SEHEMU YA 223.
Black hole
Hamza muda ule alikumbuka biashara ya vyungu , ambayo ilikuwa ikifanywa na Alex , ukweli ni kama suala hilo alilipotezea kwa muda, ni suala ambalo pia lilimgusa rafiki yake Amir , lakini ni kwa muda hakuwasiliana nae tokea mara ya mwisho kuachana Karambezi.
Hamza aliangalia yule mrembo wa haja akipatiwa mzigo wake kwenye boksi na kisha kutoa kadi ya benki na kulipa.
“Unaangalia nini?”Alikuwa ni Regina aliegeuka na kugundua Hamza alikuwa akiangalia upande mmoja.
“Hakuna tu wife” Aliongea Hamza na kisha akarudi kwenye uhalisia
“Wife mbona hiko kinywaji kifungashio chake kina mwonekano mbaya sana , kwanini ununue?”
“Mimi naona kinavutia”Aliongea Regina na palepale alikumbuka na Hamza anapaswa kunywa, “ Unataka kuchukua radha ipi?”
“Ila sio kwenye hicho kikombe cha kizombi”Aliongea Hamza akicheka.
“Nani kakulazimisha , wewe chagua kinywaji tofauti unachopenda , hiki nitatumia mwenyewe”Aliongea Regina , alionekana kuwa katika mudi nzuri mno , uso wake ulijawa na tabasamu na kumfanya awe mrembo kama malaika.
Licha ya hivyo vinywaji hivyo hakukuwa na radha ya strawberry zaidi ya kuwa soda. Hamza upande wake alichukua Coca.
Wawili hao waliingia ndani ya ukumbi na kuongozwa moja kwa moja mpaka katika siti za wapenzi . Ilionekana filamu ilikuwa imeshaanza muda mrefu tu. Tofauti na matarajio siku hio watu hawakuwa wengi sana, pengine ni kwasababu ya sherehe za christmas watafutaji wengi ambao ni wapenda filamu wamesafiri .
Walikaa na kuendelea na filamu ambayo ilishakwisha kuanza, Hamza alimwangalia Regina ambae alikuwa akinywa kinywaji chake taratibu pembeni yake na palepale aliinua mkono wake na kupitisha kwenye mabega yake.
Regina alitingishika kidogo lakini alielewa ishara ya Hamza na palepale aliegamia kwenye bega lake.
Wawili hao hawakuongea neno wakati wakiendelea kuangalia filamu inavyoendelea . Taratibu Regina alijihisi kuchoka kukaa staili moja na alisogea karibu na kuegamiza kichwa kwenye kifua cha Hamza.
Hamza aliweza kunusa marashi mazuri kutoka katika nywele za Regina na alishindwa kujizuia na kupeleka mkono na kuanza kuzigusa , zilikuwa laini mno na za kuteleza.
Hamza aliishia kuinamisha kichwa chake na kubusu kichwa cha Regina bila ya kuwa na nia nyingine , ilikuwa ni busu la kuonyesha mapenzi.
Regina aliinua kichwa chake , hakujua Hamza alikuwa akimaanisha nini kubusu kichwa chake hivyo alimwangalia kwa macho yaliokuwa na kuchanganyikiwa kidogo.
Mara baada ya kuona sura hio ya kipole ,Hamza alishindwa kujizuia na kutaka kumchokoza , hivyo alimshika kidevu na kisha aliinamisha kichwa na kumbusu lipsi zake.
Regina aliishia kutoa mguno tu huku akimpiga Hamza kwenye mapaja yake lakini mwishowe aliacha kuleta ukinzani.
Busu hilo lilidumu angalau kwa dakika kumi , wawili hao walikuwa hata wamesahau walikuwa kwenye ukumbi wa sinema , mpaka pale Hamza alivyoshika shati la Regina.
“No!”
Regina alijikuta akimaka wakati akifungua macho yake na kukumbuka walikuwa ndani ya ukumbi wa sinema.
