Alikuwa ni bwana mweupe jamii ya Wakurdish kimakadirio alikuwa umri si chini ya miaka sitini hivi kwani nywele zake zilikuwa zishaanza kubadilika rangi, ukimwangalia kwa ukaribu unaweza kusema ni muarabu lakini sio mwarabu , kilichowafanya watu hawa washangae ni muonekanp wa bwana huyu kwani alikuwa na ndevu nyingii kiasi kwamba alikuwa akiogopesha lakini pia alionekana kutokuwa na afya nzuri kwani alikuwa amekonda mno , ni kama mfungwa ambae ndio hukumu yake imeisha na siku hio alikuwa amerudishwa uraini.
Watu wote hapa ndani walimgeukia na kumwangalia Kigombola wakitaka maelezo Zaidi ya huyu bwana ni nani anahusika je kwenye mpango wao.
“Naona mmeshangaa , huyu ni seif Ramadhani ni Mtanzania , alieingia Tanzania miaka kumi iliopita , kazi yake tokea afike hapa Tanzania ni uvuvi na maskani yake ni Pangani”
“Mheshimiwa Mvuvi anatusaidia vipi kwenye kazi yetu?”
“Alex nimesema ameingia Tanzania miaka kumi nyuma, lakini haujauliza alitokea wapi na kilichomtoa huko kwao ni nini?”
Baada ya kuongea hivyo Mzee Alex alijilaumu kwa mdomo wake ulionapupa ya kuongea na kisha akatulia kumtaka mheshimiwa kuendelea kuongea.
“Seif kabla ya kuja Tanzania alikuwa ni mwanajeshi kutoka jeshi la taifa la Iran”Kila mmoja alishangaa na kujiuliza kwa wakati mmoja mwanaeshi wa Irani kaja Tanzania kufanya nini, ila wakamwacha Kigombola aendelea kuongea.
“Seif ni mgonjwa wa kansa ya Kongosho na wiki moja nyuma alikuja hapa nyumbanii kwangu kunitafuta kupitia wasaidizi wangu na shida yake kubwa anataka akafie kwenye Ardhi ya nchi yake kutokana na ugonjwa wake wa Kansa kuwa katika hatua za mwisho”
Kila mtu akashangaa na kuanza kufikiria , sasa mgonjwa ambaye anakaribia kufa kwao ni wanini …. Ila bado hakuna ambaye aliinyanyua mdodo kutaka kuongea , walitaka kusikia mpaka mwisho.
“Kama nilivyosema Seif ni Mgonjwa wa Kansa ambaye anataka kurudi nyumbani kwao , alitaka nimpe kazi huku ujira wake akitaka kusafirishwa mpaka Irani , nilijaribu kumhoji Seif ni kazi gani anaweza kufanya kwa hapa Tanzania kwa kiasi kikubwa hiko cha pesa , kwani kumtoa hapa mpaka Irani ni swala ambalo litahitaji kiasi kikubwa kuanzia mavazi , vidhibiti vya kusafiria na nauli, bwana seif akaniambia kama kuna adui yoyote ambaye nataka asilione jua ndani ya siku chache basi apatiwe hio kazi”.
“Hahaha..Mheshimiwa acha kunichekesha , huyu si atakufa kabla hata hajamfikia adui kwa afya hio”Aliongea Bakari huku akimdharau Seif na Seif hakuonekana kukasirika wala kufurahi , bwana huyu alionekana ni kweli alikuwa akihitaji msaada.
“Seif alikuwa mwanajeshi kitengo cha kusnipe kwa masafa marefu na jana tumemfanyia majaribio na aliweza kulenga shabaha kokwa ya parachichi iliokuwa umbali wa mita mia nne”
Hapa kila mtu alishangaa na hawakuamini mtu kama seif kuwa na uwezo huo , lakini watu wote hapa ndani walikuwa wakimuamini Kigombola hivyo hawakuweza kuona mheshiniwa anatania.
“Kwahio Seif atakuwa mdunguaji siku ya kusanyiko , mnachotakiwa ni kumuandalia mazingira ili aweze kufanya kazi yake vizuri , lakini faidia pia ya kumtumia Seif ni kwamba kama zoezi likishindikana atajiua mwenyewe”
Kwa maelezo ya Kigombola yalionekana kuwa na mantiki , uwezo wa Seif kulenga kokwa ya Parachihi kwa umbali wa mita mianne , sio uwezo wa kawaida.
