Nyumbani kwa mzee Sele kulionekana kuwa na ugeni, mbele ya nyumba yake kulikuwa na pikipiki aina ya 'Honda' ya rangi nyekundu na helmets iliyowekwa kwenye usukani. Mzee Sele alikuwa nyuma kidogo ya nyumba karibu na kibanda chake kipya cha kondoo. Alionekana kupeana mikono na Mtu mzima fulani hivi mweusi makadirio ya Miaka arobaini kuendelea, haikueleweka ndio walikuwa wana karibishana au ndo wanaagana. Naaam! Walikuwa wanaagana. walionekana kuja mbele ya nyumba na kusimama ilipo simamishwa pikipiki.
Mgeni huyo alipanda kwenye pikipiki huku akiongea kirafiki tu na mzee Sele. Wakati akimalizia kufunga vizuri helmeti, ndio muda ambao Nadir alionekana akiingia hapo akitokea shuleni. Baada ya kuwafikia watu wazima hao aliwasalimia na kupeana mikono na mgeni,na walionekana kujuana kiasi.
Baada ya salamu, Nadir aliingia ndani.
"Natumaini utalifanyia kazi mzee wangu, ngoja mimi niwahi sasa"
"Tuseme'Insha allah'...! Mlio wa pikipiki ukasikika! Mgeni akaondoka, mzee Sele bado alikuwa kasimama palepale huku akiwa na tabasamu lake la kizee lililopambwa na ndevu zake nyingi. Mzee Sele akaingia ndani sasa! Akasimama sebuleni, wow! Sebuleni palipendeza palikuwa na mapambo ya thamani kiasi chake, TV kubwa ukutani,meza kubwa ya kulia chakula ikiwa na baadhi ya vyombo juu yake kama ma 'hotpot' mawili kubwa na dogo, na sahani, bakuli,majagi mawili na vinginevyo.
Akiwa sebuleni hapo, mara Nadir akatokea kwenye chumba kimojawapo cha mwisho kati ya vitatu vilivyo onekana.Alikuwa ashabadilisha nguo za shule na alikuwa amevaa mavazi yaliyoonekana ni ya michezo. Akasimama katikati ya mlango akiwa anamwangalia mjombaake aliekuwa akifunua ma hotpot pale mezani.
"Njoo tule nataka nipeleke mifugo machungani......,mbona umesimama hapo mlangoni Nadir?"
"Hamna! saivi sijisikii kula, nitakula nikiludi kutoka uwanjani"
"Hapana! Njoo tule kwanza alafu ndo kila mtu anaenda kwenye shughuli zake, kula ni muhimu kutakupa nguvu ya kwenda kupambana huko uwanjani"
Baada ya kusikia hivyo, Nadir alijongea akaenda kusimama kalibu na mjombaake akaongea;
"Wiki ijayo tunaenda kushiriki mashindano ya UMISSETA, mazoezi ni kitu ambacho tulisisitiziwa sana maana tungekutana na wenzetu ambao wamejiandaa vya kutosha pia."
"Ooooh...Kumbe! Basi njoo ule haraka ili uwahi, nishapakua hapa usiende bila kula hautokuwa na nguvu za kupambana" Aliongea kwa bashasha mzee.
"Sitaki kwenda kupambana pekee ila pia naenda kupambania..!"
Baada ya kusikia maneno hayo,mzee akatabasamu kidogo kisha akasema;
"Kupambania! ndoto au...., ndoto ya kucheza mpira? Ok kaa ule sasa Nadir ili uwahi kupambana kwa ajili ya shule,na kuipambania 'talent' yako"
"Sawa nitakaa kula,ila unijibu swali langu moja, na jibu lake litanipa machaguo mawili! Niende uwanjani au nifanye maamuzi magumu". Mzee aliendelea kutabasamu tu na kukaa kimya kusubilia hilo swali la Nadir lenye machaguo mengi.
"Je, utaniruhusu kutoka kijijini hapa kwenda kijiji jirani kwa ajili ya kushiriki michezo?".
"Ndio nakuruhusu!". Nadir alishangaa akawa ana mwangalia tu mjombaake akitaka uthibitisho wa kauli yake.
"Nishakuruhusu, hivyo njoo ule uende mazoezini haraka ukapambanie kipaji chako, teh..teh..teh".