Hali hio ilimfanya Hamza kujisikia vibaya kidogo .Hio ni kutokana Regina alipiga makelele kwa nguvu kiasi kwamba mpaka watu waligeukia upande wao. Regina aliishia kushikwa na aibu za kike na ilikuwa bahati tu eneo walilokuwepo lilikuwa limejitenga na siti za kawaida na kufanya watu wasione kinachoendelea, lakini walikuwa wakionekana na kusikika.
“I'm sorry, my love is so strong … … you understand.”Aliongea Hamza akiwaomba radhi wazungu waliokuwa karibu yao. Asilimia kubwa ya watu waliopo ndani ya ukumbi huo ni wenza , hivyo walikuwa wanaelewa.
“Bro , be steady!”Aliongea mzungu akimpa Hamza ishara ya mkono akimwambia kuwa ngangari.
Kutokana na aibu iliojaa utamu , Regina alijikuta akijitenga mbali na Hamza kidogo na kukumbatia nguo zake kama vile alikuwa akiogopa kuibiwa.
“Wife kuhusu hili , sisi ni wanandoa tuliopita mambo mengi , kugusana kidogo tu sio tatizo”Aliongea Hamza.
“Hapana! Hukunichumbia , hukufanya harusi na mimi , vipi kama nikipata mtoto? Nitashindwa hata kuangalia watu usoni”Aliongea Regina akiwa siriasi.
Hamza kidogo tu acheke kwa nguvu sana , aliona Regina alifikiria mbali sana , mpaka kudhani angepata mtoto kwa kuguswa tu?.
“Nimekugusa tu , sio kama ungepata mimba bwana”
“Busu tu linatosha , ukienda mbali sikuongeleshi tena”Aliongea Regina akiwa siriasi na kumfanya Hamza apotezee kwa kuupoza moyo wake na kisha kuendelea kuangalia filamu.
Ingawa walikuwa wamepitwa na matukio mengi , Hamza na Regina hawakuwa wajinga hivyo walianza kuelewa.
“Unadhani ni kweli watu wanaweza kutabiri matukio yajayo?” Regina alishindwa kujiuliza mara baada ya kuona mwanamke sterring akionekana kujua nini kitatokea katika miaka ijayo.
“Nadhani inawezekana , isitoshe maarifa tuliokuwa nayo kwasasa ni hafifu mno, lakini hata sasa kinadharia inawezekana kupindisha muda na anga, inawezekana hata kuwa nje ya muda na nafasi , hivyo sidhani inaweza kuwa ngumu kutabiri”Aliongea Hamza.
“Kuwa nje ya muda na nafasi unamaanisha kusafiri mbele ya muda? Inawezekana vipi kusafiri?”
“Hujawahi kusikia natharia ya uhusiano wa vitu(theory of relativity)? Nadharia hii inaeleza kwamba wakati kitu chenye uzito mkubwa kinapokandamizwa na kuwa kwenye nafasi ndogo sana , kani mvutano huwa kubwa kiasi kwamba hupindisha muundo wa anga na muda(Spacetime). Mvutano huu unakuwa mkali kiasi kwamba hata mwanga hauwezi kutoroka na eneo hilo ndio hujulikana kama shimo jeusi(Black Hole). Sasa wanasayansi wanaamini uwepo wa Black Hole unaweza kutengeneza uwezekano wa kusafiri mbele ya muda”
“Ni kweli! Unamaanisha kwamba kadri kitu kitakavyokuwa na mass kubwa , ndio kinasababisha athari kubwa kwa ulimwengu na ikifikia hatua flani muda na anga huathirika?”
“Ni kama hivyo mke wangu , hebu chukulia mfano huu , chukulia anga lote juu ni kama kitambaa kilichotandazwa , ukiweka kitu chenye uzito juu ya hiki kitambaa kinabonyea kwa kuchukua nafasi na kutengeneza mlima wa shimo si ndio? Sasa kama kuna vitu vidogo ambavyo havikuwa na uzito mkubwa na sasa umeweka kitu chenye uzito ,vitu hivyo vyote vitaangukia au kusogelea katika eneo ambalo kipo kile kitu kizito. Hii ndio sababu, nyota ina uzito mkubwa na ndio maana kila nyota kuna sayari zinazunguka . Ukiwa na uzito mkubwa maana yake lazima uathiri wengine …”
Hamza wakati akiongea hivyo ghafla tu aliingiwa na kitu kama mwanga kwenye akili yake na kuacha kuongea mara moja. Alionekana kupata jambo jipya katika akili yake ambalo hakuwahi kulifikiria , jambo muhimu zaidi katika mafunzo yake.
