Reader Settings

“Edna simu yako inaita”Aliongea Blandina na kumfanya Edna kusimama  huku akieguka na kumwambgalia mama mkwe wake wa mchongo.

Aliekuwa akipiga ni Roma kwani jina lilisomeka hivyo kwenye skrini juu  n ahata Blandina aliliona na hakujua ni kwanini Roma alikuwa akipiga simu.

Edna aliichukua na baada ya kuona jina ni Roma alijikuta  akitamani kukata , lakini aligundua kuwa  Mama yake Roma anamwangalia , hivyo hakuwa na jinsi na kupokea.

“Unasemaje?”

“Em.. Babe wife  natumaini unafurahia kampani ya watto kuliko mimi mumo”Aliongea Roma upande wa pili.

“Ongea nipo kwenye haraka”Aliongea Edna  huku akipandisha kisirani.

“Kuna jambo Bi Wema alisahau kukuambia  asubuhi , hivyo kaniomba nikueleze , alishatafuta  kampuni ambayo  itahusika na kutuhamisha”Aliongea Roma na kumfanya Edna akumbuke kwamba siku kadhaa nyuma alijadiliana na Bi Wema juu ya  kuhamia Osterbay. Kwenye nyumba yake kubwa.

“Nilisahau kabisa… wewe unaonaje?”Aliongea Edna huku akishusha sauti chini.

“Kwanini unaiuliza hivyo, mimi nimekupatia taarifa hivyo”

“Lakini pia una maamuzi kwanini kila kitu lazima nikitolee maamuzi  mimi , nafasi yako ni ipi?”Aliongea Edna huku akianza kukosa utulivu.

“ Edna nini kinaendelea  huko kituoni mbona unaongea kama haupo sawa?”Edna alifikiria kidogo na kisha akamgeukia  Blandina kama vile anasoma jambo kutoka kwake.

“Kama kampuni  ya uhamishaji ishafika  mnaweza kuendelea  na vitu muhimu  vya kuhama navyo , kuhusu chumba changu vitu viachwe kama vilivyo mpaka nitakaporudi”Aliongea

“Okey  nitamueleza”Aliongea Roma na kisha simu ikakatwa .

“Mama nilisahau  siku ya leo tulikuwa na mpango wa kuhamia Osterba kwenye nyumba kubwa”Aliongea Edna akimwangalia  Blandina.

“Ooh!... Edna tunapaswa kurudi na kuangalia utaratibu wa uhamishaji  wa vitu” Edna alifikiria maneno ya Blandina na akaona  ana pointi ya msingi , lakini bado moyo wake ulikuwa ukitaka kumuona Lanlan.

“Edna  yule mtoto  sijui kakufanya nini , ila kwa sasa atakuwa na wazazi wake,,, najua unapenda Watoto sana na natamani siku uje upate wa kwako utakuwa mama mzuri”Aliongea Blandina na kumfanya Edna kushangaa  kidogo ukweli wazo  la kuzaa bado  halijawahi kujia akililini na muda huo ni kama limeingia upya.

“Kweli , lanlan atakuwa na wazazi wake  kwasasa , sipaswi Kwenda  nyumbani kwao”Aliwaza Edna na kisha akakubaliana na Blandina warejee nyumbani kwa ajili ya kusimamia  uhamaji wao kwenye nyumba yao ya zamani.

Dakika arobaini na tano ziliwatosha kabisa  kufika nyumbani  na  gari kubwa la kubeba mizigo lilikuwa ndani ya nyumba yao na wafanyakazi wa kampuni ya uhamishaji   walikuwa  wakiendelea na kazi.

Edna alirtoa maelekezo ya baadhi  ya  vitu vya  kawaida kuacha hapo ndani kwa mfano  vifaa vva kielectronics   na baadhi ya samani nah io ni kutokana  nyumba ya kule Osterbay ilikuwa na kila kitu.

Roma aliekuwa akisaidiana na  wafanyakazi kubeba baadhi ya  vitu muhimu, alishindwa kuelewahali aliokuwa nayo Edna , ni kama kulikuwa na kitu ambacho alikihisi  wakati Edna anaingia hapo ndani  ambacho hakuwa nacho tokea aonane nae kwa mara ya kwanza.

“Edna.!!”Aliita Roma baada ya kufungua mlango na kuingia ndani ya chumba cha  Edna taratibu na Edna  hakuongea chochote  baada ya kuingia Zaidi ya kujiweka bize na  anachokifanya , Edna alikuwa akipangilia baadhi ya vitu vya kuhama navyo.

“Edna  nini kimetokea mlikotoka ,  nahisi haupo sawa kama ulivyoondoka asubuhi”Aliongea Roma   lakini Edna alikuwa akiendelea na  anachokifanya huku akiwa amempa mgongo  Roma  na alionekana kuchangua baadhi ya vitu kwenye kabati  lake  pasipo mpangilio maalumu ni  kama mtu  ammbaye alikuwa akitafuta kitu muhimu pasipo kukipata na Roma aliona jambo hilo na kuishia kutabasamu , kuna kitu ambacho hakikuwa cha kawaida  kutoka kwa Edna ambacho  alikuwa  akikihisi kutoka kwake , lica ya kumwangalia Edna kwa macho yake  na kuona mwili wake hauna shida lakini kuna mabadiliko makubwa  kutoka kwa Edna ni kama vile   mtu anapokaribia eneo la hatari  zile hisia   zinazomjaa mtu ndivyo ilivyokuwa kwa Edna wakati anaingia hapo ndani akiwa na Mama yake.

