Reader Settings

“Kabla hujaamini, utaulizwa. Kabla hujatumwa, lazima ujitambue.”

Asubuhi ya Uamsho

Kulipochomoza alfajiri, sauti ya ndege wa baharini ilizunguka dirishani, ikichanganyika na harufu ya maua yaliyochanua bustanini. JackXavier aliamka mapema, hakuwa hata na usingizi mzito. Mwangaza wa jua wa kwanza ulimwangazia uso wake na kufanya sura yake ijaye nuru kama mtu aliepokea tumaini jipya na kubwa la maisha aliyokuwa ameyakatia tamaa.

Alisimama taratibu, akafungua dirisha kabisa. Hewa ya asubuhi ilikuwa na uzito wa maana. Alihisia kuwa dunia ilikuwa imeamka naye. Hakukuwa na sauti, lakini ndani yake kulikuwa na mwitikio wa ndani usioweza kufafanuliwa.

Katika ukumbi wa chakula, Padre Ian tayari alikuwa ameketi, akisoma gazeti la Vatican News lililoandikwa kwa Kiitaliano.

Jack alipoingia, Padre alitabasamu.
“Habari ya asubuhi, mwanafunzi wa maono,” alisema kwa upole, akimuachia kiti.

Jack aliketi, bila kusema neno. Lakini kwa mara ya kwanza, alichukua kikombe cha chai bila kusukumwa. Padre Ian alimtazama kwa macho ya mtu anayejua anashuhudia mwanzo wa mabadiliko.

IAN (akiwa mnyenyekevu):
“Nilikuona usiku. Ulikuwa kimya, lakini… ulikuwa na uso wa kama mtu aliyezungumza na dunia nyingine.”

Jack alimtazama. Alichezesha mikono yake juu ya meza, kisha akasema kwa sauti ya chini:

JACK (kwa mara ya pili kuzungumza):
Wanasema… si wote wanaokuita ni wa msaada. Baadhi ni mizigo iliyofichwa kwa sauti za wema.”

Padre Ian akasita kwa sekunde moja. Hakutarajia jibu hilo. Halafu alitikisa kichwa na kusema:

“Kwa hiyo ni wakati wa kuchuja. Na kabla ya kwenda Marekani, tunahitaji kuhakikisha sio tu mwili wako upo salama, bali na roho yako haijavunjika.”

Baada ya chakula cha asubuhi, Padre Ian alimpigia simu dereva wa kituo cha afya, na saa moja baadaye, gari jeupe lililoandikwa "Misioni ya Huruma – Masista wa Mtakatifu Camillus" lilifika langoni. Jack na Padre Ian walipanda, na safari ya dakika ishirini ikaanza kuelekea upande wa Kinondoni, Dar es Salaam  mahali ambapo historia, imani, na huduma ya kibinadamu vinakutana.

Kituo hicho kilipatikana ndani ya Hospitali ya Mtakatifu Filomena, iliyojengwa mwaka 1952 na wamisionari kutoka Italia waliokuwa chini ya Shirika la Camillian Order, shirika maarufu duniani kwa kazi zake katika huduma za afya na wagonjwa wa muda mrefu. Hospitali hiyo, iliyokuwa awali kliniki ya kifua kikuu (TB) na magonjwa ya ukoma, baadaye iligeuzwa kuwa kitovu cha matibabu na huduma za uchunguzi wa afya ya mwili na akili, hasa kwa watumishi wa makanisa na watoto wanaolelewa kwenye taasisi za kidini.

Majengo ya hospitali yalikuwa ya kupendeza na yenye utulivu. Kuta za mawe zilipambwa na picha za watakatifu kama St. Camillus de Lellis, St. Teresa of Avila, na hata Blessed Benedetta Bianchi Porro, ambaye alikuwa daktari aliyepofuka lakini aliendelea kuhudumia wagonjwa kwa kugusa na kusikia sauti zao pekee.

Wakiingia ndani, Jack alihisi harufu ya dawa safi na sabuni ya hospitali iliyochanganywa na harufu ya mishumaa ya ibada. Palikuwa na usafi wa hali ya juu, lakini pia uzito wa kiroho kama sehemu takatifu.

Jack alipelekwa kwenye chumba maalum cha uchunguzi wa awali kilichoitwa "Chumba cha Eligius", kwa heshima ya Mtakatifu Eligius, mlinzi wa madaktari na wahunzi.

Ndani ya chumba hicho, alipokelewa na Daktari Mkuu wa hospitali, Dr. Boniface Mnyambala, mtaalamu wa magonjwa ya ndani aliyesomea Vatican na kubobea katika neuroendocrinology, taaluma inayochunguza jinsi homoni na mfumo wa neva zinavyoathiri mwili na akili.

Dr. Boniface (akiweka glovs):
“Tunaenda kufanya uchunguzi wa kina, si tu kwa afya ya mwili, bali kwa saikolojia na athari za maono. Tumeona watoto wenye alama za vipaji vya pekee, lakini wewe, Jack... wewe ni wa tofauti.”

Jack aliketi. Vipimo vilianza:

  1. Anthropometry – Uzito wake ulipimwa kwa digital scale: 62.8kg.
  2. Height & BMI – Urefu wake ulikuwa 5'9", na hesabu ya BMI ikaonyesha afya nzuri ya mwili.
  3. Blood Pressure – Shinikizo lake lilikuwa 126/82 mmHg, dalili ya mchanganyiko wa utulivu wa moyo na hofu iliyofichwa.
  4. Ophthalmology test – Alifanyiwa uchunguzi wa macho kwa kutumia slit lamp; mboni za macho yake zilionekana kuwa na photonic flare zisizoelezeka, kana kwamba kulikuwa na mwanga wa ndani unaojirudia.
  5. Reflex Tests – Daktari alitumia neurological hammer kugonga magoti na vifundo; mwitikio wa misuli ulikuwa wa haraka kupita kawaida.