Regina alikuwa akisikiliza kwa furaha kubwa , na ndio muda huo alijua mume wake alikuwa na maarifa mengi.
“Kwanini unayajua hayo yote? Si ulikuwa mpiganaji tu?”Aliuliza Regina.
Hamza hata hivyo hakuwa katika mudi ya kusikiliza maswali ya Regina. Muda huo aliweza kuhisi pengine ameweza kujua tatizo liko wapi , alijikuta akipatwa na msisimko na kutamani kuruka kwenye siri yake.
“Wife nisubiri naja, naenda nje mara moja”
Hamza aliongea wakati akiwa amesimama tayari , Regina alionekana kushangaa kwasbabu sinema haikuwa imeisha bado na anandoka.
“Wewe , unaenda wapi?”
“Kufanya majaribio”Aliongea Hamza huku akipotea.
Kufanya majaribio ! Regina alikuwa katika hali ya mshangao baada ya kushindwa kuelewa Hamza anamaanisha nini. Hata hivyo hakuwa na furaha , alishia kushika kikombe cha kizombi na kuking’ata kwa nguvu.
“Mshenzi wewe Hamza , mara yangu ya kwanza kuja kuangalia sinema na wewe unanitelekeza” Regina alilaani sana katika moyo wake , lakini hakujua Hamza alikuwa ameenda wapi , hivyo aliishia tu kubakia hapo na kuendelea kuangalia filamu.
Muda huo huo , Hamza alikuwa ametoka nje kabisa ya ukumbi na ndani ya dakika kadhaa tu alikuwa juu kabisa ya jengo la Dosam Tower ambalo lilikuwa mkabala kabisa na ukumbi wa kuangalia Sinema.
Jengo hilo lilikuwa refu sana kwenda hewani kuliko majengo yote yanayozunguka katika eneo hilo na Hamza mara baada ya kukanyaga juu yake aliweza kupigwa na upepo mwingi.
Mara baada ya kusimama juu yake aliweza kuangalia upande wa chini uliokuwa umefunikwa na taa nyingi za umeme , na Hamza aliingia katika tafakari nzito.
“Quality as an invisible energy(Ubora kama nishati isionekakan) Au inamaanisha…”
Hamza alijikuta akiacha kuongea na palepale aliweka mkono wake katika staili ya mashambulizi , kama vile ameshikilia siraha. Alifumba macho yake na kisha akautuliza moyo wake , katika akili yake . alizikumbuka hisia ambazo zilimtokea wakati akitumia mashambulizi ya kunuia kumuua Skellidoni.
Mwanzoni Hamza alielewa kwamba nguvu za nje ni nguvu za nje tu , siraha ni siraha na mbinu za mapigano ni mbinu za mapigano. Lakini Hamza hakuelewa kwanini yeye ambae hakuwa na nishati yoyote ya mbingu na ardhi anaweza kuzalisha nishati kubwa yenye nguvu isioonekana.
Kimantiki ni kwamba , hata kama angekuwa na uwezo mkubwa wa kiimani au kuwa na uwezo wa kucheza na elementi za upepo , asingeweza kutengeneza nguvu ile. Lakini muda ambao alikuwa akimwelezea Regina kuhusu ukubwa wa uzito wa kitu na athari zake kwa ulimwengu , Hamza aliweza kuelewa tatizo lilikuwa wapi.
Hamza alifumbua macho yake , yalikuwa kama siraha , mwili wake ulipiga hatua mbele na kwa kuzungusha tu alifyatua siraha yake mbele.
BOOM!
Ghafla tu bango kubwa la mtandao , lililokuwa juu ya ghorofa , mita ishirini kutoka katika jengo alilosimama , lilitoboka kwa nguvu kubwa mno. Hamza aliangalia bango lile ambalo lilionekana kushikwa na cheche za umeme na alijikuta akipatwa na msisimko ambao ulifanya mwili wake wote kumtetemeka.
