kukiwa na viti viwili ambavyo vilikuwa wazi ni kama watu ambao walitarajiwa kukaa kwenye  viti hivyo ni kama walichelewa , kwani watu wote walikuwa washawasili  akiwemo Tikayi ambaye siku hio ndio alieonekana kuongoza mazungumzo yote yaliokuwa yakihusu  mkataba wa biashara  kati ya kampuni  ya Yamakuza Corporationi`s na  kampuni mbili kutoka Afrika yaani Maple group ambayo ilikuwa ikiwakilishwa na Neema ambaye  ndie alikuwa mmiliki na mwenyekiti wa kampuni hio , lakini pia Dorisi na Roma ambao ndio walikuwa wawakilishi wa kampuni ya  Vexto International.

Dakika chache mbele  mlango wa  chumba hiki cha mikutano ulifunguliwa na akaingia  mrembo Dorisi akiwa ameambatana na Roma Ramoni , wawakilisi wa  kampuni ya Vexto.

Kila mmoja macho yalikuwa kwa wawili hao  na kwa jinsi walivyokuwa wamependeza ni kama vile walichelewa makusudi ili kujionyesha ,  viongozi hawa wajuu walikuwa wanawaangalia Dorisi na Roma kwa namna ya macho ya kitathimini  , upande mwingine  mwanamama Neema Luwazo jicho lilikuwa limemtoka mara baada ya kumuona mtu ambaye hakuwa amemtarajia kumuona , tena kwenye nchi ya mbali kama hii ya Japani.

“How This possible?”

Alijiwazia huku akiendelea kumuangalia Roma ambaye kama kawaida yake , alikuwa akijiamini mno kiasi kwamba hata watu walijiuliza ni ninni kinamfanya   kujiamini kwa namna hio , kwani kwa Roma watu waliokuwa mbele yake ni kama alikuwa akiwafahamu wote.

Dorisi akiwa nyuma Roma alitangulia  na kuelekea upande ambao ndio nafasi zao zilikuwa zimeandaliwa , wakati wote huu Roma hakuwa amemuona Neema bado mpaka pale alipofikia kiti ndipo alipomuona mwanamke ambaye kwa kumuangalia tu kumbukumbu zake zilimrudisha ndani ya taifa la Tanzania kwenye hoteli ya New Afrika akiwa amemkunja kisawasawa  lakini sio kwa Roma tu aliemuona Neema hata pia kwa Dorisi alimtambua mara tu baada ya kumuona na alionyesha waziwazi kutofurahia uwepo wa mwanamama huyo hapa ndani.

“Mrembo ni wewe?”

Aliongea Roma mara baada ya kumfikia huku akivuta kiti kwa ajili ya kuketi , lakini Neema alishindwa kuongea chocote kwani muda wote alikuwa akimwangalia Roma kwa mshangao  mpaka pale Tikayii alipoanza kuongea na kufungua kikao hiko.

Tikayi alionekana kujiamini sana , lakini kila alipokuwa akikutanisha macho na Roma alijikuta akikosa utulivu na hali  hio  Roma na Dorisi waliishuhudia  na Roma alimkonyeza Tikayi na akatabasamu na kuendeleza kikao.

Baada ya utangulizi wa ajenda za kikao hiko kuhusu mkataba wa kibiashara juu ya uzalishaji wa material mapya ambayo  kama kampuni walikuwa wakiamini yanakwenda kuweka historia kimauzo  , ilifikia wakati ambao sasa   watafiti wa kampuni ya Yamakuza ambao ndio waliokuwa wakihusika kwa asilimia miamoja na gunduzi  ya material hayo , walitakiwa kutoa ‘representation’ kwa ufupi.

Na Tikayi alichukua nafasi hio  kumkaribisha kiongozi wa juu wa utafiti   kuingia ndani ya chumba hiko cha mkutanao kwa ajili ya jambo lililokusudiwa na baada ya kutoa ukaribisho mlango ulifunguliwa na akaingia  kijana mmoja wa kijapani mrefu mwembaba  aliekuwa na nywele ndefu lakini zilizokuwa na staili flani hivi kama  wigi, alikuwa ni kijana wa makadirio ya umri kati ya miaka  si chini ya ishirini na Tano ,bwana huyu alijitambulisha kwa jina la Mori Satoshi.

“Kabla sijaanza kutoa  taarifa  juu ya Project hii ambayo imenichukua miaka mingi kufanya utafiti na majaribio mpaka kuikamilisha   naomba kwa heshima kubwa nimtambulishe mwalimu wangu ambaye alikuwa na mimi bega kwa bega katika masomo yangu ndani ya chuo kikuu cha Oxford  Dr Clark Stephanie”

Aliongea Mori na hapohapo mlango ukafunguliwa na akaingia mwanadada ambaye  alimfanya Roma atoe macho.

Alikuwa ni mwanamke mzungu mrembo sana wa kuvutia  mno  kwa muonekano wake , mwenye  muonekano ambao ukiangalia utagundua kuwa  alikuwa na umri mdogo sana  na hii ilifanya  watu wengi hapa ndani  kushangazwa na mtu ambaye anaitwa Profesa n ani  mwalimu wa Mori kuwa ndio huyo mwanamke.

