Ukweli ni kwamba pengine Eliza hakuwa akijua tu vizuri lakini eneo hilo lilianzishwa na Mjerumani mmoja aliefahamika kwa jina la Bruno , ilikuwa ni eneo ambalo kazi yake kubwa ni kuvuna viungo vya binadamu na kuvisafirisha nje ya nchi.
Baadae serikali baada ya kuingilia ndio ikabadilishwa kutoka kuwa sehemu ya kuvuna viungo na kuwa kituo cha wagonjwa wenye magonjwa yasiowezekana kupona na msimamizi wa hilo eneo anaitwa Dokta Ivan B Bridge ni mtanzania halisi kwa kuzaliwa licha ya kuishi sana nje ya nchi kabla ya kurudi tena , chimbuko lake ni familia za kikoloni zilizotawala Tanganyika katika eneo hilo na kujikita katika biashara ya kilimo cha Katani.
Lakini licha ya eneo hili kufahamika kama hospitali na makazi ya Dokta Bridge lakini ndio sehemu ambayo biashara ya kimagendo ya kuuza viungo ilikuwa ikifanyika kwa usiri mkubwa mno, vijana wengi waliokuwa wakihitaji kuuza figo zao koneksheni ilikuwa ni kuja ndani ya hilo eneo.
Hoteli ya Troitsa ndio sehemu ambayo wauza viungo na wale wanaotaka kununua hutumia kama makazi mpaka kupata huduma na mara nyingi wanaofikia ndani ya hoteli hio wanapata huduma bure kabisa kama ilivyokuwa kwa Hamza.
Ni eneo lenye ulinzi mkali na asilimia kubwa ya wagonjwa wanaoingia hapo ni wale wanaojiweza ki uchumi , walikuwa wanaingia mpaka wagonjwa kutoka nje ya nchi kwa kigezo cha kupata huduma ya tiba ya muda mrefu lakini ukweli in kupandikizwa viungo.
Ukiachana na hayo yote Profesa Bridge ni mwanachama mwenye cheo kikubwa tu katika shirika la Utatu giza(Black Trinity)
Hamza mara baada ya kutoka kwenye gari akiwa ameambatana na Eliza walisogea kuingia ndani ya eneo hilo , lakini kabla hawajapita kwenye kizuizi walizingirwa na mabodigadi waliovalia nguo nyeusi na ilikuwa ni kama walikuwa wakimsubiria.
Hamza aliishia kutoa tabasamu baada ya kuona ni kama alivyotarajia na aliishia kumwangalia bwana wa kizungu ambae alionekana ndio kiongozi.
“You can’t be Van Bridge, right?”Aliongea Hamza akimaanisha bwana huyo hawezi kuwa Van Bridge.
“Master hana muda na nyie , ameniambia mnipatie fedha , kiasi milioni mia sita , mkimaliza kulipa baba yenu ataachiwa huru”Aliongea yule bwana kwa lugha ya kiswahili licha ya uzungu wake.
“Kwanini ni milioni mia sita na sio Mia tatu?”
“Mkataba wa mkopo ndio unavyotaka, milioni mia tatu zilizoongezeka ni riba ya mkopo , baba yako alikubali kipengele za kulipa asilimia hamsini ya madini yatakayopatikana , lakini madini hayakupatikana , Bosi ni muungwana hakutaka kupiga hesabu kamili hivyo ameweka milioni mia tatu pekee ya Riba”Aliongea yule bwana yule na kumfanya Eliza kuhisi kiungulia cha kifungua kinywa alichopata asubuhi , zilikuwa hela nyingi mno ambazo hata kama angekopa asingeweza kulipa.
Upande wa Hamza hakushangaa sana , hilo ni swala ambalo alitegemea kukutana nalo.
“Najua Van Bridge hajaniita kwa kuniharakisha kwasababu ya kuja nimlipe hiko kiasi , achana na usaili wako nataka kuonana na bosi wako, maana sijaja hata na mia hapa”Aliongea Hamza.
“Huwezi kupita hapa bila ya hela , unakujaje mikono mitupu kwa kujiamini namna hio, kama unataka kumuona bosi pita kwangu kwa nguvu tuone”Aliongea yule mzungu kwa kujiamini.
