Reader Settings

Baada ya mtiririko wa  matukio  ndani ya kampuni ya Yamakuza kuisha , hatimae   wageni walikuwa wakiagana kila mtu kurejea kwenye majukumu yake na wale ambao walikuwa ni wageni kuondoka na kuendelea na majukumu yao.

“Tunaweza kuongea  Private Pluto?”Lilikuwa ni ombi kutoka kwa Profesa Clark kwenda kwa Roma na Roma alitabasamu.

“Sawa Clark hata mimi  ninatamani kuongea na wewe  baada ya muda mrefu kutoonana , tuelekeee juu kabisa ya jengo hili nadhani ni sehemu inayofaa”

Aliongea Roma huku akiongoza njia na wakati huu  Dorisi walikuwa bize na kuagana na baadhi ya watu  lakini alimuona  Roma na Profesa Clark wakiingia kwenye lift na alishangaa , lakini sio yeye tu pia Neema Luwazo ambaye bado hakuongea neno lolote na Roma  aliliona tukio hilo , lakini pia  Mori aliekuwa akiongea na Tikayi wote kwa pamoja walimuona Profesa Clark na Roma wakifuatishana  na kuingia kweye lift na kila mmoja akabaki na swali  hao wawili wamefahamiana lini , kwani muonekano wa Roma ulikuwa wa kawaida sana kiasi kwamba hakuwa tishio lolote kwa  jamiii , yaani alionekana kama mkulima alieziotea pesa jana yake na leo kaja kuichanganya kutoa ushamba   na matajiri ambao pesa ilikuwa kama marashi kwao   na kiasi kwamba hata harufu zao zilikuwa zikitoa marashi ya kidola  dola na ki Euro , Euro.

“Nilipata taarifa  kwa mwanafunzu wangu  Ashley umepata mke pluto”Aliongea Profesa Clark aliekuwa nyuma ya Roma wakiwa juu kabisa ya gorofa hili la kampuni ya Yamakuza , kiasi kwamba walikuwa wakiliona jiji lote la Osaka , ni sehemu ambayo ilikuwa ikivuma upepo na kufanya nywele za mwanadada Clark kupepea na kumfunika uso  na kwa mapozi alikuwa akizitoa usoni na kuzidi kumfanya kuwa mrembo.

Roma  aliekuwa amefika mwishoni kabisa wa floor  ya ufuniko wa gorofa hii  alitabasamu kidogo pasipo kugeuka.

“Ndio Clark , nadhani unataarifa kama anafanana kwa kila kitu na Seventeen”.

Profesa Clark ambaye alionekana kutofurahishwa na tarifa hio alivuta pumzi na kuzitoa nywele zake ndefu  zilizojaaa usoni  na kisha kuangalia mgongo wa Roma kwa dakika  na hapohapo alifanya maamuzi na kwenda kumkutambia Roma kwa nyuma na kupitisha mikono kwa mbele huku wote wakiangalia upande wa baharini ndani ya jiji hili la Osaka na upepo ukiwa unawapuliza.

“Niliishi  kwa mateso  sana ulivyoondoka Pluto kwenye macho yangu , kila siku nilikuwa mwenye kukuwazia”Aliongea mwanadada huyu huku machozi yakimtoka na kuloanisha suti ya Roma.

“Pole sana Clark , lakini ulinipa baraka zote wakati wa kuondoka na tuliagana  , kwanini uwe katika hali ya mateso , maamuzi nilioyafanya  kipindi kile  ndio maamuzi ambayo nitayafanya pia kwa Zaidi ya mara elfu moja,Clark  nimeshaachana na kuwa mashine ya kufanyia  matajiri kazi kama mtumwa”

Aliongea Roma na hapa kama ungemuona usingedhania ni yule ambaye muda wote alikuwa akionekana kutokuwa siriasi , hapa alionekana Roma ambaye alikuwa na uchungu mkubwa lakini aliekuwa akidhirisha kile anachokiongea kwa  muonekano wake wa sura.

“Ndio najua,  najua  uliopoondoka  nilikupa baraka zote , lakini moyo wangu haukukubaliana na wewe kuniacha , niliteseka na kuwaza kila siku kuhusu ugonjwa wako  kukurudia tena , kwani dawa ambazo nilikupatia zilikuwa ni za kuutuliza tu , uliondoka katikati ya matibabu na  katikati ya utafiti wangu wa kukutafutia dawa, ni kwanini nisiwe na mawazo ilihali umekuwa mtu wa muhimu kwangu mimi na mama yangu Pluto!?”