“Ndio! Ni ubora , its Quality! Hahahaha…” Hamza alijikuta akiongea huku akicheka kwa nguvu kama vile alikuwa amegeuka na kuwa kichaa.
Uzito uliokuwa ukizungumziwa hapo , haukuwa uzito wa mtu lakini ulikuwa ni uzito wa kila seli ndani ya mwili wake na kila chembe iliomilikuwa na Hamza baada ya miaka mingi ya mafunzo makali.
Nguvu ya ndani ni imani na nguvu hivyo huvunwa taratibu taratibu mpaka kufikia katika viwango vya juu sana , inasemwa kwamba kupitia nguvu ya ndani mtu anao uwezo wa kufanya kila jambo hata kuhamisha milima na kuutupia baharini , kupitia nguvu ya ndani anao uwezo hata wa kuita mvua na upepo na hata kuukomesha.
Kama kila kitu ni asili , kwanini wavunaji wasitumie nishati za nje kutawala nishati ya ulimwengu? Kwanini wasigeuke na kuwa malaika ? Jibu ni hapana nguvu ya nje haitoshi , ni nguvu ya ndani pekee ambayo inavunwa hatua kwa hatua ndio inayofanya nishati ya mtu kuwa bora zaidi kuliko ile inayopatikana nje.
Si ni malengo ya kila mvuna nishati kuboresha mwili wake na kuwa na nguvu? Lakini bila shaka siraha ambayo inaweza kuogopesha ulimwengu ni mwili wangu binafsi.
Hamza alikumbuka siku ile , wakati akiwa mbele ya ziwa la kutengeneza hospitalini , hakugusa kabisa maji lakini alitoa nguvu isiokuwa ya kawaida na sababu ambayo Black Fog alivyoraibu hakuna kilichotokea ni kwasababu mwili wake haukuwa umepitia mafunzo ya kutosha na kuumiliki mwili wake kisawa sawa. Isitoshe pia Black Fog alikuwa akijifunza kuvuna nishati za nje hivyo nguvu zake za ndani zilikuwa dhaifu zaidi.
Hamza muda huo alijua sio tu nia ya kisiraha ambayo iliweza kutoa majawabu yale , bali ni kwasababu mwili wake umeingia katika hatua nyingine kabisa ambayo inampa ubora ambao unamfanya baadhi ya nishati za ulimwengu kujigandisha kwake mwenyewe bila kujua.
Uwezo wa Hamza ni kama sumaku, namna ambavyo inavuta vitu na kuvinasa ni kwasababu ya nguvu yake , hivyo mwili wa Hamza ni kama umekuwa bora na kuwa sumaku ambayo inaweza kunasa nishati isiokawaida ya ulimwengu wa asili , hivyo ndio maana mwili wake umekuwa bora , haukuwa bora kwa nguvu ya ndani pekee , lakini kwa mafunzo aliopitia kwa muda mrefu na kufanya aumiliki mwili wake kisawa sawa. Kwa lugha nyepesi ni kwamba mafunzo yamemfanya kuumiliki mwili wake kwa asilimia mia moja. Hamza anaamini kwamba licha ya miili yetu kuwa yetu , lakini asilimia kubwa haipo chini ya umiliki wetu bali ipo chini ya umiliki wa asili.
Lakini namna ambavyo Hamza ananasa nguvu hizo zisizo za kawaida , bado hakuelewa , alijiuliza je kuna sheria ya kifizikia ambayo bado haijawahi kufahamika kuhusu ulimwengu au kuna sababu nyingine ya kuweza kuwa na uwezo huo?.
Hata hivyo Hamza alikuwa na uhakika na jambo moja tu , hakuwa amechagua njia mbaya katika mafunzo.
Ingawa hakuwa na nishati yoyote katika mili wake , kama nishati ya mbingu na ardhi , kupitia kuuelewa vyema mwili wake, kuumiliki kwa asilimia mia moja na kuimarisha imani yake , mwili wake umekuwa mzito na wa tofauti na kuanza kuathiri nguvu iliojificha ya ulimwengu.