Profesa Clark alijikuta macho yakimtoka mara baada ya kukutanisha macho na Roma  ni kama mtu ambaye hakutegemea kumuona mtu huyo hapo ndani na mshangao wake ulifanya  watu hapa ndani kuangalia upande ambao macho ya Profesa clark yalikuwa yameelekea  na wote wakagundua kuwa Profesa alikuwa akimwangalia Roma na huku Roma baada ya kuona macho ya Profesa yanamwangalia  aliinua mkono  na kumpungia huku akiachia tabasamu pana usoni na hapa ndipo watu walizidi kushangaa ,sio Dorisi na Neema waliokuwa wamekaa karibu na Roma ,lakini pia Mori mwenyewe aliemleta profesa wake hapo ndani alikuwa kwenye  mshangao na pia Tikayi alikuwa kwenye mshangao.

Baada ya  hali hio ya mshituko kupita  Profesa Clark  alianza kuitambulisha.

“I am renowned  Professor Clark Stephanie, it has been an honor for me to attend this session which involves the success of my student Mori in his research which has led to development of new materials,

Despite having a tight schedule, it's a pleasure for me to be able to listen to what Mori prepared, but I'm also happy to meet each of you”.

“Mimi ni Profesa maarufu ninaefahamika  kwa jina la  Profesa Clark Stephanie , ni heshima kwangu kupata nafasi ya kuwa moja ya wahudhuriaji wa kikao hiki  ambacho kinahusisha  taarifa ya mafanikio ya Utafiti wa   mwanafunzi wangu Mori , ambao umepelekea kupatikana kwa Material mapya, licha ya kuwa na ratiba iliobanana ni furaha kwangu kusikiliza kile Mori alichoandaa na pia nimefurahi kukutana na kila mmoja hapa ndani”

Aliongea kwa kujiamini kabisa , huku akionyesha ile hali flani ya mtu kujiamini anapokuwa na mafanikio makubwa.

Kila mmoja alivutiwa na sauti ya mrembo huyu na kutamamani waendele kusikiliza.

“Huyu ndio Princess wa Wales ,Mtoto wa malkia Catherine Steohanie”

Walinong`onezana mabwana wawili kwa lugha ya kijapani wakati huo Profesa Clark akienda kukaa sehemu ambayo iliandaliwa,lakini mwanadada huyu mrembo macho yake yote yakiwa kwa Roma, ambaye alionekana kuanza kuchoka kukaa hapo ndani.

Ukweli utofauti kati ya Edna Clark likija swala la uzuri kama utawalinganisha Profesa Clark na Edna  wameachana kidogo sana , na kitakachombeba Edna Zaidi ni umbo.

Basi kikao kiliendelea kwa takribani   saa moja na nusu jambo ambalo kwa Roma ni kama hakuwa akielewa kile kinachoendelea na kujiamulia kulala zake kwa kujiinamisha kwenye kiti huku akibenua kichwa  juu na kufanya koo lake lionekane na hata pale alipokuwa akimeza mate Neema na Dorisi waliokuwa  wamekaa pembeni yake walikuwa wakiona misuli ikipishana.

Waandishi walikuwepo  ndani ya jengo hili refu la kampunni ya Yamakuza na kila kilichokuwa kikiendelea kilikuwa kikinakiliwa  kwa ajili ya matangazo na hio ni moja ya mbinu ya kufanya kampuni  ambazo zipo katika mfumo wa ‘Trading’ Hisa zao kupanda.

****

Edna leo hii alikuwa ndani ya kampuni yake ndani ya ofisi yake huku  macho yote yakiwa kwenye  chati  ya ‘Candlestick’ ya soko la hisa ambayo ilikuwa ikishuka na kupanda . Katika  tarakishi yake alikuwa amegawanya sehemu mbili.

Sehemu ya  kwanza kulikuwa na  chati iliokuwa ikionesha graph  ya kampuni ya  JR Group na upande wa pili ilikuwa ikionesha chati ya kampuni yake.

Utofauti wa hizi graph ni kwamba  kuna ambayo ilikuwa ikishuka na kuna ambayo ilikuwa ikipanda , graph ambayo ilikuwa na mstari wa kushuka ni ya kampuni ya JR  na hii iliashiria  hisa za kampuni hio zikishuka thamanni tena kwa  spidi kubwa lakini upande mwingine hisa za kampuni ya  Vexto zikipanda thamani kwa siku hio , hali zote mbili zilionekana kumfurahisha sana Edna   na alichukua simu yake iliokuwa kwenye meza na kutafuta namba ilioandikwa kwa jina la ATHENA  na kisha akapiga.

“I think with the ongoing situation you know what to do Amiri?”

“Yes! Madam”.

“Okay!, look at the Dow Jones Line for today when it get to the lowest point where we intended to, initiate the plan”.

“Angalia Mstari wa Dow jones kwa siku ya leo ukifikia point ambayo ndio tumekusudia , Anzisha mpango wetu”

“Rest Assured Madam , leave everything to us”

“Kaa kwa kutulia Madam , tuachie kila kitu sisi”

Sauti ya mwanaume ilisikika upande wa pili ,  mwanaume ambaye Edna alimtamka kwa jina la Amiri.