Baada ya kiongozi wao kuongea maneno hayo , wale mabidigadi wote walikaa mkao wa tahadhari ya kushambulia , Hamza aliishia kumrudisha Eliza nyuma huku akianza kuwasoma mmoja baada ya mwingine kutoka pande zote. Hakusubiri hata wao waanze kushambuia, akiwa ni kama anamzunguka Eliza alimshambulia bodigadi aliekuwa karibu yake na teke moja tu alidondoka chini kama mzigo.
Yule bwana wa kizungu alijikuta akishangaa maana ni kitu ambacho hakukitegemea , alikuwa ameshamdharau Hamza kwa muonekano wake, lakini hata hivyo hakutaka kumwangalia Hamza anamshambulia bodigadi wake mwingine , hivyo mara baada ya kuona nafasi azimu alisogea kwa spidi huku akiwa amekunja ngumi yake na kutaka kumpiga nayo Hamza tumboni.
Hamza ilikuwa ni kama amemuwekea tumbo vizuri ili ampige , lakini kabla hata hajamfikia mkono wake wa kushoto ulimdaka na kisha kupindisha kiganja cha mkono.
“Arghhhhhhhhhhh”
Yule bwana wa kizungu alijikuta akitoa yowe la hali ya juu mno , mkono wake ulishikwa na maumivu makali mpaka ukafa ganzi.
“Unaonekana una mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kwa kutumia njia ya kufanya mapenzi , lakini kitu ambacho hamjawahi kuelewa hio mbinu haina matokeo mazuri kwa mtu ambae ndio anaanza mafunzo , unahitaji msingi wenyewe wa mafunzo kabla ya kuvuna nishati, la sivyo utaishia kuongeza mvuto wa kingono na nguvu za mapambano huna”Aliongea Hamza.
“Who the hell are you?”Yule Mzungu alijikuta akipagawa mara baada ya kusikiliza maneno ya Hamza.
“Si wote mshalisikia jina langu ,au mnataka nianze upya kujitambulisha , niambie ni wapi alipo Ivan la sivyo nitaendeleza”Aliongea Hamza kwa jeuri.
“Master yupo kwenye chumba cha upasuaji?”
“Upasuaji gani unafanyika hapa ndani?”Aliuliza Hamza huku akiwa na mshangao huku upande wa Eliza akishikwa na hofu kwa kuamini pengine ni baba yake anaefanyiwa upasuaji wa kuondolewa viungo vya mwili.
“Ni mkuu wetu ndio anaefanyiwa upasuaji na washirika wote wapo hapa wanasubiri”Aliongea.
“Kuna mkuu wenu?”
“Kama hakuna mkuu unadhani hili eneo linaendeshwa na nani, namaanisha mtoto wa bosi Bridge tunamwita Mkuu”Aliongea.
“Kama washirika wote wapo hapa , je ni kwasababu operesheni ni ngumu na ya hatari au kuna kipi kingine?”
“Ndio ni ya hatari , ni upasuaji wa moyo , halafu kwanini maswali mengi?”
“Upasuaji wa moyo?”Hamza alijikuta akishangaa huku akijiambia pengine hilo eneo halikuwa la kawaida kama alivyodhani.
“Hebu nipeleke na mimi nikajionee”Aliongea huku akishikwa na msisimko wa kuona kinachoendelea.
“Hata kama uwezo wako wa kimapigano ni mkubwa kuliko wangu haimaanishi unaweza kuingia na kusumbua madaktari ambao wapo kazini na ukaachwa hivi hivi”Aliongea.
“Umenielewa vibaya mkuu , mimi situmii nguvu kuingia , kama ni upasuaji wa moyo basi mimi ni daktari bingwa wa huo upasuaji, haitakuwa tatizo pengine naweza kusaidia”
“Nini!, wewe ni mtaalamu wa upasuaji wa moyo?”Aliuliza kwa mshagao lakini kabla hata Hamza hajajibu, simu ya yule bwana iliita.
“Mruhusu Dokta Hamza aingie” Ndio alivyosikia na kuzidi kutokwa na macho ya mshangao.
Eliza alitamani kutokuingia lakini kutokana na hofu ya baba yake kutolewa viungo aliamua kuingia na Hamza.
