Karibu na jiji la Paris kulikuwa na jumba kubwa ambalo lilikuwa limejaa kijani kibichi , lililojengwa kwa mtindo wa baroque, usanifu wake ulikuwa mkubwa sana na kila kitu kilikuwa kikijielezea.
Mwanaume wa kizungu alionekana akipata kifungua kinywa nje ya kibaraza kilichozungukwa na nguzo nyeupe.
“Master! Bi Somerset amewasili” Mwanaume alievalia nguo za kinadhifu za uhudumu wa nyumba aliongea kwa lugha ya kifaransa.
Yule mwanaume mara baada ya kusikia kauli hio , aliishia kutingisha kichwa chake bila ya kubadili muonekano wake huku akijifuta midomo na kitambaa.
“Mkaribishe ndani”
Haikuchukua muda mrefu baada ya mhudumu kuondoka , mwanamke mrembo sana wa kizungu alievalia gauni jeupe aliingia.
“Haha.. congratulations to Miss Silyvie , the new president of the Set Association”
Mwanaume yule mara baada ya kumuona mwanamke huyo mrembo akiingia uso wake ulibadilika na kuweka tabasamu la ucheshi huku akimpatia pongezi Silvia.
Silvia aliekuwa na tabasamu usoni , aliishia kunyoosha mkono wake na kusalimiana na yule mwanaume.
“Mr Leibson , kama isingekuwa wewe kuwahonga wafanyakazi wote wa Set , mambo yasingeenda vizuri kama hivi”
Mwanaume huyo mzungu alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa siraha , Leibson ambae alikutana na Hamza siku chache nyuma katika Alice’s Party.
“Nilishawahi kusema , kwenye huu ulimwengu hakuna kitu ambacho hela haiwezi kununua. Haijalishi ni mtazamo gani unao , haijalishi una msimamo namna gani , kila kitu ni upuuzi mbele ya hela , ili mradi pesa iwe mbele kila kitu kinaweza kutekelezeka”Aliongea Leibsoni huku akicheka kwa kujikweza.
“Ndio sasa ninaamini , hakika Mr Leibson una busara sana upande huu”Mara baada ya kucheka kidogo alimpa ishara Silvia kukaa na yeye mwenyewe alichukua jukumu la kummiminia chai.
“Madam Silvie , sasa umeshakuwa raisi wa Set, unapaswa kuanza kutimiza ahadi na kumzingatia rafiki yangu”Aliongea kwa sauti iliojaa zaidi ya maana.
“Bila shaka nakumbuka vyema. Soko lote la siraha la Black Market ya Sharia litakuwa chini yako , Mr Leibson..”
“Miss Silvie mimi sina ukosefu wa hela , kwangu hela ni namba tu . Ninachotaka ni muda wa kuzifurahia hela zangu”
“Najua” Aliongea Silvia na tabasamu “Unachohitaji ni maisha marefu, hivyo unaitaka dawa ya kifo, si ndio?”
“Nataka kuendelea kuwaona wewe na mwalimu wako Mr Black . Nataka kujifunza namna ya kuishi milele na ili mradi nitaweza kutunza mwonekano wangu , nipo tayari hata kukugawia nusu ya utajiri wangu”
“Oh! Nusu ya utajiri wako , ni hela nyingi sana , naweza kununua nchi kadhaa Africa”
“Mh! Familia yetu imekuwa ikiendesha biashara ya uuzaji wa siraha kwa zaidi ya miaka mia moja sasa. Nusu ya utajiri wetu unatosha kununua nusu ya bara lote la Africa”Aliongea Leibsoni kwa kujivunia.
“Wewe ni tajiri mno , ila haujikwezi , ndio maana Gwiji kama Skellidoni unaweza kumuendesha utakavyo , Mr Leibson..”
“Haha.. Skellidoni mwenyewe wakati alipokuwa mdogo , alikuwa na binti yake ambae ni mchawi. Alidhani hakuna anaefahamu , lakini angewezaje kuuficha ukweli nisijue? Nikaona kama nitaweza kumtawala binti yake nitakavyo si yeye pia atasikiliza kila ninachomuambia? Sio yeye tu , ili mradi nikifanikiwa kuishi maisha marefu , kama nipo tayari naweza kuwafanya na magwiji wengine wote kuwa chini yangu , Hela na siraha za kutosha zinaweza kunifanya kuutawala ulimwengu wote”Aliongea Leibson na kisha alisimama na kupanua mikono yake.
“Kitu pekee ambacho siwezi kutawala ni uhai wangu , lakini lazima niishi muda mrefu”
Tabasamu ambalo halikuwa tabasamu , lilionekana katika uso wa Silvia
“Inasikitisha , Awamu hii Mr Leibson , hujaweza kumtawala ikatosheleza..”