Mzee Alex alijikuta akitabasamu , kwani aliamini kwa uwezo huo wa Seif ni rahisi kwa tukio hilo kufanikisha , lakini pia kwakua wao ndio walikuwa waandalizi wakuu wa kusanyiko , basi wangehakikisha ulinzi unakuwa wa kawaida ili kumruhusu Seif afanye kazi yake.
****
Ni ndani ya jumba kubwa ambalo lilikuwa ndani ya eneo la Mbezi Beach , mita kadhaa tokea lilipo kanisa kubwa la KKKT upande wa kushoto , alioneakana mwanadada mrembo Nadia Alfonso akiwa anaangalia channeli maarufu kutoka japani iliokuwa ikionyesha taarifa mbalimbali za kibiashara , huku akionesha umakini katika taarifa ambayo ilikuwa ikionyesha kampuni ya Vexto , Maple na Yamakuza kutia Saini ya mkataba wa kibiashara baina ya kampuni hizo.
Mwanadada huyu aliangalia Taarifa hio kwa muda huku akiwa na sura ya mtu ambaye hakuwa na furaha wala huzuni , wakati akiendelea kuangalia Taarifa hio mara simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina alijikuta akitoa macho na kisha akapokea.
“Nadia umefikia wapi mpaka sasa katika kazi yako?”.Ilisikika sauti upande wa pili ambayo ilikuwa ni ya mwanaume , ambayo kwa kuisikiliza tu ungejua mtu anaeongea na Nadia alikuwa mtu mzima.
“Boss mpaka sasa sijapiga hatua yoyote ile , kwani nimeshindwa kuwa karibu na Roma , mara nyingi amekuwa wa kuniepuka”
“Hio sio sababu Nadia , kama anakuepuka unatakiwa kumfanya asikuepuke na akufuate mwenyewe , misheni niliokupa ni kuhakikisha Edna na Roma wanaachana, na ulinihakikishia kwamba utaweza kuisambaratisha ndoa yao kwasababu unampenda Roma , kwanini unatoa sababu dhaifu hivyo Nadia?”
“Boss kama nilivyokuhakikishia kama wataachana hiko ndio kitakacho tokea , ninampenda Roma ndio na hio ni sababu pekee ambayo inanifanya nihakikishe ndoa yao haidumu”
“Una uhakika utaweza hio kazi Nadia?”
“Boss mpaka sasa naamini hilo linawezekana ,kwani nimepata taarifa muhimu sana”
“Taarifa gani?”
“Edna na Roma hawalali chumba kimoja”
“Unauhakika na hio taarifa Nadia?”
“Ndio boss nina uhakika nayo asilimia mia na imetoka kwa mtu wa ndani kabisa ya familia, Boss naamini kuna swala ambalo linaendelea kati ya Edna na Roma na muda si mrefu nitapata ukweli wote , nishapandikiza mtu wangu ndani ya nyumba ya Edna”
“Hio ni Taarifa nzuri Nadia , hakikisha swala hili linafanikiwa , Edna ni mwanamke pekee ambaye anapaswa kuwa na mimi kwenye Dunia hii , ukisnindwa kufanya hivyo , Nadia naamini unajua uwezo wangu nitahakikisha Hades anakufa na mpaka sasa yupo hai kwasababu yako una miezi miwili tu ya kuhakikisha ndoa yao inasambaratika”
“Sawa Boss nitahakikish a swala hilo linafanikiwa kwa namna yoyote ile”
Baada ya maongezi hayo Nadia alirudisha simu yake chini huku akiwa ni mwenye kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa kwa wakati mmoja.
“Roma haujui upo kwenye hatari gani kuwa karibu na mwanamke kama Edna ,Ila usijali sipo tayari kukuona ukipatwa na jambo lolote baya , njia pekee ni kukuachanisha na Edna”Aliongea mwanadada huyu ambaye alikuwa akihamika kwa ubobezi wa kutafsiri sharia na alionekana yupo siriasi kwa kile alichokuwa amedhamiria katika kichwa chake.
