Reader Settings

  Baada ya kama dakika moja hivi, Sir John alionekana kupata ahueni kidogo lile jinamizi lililokuwa limemkaba lilimuachia. Shati lake la rangi ya bluu bahari lililowa jasho, haikujulikana ni jasho la hofu au ni kwasababu hakuwasha feni lililo ning'inizwa juu. Macho yalimuiva kama ndulele ya mganga.!

Muda huo alimuangalia mzee aliyekaa mbele yake kwenye kiti huku akiwa kaegamiza gongo lake la kutembelea kwenye meza. Kulia kwake kidogo alisimama Nadir. Alijiuliza ni huyu mzee ndiye kamsababishia kukabwa shingo muda mfupi uliopita? Ila hakumshika wala hakuonekana kuchukia kwa maneno aliyoyasema, mzee wa watu alikuwa na tabasamu lake la kawaida la kizee, lakini kwanini hakuonekana kujali? Yaani hakuwa hata na nia ya kumsaidia mwalimu huyo, angalau Nadir alionesha kushangazwa kidogo lakini na yeye hakusaidia chochote. Muda huohuo mzee Sele alisikika;

"Ooooh! Nadir shika hiki chakula nenda ukale haraka uwahi masomo, muda wa mapumziko utaisha...."  Nadir alipokea mfuko huo kutoka kwa mjombaake, kisha akamuangalia mwalimu wake, akatoka nje akiwaacha wawili hao ofisini hapo.

"Mwalimu mbona umemsema vibaya Nadir Yani ninavyomjua leo akiludi nyumbani hapakaliki heheee!" Aliongea kizembe.  Alionekana kama anamdekeza sana Nadir, Nadir nae hakuonekana kumhofia mjombaake kabisa, aliingia na kutoka bila hata kusalimia wala kuongea neno lolote mpaka alivyo toka, hata mwalimu John aliliona hilo na alibaki kumuangalia tu mzee huyo.   Mwalimu John alishusha pumzi ndefu kisha akaendelea kumuangalia mzee aliyekuwa mbele yake muda huo. Mzee alikuwa akitabasamu tu kawaida, Sir John akajipa ujasiri wa kuongea;

"Mzee wangu! Hukuonekana kujali kuhusu hali iliyo nikuta, wewe ndiye uliye nisababishiaa? Ulionekana unajua nilichokuwa napitia..., Na sio wewe tu hata Nadir licha ya kushangaa kidogo lakini hakunisogezea hata chupa ya maji iliyokuwa karibu yake pindi nilipo achiwa na jinamizi..., Ama kweli mzee una Uswahili kama wanavyosema watu" 

"Kwenye maelezo yako hayo ulianza kwa kunilaumu,kisha ukaniuliza,alafu ukanishuku, mwishowe ukajijibu mwenyewe..., Sina tena cha kuongezea hapo mwalimu, ila tu jaribu kuheshimu mistari iliyowekwa baina yake, usipende kuivuka..., Kuhusu huo Uswahilii...,hapana! Labda wewe uliejaa chale kila sehemu ya mwili wako..., Ooooh alafu mwalimu nimekumbuka! Acha niwahi nyumbani nikawahamishe kondoo wangu kwenye banda lao jipya, hahaha!..." Mwalimu alibaki ameduwaa kama kafumaniwa na kichaa!, huku akimuangalia mzee huyo akitoka ofisini humo kwa kuchechemea!.

"Huyu mzee ni mwanga kweli kama wanavyosema, sa kajuaje kama nina chale mwilini"  Alijiongelesha mwenyewe huku akisimama na kwenda kuwasha feni, akajiweka sawa kisha akachukua simu yake iliyokuwa mezani muda wote, kisha akapangusa kidogo akaweka sikioni, akasikilizia.

Muda haukuganda! Saa tisa na nusu alasiri kengele ya shuleni hapo iligongwa, wanafunzi walionekana wakielekea 'assemble'.  '4m4' ni maandishi yaliyosomeka juu kidogo ya mlango wa darasa ambalo Nadir alionekana akitoka. Nadir alikuwa akisoma kidato cha nne.

Baada ya kufika assembly, Walielezwa wiki ijayo yangeanza mashindano ya 'inter school' yale ya  'UMISSETA'. Wanafunzi walishangilia. Walitangaziwa shule watakazo shindana nazo, wachezaji wakisisitizwa kufanya mazoezi, na baadae wakaruhusiwa kuludi majumbani kwao. Muda mfupi tu, 'SAMARA SECONDARY SCHOOL' kama ilivyosomeka katika kibao chake ilikuwa pweke!.