Baada ya wote wawili kuingia kwenye lift na kushushwa chini kwenye vyumba Hamza aijikuta akishangaa baada ya kuona mazingira ndani ya hospitali hio , ilikuwa ni eneo ambalo lina kila kifaa cha teknolojia ya hali ya juu , ilikuwa ni sahihi kusema ni taasisi ya daraja la kwanza ya kitabibu.
Sehemu iliokuwa ni kama ukumbi , kulikuwa na kusanyiko kubwa la watu waliokaa kwenye viti huku macho yao yakiangalia runinga kubwa iliokuwa ikionyesha kinachoendelea, moja wapo ya watu hao alikuwa ni Dokta Bridge mwenyewe , watu wote walionekana kuwa na ukwasi wa pesa kutokana na sura zao na mavazi yao huku wakiwa wamezungukwa na kundi la mabodigadi.
“Nini kinaendelea?”Aliuliza bwana mmoja aliekuwa na muonekano wa kizungu , alikuwa mzee hivi na nywee zake zilikuwa nyeupe.
“Dokta Hamza amefika”Aliongea yule bodigadi mzungu na kumfanya yule mzungu kukunja sura kama amekula pilipili.
“Nani kasema Hamza ni dokta , inakuwaje mwanafunzi wa chuo cha uchumi na dereva ndani ya kampuni kuwa Daktari , umeanza lini kunitania Lamberk?”Aliongea kwa hasira.
“Lakini bosi wewe ndio umesema ni Daktari ni mruhusu”Aliongea kwa wasiwasi kujitetea na bwana yule wala hakujali na macho yake yalimgeukia Hamza.
“Dogo ukiambiwa uje sehemu unafanya safari bila ya kujifikiria, huna msimamo binafsi na nani kakuambia uje na mwanamke?”Aliongea yule bwana tena kwa lugha ya kiswahili.
“Huyu ni binti wa baba uliemteka na mpenzi wangu acha porojo?”Aliongea Hamza.
“Mimi Dokta Bridge ni raia mwema ndani ya nchi hii , siwezi kuteka mtu nniombe radhi kwa kunisingiizia”Aliongea.
“Kama hujamteka umefanya nini? , nyie ndio mliemuingiza kwenye mtego ili aingie kwenye madeni , mmefanya hayo yote kwasababu ipi?”.
“Tunafanya vitu kwasababu nyingi , ikiwemo kujilipa fidia kwa wadeni wetu ambao wameshindwa kulipa kiasi cha pesa ila hatujawahi kuteka mtu”Aliongea.
“Unamaanisha kuondoa viungo vyao vya mwili?”Aliuliza Eliza.
“Binti kuwa makini na unachoongea , hakuna kitu kama hicho hapa ndani , ila baba yako akitaka kutuuzia figo na mwenye kuhitaji akajitokeza litakuwa ni dili zuri”Aliongea.
Hamza alijiambia huyo jamaa sio mzungu kabisa , kuishi ndani ya Tanzania kumemfanya kuwa mswahili.
“Najua sababu ulioniitia hapa ni kwa ajili ya kukusaidia upasuaji wa mtoto wako , sijui umezipatia wapi taarifa za mimi kuwa daktari wakati ni siri yangu , lakini naweza kukusaidia kama upo tayari kutimiza masharti yangu”Aliongea Hamza.
“Well!, japo ni kweli nimesikia taarifa za wewe kuwa daktari , ila siwezi kukuamini na kukupatia mtoto wangu kwa ajili ya kumpasua,haiwezekani kwa kijana kama wewe ambae huna cheo na sikujui vizuri uwe Daktari,hata Leseni unayo?”Aliongea.
“Kama unaamini siwezi kuwa daktari hizi hila zote zilikuwa za nini?”
“Hakuna hila yoyote , taarifa za siri zimenifikia na nikaambiwa wewe ni daktari, lakini sijaweza kuamini wala hakuna uthibitisho wa wewe kuwa daktari..”Aliongea kufikiria kituo na akaishia njiani na kumwangalia Eliza.