🧠 Psychospiritual Evaluation with Sister Magdalena

Vipimo vya kimwili vilipomalizika, Jack alipelekwa kwenye chumba cha pili kilichoitwa “Chumba cha Mt. Augustine”, chumba tulivu kilichojengwa kwa mbao ya mninga, na kupambwa na sanamu ndogo ya Yesu Mchungaji Mwema.

Hapo, alikutana na Sister Magdalena, mtawa mzee wa Kijerumani mwenye sauti ya upole lakini yenye mamlaka ya hekima. Alikuwa amehudumu kwa zaidi ya miaka 40 katika psycho-spiritual counseling kwa watoto waliopitia trauma, na alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa kitengo cha Faith-Integrated Psychiatry.

Sister Magdalena (akiweka daftari juu ya meza ya maombi):
“Nitataka kuelewa sio tu kile unachokiona, bali pia jinsi unavyokielewa. Maono huja kwa macho, lakini ukweli huja kwa roho.”

Jack alitulia. Vipimo vyake vilihusisha:

  • Rorschach Inkblot Test – alioneshwa madoa ya wino yenye umbo la kale; majibu yake yalihusiana na moto, majini, na nyuso zenye macho mengi.
  • Drawing Response Test – aliombwa kuchora ndoto yake ya usiku. Alichora bustani, sanamu na saa ya spiral, na maneno ya mwanga yaliyofichwa ndani ya kivuli.
  • Electrodermal Response (EDA) – kifaa maalum kilichopimwa mabadiliko ya msongo wa mawazo katika ngozi, kilionesha kiwango cha arousal ya kipekee alipotajwa neno “Mwisho.”

🏽 Matokeo

Baada ya dakika tisini za vipimo, Sister Magdalena alifunga daftari lake, akanyanyua macho yake, na kusema kwa Padre Ian:

“Huyu mtoto hakui tu na historia yake. Anaishi ndani ya historia ya wengine.
Na hiyo ni zawadi, lakini pia ni msalaba.”

Jack alimtazama. Hakujua hata maana ya hayo yote. Lakini moyoni mwake, alihisi jambo moja tu:
Hakuwa tena wa kawaida. Na hakuna kipimo kingine kilichoweza kuthibitisha hilo zaidi.

********

Waliporudi kutoka hospitalini, jioni iliwakuta kwenye bustani ya makao makuu. Kengele za kanisa zilipiga taratibu. Jack alisimama nje ya ukumbi, akitazama jua likizama baharini.

Padre Ian alikuja na kumkabidhi karatasi ya mwisho kutoka Vatican:

“Umeidhinishwa rasmi. Safari ya kuelekea Marekani ni keshokutwa usiku.”

Jack alishikilia karatasi hiyo kwa nguvu. Halafu akasema:

JACK:
“Na nikifika… je, wataniamini?”

IAN (akimtazama kwa uzito):
“Watakushangaa. Lakini imani… haitaji makubaliano. Inahitaji moyo wa kuona zaidi ya macho.”

Usiku huo, Jack alilala mapema. Mwili wake ulikuwa umechoka, lakini ndani yake kulikuwa na nguvu mpya iliyomchokonoa kwa utulivu wa ajabu. Chumba kilikuwa kimya. Hata bahari ya mbali ilionekana kuviringisha mawimbi yake taratibu.

Lakini kabla hajazama kabisa usingizini, mwanga wa dhahabu ulianza kutokea mezani. Si ndoto, bali kitu halisi, ndicho kilichokuwepo pale.
Kitabu cha Majira kilikuwa kimesimama wima, kikiwa hakiguswi na chochote, lakini kiking’aa kama kiota cha roho.

Jack alitazama, macho yake yakiwa makubwa kwa mshangao na hofu nyepesi.
Hakujua kusoma. Hakujua hata jina lake linavyoandikwa. Lakini bado... alielewa.

Maneno yaliyojitokeza juu ya ukurasa wa kwanza hayakuwa ya kawaida.
Hayakuwa maneno ya kawaida kwenye karatasi.
Yalikuwa mawimbi ya mwanga, yanayojigeuza kuwa hisia.

Na ndani ya kichwa chake, alisikia sauti, si kutoka nje, bali ndani ya moyo wake mwenyewe:

"Safari yako ya kwanza haiko Marekani. Iko ndani yako."

Jack alishindwa hata kupumua kwa sekunde kadhaa.
Halafu, bila mtu yeyote kugeuza kurasa, kitabu kilianza kujipeperusha chenyewe.
Kila ukurasa uligeuka kwa upepo ambao haukuwepo.
Na alipokisogelea kwa tahadhari, uso wake mdogo ukimulikwa na mwanga wa kurasa...

Aliona kitu kilichomfanya asimame kwa ukimya mkali:
Picha ya uso wake mwenyewe. Lakini si kama alivyo sasa, bali akiwa mzee, mwenye macho ya roho iliyoishi karne nyingi.

Na ndani ya picha hiyo, alihisi kitu kimoja tu:

“Siku moja, utamkumbuka huyu mtu. Sio kwa jina, bali kwa jukumu lake.”

Previoua Next