Reader Settings

FOR YOU 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★

 SEHEMU YA SABA

★★★★★★★★★★★★


Baada ya miezi mingi kupita, Kendrick alifanikiwa kuwapata watu ambao wangemsaidia kuiba pesa au dhahabu nyingi zaidi. Alikuwa ametafuta watu wenye uzoefu mzuri katika mambo fulani hususa. Kutokea Ghana walikuwa ni Oscar, Victor na Mensah, huku Torres akitokea Jamaica. Wote hao walikuwa na aina fulani za kesi kipindi cha nyuma kutokana na kutumia vipawa vyao kufanya mambo haramu (illegal) yaliyohusisha wizi, naye Kendrick aliwaahidi kwamba wangepata faida kubwa kwa kufanya kazi pamoja naye.

Kazi ya kwanza waliyoifanya iliongozwa na Torres, nao walitakiwa kuiba pesa zilizokuwa zikihamishwa kwa kutumia magari kuelekea Manispaa fulani. Lakini mipango yao iliharibika, na ilikuwa kidogo tu Victor na Mensah wakamatwe ila wakafanikiwa kuponyoka bila kutambulika. Kwa kuwa kazi walizojipanga kufanya zilionekana kuwa ngumu, walihisi wangejihatarisha zaidi na kujadili kuhusu kuacha tu kuzifanya, na ndipo Sandra (Xander) akajiunga nao.

Kendrick hakutaka Xander ajiingize kwenye mambo hayo, lakini alikuja na mbinu mpya kisha kuiingiza katika mpango mmoja wa Torres. Aliwasaidia kuona njia nzuri zaidi ya kufanikisha kazi fulani, nao wakakubaliana kuitumia ili kuona matokeo yangekuja vipi. Walikuja kufanikiwa kuiba kontena dogo lenye dhahabu zilizokuwa zikisafirishwa kuelekea nje bila hata kujulikana kwa sababu ya mbinu hiyo aliyowapa Sandra (Xander). Walifurahi sana, nao wakamuuliza Kendrick "binti" huyo alitoka wapi, na kwa nini hakuwa pamoja nao kwenye kazi ya kwanza iliyoshindikana.

Ikambidi Kendrick akae na kuongea na Xander. Alimuuliza kama angetaka kujiunga nao kwa ajili ya kazi zingine, naye Xander akakubali. Ila akamkumbusha kwamba wangefanya kazi hizo ndiyo, lakini hawakupaswa kusahau kuwa walizifanya ili kuja kutimiza malengo yao, naye Kendrick akamwambia aondoe shaka kuhusu hilo. Alipokuja kujitambulisha vizuri zaidi kwa Torres, Victor, Mensah pamoja na Oscar, Xander alibadili jina na kujiita Lexi. Kwa hiyo, kuanzia hapo wote walimtambua kama Lexi.

Kendrick alikuja kumuuliza baadaye kwa nini aliamua kujiita hivyo, naye akamwambia ni kwa sababu sikuzote Sandra alitamani jina lake lifupishwe namna hiyo, lakini kwa kuwa ilizoeleka kumwita "Sandra," basi ikawa hivyo tu. Kwa hiyo kwa kujiita jina hili, Xander angeendelea kukumbuka kwamba pacha wake ni sehemu muhimu sana kwenye maisha yake kutokea hapo na kuendelea, nayo ingekuwa ni moja kati ya njia nyingi za kuendelea kumuenzi akiwa sehemu ya mwili wake.

Katika kazi zao zote za kupokonya pesa au vito, walihakikisha hawamuumizi yeyote, isipokuwa labda kuwe na ulazima wa kuwaumiza wale waliowazingua moja kwa moja. Wangeiba vitu hivi wakiwa wanajua haingeleta hasara yoyote kwa wanyonge, bali kwa watu wabinafsi tu walioziendesha shughuli hizo. Lexi sasa akawa pamoja nao, na kutokea hapo, wizi walioufanya wa mali ulifanikiwa sana bila yeyote kuwajua. Wangefanya wizi mara moja kwa mwezi katika pindi na sehemu zisizotabirika kabisa.

