Siku iliofuata , Hamza alivyofika kazini , aliweza kumuona Rhoda akiwa amefika na amevalia suti safi na kuonekana kama mtaaluma flani hivi.
Linda mara baada ya kupewa taarifa Hamza amehamishwa na nafasi yake kuchukuliwa na mwanamke mwingine , alijikuta akipatwa na presha kubwa na mwonekano wake ulizidi kuwa siriasi.
Hamza alimkabidhi Rhoda ofisi yake huku akimpa maelekezo ya kutokugombana na Linda na kufuata wajibu wake kama bodigadi.
Mara baada ya hapo Hamza alikusanya vitu vyake na kuelekea katika idara ya usalama na ulinzi , alipewa nafasi ya kuwa meneja msaidizi , ijapokuwa bosi wake alikuwa ni Anna ambae alirithi nafasi ya Yonesi , lakini Hamza alikuwa ni kama bosi tu.
Wafanyakazi wengi wa makao makuu walikuwa wakijua Hamza ndio mtu ambae alikuwa na msaada mkubwa pembeni ya Regina , kwani tokea ajiunge na kampuni mambo mengi yalikuwa yakienda sawa kabisa.
Mara baada ya kupita katika ofisi kubwa ya idara ya ulinzi , hakuweza kuona wale walinzi wa kike kwasababu asilimia kubwa wengi wao walikuwa aidha katika floor nyingine kuhakikisha usalama na wengine walikuwa wakikagua kampuni Tanzu.
Unachopaswa kuelewa Idara zote za makao makuu zilikuwa zikisimamia kampuni zote tanzu. Hivyo kufanya kazi makao makuu ni kama kuwa bosi kwa kampuni nyingine. Hivyo wafanyakazi wa makao makuu walikuwa mabosi moja kwa moja ndio maana idara ya ulinzi ilipewa floor yao kabisa inayojitegemea.
Hamza mara baada ya kuingia katika ofisi ya Anna , pua zake zilinasa harufu ya marashi ilioambatana na ile inayotolewa na AC. Yalikuwa marashi yaliokuwa yakiashiria utu uzima.
Mapambo ndani ya ofisi hio yalikuwa mengi sana , kulikuwa na kila aina ya vitu vya kuchonga vya kila aina na pia kulikuwa na picha nyingi ambazo zilikuwa ni za Anna alizopiga katika kila inchi aliowahi kufika.
Mara baada ya kumuona Hamza akiingia , mrembo Anna uso wake wa duara ulionyesha tabasamu pana.Alikuwa na nywele ndefu alizozifunga kwa nyuma na kibanio na ngozi yake ilikuwa imetakata zaidi kuliko alivyokuwa ninja.
Licha ya ubaridi wa AC , Anna alikuwa amevalia shati la mikono mirefu ya kitambaa cha mtelezo , ukweli ni kwamba kutokana na amani ambayo alikuwa nayo kipindi hicho imefanya kubadilika sana , Anna alikuwa amenenepa na kufanya eneo la kifua chake kuwa zito sana.
Hamza alikuwa na habari zote , tokea Anna aanze kufanya kazi ndani ya hio kampuni , wanaume wengi nje na ndani ya kampuni walikuwa wakijaribu bahati zao kumtaka Anna kimapenzi , wengine walifanya kwa siri na wengine waziwazi. Lakini hata hivyo aliona walikuwa na kila haki , Anna alikuwa amebarikiwa rangi nyeusi ya kuvutia sana , ukijumlisha na lipsi zake na meno yake yalivyokuwa meupe ilitosha kutetemesha mioyo ya wanaume wengi.
Hamza kuchunguza uzuri wa mwanamke huyo uamna ulivyoongezeka , alijikuta akishindwa kujizuia na kukumbuka mchezo waliofanya.
“Karibu kwenye idara yetu , Meneja Msaidizi , Mr Hamza”Aliongea Anna huku akisimama na kumkonyeza Hamza kimadaha huku wakiwa wameshikana mikono.
Hamza aliishia kuushika mkono wa mwanamke huyo na hakuwa na haraka ya kuuachia.
“Anna kwanzia sasa nitakuwa chini yako , naamini tutafanya kazi nzuri pamoja”
“Hebu acha zako , upo hapa kwasababu bosi anataka kukuchunga. Nathubutu vipi kufanya kazi nzuri na wewe?”Aliongea Anna huku akimwangalia na macho ya kurembua.
Hamza aliishia tu kuvuta pumzi ya hewa ya baridi na kujiambia mbona sauti ya huyu mwanamke ni tofauti na mwonekano wake , alionekana kuwa siriasi huku usoni akimchokoza.