“Kwanza ni tukiachana na  hayo  ,Catherine anaendeleaje?”

Aliongea Roma na wakati huu akiwa  washaachiana na walikuwa wote wamesimama upande upande kuangaia upande wa baharini.

“Unamkumbuka? ,yeye yupo ni mwenye kutamani  kila siku kukutana na wewe kwa mara nyingine , kila siku amekuwa wakunilalamikia kukuhusu kurudi Tanzania”Roma alitabasamu .

“Naamini siku moja tutakutana , mpe salamu zangu Clark,sidhani kama tunayo mengi ya sisi kuongea Clark mimi ni yule yule na maamuzi yangu , imekuwa jambo jema kukutana na wewe daktari wangu , umezidi kuwa mrembo”

Aliongea Roma  na kumfanya mwanadada huyu atabasamu lakini pia kuhudhunika kwa wakati mmoja.

“Mimi  siku zote nitakuwa mwenye kuwa upande wako kwa  kila maamuzi utakayo yafanya  Pluto”Roma alitabasamu na kumgusa shavu kwa namna ya kuliminya

“Okey! Clark nadhani ni muda wangu sasa wa kurudi chini , Dorisi mfanyakazi mwenzangu atakuwa ananisubiri , kwasasa nafahimika kwa jina  jipya la Roma  unaweza kuniita hivyo tukionana kwa mara nyingine , kwaheri Clark msalimie malkia Catherine” Aliongea Roma na kisha akageuka kuondoka .

“Wait..!!” Aliongea clark na kumsogelea kwa mara nyingine   Roma  na kisha alitoa Pentorch(Kalamu  za mwanga wanatumia sana madaktari) iliokuwa kwenye koti lake la suti ya rangi ya bluu na kumsogelea Roma kwa mbele.

“Naomba  angalau nione macho yako”Aliongea na Roma aliitikia kwa kichwa na kisha  mwanadada huyu alimmulika kisha akabonyeza maratatu  ile pentorch kwa kila jicho.

“Hii ni teknolojia mpya  ya  kuscan Nevu(nerve) ambayo nimeitengeneza  , inaweza kunisaidia  kujua kwa sasa hali ya ugonwa wako nitaenda kuzichambua picha nilizozipiga hapa” Aliongea na kisha aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti na kutoa  mkebe mwingine na kumpatia Roma.

“Humo ndani kuna dawa mpya ambazo nimefanikiwa kuzitengeneza , kama utahisi tatizo lako kukurudia jaribu kumeza , tukikutana kwa mara  nyingine nitakupima na kujua kama zinafanya kazi kwa ufanisi”

“Asante sana Clark kwa kunijali , unaonekana  ulikuwa ukitembea na dawa zangu muda wote kwenye koti lako kwa kuamini tunaweza kukutana”Roma alionekana kuguswa na matendo ya mrembo huyu.

“I just Could `nt  help my Self Pluto , this is how I relieve my worries  , I told my self we will meet again even by chance and here we are”(Sikuweza kujisadia mwenyewe Pluto , hii ndio ilikuwa namna nilivyokuwa nikipunguza wasiwasi wangu , nilikuwa nikijiambia ninaweza kukutana na wewe kwa bahati mbaya na  leo  imetokea)

“Clark you are  good woman whom  I had ever know  in my life and every act  of your kindness  has  a lot  of meaning  to me ,Thank you So much  and goodbye”(Clark umekuwa mwanamke mwema kwangu sana ambaye nimewahi kukutana nae kwenye  Maisha yangu na kila tendo la kikarimu  unalofanya linamaana kubwa sana kwangu , Asante sana  na kwaheri)

Aliongea Roma na kisha akaondoka na kumuacha mwanadada huyu akiangalia kivuli chake kinachotokomea  kwenye macho yake na alijikuta akipeleka mkono kwenye macho yake  na kufuta machozi ambayo hakujua yameanza kumtoka , huzuni aliokuwa nayo huyu mwanadada ni kama vile hatomuona tena Roma , haikueleweka ni hisia gani za huyu mwanadada anazo juu ya Roma.

*****

Mzee Alex alionekana kuwa ni mwenye hasira sana , alikuwa akitweta huku akitoa jasho , hakuamini dili kama hilo  kampuni yake imeshindwa kulipata , hakuelewa ni kitu gani abuu anakifanya  huko Japani mpaka kukosa dili kubwa kama hilo , aliapia kwa majina yote ya ukoo wake Abuu akirudi lazima amtandike risasi.