Muda ulipita, nao waliendelea kuzoeana hata zaidi. Baadae, Kendrick aliwaweka wazi wengine kwamba alikuwa akisaidiana na Lexi kuunda mpango wa kulipiza kisasi utakaowapeleka Tanzania, hivyo endapo wakati huo ungefika, kama wangehitaji kurudia maisha yao mengine basi wangekuwa huru kufanya hivyo. Lakini vijana hao wakakanusha na kusema kwa lolote lile ambalo boss wao angefanya, wangekuwa pamoja naye kwa sababu aliwabadilishia sana maisha yao.

Wote kwa pamoja wakaendelea kuwa kama familia ndogo ya "wezi" wenye ufundi wa hali ya juu sana.


★★★★


Miaka mitatu kutokea hapo ilipita, na kufikia wakati huu, Kendrick Jabari alikuwa amekusanya mali yenye thamani ya dola bilioni 1 za kimarekani, yaani trilioni 2.2 za kitanzania wakati huo (2,200,000,000,000), kutokana na kutunza vitu alivyopata kwa kazi nzuri za kimya kimya walizofanya vijana wake kwa kuwaunga mkono. Alikuwa akiwapa mafungu yao bila shaka, nao walifurahia maisha mazuri lakini kwa kuwa makini sana ili wasijitie kwenye matatizo. Mwongozo walioupata kutoka kwa Torres na Lexi uliwasaidia kujiendesha vizuri wakiwa hadharani, nao wakawa wakiishi maisha ya aina mbili tofauti kabisa; wezi, na raia wema.

Mambo yote hayo yaliyoendelea gizani hayakujulikana kwa Margaret hata kidogo. Bado aliendelea kuonana na Kendrick, hasa kwa kuwa Kendrick alimwongezea ufanisi mwingi kwenye biashara zake za pembeni. Lexi alikuwa akiwafundisha wengine lugha ya Kiswahili, nao walikuwa wameanza kuizoea ijapokuwa ni Mensah ndiye iliyempa shida sana. Oscar alikuwa ndiye kijana mdogo zaidi, lakini alichangamana nao vizuri, nao walimheshimu akiwa kama mmoja wao. Victor mzee wa kutengeneza vitu bandia ndiye pekee kati yao wote aliyekuwa na watoto, wawili, nao waliishi upande mwingine wa nchi hiyo, jijini Accra. Angewasiliana nao mara kwa mara na kuwatumia pesa nyingi pia za matumizi, huku akifurahia bata na familia yake hii mpya.

Sasa ilikuwa imefikia hatua ambayo vijana hawa wangepaswa kujiandaa kwenda Tanzania ili kuanza kazi. Lexi na Torres walikuwa wamebuni mpango huu kwa umakini wa hali ya juu ndani ya miaka hiyo, na sasa wangeanza kufanya mambo kwa vitendo. Wangeanza kutengeneza na kununua vifaa muhimu walivyohitaji, kisha baadhi yao wangetakiwa kwenda Tanzania ili kuweka mambo sawa kule kwa ajili ya kuwakaribisha waliobaki. 

Kulikuwa na kazi moja iliyobaki ya kuiba dhahabu, kisha ndiyo wangeanza kupiga hatua za mipango hiyo ya kisasi. Mpaka kufikia sasa hawakuwa wamegundulika kwa sababu waliiba kwa kiwango hususa walichopanga kila mara dhahabu ziliposafirishwa, hivyo mara nyingi wangewaacha wamiliki na wasimamizi wa mambo hayo wakilaumiana wenyewe kwa wenyewe huku wao wakiwa wameshatembea mbele.


★★★


Siku fulani kabla ya kazi hiyo kufanyika, Lexi alikuwa akitembea mitaa ya mji mmoja kama kufanya mizunguko tu ya kawaida. Sikuzote wanasema kabla ya dhoruba kali hali ya hewa huwa inakuwa imetulia, na kwa timu yao ndivyo ilivyokuwa. Maisha ya kawaida waliyoishi baada ya kumaliza kuiba yasingewatia mikononi mwa sheria kwa kuwa haingekuwa rahisi kuwajua. Akiwa anapita eneo lenye soko dogo la biashara, aliweza kuwaona wanaume kadhaa sehemu iliyojificha sana.

Kwa udadisi, akapitia njia nyingine na kwenda upande ambao alijibanza ili kuweza kuwachungulia. Aliwaona wanaume hao watano wakimpa mwanamke kijana bunda la pesa kwa kificho, naye akawapatia fuko dogo lenye vitu vyeupe kwa ndani. Mwanamke huyo alionekana kuwa na haraka kutaka kuondoka, lakini wakamzuia kwanza, mmoja wao akachomeka kidole kwa ndani na kukitoa kikiwa na unga mweupe, kisha akakilamba. Kwa haraka Lexi akatambua yalikuwa ni madawa ya kulevya. Wanaume hao wakamwachia mwanamke huyo, naye akaondoka upesi.