Baada ya Mrembo huyu ambaye alikuwa akionekana kiprofesheno Zaidi baada ya kuongea na simu yake aliendelea kukodolea macho tarakishi yake  na kutabasamu  lakini muda huo huo mlango ulifunguliwa na akaingia mrembo Nasra akiwa amependeza kama kawaida huku mkononi akiwa ameshikilia kishikwambi(Tablet).

“Boss Taarifa ya kampuni yetu kutoka japani ipo mtandaoni”

Aliongea Nasra huku akimpatia Tablet   alioshika mkononi na Edna aliichukua  na kuangalia picha mbalimbali zikimuonesha Roma na Dorisi wakipeana mikono na wafanyakazi wa kampuni ya Yamakuza.

Edna alishindwa kuzuia tabasamu lake mara baada ya kumuona mume wake kwenye picha hio huku moyo wake ukipata  kajimsisimko  flani hivi ambako mwenyewe ameshindwa kukatafsiri kwani kalisafiri kuwanzia kichwani na kwenda kuishia katikati ya mapaja.

“Boss  nadhani  huu ndio mkataba ambao kampuni imeufanikisha tokea kuanzishwa kwake  , shukrani ziende kwa Roma na Dorisi walioweza kupata asilimia kubwa za gawio la Faida”Aliongea Nasra  huku akimwangalia Edna.

“Hakika Nasra lakini haya yote ni juhudi za kila mfanyakazi wa Vexto nitahakikisha tunaendelea kusaini mikataba  mikubwa zaidi na kuipanua hii kampuni  duniani kote”.Nasra alitabasamu na kisha akasema:

“Nadhani muda si mrefu Forbes watakutoa kwenye nafasi  yako ya mwanamke tajiri  duniani uliopo na kukupandisha juu Zaidi , kutokana na mauzo ya hisa ya leo yanavyopanda,natamani Madam Rahel angekuwepo hai  Edna”Aliongea Nasra huku machozi  yakianza kutoka, machozi ya huzuni.

“Ni kweli Nasra , unaonekana kummiss sana Mama eti eh?”

“Huwezi amini Edna kwenye siku mbili hizi   nilikuwa nikimuota  kwenye ndoto , nammissi kila siku , wema wake alionitendea kwenye Maisha yangu umemfanya kuwa mtu muhimu sana kwenye Maisha yangu”

Edna alitabasamu na kutoka kwenye meza yake  na kisha akamsogelea Nasra na kumkumbatia huku na yeye akitoa machozi na walionekana kufarijiana.

Upande mwingine hapa  ndani ya jii la Dar kwa upande wa  Masaki alionekana mzee Alex akiwa kwenye Runinga huku akiwa na mtoto wake wa kike aliekua ameshikiria simu yake ya  I phone akichati huku akiwa si mwenye kuzingatia kile alichokuwa akiangalia baba yake sebuleni hapo kwani alionekana kuwa bize , lakini Ghafla mzee huyu alirusha  rimoti kwa nguvu na kuipigiza kwenye Tv iliokuwa ikionesha channel ya Bloomberg  , huku taarifa mbalimbali zikiendelea ikiwemo ya  kampuni ya Vexto international  kusaini mkataba mnono na kampuni ya Yamakuza  , lakini pia wakati taarifa hio ikiwa nzuri ,pia kulikuwa na taarifa mbaya ya Kampuni ya JR kutolewa katika   mkataba huo na ilionekana jambo hili ndio ambalo lilimkasirisha sana  mzee Alex.

“Dadiii…!”Aliita mrembo huyu kwa sauti yake nyororo huku akimwangalia baba yake aliekuwa akipandisha ngazi lakini mzee alimpotezea  ,  mrembo huyu ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Queen alionekana kushangazwa na kitendo ambacho  baba yake amekifanya na alijikuta akigeuza macho yake kuangalia kwenye TV hio kubwa ya teknolojia ya OLED  na kuona taarifa  ambayo ilimkasirisha baba yake na  alijikuta akitoa kicheko kwa nguvu.

“Masikini Abuu… sijui awamu hii baba atamfanya nini?”

Aliongea mwanadada huyu kwa kufurahi huku akiendelea kuchatika kwa mapozi  mara akae uchi mara ajibinue  na simu yake hio kubwa na hakuoneskana kuguswa na chochote kilichokuwa kikiendelea kwenye kampuni ya baba yake.

Baada ya mzee Alex kuingia kwenye Ofisi yake ndani ya jumba hilo alivuta mtoto wa meza na kisha akatoa Bastora na  kuchukua funguo  na kushuka chini  na kumfanya Queen azidi kushangaa baada ya kumuona baba yake na siraha … alishindwa kuongea chochote mpaka pale baba yake alipotokomea nje na kusikilizia mngurumo wa sauti uliokuwa ukifubaa kwenye masikio yake..

“Hahahahaha…”Lilikuwa ni cheko la kishambenga la Queen.

Nini kitendelea ….. usichoke.

Previoua Next