“Vipi hali ya kazi ndani ya kampuni kwa ujumla , ndugu zako vipi?”Aliongea Hamza kwa wasiwasi kidogo.
Anna hakuwa na haraka ya kujibu na aliishia tu kumwangalia Hamza usoni kwa sekunde kadhaa huku bado wakiwa wameshikana mikono.
“Kabla hatujaendelea kuongea , Meneja Hamza unaonaje tukiachiana mikono kwanza?”
Hamza alijifanyisha ndio alikuwa anajua wameshikana mikono na kucheka kwa nguvu na ile anataka kuondoa mkono , Anna alimtekenya Hamza kwenye kiganja chake na kuifanya akili ya Hamza kuchafuka , huku akijiambia huyu jini ananitafutia matatizo.
Kitendo cha kumwangalia Anna , aliona kabisa kulikuwa na nguvu kubwa inayotumika kuzuia hisia.
“Nimezisikia habari , umekuwa maarufu sana ndani ya kampuni kwa muda mfupi , vibosile wengi wa kampuni wanakufukuzia , lakini hakuna alieweza kung’oa jimbo”
“Wanaume wengi wa hili jiji wamekaa kistaarabu sana na mimi sijazoea ustaarabu wa kugandana, nimi nataka ile mambo heavy” Aliongea Anna na kisha alirudi kwenye kiti chake na kutoa sigara na kuiwasaha na kuvuta moshi huku akipiga nne na kufanya mapaja yake kutuna yalionona kutuna.
Hamza aliishia kuangalia mapaja ya mwanamke huyo yalivyo tuna na kujikuta akimeza mate mengi.
“Kama ni hivyo basi itakuwa ngumu sana kwako , kwa kambini huko sawa, ila show za kibabe huwezi kuzipata kwa hawa wazee wa viyoyozi”
“Show za kibabe , sio kitu ninachokitafuta , ninachotaka ni mwanaume muungwana na anaejua , ukweli kwenye moyo wangu nahitaji mwanaume mwenye njaa kama mbwa mwitu . Mfano mwanaume wa haiba ya Meneja Hamza na kadhalika ..”
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio ya pua , moto uliokuwa umejificha chini ya kiwiliwili cha chini uliamka na kubaunsi na kutamani kuchukua hatua. Lakini mara baada ya kufikiria namna alivyomkasirisha Regina siku ile alipotoka kwa Anna , alijikuta ni kama anamwagiwa ndoo ya maji ya baridi na bwana yule alinywea haraka.
Dunia ina wanawake wengi sana wazuri , kama atashindwa kujizuia kwa Anna basi atakuwa amepoteza juhudi zake za miaka kumi au kadhaa hivi. Aliona apotezee , isitoshe alikuwa ndani ya kampuni na angalau mahali hapo anapaswa kumuonyeshea mke wake heshima.
“Anna kwasababu unajua kabisa unachokitaka , hio ni hatua nzuri , nadhani haina haja ya kukataa wanaume , wape muda na weka hisia zako wazi , sidhani kama utakosa na pengine unaweza kupenda kabisa. Unajua katika maisha haina haja ya kuleta mikanganyiko mingi, zingatia ninachokisema , itakuwa vizuri ukiwa na familia yako”
Anna aliishia kumwangalia Hamza kwa mshangao na kisha palepale alitoa moshi mwingi wa sigara.
“Inaonekana nimekuchukulia poa uwezo wako wa kujizuia. Au nimekuwa mzee na ucheshi wangu umepungua?”
“Haha.. ukweli ni kwamba kama ningekunywa pombe kidogo , nisingeweza kuhimili. Usiudharau kabisa ucheshi wako , ili mradi utafungua mlango , wanaume wanaokufukuzia wataongezeka maradufu na nina uhakika hautokosa anekufaa”
“Lakini haijalishi ni wanaume wangapi watanifukuzia , hakutokuwepo mwanaume kama Hamza”
Hamza alihisi mtekenyo kwenye moyo wake kama vile alikuwa akiogopa kuendelea kukaa hapo na Anna ataongea kitu ambacho kitamkuna, hivyo haraka aliona aondoke.
“Nitaenda kusalimiana na wengine ili watambue uwepo wangu. Halafu huyo kwenye picha ni Yonesi?”
“Ndio, Vipi una taariza zake zozote?”Aliuliza Anna na Hamza aliishia tu kutingisha kichwa kukataa , ilionekana sio yeye tu anaemkumbuka bali hata marafiki zake wa jeshi.
Hamza aliishia kutoka nje na kufanya ofisi hio kuwa na utulivu kwa mara nyingine.