Lexi akatikisa kichwa kidogo, kisha akajiondokea hapo. Alipokuwa akitembea njiani kurejea kwenye gari lake ili aende kule walikoishi, alishangaa kumwona tena mwanamke yule akiwa anakimbia kwa kasi sana, na ndipo wanaume wale wakaonekana wakimkimbiza kwa nyuma. Lexi alijiuliza tatizo lilikuwa ni nini, lakini kwa kuangalia sehemu ambayo mwanamke huyo alikimbilia akajua hangefika mbali nao wangemkamata na hata kumfanyia jambo fulani baya. Akaamua kuelekea huko pia ili kujua nini kingefuata.

Alifika mpaka sehemu ambayo aliwakuta wanaume wale wakipiga kitu fulani chini kwa miguu yao kikatili sana. Alizisikia pia kelele za vilio za mwanamke yule, naye akatambua watu hao walikuwa wakimpiga namna hiyo. Hakukuwa na watu wengine sehemu hiyo, hivyo Lexi akafika hapo upesi na kuwasukuma kwa nguvu, nao wakasogea pembeni huku wakimtazama. Alipomwangalia mwanamke huyo, alikuwa amejikunja chini huku akitoka damu puani na mdomoni, naye akamwonea huruma sana.

Mmoja wa wale wanaume akamfata Lexi na kutaka kumpiga, lakini akawahi mkono wake na kuukunja, kisha akauvunja. Jamaa alipiga kelele kama jogoo anayewika (ila sauti iendelezwe), naye akaanguka chini. Wengine wakashangaa sana, nao wakamfata Lexi ili kumshambulia, lakini akawachambua wote kama karanga. Walifanikiwa tu kumpiga sehemu chache za usoni na mgongoni, lakini wote wakaambulia kulala chini huku wanakoroma kwa maumivu. Lexi alikuwa anapumua kwa nguvu, kisha akamwangalia mwanamke yule, ambaye alikuwa anamtazama kwa wasiwasi.

Mwanamke huyo akajitahidi kunyanyuka na kuanza kukimbia, akifikiri Lexi ni askari. Lexi akaanza kumfukuzia pia mpaka akamshika na kumsukumia ukutani.

"Don Allah kar ka cutar da ni... (tafadhali usiniumize)" mwanamke huyo akaongea kwa kikabila.

Lexi akawa anamwangalia tu asielewe anamaanisha nini.

"Ba ma gaske ba ne... ba zan iya sake shiga kurkuku ba... don Allah.... (hata hazikuwa halisi.. siwezi kurudi jela tena.. tafadhali...)"

"Shut up!" Lexi akamwambia kiukali kidogo.

Mwanamke huyo akabaki kumwangalia huku akiwa amekunja sura kuonyesha alihisi maumivu. Lexi akamvuta na kuanza kuondoka naye. Akampeleka mpaka sehemu aliyoacha gari lake na kumwingiza, kisha akaanza kumpeleka kule walikoishi. Njia nzima hawakusemeshana lolote, na mara kwa mara mwanamke huyo angemwangalia kwa wasiwasi, lakini pale ambapo Lexi angemwangalia tu, angekwepesha macho na kutazama pembeni.

Walipofika, ilibidi Lexi alazimishe kumvuta kwa sababu alikuwa akigoma kwenda kwa kuhofia usalama wake kutokana na kutoijua sehemu hiyo iliyokuwa mbali, na imejitenga sana. Akampeleka mpaka ndani ya nyumba, na wale waliokuwepo wakashangaa. Alikuwepo Torres, Victor, na Oscar.

"Who's this? Why'd you bring her here? (Nani huyu.. kwa nini umemleta hapa?)" akauliza Victor.

"Found her getting beat up from her boyfriends. I don't think she speaks English... or not (nimemkuta anapewa kipigo na wapenzi wake. Sidhani kama anazungumza kiingereza.. au la)," akasema Lexi.

"Man! Look at her (Dah! Hebu mwangalie)," Torres akasema huku akisogea karibu.

"Well, what language does she speak? (basi anazungumza lugha gani?)" akauliza Oscar.