“Unamaanisha nini?”Aliuliza huku akishangaa.
“Lucifer ashanifahamu tayari. Mchezo kati yangu na Skellidoni ulishatambuliwa na Lucifer , hivyo ni sawa na kusema watu wengine muda si mrefu wataweza kuanza kunishuku”
“Usiwe na wasiwasi , Lucifer anaweza kuwa na nguvu lakini Skellidoni aliniambia yeye mwenyewe jana usiku , ana mbinu ya kuweza kumuua Lucifer. Nina uhakika muda si mrefu nitapokea taarifa za kufurahisha kutoka kwa Skellidoni”
“Mh ni hivyo?” Silivia aliguna na kucheka kikauzu “Lakini mpelelezi wangu ameniambia Lucifer , namaanisha Skellidoni ameuliwa na Lucifer” Leibsoni mara baada ya kusikia hivyo aligeuka kwa mshangao.
“Nini!? Inawezekanaje?”
“Kwamba hauniamini? Unaweza kutuma mtu kwenda kuchunguza kama ni kweli na sio kusubiri taarifa nzuri , kwasababu Skellidoni hawezi kukuletea hizo taarifa tena”
Leibsoni haraka haraka alituma mhudumu kwenda kuchunguza na hazikuchukuwa hata dakika kumi taarifa iliweza kurudi na kuambiwa Hamza yupo hai na Skellidoni hafahamiki alipo.
Mara baada ya kusikia taarifa hizo , Leibson hasira zilimvaa na kupiga kofi meza na kupasua pasua vikombe.
“Mr Leibsoni kama unataka kuonana na mwalimu wangu , hakuna shida lakini vigezo vinapaswa kuzingatiwa na ni wewe kulimaliza hili suala vizuri ili mwalimu wangu kukuruhusu kuonana nae”Aliongea na kisha alisimama.
“Lucifer ana kila sababu ya kutufanya tufeli. Anatisha zaidi kuliko miaka mitano iliopita. Kama tusipommaliza , hata kama tukianzisha mipango yetu , tunachokaribisha ni vita nyingine takafifu. Ni matumaini yangu wewe na watu wa jamii yenu ya muungano wa siri mnalizungumza hili na kujua ni namna gani mtaweza kummaliza. Ni yeye pia ambae amefelisha mpango wa kutengeneza dawa ya kifo mwanzo , au nakosea?”Aliongea na kumfanya Leibsoni kung’ata meno kwa hasira na kisha akaongea kwa sauti nzito.
“Najua , huyu Lucifer , nimemchukulia poa sana ,ila dawa yake inakuja”
Silvia hakuongea neno na alitembea kimadaha kutoka ndani ya aneo hilo na ile anapita eneo la bustani aliweza kukutana na msichana mnene kiasi, mwenye nywele zake za dhahabu na macho ya bluu , alikuwa ni binti wa Leibsoni aliefahamika kwa jina la Barbara.
Dakika ambayo Barbara alisogeleana karibu na Silvia , macho yao yalikutana na palepale midomo yao ilicheza na kuonyesheana tabasamu lisilo la kawaida.
*****
Hamza aliendesha gari moja kwa moja mpaka hospitalini , Mganga mkuu na mkurugenzi wa hospitali alikusanya kundi la watumishi wa hospitali hio na kuwasubiria nje kuwapokea.
Hamza hakujali sana mapokezi hayo na aliishia tu kutoa maelekezo haraka , kwamba mke wake apatiwe wodi ya daraja la juu kabisa na kisha afanyiwe vipimo vya mwili mzima.
Mpaka inatimia mchana , vipimo vilionyesha hali ya Regina ilikuwa sawa kabisa. Huku madaktari wakienda mbali na kusema alikuwa na afya tena zaidi ya afya nzuri na ni kwamba tu muda huo kapoteza fahamu kwasababu ya uchomvu , hivyo wangempa dripu za virutubisho na kumsubiri aamke mwenyewe.
Hamza alitaka kuendelea kukaa hapo wodini , lakini Nyakasura alipanga kuondoka Ufaransa kurudi Tanzania na ndege ya saa tisa , hivyo alitaka kabla ya kuondoka kujua ni kwa namna gani Hamza aliweza kumdhibiti Skellidoni , mathalani kujua mbinu yake aliotumia.
Kwasababu Nyakasura alimuokoa, Hamza hakuwa na pingamizi na kumfanya aone, maelezo hayo yalimjumuisha na Rhoda pia.