Nishati ya mbingu na ardhi ilikuwa ikiisha ikitumika sana na mtu , lakini ukifananisha na nguvu yake yeye , ilikuwa haina kikomo. Kwa lugha nyepesi wavuna nishati wanaomba asili iwapatie nguvu ilihali Hamza yeye anaamini sisi binadamu ndio tunapaswa kuimiliki asili na kuiamrisha ifanye mambo yenye nguvu , kuumiliki mwili maana yake ni hatua ya kwanza ya kujitoa katika minyororo ya asili na kuifanya ikutumikie.
Hamza muda huo alihisi ni kama alikuwa na nishati ya mbingu na ardhi bila kuomba umiliki , hivyo kupata fursa wa kutumia bila kumuishia tofauti na wavuna nishati wa kawaida ambao lazima wavune nishati nyingi ya asili na kisha ndio waitoe kufanya matendo yenye nguvu. Hamza hakuhitaji kuvuna, alikuwa akitumia. Moja ya sababu ambayo ilimfanya tokea mwanzo kuachana na mafunzo ya kuvuna nishati ni kwasababu hata ajitahidi vipi kupanda levo kuna ukomo akifikia hawezi kwenda mbele.
Yule aliesema unaweza kuhamisha mlima na kutupia baharini , kumbe ilikuwa ni kitu kinachowezekana na siri ilikuwa kwenye kuumiliki mwili wangu kwa asilimia mia moja na kuwa bora zaidi kuliko asili.
Muda huo Hamza akiwa na furaha , ghafla alihisi kuna kitu hakipo sawa , ni kama akili yake ilirudi na kumwambia si alifika hapo akiwa ametangulizana na Regina. Kwanini ghafla tu yupo juu ya jengo anatafakari.
“Shit! Nimemsahau kumbe nilimwacha ndani peke yake”
Hamza palepale haraka sana alishuka chini na kukimbilia ukumbini, mara baada ya kufika , filamu ilikuwa imeisha tayari. Bila kujua Hamza alikuwa ametumia zaidi ya lisaa akifikiria.
Hamza aliweza kumuona Regina akiwa amesimama nje na sura iliovimba na alimwangalia na macho makali sana. Hamza mara baada ya kuona ukauzu huo alijikuta akijilegeza tu na kwa aibu aliishia kutabasamu huku akimsogelea na kutaka kumsaidia kubeba mkoba wake.
“Wife , kulikuwa…”
“Hebu niache , usichukue mkoba wangu” Regina alikoroma na kisha palepale alielekea upande wa maliwato.
Hamza aliishia kushika paji la uso wake tu , alijua amekosea hivyo hakuwa na namna zaidi ya kusubiri hapo nje.
Dakika chache Regina alitoka , hakumjali Hamza na badala yake alimpita na kutembea kuelekea upande wa maegesho ya magari. Hamza aliishia kumfuata nyuma nyuma huku akijaribu kumuongolesha.
“Mke wangu najua nimekukosea. Nilipatwa na ufunuo mpya kuhuisu mafunzo yangu na nilikuwa na shauku kubwa ndio maana , nakuahidi haitojirudia siku nyingine …” Regina kimya.
“Wife , acha basi kunichunia. Nifanye nini ili unisamehe?”
Regina aliendelea kuwa kimya na kuendelea na safari ya kuelekea eneo la maegesho ya magari. Hamza alijiambia katika moyo wake sio mbaya sana , zamani kama angemkasirisha hivyo asingeruhusiwa hata kupanda nae gari moja.
Hamza mara baada ya kuondosha gari , kimya kilitawala na hakujua ni neno gani aongee kulegeza hali.
“Sina furaha..” Ilikuwa ni sauti ya Regina mara baada ya kimya kirefu na Hamza mara baada ya kumsikia , alijua njia ipo.