****
Ilikuwa ni muda wa saa Tisa mchana siku hiohio ambayo masaa Zaidi ya tisa Roma na Dorisi kusaini mkataba.
Nchini Kenya alionekana mwanamke ambaye kwa kumuangalia tu ungemtambua ni mwanamke ambaye alikuwa kwenye picha ambayo Roma aliiona kule Bagamaoyo kiwangwa kwenye kituo cha kulelea Watoto ca Son and Daughter orphanage , picha ambayo ilimfanya hadi Roma macho yake kubadilika Rangi na kuwa ya kijani.
Mwanamke huyu alionekana kukaa kwenye kitanda chake kikubwa cha kifahari kilichokuwa ndani ya jengo hili la Ikulu ya wananchi wa Kenya , wakati mwanamke huyu akiangalia miguu yake kama mtu aliekuwa akitafuta kasoro , mlango wa chumba chake uligongwa na akainuka na kwenda kufungua na alionekana mwanamke alievalia mavazi ya suti mweusi akiwa mbele ya mlango.
“Madam Dokta kashafika”Aliongea mwanadada huyu kwa heshima kubwa.
“Sawa Njiro nakuja baada ya dakika kumi”.Aliongea huyu mwanamama na kisha akarudi kwenye chumba chake , huku akionekana hali ya uso wake kubadilika tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
“Haya Maisha ya kuigiza nitaishi mpaka lini , nimechoka Zaidi ya kuchoka”
Aliongea mwanamke huyu huku machozi yakianza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake.
Alisogelea kioo na kujiangalia kwa takribani dakika tano na kisha akatoka ndani ya chumba hiki.
Baada ya kutoka mwanamke huyu aliingia kwenye chumba kingine kilichokuwa mita mia kutoka kilipokuwa chumba alichotoka upande wa kulia.
Chumba alichoingia mwanamke huyu hakikuwa na tofauti na chumba cha Daktari.
Baada ya mwanamke huyu kuingia hapa ndani aliketi kwenye kiti flani kama vile vya kufanyia tiba ya meno na baada ya kukaa kwa mtindo wa kulala , aliingia mwanaume mmoja ambaye amevalia mavazi ya kidaktari na Glovusi huku mkononi akishikilia beseni flani ambalo ndani yake kulikuwa na vitu kama vikaratasi muundo wa plastiki na vichupachupa vingi.
“Madam upo tayari”
“Ndio unaweza kuendelea”
Yule mwanaume alisogelea mpaka kwenye kile kiti na kisha akakizungusha kulia kidogo na kisha akakiinamisha , baada ya kumaliza kazi hio alichukua kifaa flani hivi rangi nyeupe ambacho kilikuwa kina mshikio , kifaa ambacho ukikiangalia kwa harakaharaka ni kama Hair Dryer.
Baada ya mwanaume huyu kushika mashine ile aliiwasha na kisha kumsogelea mwanamke huyu na kuanza kumpuliza nalo usoni huku huyu mwanamke akiwa amefumba macho , ndani ya dakika mbili ya mwanaume kumaliza kazi yake , sura ya yule mwanamke ilionesha kuwa na aina flani ya majimaji mazito ambayo hayakuwa mengi sana , lakini yaliogandia katika sura ya huyu mwanamke , baada ya Daktari kuridhika na kazi hio , alichukua kifaa kama Brashi na kuanza kupitisha katika sura ya mwanamke huyu na alionekana ni kama akisawazisha.
Ni Zaidi ya dakika kama kumi na tano za huyu daktarin kufanya kazi kwakutumia karibia vifaa vyote vilivyokuwa hapo ndani , hatimae mwanamke huyu aliinuka kwenye kiti kile na yule daktarin akampa kioo , lakini ajabu ni kwamba sura ya yule mwanamke ilibadilika kwa asilimia mia moja na kuwa ya mwanamke mwingine ambaye wananchi wa Taifa la Kenya walikuwa wakimtambua kama First lady
Huyu mwanamke ni nani , kwanini kajibadilisha sura… itaendelea
Siku nzima nzima Dorisi na Roma waliimaliza kwa kuzungukia miundombinu ya kiwanda ambacho ndio kitahusika kwenye uzalishaji wa material mapya,Neema Luwazo hakuweza kuambatana nao kwani wakati Roma akiwa juu ya ghorofa akiongea na Profesa Clark , Neema alionekana kupokea simu ambayo baada ya kuongea kwa dakika chache tu alimsogelea Tikayi na kumuaga kwamba anapaswa kwenda Tokyo kwenye maswala yake ya kibiashara , alimuaga pia Dorisi na kisha akampa kikadi ambacho ni cha mawasiliano na kumuambia kama kuna lolote jipya asisite kumpatia taarifa.