Hamza hata hivyo hakuwa mtu wa kuficha uwezo wake . Aliamini uwezo wa mtu unategemeana na juhudi zake mwenyewe na kipaji na kwa hao ambao hawawezi kuweka juhudi kwenye kujifunza , hata kama waambiwe siri zote za ulimwengu juu ya kumfanya binadamu kiumbe hatari itakuwa ni ngumu kwao kufanikiwa.
Wawili hao walisogea mpaka eneo lililojitenga nyuma ya hospitali kando kando ya ziwa la kutengenza . Hakuna aliesogea kuwasumbua hata baada ya wakati wa chakula cha mchana.
Hamza alimuomba Black Fog kisu chake na kisha alitoa maelezo mepesi sana juu ya uelewa wake mpya juu ya mapigano.
“Ukweli ni kwamba mbinu za nje zimejitosheleza zenyewe kumfanya mtu kuwa na nguvu , kama ilivyo mbinu za ndani . Lakini mahitajio ya mbinu za nje yanachanganya sana tofauti na ule uwezo ambao mtu anazaliwa nao , ndio maana watu wanaongeza uwezo wao taratibu taratibu kwa kukusanya nguvu ya kiroho na kunyonya nishati ya mazingira…”
“Mwenyewe nilidhani ni hali ya kushangaza sana , kwani mpaka kufikia umri huu nimejifunza mbinu zaidi ya elfu tatu za kumfanya bidanamu kuwa na uwezo wa ziada. Lakini mara baada ya kukutana na shambulizi ambalo lilinifanya mwili wangu kujihisi kuwa dhaifu kiasi kwamba ni kama nimerudishwa katika kipindi nilichokuwa na miaka mitano ndio nimekuja kugundua , haijalishi utajifunza vipi lakini nguvu unayoingiza ndani ya mwili kutoka nje ina kikomo chake, tofauti ya ile unayotoa ndani kwenda nje”Aliwaangalia na walionekana kushangaa tu.
“Hamuwezi kunielewa ninachoongea, angalieni namna ambavyo nitatumia hii siraha na ndio mtaona”Aliongea Hamza.
Na mara baada ya meneno hayo , Hamza alijituliza na kugandisha macho yake katika ziwa.
Hamza alikusanya mawazo yake na kuwa kitu kimoja na kisha akayabadilisha kuwa nia na makusudi ya kimatokeo. Kadri alivyokuwa akikusanya mawazo yake ndio namna ambavyo misuli yake ilionekana kumuitikia vyema na palepale kwa wepesi zaidi na kwa umakini mkubwa aliinua ile siraha akiwa ameipa presha kubwa na kuipigiza juu ya maji ya ziwa lile.
Kilichoonekana kilishangaza , ziwa lile ilikuwa ni kama vile ghafla tu kumetokea ukuta ambao ulitenganisha maji ya ziwa sehemu mbili na kutengeneza mwinuko mkubwa wa maji.
Ziwa hilo la kutengenezwa lilikuwa na kina cha mita tatu kwenda chini , lakini kupitia kisu kidogo tu Hamza aliyakata maji na kutengeneza njia ambayo mpaka matope chini yake yaliweza kuonekana. Tukio hilo liliwafanya Nyakasura na Rhoda kushangaa mno.
Hawakuweza kuhisi nguvu yoyote ya kinishati wala nguvu ya kiroho kutoka kwa mwili wa Hamza na shambulizi lake.
“What the hell! Umewezaje kufanya hivi?” Nyakasura alimaka.
“Kila tunachoweza kukifikia kuna sababu ndani yake , hili ndio fumbo kubwa kwetu binadamu tunalopaswa kufumbua, lakini ukweli mchache ndio pekee ambao naweza kuelezea kwa maneno”
Black Fog yeye pia aliona haiwezekani kabisa na alijikuta akichukua kile kisu kutoka kwa Hamza na kukikagua kwa mshangao mkubwa.
“Bro naomba na mimi nijaribu”
Hamza hakuwa na pingamizi lolote na kumuacha Black Fog kuigiza kile alichofanya.
Lakini kadri ambavyo Rhoda alifanya kama alivyofanya Hamza hakukuwa na matokeo ya aina yoyote kabisa na aliishia kupoteza kisu chake ndani ya ziwa.
“Hii inashangaza , nimetumia mbinu sawa kabisa na wewe , lakini kwanini hakuna kinachotokea?”Aliongea Black Fog akionekana kuchukia.
“Labda utakuwa dhaifu sana?”Aliongea Nyakasura.
“Ndio kusiwe hata na mtikisiko wa maji?”