“Binti baba yako yupo kwenye mtatizo kwasababu yako , nikikuangalia naona kila sababu kwanini ulikuwa ni shabaha ya Gabusha kama Spiritual host , lakini inasikitisha mpango wake umefeli baada ya kuonja umauti?”Aliongea na kauli ile ilimshangaza Eliza.
“Mzee Gabusha amefariki!!?”
“Anakaribia kufariki”Aliongea.
“Unamaanisha nini kukaribia kufariki?” Aliuliza Hamza awamu hio.
“Hii ni sehemu ya kulaza wagonjwa ambao wamekufa ubongo”Aliongea na Hamza alijikuta akimwangalia Eliza kama kwamba hawakuwa wakiamini.
“Baada ya kusikia una uwezo wa kufanya upasuaji wa moyo nimekataa kuamini lakini sikutaka kudharau pia , Binti nimenunua deni la baba yako kwasababu una mpenzi aneonekana kuwa na ka’uwezo, ni aidha unilipe au yeye anilipe ndio baba yako aachiwe huru au alipe yeye mwenyewe kwa kutoa figo zote mbili”
“Figo zote mbili!?”Aliuliza Eliza kwa mshangao.
“Nani wa kukubali kuingia hasara kwa figo ambazo zimeharibiwa na pombe , binti baba yako hana kiungo kizuri kwenye mwili wake kutulipa vyote vimechakaa”Aliongea na angalau kauli ile ilimfanya Eliza kupatwa na ahueni baada ya kuona baba yake yupo hai.
“Kama umeniita kwa kunidhania mimi daktari basi nipo tayari kulipa deni lote kwa kumfanyia mtoto wako upasuaji wa daraja la kwanza, kama upo tayari kutii masharti nipo tayari kuona medical history na surgery plan kisha nitatoa maoni yangu”Aliongea Hamza.
“Dokta anaefanya upasuaji ni bingwa niliemtoa Italy , Dokta Antonio Salazer si tu ana ujuzi wa upasuaji lakini vilevile amefanikiwa kufanya aina nyingi za upasuaji wa moyo, nimekuita hapa kwa dharula lakini hata kama unaweza kusaidia ushachelewa maana upasuaji ushaanza”Aliongea Dokta Bridge.
Ukweli Hamza hakujua kwanini mzee huyu kaamua kumfanyia mtoto wake upasuaji ndani ya hilo eneo , alikuwa na hela za kutosha za kumpeleka nje ya nchi kwenye hospitali kubwa , jibu moja tu la makisio yake ni kwamba pengine mtoto wake ni mhalifu na popote atakapoenda atakamatwa, ila kwasababu alikuja kumaliza swala la Eliza alitaka kufanya namna yoyote ile kulipa deni lake.
“Dokta Salazer anaweza mtaalamu , lakini operesheni anayoendelea nayo sio nyepesi , kama kweli unamwamini kumponyesha mwanao kwa asilimia mia moja usingefanya hila za kununua deni ili kufanya hila za kunileta hapa na pili msingekuwa mmekakamaa sura kwa namna hii”Aliongea Hamza huku akiangalia runinga inayoonyesha upasuaji unaoendelea.
Dokta Bridge hakupingana na maneno ya Hamza , hata yeye ni dokta wa upasuaji , licha ya kubobea kwenye upasuaji wa kawaida lakini kama dokta alikuwa akijua kinachoendelea, ndio maana hata alipoletewa Intellijensia na ushirika wake wa Black Trinity juu ya Hamza kuwa mtaalamu wa kitabibu hakuidharau.
Hamza upande wake hakushangaa sana taarifa za yeye kujua kufanya upasuaji wa moyo kumfikia Dokta Ivan Bridge , ukweli ni kwamba chata za fuvu alizoziona ndani ya eneo hilo tokea anaingia alijua fika hii hospitali inaendeshwa na Black Trinity na kama ni hivyo ni rahisi kwa taarifa zake kuvuja kupitia koneksheni za nje ya nchi.
Baada ya dokta Bridge kufikiria kwa muda alitoa maagiizo ya Hamza kupewa taarifa za kimatibabu za mtoto wake Christian, Hamza mara baada ya kupitia pitia ikiwemo picha za CT Scan macho yake yalionekana kama mtu anaefikiria jambo kwa kina.
“Kwa ripoti hii hakuna kitakachofanikiwa”Aliongea Hamza.