Ilikuwa ni muda wa saa mbili za jioni baada ya Dorisi na Roma kurudi ndani ya hoteli ambayo walikuwa wamefikia baada ya kutoka Twillight Villa yaani Caprino Hotel ,Baada ya kupiga kimoja ambacho kilidumu kwa zaidi ya dakika hamsini, Roma aliona amchukue Dorisi kwenda kutembea nae ndani ya jiji hili kama 'date' na jambo hilo lilimfurahisha sana Dorisi.
Basi walijiandaa na kisha wakatoka , walitumia Taxi ambayo iliwachukua mpaka kwenye mtaa unaofahamika kwa jina la Namba , jambo ambalo lilimshangaza sana Dorisi baada ya Roma kupendekeza mtaa huo na kujiuliza aliufahamu vipi.
Mtaa wa Namba ni moja ya mitaa maarufu sana ndani ya Osaka kwa ajili ya kutembea usiku na wenye usalama wa hali ya juu , ni mtaa ambao unamaduka mengi ambayo unaweza kufanya Shopping na mambo mengi ya burudani, na maduka ndani ya Namba huwa hayafungwagi Zaidi ya masaa ishirini na nne na hivyo hufanya mtaa huu kuwa na pililikapilika za watu muda wote.
Dorisi alifurahishwa na uchangamfu wa eneo hilo mno , walitembea kiupande upande huku wakinunua baadhi ya vitu ambayo Dorisi alikuwa akipenda na Roma alimsaidia kubeba , sehemu hii ilikuwa na watu mchanganyiko waliokuwa wapenzi ambao wapo ‘Date’ na pia kulikuwa na watu ambao walikuwa wenyewe wakionekana kurefresh mind’ ,wazungu , waarabu , Waafrika wote walikuwepo.
Ilikuwa ni muda mzuri sana kwa Dorisi kuwa karibu na Roma na alitamani siku zote wawe na nafasi kama hio ya kuwa pamoja , Dorisi hakumjali tena Rafiki yake Edna kiufupi alikuwa hajiwezi kwa Roma na hakuwa akijua hata afanyeje kwani hisia za Mapenzi zilikukuwa zikimpelekesha sana, lakini alijiambia katika akili yake kwamba watashea mwanaume mmoja ne Edna hata kama hapendi.
Ni baada ya masaa kama mawili ya kununua makolokolo sasa , walikuwa wameketi kwenye mgahawa wakipata kahawa kwa ajili ya kupasha miili joto kwani hali ya hewa ilikuwa ya ubaridi , wakati wakiendelea kufurahia huku wakiangalia watu waliokuwa wakipita kwa chini yao , kwani sehemu waliokuwa wameketi ilikuwa kwa juu , mara kulitokea tukio.
Dorisi na Roma walijikuta wakivamiwa na mwanamke wa Kijapani aliekuwa mzee hivi kutokana na sura yake kuwa na mikunjo , aliekuwa amenyoa kipara , mwanamke alikuwa amemshikilia Roma mguu huku akiongea kwa kijapani Lugha ambayo Dorisi hakuwa akiielewa lakini Roma alielewa .
Mwanamkke huyu alikuwa akiomba msaada huku akisema kwamba wamemchukua mtoto wake wa kike anaaefahamika kwa jina la Hirashia , sasa jambo hili lilimshangaza Roma kwani mwanamama huyu alikuwa amevuka karibia watu wote na kumkimbilia yeye na Dorisi.
Roma alimwangalia huyu mwanamke mzee na kumuonea huruma kwa wakati mmoja , hakuona namna yoyote ya mwanamke kudanganya , alionekana ni kweli alikuwa akihitaji msaada , lakini bado swali lilibaki kwanini kaona wao ndio wanaoweza kumsaidia na sio ndugu zao wa kijapani , kwani eneo hilo lilikuwa na watu weupe tu na baaadhi ya wazungu ambao pia walionekana kuwepo ndani ya eneo hilo kutalii.