Nadir hakuamini kabisa kama mambo yangekuwa marahisi hivi. Akakaa kwenye kiti akasogeza chakula chake akaanza kula. Ila kichwani bado alikuwa na wasiwasi kwanini mjomba akawa mpole hivi kwenye suala ambalo alikuwa hataki hata kulisikia? Uvumilivu ukamshinda;
"Hivi mjomba kwanini ulikuwa unanikataza nisivuke MELE? (Mto), na leo ghafla tu unaniruhusu?
"Ulitaka jibu la swali moja, nishakujibu! 'No trial remains' Maliza kula uende mazoezini".
Nadir alishusha pumzi ndefu, akaendelea kula. Alivyo maliza akaamsha zake mazoezini,na mzee nae machungani.
Nadir Sporah! Kijana mweupe wa kuchanganya rangi mbili,nyeusi na nyeupe (chotara), japo uchotara wake uli 'level'. Yaani alikuwa na weupe ambao unaweza kuupata hata kwa mwafrika asiyechanganya rangi ila tu nywele zake ndo zilizidi uzungu.
Katika maisha yake alimjua mzee Sele kama mjombaake, hakuwahi kumjua mama wala baba yake. Angalau analijua jina la mama yake mzazi tu na ndo analotumia hata shule, yaani jina la Sporah ni la mama yake.
Kwa maelezo ya mjombaake ambaye ameishi naye tangu akiwa na miaka mitano tu! Anasema kuwa siku ambayo alikabidhiwa kumlea Nadir, ndo siku ambayo Nadir alimpoteza mama yake.
Kwa maelezo zaidi kutoka kwa mzee Sele kumuendea Nadir ni kwamba, walizaliwa wawili tu yaani Mzee Sele na mdogo wake Sporah, baba yao alikufa tangu sporah akiwa tumboni, mama yao alikufa kipindi ambacho Sporah alikuwa na miaka 10. Hivyo wakawa wamebaki wawili tu kitu na mdogo wake, na mzee Sele ndio aliyekuwa anamlea mdogo wake maana yeye alikuwa mkubwa zaidi, walipishana miaka mingi.
Sporah baada ya kumaliza darasa la saba, wakati huo kaka mtu alishaoa alisafiri kutoka kijiji walichokuwa wanaishi yeye na familia yake na kwenda mjini kutafuta kazi. Baada ya kufika mjini alipata kazi kwenye jumba kubwa la mzungu yeye na wenzake wengine. Kutokana na kipindi hicho mawasiliano kuwa ya shida nyumbani walikosa taarifa kamili ya kinachoendelea, vilevile hata kwa Sporah hakupata taarifa yoyote kuhusu hali ya familia yake.
Baada ya miaka sita, Sporah alirudi kijijini muda wa usiku wa saa kumi kuelekea kupambazuka akiwa na mtoto aliyefanana nae sana huku akiwa na taharuki kubwa, akisema kuwa watu wabaya wanataka kumuua mwanae hivyo alimtaka kakaake aende akamfiche mwanae. Kipindi hicho pia kakaake alikuwa na watoto wawili. Kaka mtu japo hakuelewa vizuri ila aliamua kumchukua mtoto wa mdogo wake na kwenda naye mbali kidogo kumtoa pale kijijini maana anafuatiliwa tangu wakiwa mjini eti.
Mzee Sele anasema "Baada ya kutoa mguu tu pale kijijini,nikiwa mlimani huko nikasikia vilio vingi kule kijijini ninakotoka, hivyo nikalazimika kuludi. Baada ya kuludi tena kijijini nikakutana na hali ya kutisha mno....,mke wangu, watoto wangu, pamoja na mdogo wangu Sporah..,wote walikuwa wameuawa kikatili sana, wale wauaji wakanishtukia wakaanza kunifukuza, wakanipiga risasi ya mguuni nikadondokea mtoni nikiwa na mtoto wa miaka mitano mgoni. Na hiyo ikawa ndio pona yangu mimi na mtoto maana walijua nimekufa ila tulisombwa na maji hadi katika kijiji hiki cha SAMARA.
Hadithi hii ishawahi kumhuzunisha sana Nadir huko nyuma akiwa mdogo, lakini kadri alivyokuwa akikua, ni kama kuna hisia zinamwambia ni ya kutunga. Kwanini iwe ya kutunga....? Ana sababu zake!.
Comments