“Wife najua huna furaha kwasababu yangu , nimekukosea , ngoja nikupeleke sehemu nzuri ukale chakula kitamu , nakupenda sana mke wangu , usiwe na hasira basi vinginevyo moyo wangu utavunjika vipande vipande”
“Wewe kibudu, nani akuamini .. sijali chochote kama unanipeleka kula au nini , sitokusumbua kwa wiki nzima”
“Nitakupeleka mahali , kwenda kula mishikaki , kuna sehemu naijua wanaichoma vizuri sana’
Regina mara baada ya kusikia hivyo , aliishia kutingisha kichwa tu. Hajawahi kula mishikaki zaidi ya kuona tu ikichomwa hivyo alijawa na matarajio.
Dakika chache tu Hamza aliweza kufika katika mgahawa mmoja ambao ni maarufu kwa kuchoma mishikaki mitamu na saladi. Eneo lilikuwa na watu wengi sana , lakini huduma ilikuwa safi sana na Hamza alichangamka na kuagiza mishikaki na kila kitu kinachopatikana kwa ajili ya Regina kuonja.
Mara baada ya kuletewa oda yao na harufu tamu ya nyama za kuchoma kufikia pua zake , Regina hamu iliongezeka , isitoshe hakula sana chakula cha usiku , hivyo hata kule kununa kulipotea mara moja.
“Wife nimesahau kuagizwa vinywaji , utapendelea nini , huna haja ya kuendesha gari hivyo unaweza kunywa kidogo” Hamza aliongea huku moyoni akijiambia nikifanikiwa kumlewesha huyu mrembo , pengine naweza kupata faida.
Regina mara baada ya kusikia neno kinywaji , palepale alikumbuka kuna kitu amesahau
“Aaa! Kinywaji changu cha kizombi jamani!” Hamza mara baada ya kusikia hivyo alikumbuka ni kinywaji kile kilichowekwa kwenye kikombe kilichokuwa na chata la zombi na hakujua acheke ama alie kwa muda huo.
“Wife nilikuona ukiingia nacho toilet , ulisahau kutoka nacho”
“Ndio! Wewe mjinga kwanini hukunikumbusha? Unadhani elfu kumi na tano ni ndogo?”
“Wife unatumia zaidi ya mamilioni ya hela kununua magari , unaumia kupoteza kikombe cha elfu kumi na tano?”
“Ile nilipenda chata lake la kizombi”Aliongea Regina kinyonge.
“Kula kwanza huu mshikaji , nyama yake imenona kweli , itakufanya usahau kabisa kuhusu kinywaji chako cha Zombi , usiposahau utanunua tu , si karibu na kazini pale?”
“Ah! Sasa na wewe kwanini unanichagulia hio yenye mafuta mengi” Hamza mara baada ya chaguo lake kukataliwa aliishia kuweka chini.
“Usinichagulie , nitachukua mwenyewe ninayoona nzuri”Aliongea Regina na kisha alianza kuchagua unaomfaa na kuchanganya na saladi na kutafuna.
“Wife kakipande kadogo hivyo , saladi kibao , si uharibifu tu unaofanya?”
“Nimependa hivyo , wewe kinachokusumbua nini , kama unahisi nafanya uharibfu basi kula mwenyewe , sitaki tena” Mara baada ya kuongea hivyo palepale alibeba mkoba wake na kugeuka kutaka kuondoka.
Hamza aliishia kujishangaa na kujiulizza imekuwaje amemkasirisha tena! Mbona ni kama ameongea kawaida tu au ni hasira ndio zinamwendesha.
“Mke wangu kaa basi na wewe , sitoongea tena”Aliongea Hamza huku akisimama na kujaribu kumkarisha chini.
“Nina hasira , halafu umesema mwenyewe unataka kuomba msamaha , lakini unanifanya nisiwe na furaha tena..”
Hamza aliiishia kujiambia wanawake bwana , ni kama watoto , lakini hata hivyo alijituliza.
“Wife unataka nifanye nini ili kurudisha furaha yako?”
“Nenda ukumbini ukaniletee kikombe changu cha kizombi”
“Ah! Yaani turudi hadi kule , dakika ishirini kwenda na ishirini kurudi si tutakesha barabarani kwa ajili tu ya kikombe cha plastic”
“Kama hutaki potezea , kula nyama zako mwenyewe”Aliongea Regina huku akionekana hakutaka kuendelea kubaki hapo. Hamza aliishia kung’ata meno kwa nguvu kujituliza.