"Native aam... Hausa (kikabila.. kihausa)," Lexi akajibu.

"Oh..." Victor akasema na kumsogelea pia.

Mwanamke huyu akawa anawaangalia wote kimashaka.

"Menene sunanka? (unaitwa nani?)" Victor akamuuliza kwa kikabila hicho.

Mwanamke huyo akamwangalia tu.

"Kuna jin turanci? (unaweza kuzungumza kiingereza?)" Victor akauliza tena.

Tena, akabaki kimya.

"Torres, help her... (Torres msaidie)" Lexi akamwambia.

"Okay. Hey... come on, let's go (Sawa.. wewe, twende)," Torres akamshika kiupole na kuanza kuondoka naye.

Wote walikuwa wanamwangalia kwa huruma kiasi. Torres akawa amempeleka kwenye chumba chenye vifaa vya kitiba ili kumpa huduma za kupunguza maumivu yake.

"You sure boss is gonna go cute with you bringing a total stranger here? (Unadhani 'boss' atapenda wewe kumleta mtu asiyefahamika hapa?)" Victor akamuuliza Lexi.

"You were a stranger (Hata wewe ulikuwa haufahamiki)," Lexi akamwambia.

"Boom! Burned... hahahahah (umeunguzwa)," Oscar akamwambia Victor kiutani.

Lexi akawaacha na kwenda chumbani kwake.


★★


Baadaye, Kendrick na Mensah wakawa wamerejea kutoka safari yao mida ya usiku. Oscar, akiwa pamoja na Victor, akamwambia Kendrick kwamba Lexi alikuwa ameleta mgeni mwingine hapo leo, naye Kendrick akamwambia amwite Lexi. Baada ya kufika, Kendrick akamuuliza ni nini kilikuwa kinaendelea. Lexi akaelezea jinsi alivyoyaona mambo yaliyotokea, na kusema alimwonea huruma mwanamke yule kwa kuwa watu wale wangemuua ikiwa asingemsaidia.

Kendrick akamwambia Lexi halikuwa jambo la busara kuleta mtu yeyote tu hapo bila kumjua vizuri kwa sababu ingekuwa hatari kwa mambo yao mengi. Akamuuliza baada ya kumpatia huo msaada nini kingefuata sasa? Atoke nje huko na kwenda kumwambia mtu fulani ambaye atamwambia mtu fulani kuhusu sehemu hii waliyokuwa? Lexi akatazama tu chini akitafakari maneno ya "uncle" wake, naye Kendrick akamwambia Oscar akamlete mwanamke huyo hapo. Bila kukawia Oscar akamfata na kufika naye.

Mwanamke huyo alikuwa amevaa nguo safi sasa; sweta la mikono mirefu na kaptura ya kijani yenye mifuko mingi. Sehemu hii waliyokuwemo ilikuwa kama ofisi ya ndani ya Kendrick, naye Torres akafika hapo pia kukamilisha kundi lao lote. Mwanamke huyo akawa amesimama mbele ya meza pana kiasi ya kioo, ambapo alitazamana uso kwa uso na Kendrick aliyeketi kwenye kiti chake upande wa pili. Alikuwa amewekewa bendeji ndogo usawa wa jicho lake, na mdomo wake wa chini ulivimba kidogo. Akamwangalia Lexi kiufupi, kisha akamtazama tena Kendrick. Kwa kumwangalia tu alitambua kwamba Kendrick bila shaka ndiye aliyekuwa fahali kwenye zizi hili.

"What's your name? (jina lako nani?)" Kendrick akamuuliza.

"I don't think she understands English. Anaongea tu Hausa language (sidhani kama anaelewa kiingereza.. anazungumza tu kihausa)," akasema Victor.

"LaKeisha," mwanamke huyo akasema.

Wote wakamwangalia.

"What?" Kendrick akauliza.

"LaKeisha. That's my name (LaKeisha.. hilo ndiyo jina langu)," akasema tena.

"Sucks to be you," Oscar akamtania Victor, akimaanisha hakuwa sahihi kufikiri mwanamke huyo hajui kiingereza.

"Kumbe anajua... why the hell were you quiet all that time? (kwa nini sasa ulikuwa kimya muda wote huo?)" Victor akamuuliza.

LaKeisha akabaki kimya tu. Wakati huu alionekana kama vile haogopi, bali yuko makini.

"How old are you? (miaka yako mingapi?)" Kendrick akamuuliza.