Watu waliwazunguka huku wakimwangalia Roma atafanya nini kwa wale waliokuwa wameelewa mwanamke huyo alikuwa akihitaji msaada, na wakati huu Dorisi na yeye alikuwa kwenye mshangao , alikuwa akijua kuwa mwanamke huyo alikuwa akihitaji msaada lakini hakujua alikuwa akihiraji msaada gani kwani alikuwa akiongea lugha ambayo hakuwa akiijua yaani kijapani.
“Wamemchukua kwenda wapi?”Aliuliza Roma mara baada ya kuona watu wanazidi kujaa kitendo ambacho kilianza kumfanya Dorisi kujisikia vibaya.
“Kule”
Aliongea mwanamke kwa kuonyesha kidole upande ambao kulikuwa na majengo kitendo ambacho kilimfanya Roma ashindwe kumuelewa kwani sehemu ambayo alikuwa amenyooshea mkono ni upande wa pili sehemu ambayo majengo yamejengewa kiupande upande na katikati kuna mto ambayo watu wengi muda wa mchana hupenda sana kutumia mitumbwi kufurahia kuendesha ndani ya hilo eneo.
“Elezea vizuri mama”Aliongea Roma na hapo ndipo mama huyu alipoelezea ,na baada ya Roma kuonekana kumuelewa alimwangalia Dorisi na kumwambia waelekee mtaa huo kwani anajisikia kumsaidia.
“Nini kimempata?”
“Anasema kuna watu wamemshikilia binti yake kutokana na kwamba wanamdai pesa , ila anaogopa wanaweza kumfanyia vitendo viovu hivyo anaomba msaada na kutuona sisi watu pekee ambao tunaweza kumsaidia”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi ashangae.
“Sasa tunaenda kufanya nini kama mtu anadaiwa? , tungemsaidia kiasi cha pesa tu”
“Kuna kitu hakipo sawa na maelezo yake na nataka nikahakikishe”
Walifika upande wa pili upande wa kushoto , ng`ambo ya pili ya mto , sehemu ambayo ilikuwa ni makazi ya watu ambao kwa kuangalia tu muundo wa majengo utajua watu wanaoishi mtaa huo ni wale wenye kipato cha juu , walikuja kusimama kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa na geti rangi nyekundu lakini lililokuwa limenakshiwa kwa michoro ambayo haikuwa ikieleweka lakini ya kupendezesha , ni jengo ambalo kwa nje liilikuwa likionekana, na muundo wake ulikuwa ni ule wa majengo ya kitamaduni yaani Minka.
Sasa cha kushangaza ni kwamba , baada ya wao kufika tu nje ya geti ni kama walikuwa wanasubiriwa kwani geti lilifunguliwa na wa kwanza kuingia ni yule mama jambo ambalo lilimshangaza Roma , ila kwakua Roma ni mtu wa kujiamini , alifuatia na akaingia ila Dorisi alionekana kuwa na hofu.
Licha ya kwamba eneo hili lilikuwa na mwanga hafifu wa taa , ila mazingira yake yalikuwa yakionekana kupendezesha nyumba hii , ni sehemu ambayo haikuwa na eneo kubwa kwani bustani zilikuwa kwa mbele tu huku eneo lote la nyuma lilikuwa ni jengo.
“Arrgh…!!!!”Kilikuwa ni kilio cha Dorisi kilichomshtua Roma na kugeuka haraka na akamsogelea kwa haraka Dorisi na kumdaka , huku macho yake yakijifumba na kujifumbua,Roma alimwangalia upande wa shingo na kuona kijisindano kimemchoma shingoni.
“Sh***t ni kama nilivyofikiria huu ulikuwa mtego”
Aliwaza Roma huku akimwangalia Dorisi aliekuwa kwenye mikono yake ,lakini sasa wakati akichomoa kile kijisindano hapohapo milango ya ile nyumba ilifunguliwa kwa kasi kulia na kushoto na hapohapo walitoka wajapani waliovalia mavazi ya suti na kumzingira Roma , aliangalia upande wake wa kushoto na kulia na kuwahesabu na kuona jumla yao ilikuwa kumi na sita yaani nane kulia na nane kushoto, aliinua na kuangalia macho mbele hapo ndipo alipomuona yule mwanamke kwa kijapani mzee akisogea pembeni akimpisha mtu aliekuwa nyuma yake.