Nadir alikuwa na rafiki yake aliyeitwa Zuberi, walikuwa wakisoma wote darasa moja. Walikuwa marafiki wakubwa tu waliotambuliwa hata na walezi wao. Zuberi alijulikana hata kwa anko wake Nadir,yaani Mzee Sele, vilevile Nadir alijulikana kwa shangazi yake na Zuberi. Zuberi ni kama Nadir tu! Alikuwa akiishi na mlezi mmoja ambaye ni shangazi yake.

Muda huu wakati wanatoka shule walikuwa wakiongea;

"Duuh kwaiyo unasema mjombaako alikinukisha tena kwa Sir John Leo" aliuliza Zuberi.

"Ndio ticha alitapatapa kwa muda akili ikamkaa sawa .., kawaida ileile ukinisema vibaya mbele ya yule mzee kinaumana! Yani bola hata umseme vibaya yeye" 

"Aisee! Nashindwa kuelewa kabisa kuhusu yule mzee..., Ehee vipi kuhusu ndoto uliyo ota jana ni ipi, ni ile ya 'LAILATUL QADIR' au ni ile ya kufunzwa mapigano ya kichawichawi?"

"Ni ya mapigano ya kichawichawi, na mara nyingi ndio inanicheleweshaga shule".

"Na anko wako bado hajakuweka wazi licha ya kuonekana kujua?" 

"Licha ya kuniambia kuwa muda ukifika nitajua kila kitu lakini inaonekana hayupo tayari kabisa kuniambia hasa hilo suala la kufundishwa mapigano ndotoni..., Kuhusu hiyo ndoto nyinginee... Anaonekana kama hana maelezo ya kutosha maana hata siku ya kwanza alionekana kushangaa kidogo"

Zuberi alishusha pumzi kidogo kisha akaonekana kusikitishwa na mambo yanayoendelea kwenye maisha ya rafikiye huyo.

"Kwaiyo umepanga nini sasa mpaka saivi wewe kama wewe" 

"Leo tumetangaziwa kuwa wiki ijayo yangeanza mashindano ya UMISSETA, na unajua jinsi ninavyo penda mchezo wa mpira wa miguu. Lazima tungetoka kwenda shule jirani kwa ajili ya kushiriki, na mjomba hajawahi kuniruhusu kuvuka mto MELE uliozunguuka kijiji hiki, na hajawahi kuniweka wazi kwanini hataki nitoke kwenye kijiji hiki, licha kusisitiza sana kwa sauti ya mamlaka"..!   Anacho ongea Nadir ni kweli, kijiji cha SAMARA kimezunguukwa na mto mmoja pande zote! Mto ulichora kama herufi C, na upande mwingine kulikuwa na mlima wa majabari makubwa ulioinama kwa nje, yaani nyuma ya huo mlima ndio kulikuwa na kijiji, na mto ulizunguuka kutoka kushoto kwa mlima ukakiweka kijiji kati na kwenda kutokea kulia kwa huo mlima. 

Mlima wa majabari haukupandika kabisa, hivyo iliwalazimu wanakijiji kwenda kushoto,kulia, na nyuma ambako wangekutana na mto MELE.

"Aloo! Yani mjombaako mambo yake ni ya kutisha tu na kushangazaa. Una kipaji kikubwa sana cha mpira wa miguu, na ungefika mbali lakini mtazamo wa mjombaako upo nje ya fikra za kawaida"

"Yani leo naenda kumwambia kuhusu haya mashindano, na nitatoka nje ya hiki kijiji kama ikihitajika! Nitamuuliza kwanini hataki nitoke kwenye kijiji hiki. Nishachokaa sasa! 'Na hii ni kwa mara ya mwisho' naenda kuzungumza naye kiupole, baada ya hapo nitajua mwenyewe cha kufanya".

"Unataka umtoroke bila kumuaga..! Ushasau kuwa ushawahi kujalibu kuvuka mto na kwa maajabu kabisa ukajikuta upo kwenu hahahaa"

"Ile ilikuwa zamani na tulikuwa na tunacheza tu, michezo ikatufanya tutake kuvuka daraja kuelekea upande wa pili lakini hatukuwa na nia thabiti kama niliokuwa nayo sasa"

"Hayaaaa tutaona ila ni vyema kama vipi umwambie muongozane wote ili kuondoa wasiwasi anaokuwa nao juu yako"

"Yaani kaniambia siruhusiwi kwa namna yoyote kuvuka mto kwa namna yoyote ile! Yan hadi najiuliza au ameniiba huyu, maana sio kwa kunilinda huku".

"Aaah kama kakuiba basi kakuiba mbali sana maana we mwenyewe unaonekana una asili kama ya kizungu alafu na yeye ana asili ya kiarabu".  Wote wakachekaa! na ndio muda ambao waliagana na wangekutana uwanjani kufanya mazoezi kujiandaa na mashindano ya shule.

          Itaendelea kila siku sasa!

Previoua Next