"I'm 25," akajibu Lakeisha.

"I understand my niece helped you today from an unpleasant crisis. Mind telling me why those men were beating you up? (naelewa mpwa wangu amekusaidia leo kutoka kwenye shida fulani.. unaweza kuniambia kwa nini wanaume hao walikuwa wakikupiga?)" Kendrick akamuuliza.

LaKeisha akatulia kidogo, kisha akaanza kuongea.

"Those men are drug dealers. I was set by my boss to bring them a package, and in return they'd give me money to take back to him. They gave me the money, but then all of a sudden they started attacking me... until your daughter found me... and helped me... (wanaume wale wanafanya kazi ya madawa ya kulevya.. nilipangwa na 'boss' wangu kuwapelekea mzigo, halafu wangenipa pesa ili nimpelekee, lakini ghafla wakaanza kunishambulia.. mpaka mwanao alipokuja kunisaidia..)"

LaKeisha akayasema hayo na kumwangalia Lexi tena.

"Why would they just start... attacking you? (kwa nini wangeanza tu kukushambulia?)" Mensah akamuuliza.

"Because I cheated (kwa sababu nilidanganya)," LaKeisha akasema.

"With what? (na nini?)" akauliza Oscar.

"With the drugs. They were fake (na madawa.. yalikuwa bandia)," Torres akajibu kwa ajili yake.

LaKeisha akatikisa kichwa kukubali.

"Why'd you do that? What about your boss? (kwa nini ulifanya hivyo? vipi kuhusu boss wako sasa?)" Mensah akauliza tena.

"I had a huge debt... that I owed another man. I wanted to clear it out first because he was going to kill me if I didnt, and my new boss... he shouldn't have known about that. So I sold those goods elsewhere and paid off the other guy, and then... (nilikuwa na deni kubwa sana kwa mtu mwingine.. nilitaka kulifuta kwanza kwa sababu angeniua kama nisingemlipa, na boss wangu mpya hakutakiwa kujua.. kwa hiyo niliuza madawa aliyonipa kwingine ndiyo nikamlipa yule wa zamani, halafu..)" akaishia tu hapo na kuangalia chini.

"You made fake goods and went out to sell them to the men whom you were supposed to give the real ones. Good thinking! You got bruised all over your face to show that (ukatengeneza madawa bandia na kuyapeleka kwa wale uliotakiwa kuwapa yale halali.. una akili sana! uso wako wote umejaa majeraha kuonyesha hilo," Torres akasema kikejeli.

"So what happens now that you've lost your new boss' goods and the money? (kwa hiyo nini kitafuata sasa kwa kuwa umepoteza bidhaa za boss wako wa sasa na pesa yake?)" Lexi akauliza.

"He's going to kill me! I don't know what I'm going to do (Ataniua!.. yaani sijui nitafanya nini)," LaKeisha akasema.

"Well its your fault. I'd kill you too (ni makosa yako.. hata mimi ningekuua pia," akasema Mensah.

"I had no idea they were smuggling drugs in this country. What type were they? (sikujua kulikuwa na biashara za madawa hii nchi.. yalikuwa ya aina gani?)" akauliza Oscar.

"Cocaine... heroine," LaKeisha akasema huku akiwa ametazama chini.

"Damn!" Oscar akashangaa.

Kendrick akatazamana na Lexi kwa makini. Ni kama walikuwa wanaongeleshana kwa macho yao.

"Boss... what are we going to with her? You know we can't just let her walk out of here (mkuu, tutamfanya nini huyu? unajua hatuwezi kumwacha aondoke hapa)," akasema Victor.

"Yeah. I think we should just help her boss with the killing. She'll definitely talk this place out with the first knucklehead she meets, all thanks to Lexi (ndiyo.. nafikiri itakuwa vyema tukimsaidia tu boss wake kumuua huyu.. maana bila shaka ataenda kuropoka huko nje kuhusu sehemu hii na mpuuzi wa kwanza atakayekutana naye.. hiyo yote kwa sababu ya Lexi)," Mensah akasema.

"Aagh... f(...) you," Lexi akamwambia Mensah.

"No... no I wouldn't. I swear. I can't go back there again, he'll kill me. I... please help me. I'll do anything for you sir. I'll be your slave if you want... I will. I won't betray you sir, please... (Hapana... sitafanya hivyo.. naapa.. siwezi pia kurudi huko, ataniua.. tafadhali nisaidie.. nitakuwa hata mtumwa wako ukitaka.. sitakusaliti bwana wangu, tafadhali..)" LaKeisha akawa anamwomba Kendrick kwa hisia.