“Basi sawa mke wangu , nisubiri muda mfupi tu nitaenda kukuletea”Aliongea Hamza huku akisimama na Regina mara baada ya kuona kweli Hamza anataka kwenda alimshika mkono.
“Umekuwa mjinga? Unataka kweli kwenda , si kutakuwa kumefungwa sasa hivi?”
“Lakini si umesema unakitaka hicho kikombe?”Aliongea Hamza kinyonge na kumfanya Regina kumwangalia usoni na palepale mwonekano wake ulilainika.
“Nilikuwa nakuchezea akili tu , sina hasira tena , usiende bwana”
“Wife , hivi ni sentensi gani ambayo ni ya kweli kutoka kwako? Unanifanya niogope unajua?”Aliongea Hamza.
“Wewe ndio mtawala mkuu wa ulimwengu wa giza, Lucifer mwenyewe , kwanini unaniogopa kiasi hicho. Huoni kama nakusumbua bila sababu?”
Hamza hata yeye alishajisahau kama ana hiko cheo na ni kama amekumbushwa na kuishia kujisikitikia tu.
“Sio kama nakugopa , nilitaka kukuona ukiwa na furaha kasababu nakupenda”
“Mh! Unahisi nakutosheleza kwa kuwa hivi?”Aliuliza Regina na Hamza alitaka kutingisha kichwa lakini alijua atajifunga na kubadilisha mara moja.
“Vyovyote vile mke wangu , mimi nakupenda sana na najali furaha yako”
“Hebu malizia huko hio mishikaki, inapoa”Aliongea Regina ambae mudi yake ilionekana kurudi upya na kumtaka Hamza kukaa chini na kuendelea kula mishikaki.
Hamza alirudi zake chini na kisha alichukua mshikaki na ile anataka kupeleka mdomoni aligundua Regina alikuwa akimwangalia.
“Wife kula na wewe , hizo zenye mafuta niachie mimi , chagua inayokufaa”Aliongea.
“Hamza , kwanini hukasiriki wala kunigombeza?”
“Eh!”Hamza alishindwa kuelewa ni swali gani hilo linamtoka huyo mwanamke.
“Kila muda mimi ndio nakasirika na wewe unakubali tu makasiriko yangu , kwanini huonyeshi kukasirika wala kunigombeza kwa kukasirika bila sababu za msingi , hujawahi kuwaza kunishikisha adabu?”Aliuliza Regina akiwa na shauku.
“Kwanini nikushishikishe adabu? Si kawaida kwa mke kubembelezwa , isitoshe hujaniambia nifanye kitu kibaya , hivyo nafanya tu kile unachotaka”
Regina mara baada ya kusikia hivyo , aliishia tu kutoa tabasamu lililompendezesha.
“Licha ya kuwa na wanawake wengi lakini bado unanijali . Labda ni kwasababu unajua kuna baadhi ya vitu naweza kuvumilia”
“Ndio hivyo , kama nina mwanamke nje na familia yangu kunichukia , siwezi kuwachukia, kwasababu mimi ndio mwenye makosa”Aliongea Hamza.
“Mh! Unakiri kabisa waziwazi , una wanawake nje. Kuna haja ya kuongelea hilo suala hapa ,ona sasa umenikasirisha tena, kwanini uwazungumzie wanawake wako muda kama huu?”
“Wife , lakini wewe ndio umeanzisha ..?”
“Sitaki kujali mimi. Nipe na mimi nyama , nichakulie isio na mafuta na pilipiuli nyingi na ilioungua kiasi”
“Sawa sawa , ngoja nikuchagulie nzuri utakayopenda”
Usiku huo Hamza alifaidika na vingi , licha ya kwamba alihisi ni kama akili yake ni kama inazungushwa kwa kuteswa na Regina lakini licha ya hivyo aliweza kupata ufunuo muhimu sana juu ya mafunzo yake na kuwa na uelewa mpya.
Comments