Alimfikiria Abuu kama toto jinga ambalo halikupaswa kupewa nafasi kubwa katika uongozi wa kampuni ,  kiasi cha kwamba aliamini huenda angempa mtoto wake mkubwa  wa kike nafasi hio huenda angeleta mabadiliko makubwa.

“Abubakari ni mjinga sana , kashindwaje  kusaini  mkataba  mnono kama ule na kumuachia Edna , anajua ni kiasi gani gepu ambalo lipo kwasasa baada ya kampuni yetu kukosa hilo dili na Edna kulipata ,, sh**t huyu mtoto nikimuacha hai labda sio mimi Alex , labda asirudi na anabahati  hata  kazima simu ningemtukana mpaka matusi ambayo hayajavumbuliwa bado”

Alijiongelesha maneno yasio na mpangilio kwa sauti huku akigonga stering ya gari wakati likiendelea kuwa katika mwendo, na wakati huu alikuwa akipita  Kongowe na kuchanja mbuga na  ndani ya madakika kadhaa tu alikuwa ashafika sehemu aliokusudia na kukata kushoto na Range yake kuingia kwenye barabara iliokuwa na rami lakini iliokuwa imependezeshwa na miti midogo  ya miarobaini iliopandwa kwa mstari pembezoni mwa barabara na kufanya eneo hili lipendeze.

Baada ya kutembea umbali wa mita chache   tu alikutana na kizuizi cha geti na kusimammisha gari na alitoka askari aliekuwa ameshikilia SMG  na baada ya kumuona ni mzee Alex alitingisha kichwa  chake kwa heshima na kumruhusu.

Naam hapa ndio anapoishi mheshimiwa mstaafu  Kigombola , sehemu ambayo ilikuwa  ikifahamika kwa jina la Village G , ni sehemu ambayo ilijaa ufahari kuanzia  mazingira  mpaka nyumba.

Mheshimiwa huyu alionekana alipenda muundo   wa jengo la ikulu ya Dar kwani , hapa ndani palikuwa pakifanana san ana ni kama  injinia aliejenga hapa ndani alikopi  tu muundo na kujenga ,hivyo hii sehemu  ni sahihi kusema ni kopi ya ikulu, mheshimiwa kigombola alionekana kupenda ‘vibe’  la ikulu.

Baada ya Mzee alex  kuegesha  gari  alitoka moja kwa moja , huku siraha yake ikiwa  kiunoni  bila ya kuonekana.

Baada ya kuingia kwenye sebule kubwa iliokuwa ndani ya jengo hili , sebule maalumu kwa ajili ya maongezi ya mheshimiwa Kigombola na  wageni  wake ,Mzee Alex alijikuta akishangaa watu waliokuwa hapo ndani na ghafla tu akachomoa Bastora yake na kuikoki.

“Baba….Babababa .. naomba unisamehe .. babba najua nimeboronga.. lakini naomba unisameh…aaa”Alikuwa ni Abuu  aliekurupuka mara baada ya kumuona baba yake mlezi, haikueleweka alikuwa amefika saa  ngapi nchini na  hapo ndani.

Kila mtu alishangazwa na kitendo cha mzee Alex kutoa siraha , waliokuwa hapa ndani  walikuwa ni Abu , Mheshimiwa Kigombola ,Elvice Temba , mzee Temba mwenyewe ambaye alikuwa ni Mkuu wa  mkoa wa Dodoma , alikuwepo pia Meya wa jiji la Dodoma mzee Abubakari Juma lakini pia kiongozi mkuu wa kundi la Black Mamba .

“Alex hebu punguza jazba… weka siraha chini tupo hapa kwa ajili ya kujenga sio kubomoa , acha kuonesha  udhaifu mbele ya kila mtu”

Aliongea mheshimiwa Kigombola kwa hasira na muda ule ule tu Aliingia kwa kitaalamu kabisa mlinzi  wa Kigombola wa kike  na kubetua siraha na ikadodokea mikononi kwake na kumpiga Roba Alex.

“Scorpion , unaweza kumuachia”

Aliongea  Kigombola na Scorpion aliekuwa amempiga Roba mzee Alex alimuachia , lakini ni kama Alex alifunguliwa kwani alimkimbilia Abu na kuanza kumpiga mangumi na Abu ambaye alikuwa amepiga magoti alijikuta akidondoka  chini , lakini mzee Alex  hakuacha aliandelea kusindilia mateke , ngumi , Scorpion alitaka kuingilia lakini Mzee kigombola alimpa ishara   asifanye chochote.