“Unasemaje wewe , nini hakiwezi kufanikiwa” Dokta Bridge alimaka.
“Huyo dokta wako unaemuita Profesa Salazer ametumia njia rahisi sana ya kubadilisha Aortic Valve na kuweka bandia, lakini hata kama akifanikiwa katika hili Christian hali yake itakuwa mbaya zaidi na anaweza kupoteza maisha siku chache baada ya upasuaji”Aliongea Hamza , ukweli ni kwamba haikueleweka Hamza ni dokta kweli au anataka kujipatia sifa kwa kuhatarisha maisha ya mgonjwa.
Lakini watu wote waliokuwa ndani ya hilo eneo ni kama hawakumwelewa, hata Eliza hakuelewa na hakuongea chochote licha ya kuwa na mshangao wa kutotaka kuamini Hamza ni daktari, katika mawazo yake Hamza asingeweza kuwa dokta kwa umri wake aliokuwa nao , maana madaktari wa moyo walikuwa wakisoma zaidi ya miaka kumi na tano mpaka kuwa bingwa , udaktari wa aina hio sio swala pekee la kuwa na akili nyingi bali ni swala la kuwa na uzoefu.
“Dokta Bridge , kama unataka mtoto wako kupona basi ni vyema kama utafanya maamuzi haraka na upasuaji kusitishwa na mimi kuendelea nao”
“Unaongea kichekesho gani , wewe ni nani mpaka kwa maneno yako tu tumsitishe Dokta Salazer kuendelea na upasuaj, unajua nimelipa bilioni ngapi na koneksheni kubwa kiasi gani kumshawishi Dokta Salazer kuja kufanya upasuaji wa siri hapa Tanzania?”Aliongea huku awamu hio akifoka.
“Since I dared to say that , I naturally have my own reasons , if you don’t believe me , you can let me confront that professor and see what he’ll say”Aliongea Hamza akimaanisha kwamba kwasababu ana ujasiri wa kusema hivyo basi ana sababu zake na kama haamini ampe nafasi ya kuongea na Profesa anaefanya upasuaji aone ataongea nini.
*****
Masaa nane baadae jina la Hamza lilibadilika moja kwa moja , kila mtu alikuwa akimwita Dokta Hamza Mzee , Eliza hata yeye alishangazwa na uwezo wa Hamza katika wakati wote alioshuhudia akifanya upasuaji na kuelekeza manesi na watu wa ganzi nini cha kufanya.
Ukweli ni kwamba Dokta Bridge hakumwamini kabisa Hamza kwenye maswala ya upasuaji na hakutaka kumruhusu Dokta Salazer amwachie Hamza , hivyo alimwambia Hamza aangalie upasuaji unavyoendelea na atoe ushauri kwa Dokta Salazer ikionekana amekosea.
Lakini sasa upande wa Dokta Salazer ambae aliongea na Hamza kabla ya kuendelea na upasuaji alikasirika sana , kwake alichokuwa akifanya Hamza alikuchukulia kama tusi kwa utaalamu wake aliojijengea kwa muda mrefu , alikuwa ni daktari bingwa na sio mtoto kama alivyokuwa akionekana Hamza.
Lakini Hamza upande wake hakutaka kuonekana mtoto , aliongea kwa kutoa sababu kwanini mpango wa upasuaji anaoendelea nao hautofanikiwa, lakini licha ya hivyo dokta huyo alipandisha mabega na kuamua kutumia uwezo wake wote kutaka kumuonyesha Hamza kwamba yeye ni mzoefu na hajabahatisha kupata cheo cha uprofesa , lakini masaa sita mbele hali ya mgonjwa ilibadilika ghafla na moyo uliacha kudunda kiasi cha kuanza kuhangaika kuurudisha hai kwa kutumia electrical plate kwa ajili ya kuushitua na hata kuufanyia masaji kwa mkono.
Kitendo kile kilimfanya Dokta Salazer kuachia nafasi yake kwa Hamza kwa maagizo kutoka kwa Dokta Bridge , Hamza alikuwa amekwisha kujiandaa muda mrefu kuvaa Scrub na hata kujisafisha hivyo baada ya kuachiwa uwanja alionyesha maajabu ambayo yalimuacha mdomo wazi. Hamza alifanya upasuaji kama vile alikuwa na uzoefu wa miaka hamsini.