"Betray? Bitch, you don't even know us! (kusaliti? hata hautujui, malaya wewe!)" akasema Mensah.

LaKeisha akamwangalia Lexi kwa njia ya kumwambia amwonee huruma. Lexi akamtazama tena Kendrick, naye LaKeisha akamwangalia pia.

"What's your boss' name? (boss wako anaitwa nani?)" Kendrick akamuuliza.

"Abbo-... Abbo-Pierre Kwame," LaKeisha akajibu.

Kendrick akatulia kidogo, kisha akauliza, "You'll do... ANYTHING? (utafanya.. CHOCHOTE?)"

"Yes sir... I'll do anything you want (ndiyo.. nitafanya chochote unachotaka)," LaKeisha akasema kwa uhakika.

"Take off your clothes (vua nguo zako)," Kendrick akamwambia.

"Uncle..." Lexi akasema kimshangao kiasi.

Oscar akaanza kuchekelea. Wanaume wote walikuwa wanamwangalia LaKeisha wakisubiri itikio lake, naye akaanza taratibu kuvua nguo. Alivua sweta na kubaki na T-shirt nyepesi, kisha nayo akaitoa pia na kubaki na sidiria nyekundu iliyoonyesha sehemu ya juu ya matiti yake. Kisha akaivua kaptura na kubaki na tight nyeusi iliyofikia chini ya mapaja yake, nayo pia akaitoa na kubakiza chupi nyeupe (tena kandambili). Oscar akamtania Victor kwa ishara kuwa alikuwa ameanza kudindisha, naye Victor akacheka kidogo. Lexi na Torres walisumbuliwa kiasi na jambo hilo, nao wakawa wanajiuliza nini maana ya Kendrick kumwambia afanye hayo. Kendrick alikuwa tu akimwangalia mwanamke huyu kwa umakini.

LaKeisha alipoanza kuishusha mikanda ya begani ya sidiria yake, Lexi akamwahi na kumzuia.

"Nafikiri hiyo inatosha," Lexi akamwambia Kendrick.

"Okay. Kama uko tayari kuvua nguo kwa ajili ya mwanaume wa kwanza anayekupatia msaada, basi wewe hauna faida yoyote kwangu," Kendrick akasema.

"What was that?" LaKeisha akauliza kwa kutoelewa.

"Its nothing, put your clothes on... (siyo kitu.. vaa nguo zako)" 

Lexi akamwambia hivyo Lakeisha, naye akatii. Kisha akamsogelea Kendrick. 

 "Uncle, huyu msichana anahitaji msaada. I know, I know hujapenda mimi kumleta, lakini sikuona njia nyingine salama ya kumsaidia hasa kwa sababu ya mishe alizojiweka ndani yake...."

"Hilo siyo tatizo langu," Kendrick akamwambia.

"Basi niruhusu nilibebe mimi," Lexi akasema kwa uhakika.

"Unajua Lexi... huyu ni aina ya mwanamke ambaye akiona anakaribia kuanguka atakuangusha pamoja naye. Sitaki kukuona unaburuzwa namna hiyo," Kendrick akamwambia.

"Labda uko sahihi... labda hauko sahihi. Nipe nafasi nimsaidie. Hatuwezi kujua matokeo yatakuwa vipi sikuzote, lakini hiyo haimaanishi tuache kujaribu. Please uncle..." Lexi akamwomba.

Kendrick akashusha pumzi tu huku akimwangalia Lexi kwa umakini. Kisha akamtazama LaKeisha, ambaye alikuwa amemaliza kuvaa nguo zake zote.

"She's all yours (yeye ni wako sasa)," Kendrick akamwambia Lexi.

Kisha akanyanyuka na kuondoka hapo, akifuatwa na wengine isipokuwa Lexi na Torres. Torres akamwangalia tu Lexi kwa njia ya kuuliza kama ana uhakika na jambo alilochagua kufanya, naye Lexi akamwonyesha kwa ishara ya kichwa kuwa angefanikiwa tu. Kisha akatazamana na Lakeisha, ambaye alikuwa anamwangalia kwa matumaini mengi sana, naye akampa tabasamu dogo kama kumtia moyo.

★★★★★★★★★★

 ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Previoua Next