Abuu alipigika na mpaka damu zikaanza kumtoka ndipo mzee Alex alipomuachia huku Abuu akilia kama mtoto.

“Mzee Alex kama hasira zako  zimepungua unaweza ukaketi tukaongea tuyajenge  sasa , sio muda wa malumbano sasa , mwenyewe sijapenda yalitokea huko Japani , lakini hata  kama ni wewe usingeweza kumdhibiti Roma.”

Aliongea Kigombola  na mzee Alex  alionekana kupoa kidogo na muda huo huo aliingia mhudumu na kumpa glasi ya maji na akayanywa yote kwa pupa na kisha akasogelea  sofa na kukaa.

Ilionesha Abu alikuwa ashahadithia kila kitu kilichotokea  huko Japani mpaka kujikojolea kwake  na sasa Kigombola  alikuwa akimpasha  habari kwa ufupi ya kile walichoambiwa na  Abu.

“Niseme tu hata mimi naelewa Roma sio mtu wa kawaida , nimejaribu hata mimi kufukunyua kupata taarifa zinazomuhusu Roma lakini sikufanikiwa , badala ya kupata taarifa inayoonesha , alikuwa akiishi nchini Marekani kabla ya kuja hapa Tanzania na inasemekana nchini Marekani alikuwa  akilelewa  na moja ya matajiri wakubwa , jimbo la Michigani , Tajiri mmoja anefahamika kwa jina la  Robert Eglon”Aliongea  Kigombola.

“Hata kama sio wa kawaida , tunashindwaje kumuua mtu mmoja watu wote sisi na nguvu yote tulionayo , tunaachaje mtu mmoja aharibu kila kitu tulichokijenga kwa miaka”Aliongea Mzee Alex na Mstaafu kama kawaida yake aliachia tabasamu.

“Alex kwenye vita ili  uwe na uhakika wa kushinda  mbinu ya kwanza  ni kujua adui yako  anauwezo wa namna gani , huwezi kwenda kichwa kichwa utashindwa , na sisi kusema Roma sio wa kawaida  ni swala la kuutambua uwezo wake , lakini haimaanishi tumeshindwa”

Aliongea na kisha alimimina maji kwenye glasi na kunywa kidogo na akageuka na kuwaangalia kila mmoja hata Abuu ambaye alikuwa akimwangalia baba yake kwa woga.

“Mpango mzima wa Yamakuza  mpaka sasa  tuseme umefeli kwa asilimia mia moja  na tumezidiwa akili , lakini haimaanishi kwamba tumeshindwa , Roma ni kama nzi kwetu na cha kufanya ni kuitega na  viganja viwili na kisha kuimaliza”

Kila mmmoja alimwangalia mzee wa mipango bwana mstaafu  kwa  kumtaka endelea kuongea Zaidi.

“Najua wote mnaelewa  The Doni alikuwa ni  mtu ambaye  siku zote ni mwenye kutaka  upatikanaji wa  ‘Safe Root’ katika biashara zetu na niwaambie tu , hilo swala lazima lifanikiwe na hakuna njia nyingine  ,Vexto ni kama  zao la mkulima aliepanda mbegu  njiani na hakuna budi kwa   wapita njia kukanyaga na kutengeneza njia”

“Kwa hio mhesimiwa nini kifanyike?”

“Nadhani kila kitu kipo kwenye mipango Bakari , kwani mpango B  wenu   mliopanga ulikuwaje?”

“Mpango B ilikuwa ni kumua Roma  na Edna siku ya  kusanyiko la wafanyabiashara”

“Nadhani   tuendelee na mpango huo huo  cha kufanya tu ni kwamba  mpango  huu  tunatakiwa kuongezea nguvu ili uwe na  asilimia kubwa za mafanikio” Kila mmoja alishangaa lakini mheshimiwa alitabasamu  na kisha akamgeukia  mlinzi wake.

“Mwambie aingie”

Mlango ulifunguliwa na  hapohapo akaingia bwana  ambaye aliwafanya kila mtu kugeuza macho  na kushangaa.

Make kwa kutulia nitaleta muendelezo saa nne kamili usiku , kama huwezi kusubiria lala utaukuta asubuhi………

Previoua Next