Dokta Salazer akili yake haikutaka kuamini kwa umri aliokuwa nao Hamza ameweza kusoma masomo ya udaktari kuhitimu na kisha kujijengea uzoefu.
Hamza hakujali alikuwa akiangaliwa kwa macho ya mshangao, kwa spidi yake ya upasuaji , wala hakujali Eliza ambae alikuwa kwenye mshituko akiwa haamini ni Hamza aliekuwa akicheza na mikasi ndani ya chumba cha upasauji , mchakato ambao ulipaswa kufanyika kwa masaa saba Hamza aliufanya kwa masaaa matatu na nusu pekee.
Mpaka anakwenda kumaliza Profesa Salazer alijiktua akimwangalia Hamza kwa macho yaliojaa maswali, hakuwa na mshangao lakini alikuwa na maswali, ni kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akijaribu kukitafuta kutoka kwa Hamza.
“Hapana, haiwezekani uzushi niliowahi kusikia ukawa kweli, huo muonekano unaendana na mwili wake haiwezekani akawa na miaka mingi tofauti na mwonekano wake”Alijiwazia Profesa Salazer huku akimwangalia Hamza kama kiumbe cha ajabu.
Kwa mtu ambae angeweza kujua mawazo aliokuwa nayo Dokta Salazer basi pengine angeonekana amepandwa na ukichaa, lakini kwa upande wake licha ya upasuaji huo kuisha hakutaka kukubali kirahisi na mpango mpya wa kufuatilia kile alichokuwa akiwaza ulianza kwanzia dakika hio hio.
Ilikuwa ngumu kwa Dokta ambae alikuwa akiaminiwa na nchi nzima ya Italy kushindwa na mtu aliechanganya rangi kama Hamza ambae hana kitu kisichokuwa cha kawaida cha kutisha.
Upande wa Hamza hakujua kama kuonyesha ujuzi wake ambao hautabiriki,ulikuwa umeibua kitu kingine katika kichwa cha Muitali Dokta Antonnio Salazer Slytherin.
*******
Asubuhi siku iliofuata Eliza na Hamza walianza safari ya kurudi Dar Es salaam, isitoshe wote walikuwa na kazi za kufanya kwa siku hio na isingekuwa vizuri kuchelewa.
Kuhusu baba yake Eliza aliachiwa huru na Dokta Bridge alikubali kufuta deni kutokana na kile Hamza alichofanya.
Hamza alipata nafasi ya kujitambulisha kwa baba yake Eliza na mzee huyo mara baada ya kusikia Hamza ndio kasababisha kuachiwa huru alimshukuru sana.
Eliza hatimae alijihisi kuwa huru kwa mara ya kwanza na amani kumrudia, ijapokuwa haikuwa vizuri kufurahia matatizo ya binadamu mwenzake lakini bila ya kupenda taarifa za Mzee Gabusha kuwa mgonjwa mahututi aliekufa ubongo kutokana na kupata ajali zilimpa amani.
Saa tatu asubuhi muda ambao Hamza alikuwa akitoka kwenye treni ya mwendokasi akifikiria kuchukua taksi kumpeleka kwenye kampuni , simu yake iliita na alivyoangalia aliekuwa akipiga ni Shangazi.
“Hamza upo wapi?”Ndio kitu cha kwanza alichoweza kusikia Hamza huku sauti ya Shangazi ikionyesha kuwa na utofauti.
“Nipo nje ya stendi ya treni ya mwendokasi Posta nataka nielekee kazini,nini kimetokea shangazi?”
“Madam.. ametutoka” Sauti ya Shangazi ilionyesha alikuwa akishindana na majjonzi.
Hamza alishikwa na mshituko kwa sekunde kadhaa licha ya kwamba ni kitu ambacho alitarajia.
“Regina anafahamu?”
“Ndio maana nimekupigia , nimeshindwa kumpata kwa simu na nyumbani hayupo, nilijua upo nae”Aliongea Shangazi na kauli ile ilimpa mshituko Hamza na kujua lazima kuna kitu kilichomtokea Regina.
Comments