Anna aliishia kuvuta sigara na kutupa kipisi kwenye dustibin na kisha alichukua mkonga wa simu na kubonyeza bonyeza na palepale simu iliunganishwa.
“Limeendaje?” Sauti upande wa pili ilikuwa ni ya Regina.,
“Bosi! Hamza amefanikiwa kufuzu jaribio. Ameenda mbali na kunishauri nitafute mwanaume wa kuanzisha nae familia”
“Ndivyo hivyo. Kazi nzuri , endelea kumchunguza”
“Sawa , nitawachunga na wadogo zangu pia na kutowaruhusu kumsogelea Hamza”Aliongea Anna.
“Anna , wewe una busara sana. Unapaswa kujua nimekuomba ufanye hivi kwasababu yako na dada zako. Ili mradi mume wangu ataendelea kuwa chini ya idara yako na hasababishi matatizo , sitowafanyia chochote”
“Usiwe na wasiwasi Bosi Regina , najua chakufanya”Aliongea Anna kwa upole na kisha akakata simu.
Muda huo Hamza aliekuwa ametoka nje ya ofisi , hakujua alikuwa kwenye mtego wa Regina na ameweza kuukwepa. Ukweli ni kwamba hata kama afahamu kuhusu hilo asingeweza kufanya chochote , isitoshe alishalala na Anna . Hivyo hata kama asingependa majaribio hayo , angeishia tu kukubali majaliwa yake.
Anna pia alikuwa akielewa , alijua fika hata kama alikuwa akimtamani Hamza , lakini bado ni mume wa mtu. Na huyo mtu mwenyewe ndio huyo anaempa mshahara wa kuweza kulipia kodi na mahitaji mengine ya kuishi maisha mazuri yeye na ndugu zake, hivyo asingeenda kinyume. Ndio maana aliamua kukubali kufanya jaribio hilo licha ya kwamba hakupenda. Ni kwa bahati walifanya siri na Hamza hakujua na mpango ulifanikiwa kwa amani.
Hamza alienda katika ofisi ambayo Yonesi alikuwa akitumia , lakini ndio hivyo hakuwepo. Hakujua ni wapi Yonesi alipo na alikuwa akifanya nini.
Mara baada ya kuweka vizuri vitu vyake , aliwasha tarakishi na kama kawaida alipanga kuiset vizuri ili isionekane na mitandao ya kampuni , lakini ni muda ule watu waliingia katika ofisi yake.
“Bro!”
Mwanaume alieita alikuwa ni Aroni na nyuma yake alikuwa ameongozana na sura ambazo hakuzifahamu.
“Tumepata taarifa umehamishiwa kwenye idara yetu kama meneja msaidizi na hatukupata usingizi kabisa. Sikutarajia utakuja kweli , kwa uwepo wako hapa, idara yetu itakuja kuwa levo nyingine kabisa”
“Vipi kwanza , naona watu wapya?”
“Ndio kampuni inazidi kutanuka na majukumu kuwa mengi na hakukuwa na walinzi wengi wa kiume , hivyo bosi Anna kaniambia nilifanyie kazi , ndio wameanza hivyo nawazunguza zungusha. Wale wengine wapo likizo ya christmass”
Hamza pia alijua biashara za Regina zilikuwa zikikua kwa kasi mno na kulikuwa na maeneo mengi yalihitaji ulinzi , hivyo aliishia tu kutingisha kichwa kwa kuelewa.
Mara baadda ya kupiga soga na Aroni na wenzake , na kisha kwenda kupata chakula pamoja. Hamza aliona hayo ndio maisha sasa. Hakukuwa na kazi nyingi alizopangiwa kwa siku hio, hivyo alijitengenezea kinywaji na kwenda kucheza na tarakishi yake.
Baadhi ya marafiki zake Eliza na wengine aliokuwa na ukaribu nao walimtania sana siku hio na kumfanya kufurahi.
Muda wa kuondoka Hamza alikumbuka alikuwa na miadi na Irene kuonana eneo walilopanga kukutana , lakini ni muda huo huo alipokea simu kutoka kwake.
“Wewe mtoto , ndio najiandaa kwenda eneo letu la miadi , ushafika?”
“Hamza , nimepata ajali”
“Ajali ! Vipi , umeumia?”
“Hapana , nilikuwa nikirudisha gari nyuma ili kuliegesha ila nikagonga nguzo ya taa. Sijui hata cha kufanya hapa?”Aliongea na Hamza alipatwa na ahueni.
“Uko wapi?”
“Nipo Haille sellasie , mkabala na jengo la Conn supermarket”
“Nitumie link ya eneo ulipo , nakuja hapo sasa hivi”Aliongea Hamza na kukata simu.
Comments