Alikuwa ni mwanaume alievalia kitamaduni(Kimono) rangi nyeusi huku mkononi akiwa ameshikilia kifimbo ,alikuwa na nywele fupi kama yule mwanamke, kimakadirio alikuwa si chini ya miaka hamsini, alimsogelea Roma ambaye alikuwa amemshikilia Dorisi alieonekana kutoelewa kinachoendelea.
“Nice To meet you , mimi ni Kapteni Kisu Mvunjiko kutoka kikosi namba moja cha Dragon
Roma alimwangalia huyu mzee na kisha akamgeukia Dorisi , lakini kabla hajaongea chochote yule mama alimsogelea na kumshikilia Dorisi , Roma alimkata jicho lakini mama huyu hakujali Zaidi ya kuachia tabasamu na Roma akasimama vizuri.
“Naitwa Roma Ramoni mfanyakazi kitengo cha ‘Public Relation’ Vexto international Group”Alijitambulisha na mzee akatabasamu.
“Kwanini haujitambulishi kwa majina yako halisi?”
“Majina gani?”
“Pluto founder of the Eagles, and inheritor of the King of Hell, Hades’ ring… I’m not going to mention your other identities, but you shouldn’t be denying these two identities of yours”(Pluto mwanzilishi wa kundi la The Eagles ,mrithi wa kiti cha mfalme wa kuzimu na pete ya Hades … sitoendelea kutaja majina yako mengine lakini naamini huwezi kukataa haya majina yako mawili).Roma alikuna kichwa chake huku macho yake yakiwa hayabanduki kwa Dorisi.
“Ilikuwa zamani na sasa natambulika kama Roma Ramoni mfanyakazi katika kitengo cha ‘public relation’ hivyo haina haja ya kutaja hapa majina ya zamani”
“Lazima niyataje lasivyo mazungumzo yetu hayawezi kuendelea”
“Bora yasiendelee tu,Najua mmetumia sumu kumchoma nayo Mpenzi wangu hivyo nahitaji dawa yake niondoke , sina muda wa kukaa hapa”Mzee alitabasamu
“Hapana mpaka maongezi yetu yaishe kwanza”
“Ongea sasa mzee unachotaka kuongea”Muda wote walikuwa wakitumia kingereza na mzee alikuwa akiongea kwa ufasaha Zaidi.
“Kwasababu ni mara yetu ya kwanza kukutana , unao waona hapa ni sehemu ya kikosi changu , mama aliekuigizia mpaka kuja hapa ni luteni mstaafu kitengo cha ujasusi na mawasiliano amestaafu lakini tunamtumia kutokana na kipaji chake cha kuigiza”
“Nishajua kuhusu kikosi chako , sasa ni wakati wa kusema kwanini mmetumia mbinu ya kunileta hapa , mnataka nini kutoka kwangu?”.
“Sir Pluto kwanza tutangulize radhi kwa kukudanganya , lakini nia ya kukuleta hapa ni juu ya kazi ambayo tunataka utusaidie , idara ya intellijensia ya Osaka ilitupitishia uwepo wako”.
“Kazi gani hio na mna uhakika gani ninaweza kuifanya?”
“Sitaki kukuudhi Pluto lakini kazi yetu lazima utusaidie kwani mpenzi wako tumemchoma na sumu ambayo ikipita masaa manne bila ya kupatiwa dawa yake(antidote) atakufa”
Roma alijikuta akizuia hasira zake , huku akimwangalia Mzee huyu na para lake na alitamani amvunje shingo , kwani kwenye Maisha yake alikuwa akichukia sana watu ambao wanatumia watu wake wa karibu kumtaka afanye jambo.
“Mzee nachukia watu watu wanaotumia watu wangu wa karibu kunipata , lakini kwasababu leo wewe ndio umeshikilia mpini nitaacha hili lipite lakini sio kama nakuogopa , nina uwezo wa kuua kila mtu hapa,ni hivyo tu nipo ndani ya nchi yenu na nimebadilika ila mpaka dakika hii nisingekuwa naongea Zaidi ya vitendo”
Kuna jamaa la Pembeni ambaye anamwili mkubwa alievalia suti ambayo kwa ukubwa wa tumbo lake ilifanya suti isifunge kifungo cha katikati na shati kuonekana huyu bwana alionyesha chuki za waziwazi kwa Roma , alikuwa akitamani amfanyie shambulizi Roma kwani hakuwa akipendezwa na majigambo.