Unapaswa kuelewa Hamza kabla hajagusa maji hayo , misuli yake ilikuwa ikionekana kile anachofanya , ni kama alikuwa akielezea kila kiungo cha mwili wake ni tukio gani anakwenda kufanya.
“Inaonekana uelewa wangu ni mdogo mno , hii mbinu hata kama unifundishe kwa muda mrefu , sidhani kama nitaweza kuijua”
“Nilishawahi kusikia kuhusu manuio ya kisiraha, lakini inasemekana lazima moyo wako uwe umejazwa na imani ya kiroho , lakini kwanini wewe unafanya kwa nia pekee bila ya imani? Kama umeweza kugawanya maji ya ziwa basi lazima kutakuwa na nishati ambayo umetoa , ila hio nishati sio ya mbingu na ardhi wala haitokani na nguvu ya kiroho , kama sio hivyo ni nini?”
Hamza hata yeye mara baada ya kusikia swali la Nyakasura , alikumbwa na hali ya kuchanganyikiwa , ukweli aliamini alichofanya ni nia tu ambayo aliiweka katika siraha alioshika mkononi , lakini ni kama kulikuwa na maelezo yalikosekana.
Hamza alijiuliza au bila kuelewa ametumia aina ya nishati nyingine ambayo hakuwahi kuifahamu?.
Wakati Hamza akjifikiria , sauti ya mwanamke ilisikika na mara baada ya kugeuka waligundua ni dokta .
“Mr Hamza , mke wako ameamka” Aliongea Dokta.
Hamza mara baada ya kusikia ripoti hio , hakuwa hata na muda wa kufikiria kitu kingine na alikimbia kuelekea wodini.
Nyakasura na Rhoda pia walitaka kujua hali ya Regina ipoje baada ya kuamka hivyo walifuata nyuma.
Mara baada ya kufika kwenye wodi ya VIP , dirisha lilikuwa limefunguliwa na kuruhusu mwanga wa jua kuingia ndani na chumba kilikuwa angavu sana.
Regina ni kweli alikuwa ameamka na alikuwa amekaa huku nywele zake zikiwa zimeogeshwa na kuvalishwa gauni la hospitalini na kumfanya aonekane msafi zaidi na wa kuvutia.
‘Wife!”
Hamza aliita huku akimwangalia mwanamke huyo aliekuwa ameamka kwa furaha.
Regina aliishia kugeuza sura yake na kumwangalia Hamza , Rhoda na Nyakasura na mara baada ya sekunde sita kupita alionekana kuwa katika hali ya kushangaa.
“Wewe , umeniita mimi?”
Tabasamu la Hamza lilikakamaa , huku mapigo yake ya moyo yakiongezeka kwa kasi na aliishia kujilazimisha kutabasamu.
“Mke wangu nini tatizo , acha utani basi ni mimi”
“Wewe ni nani kwani! Kwanini unaniita mkeo?” Regina alionekana kukunja sura huku akionyesha hali ya kumshangaa Hamza . alikuwa pia hana furaha huku uso wake ukijaa ukauzu.
“Jamanii , Inamaana aliumia sana na kumfanya ubongo wake kuathirika mpaka kumpelekea kupoteza kumbukumbu?!”Aliongea Nyakasura kwa mshangao.
“Hapana , haiwezekani , Sister Regina ni mimi Rhoda , hunikumbuki?”Aliongea Rhoda kwa wasiwasi.
“Sikujui , hapa ni wapi na kwanini nipo hospitalini?”
Mapigo ya moyo ya Hamza yalikuwa yakidunda kwa hali ya ajabu mno , ile furaha aliokuwa nayo ilipotea ghafla, aliishia tu kujituliza ili kuonekana kawaida na kutokumchanganya Regina zaidi.
“Wife , mimi ni mume wako , usiwe na wasiwasi , umepoteza tu kumbukumbu zako lakini nitakuaminisha haraka iwezekanavyo mimi na wewe ni mume na mke , unaweza kuniamini”
“Mimi! , ni lini nimeolewa? Wewe ni nani na una kusudi gani kwangu?”Regina aliongea kwa kufoka.
Hamza aliishia kukunja sura na kisha alitoka kitandani na kutoka nje na kumwangalia dokta.
“Wewe si ndio uliesema , mke wangu yupo sawa?”
Dokta bingwa huyo alikuwa akitokwa na jasho sio kawaida. Mara baada ya kusikia tafsiri , ndio sasa anajua Regina alikuwa amepoteza kumbukumbu zake na haraka sana alijielezea.
“Hamza .. Mr Hamza nitaongea na watu kuandaa haraka vipimo yakinifu vya ubongo’Aliongea.
Comments