Roma  baada ya  kuona ajibiwi alikata hsauri ya kumsogelea  na kumkumbatia kwa nyuma na kumfanya Edna asimame wima huku  akitulia kama mtu anefikiria  hatua ya kuchukua  kwa tukio ambalo kafanyiwa.

Roma alifahamu  Edna angeleta shida kwa  kumkumbatia kwa nyuma , lakini  majibu yake yalikuwa nje ya mategemeo yake , kwani  aligundua  Edna Zaidi ya kuleta  ukinzani alianza kulia kwa kwikwi na kumfanya  Kushangaa,  mbaya ni kwamba sasa staili ya namna Edna anavyolia ni  tofauti na aliokuwa ameizoea  , Edna alikuwa akilia kwa kwikwi huku akiwa ameshikilia moyo wake  ni kama mtu ambaye amepoteza kitu kikubwa kwenye Maisha yake.

Roma ilibidi amuache Edna aendelee kulia atakavyo , alijua moja kulia ni sehemu ya mtu kutoa sumu moyoni na ndio maana hakutaka kumzuia Edna kutoa kilio, lakini licha ya kwmaba alikuwa amemuacha Edna kulia , lakini moyo wake ulikuwa ukiuma ajabu, hakupenda kumuona Edna analia  na pia alijiambia Edna ni mwanamke ambaye siku zote anajua ni imara katika kuziendesha hisia zake na ndio maana hakuwa mtu wa kuwaza sana , lakini kitendo cha Edna kulia waziwazi mbele yake, lakini pia mabadiliko ya Edna aliokuwa nayo vilimfanya kuwa na wasiwasi na kuwa na uchungu kwa wakati mmoja.

Roma ilibidi amsogelee Edna alierudi kukaa kitandani na kisha kumkumbatia na kumruhusu Edna kulia kwenye kifua chake.

“Edna niambie ni nini kimetokea kituoni leo?”Aliuliza Roma baada ya Edna kunyamaza huku akijifuta machozi na kusimama na kuanza kuweka nguo zake kitandani.

“Hakuna kilihotokea”Aliongea Edna huku akirudiwa na hali yake, Roma alijiambia kama Edna ndani yake kulikuwa na pepo , pasi hhilo pepo ni la  aina yake kwani lilikuwa likimuenbdesh Edna kwa  namna ambavyo sio ya kawaida.

Roma alijiuliza inakuwaje mtu dakika kadhaa nyuma alikuwa akilia kama mtoto , lakini sasa hivi anaonekana kama vile sio yeye na ukauzu wake kurudi kama kawaida, Roma kwa jinsi alivyomuona Edna aliamini kabisa hapo hakuna maongezi tena ya kuendelea kwani Edna asingeongea chochote.

“Unamaanisha kweli hakuna kilichotokea au unanikalia kimya”Aliuliza Roma.

“Roma.. nishasema hakuna kilichotokea”Aliongea Edna huku akiendelea na kazi yake ya kuanza kupangua nguo  baadhi na kuziweka kitandani .

“Kama hakuna kilichotokea kwanini ulikuwa ukilia kama mtoto dakika moja iliopita?”Aliongea Roma na kumfanya Edna kusimama  na kumgeukia Roma na kumwangalia usoni , ni kama alikuwa akaitafuta jibu  la kumpatia.

“Sijui.. nilijikuta natamani kulia  na sababu sina”Aliongea Edna kinyonge na kisha akageukia kabati na kuendelea.

Upande wa Roma alitamani kucheka , yaani alishindwa kabisa kumuelewa Edna na alijiambia  sijui ni lini ataweza kumuelewa  maana    alioan muda mwingine Edna  hakuwa mtu wa kawaida , alijiuliza inakuwaje mtu kulia  pale anapojiskika pasipo kuwa na sababu maalumu.

Roma alimwangalia Edna kwa dakika kama nne huku  Edna akijifanya hajali uwepo wake na baada ya hapo aliamua kupiga hatua kutoka nje.

“Romaa..!!”Aliita Edna kabl aya Roma kufunga mlango na Roma aligeuka na kumwangalia.

“Juzi niliwaambia Daudi na Wendy  wakutafute juu ya maswala ya kampuni , ila sijapata mrejesho wa kile kinachoendelea”Aliongea Edna na Roma alitabasamu.

“Boss  unataka ripoti hio  sasa hivi?”Aliuliza Roma kiutani , lakini Edna aliendelea kuwana  mwonekano wake uleule na kisha aktingisha kichwa.

“Unahisi  siwezi kuongoza vyema kampuni , kama ulikuwa huamini kama naweza kuongoza kwanini umenipatia  niongeze”Aliongea Roma.

“Nimekuuliza kwa ajili ya  kupata mipango yenu , sijawahi kufanya maamuzi ambayo nitajutia  baadae , amini  kwamba nayaamini maamuzi yangu” Aliongea Edna.na Roma alirudi  nyuma na Kwenda kuketi kwenye kitanda.

“Njoo ukae hapa kwanza  pembeni yangu”Aliongrea Roma hhuku akipa ishara Edna ya kusogea mpaka  kitandani lakini Edna alijikuta kukosa maamuzi kwa  dakika kadhaa, lakini mwishowe alisogea na  kuketi  kitandani.

Sasa kitendo  cha Edna kuketi kitandani tu , alijikuta akifanyiwa shambulio ambaclo hakulitegemea kwani Roma alimbeba juu  kama mtoto na kubwaga  katikati ya kitanda ,  wakari Edna hajachuku hatua   juu ya kipi cha kufanya , alijishutikia Roma yupo juu yako.

“Roma..Acha..”Aliongea Edna kwa kusitasita , kwani mpaka hapo alikuwa shajua  Roma anataka kufanya nini.

Previoua Next