“Mpuuzi wewe hata kama unaitwa Mungu wa Wafu , misheni hii ikiisha lazima nikomeshe hizo dharau zako”Jamaa lilikuwa likiwaza kwenye kichwa chake
Ni baada kama nusu saa hivi Roma alikuwa kwenye chopa iliokuwa ikiambaa kuelekea mashariki ,mbali na Mji wa Osaka.
Ndani ya chopa hio kulikuwa na jumla ya watu sita, Roma aliekaa karibu na jamaa kibongea ambaye alikuwa akiitwa kwa jina la utani Mbwa Mwitu, mbele yake kulikuwa na Jamaa ambaye alikuwa akiitwa Kobota , mbele kulia alikuwa ni mwanamke wa kijapani aliefamika kwa jina la Hirashia , halafu kulikuwa na jamaa mfupi mwembamba alishikilia nyundo aliefamika katika kikosi kama Abbesi , halafu kuna Jani rubani msaidizi na Sunami Rubani mkuu wote walikuwa wamebadilisha mavazi na kuvaa Gwanda Roma pekee ndie alikuwa kwenye mavazi ya kawaida.
Roma alikubali kufanya kazi hio ili kumuokoa Dorisi ambaye alikuwa kwenye usingizi uliokuwa umesababishwa na Sumu.
Kazi ambayo Roma alitakiwa kufanya pamoja na wenzake wanne ni kuzuia (intercept) wezi wa Sanamu la dhahabu lililopewa jina la Varicana.
Varicana ni sanamu ambalo lilikuwa kama utambulisho wa mji wa Osaka , kwa maelezo ya Kapteni Kisu Mvunjiko alimwambia Roma kwamba kuna watu kutoka Korea Kaskazini walioiba hilo sanamu.
Yaani ni kama Tanzania wahuni waibe Mwenge wa Uhuru wakati wa kuutembeza , sasa ni kama kwa hilo Varicana , sababu kuu ya kapteni kutaka kumtumia Roma ni kutokana na kwamba sehemu ya wezi hao kuna Mchina anaefamika kwa jina la Tzeng , huyo Tzeng ni ‘Monk’ ambaye anamafunzo ya hali ya juu ya Kung fu(Martial Art) lakini pia anaaminika kwa kutumia nguvu za Giza(High level of spirit energy cultivation) katika kupambana, na kikosi cha kwanza ambacho kilitumwa, kwa maelezo ya Kapteni ni kwamba wanajeshi wote wamekufa,lakini pia kwa maelezo ya Kapteni ni kwamba Sanamu hilo linapelekwa Marekani na watu ambao wanapaswa kulipokea nje kidogo na kisiwa cha Honshu ni kundi la kijasusi linalofahamika kwa jina la Dhoruba Nyekundu au RedStorm.
Sasa Intelijensia ya uwepo mfalme Pluto au Hades Mungu wa wafu ndani ya Osaka Kapteni Kisu Mvunjiko aliona swala hilo ni kama bahati , kwani hakutaka kupoteza vijana wake wengi katika kupambana na Tzeng.
Ni ndani ya dakika ishirini baada ya chopa kutembea umbali wa kilomita kadhaa , hatimae Sunami aliwapa taarifa kwamba wanaona Boti ambayo ina wahalifu ,Roma alisimama na kisha akachungulia kwa nje na ni kweli kwa mbele yao ilionekana Mashua ndogo ambayo ilikuwa ikitembea Taratibu mno.
“Nyie wote inabidi mnisubiri nitaenda mwenyewe”Aliongea Roma huku wanajeshi wakimshangaa.
“Hayo sio maelekezo ya Kapteni , inabidi twende wote”Aliongea yule kibonge na Roma alimwangalia na hakuongea chochote, lakini walijikuta wakishangazwa mara baada ya Roma kuruka kwenye ndege na wote kwa pamoja walijikuta wakikimbilia mlango kuangalia chini.
Comments