Mbwa wa kijerumani
Hamza mara baaada ya kaungalia uelekeo aliotumiwa na Irene hakuona haja ya kutumia gari na badala yake aliona achukue taksi ndio ingeweza kumuwahisha haraka.
Mara baada ya kufika ni kweli ni kama ambavyo
Irene aliongea , kwani aliweza kuona gari aina ya Porsche ikiwa imeengeshwa mshazari karibu na nguzo ya taa huku mlango upande wa siti ya mbele ukiwa umebonyea kwa kuingia ndani.
Nguzo ya taa yenyewe ilikuwa imepinda , ilionekana iligongwa kwa nguvu sana na gari hio.
Hamza aliishia tu kusikitika na kujiuliza ni uendeshaji gani wa gari wa namna hio?.
Pembeni ya Irene kulikuwa na wasichana wawili watu wazima hivi na wanaume kama wawili , na walionekana wote walikuwa wakizungumzia ajali hio iliotokea.
Irene mara baada ya kumuona Hamza alijikuta akimkimbilia haraka kama mtoto mdogo na kwenda kumkumbatia.
“Hamza..!”
Alijikuta akianza kujidekeza kwenye mikono ya Hamza.
“Nini kinaendelea hapa , mbona huu ugongaji sio wa kawaida ?”
“Nilitaka kurudisha gari nyuma niliegeshe , ila nilisahau kumbe sikuweka gia ya nyuma na ile nakanyaga pedeli gari ikaenda mbele na kugonga nguzo”
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio , hakujua acheke ama alie.
“Ndio maana nasema bado hujaiva kwenye uendeshaji gari ila king’amg’anizi tu”
“Lakini naogopa mwenzio hili gari sio ya kwangu , kuna dada nilibadilishana nae , akiona gari yake nzuri hivi nimeiharibu sijui atanifanyanyaje. Hamza please nisaidie”Aliongea Irene kwa kupasha viganja moto.
Hamza kweli kwa kuangalia gari hio , aligundua ilikuwa ni zile gari za hela nyingi , na hata yeye pia alishangaa mwanzoni kuiona , kwa uelewa wake mahesabu ya haraka haraka ya gari hio yangegharimu zaidi ya milioni mia nne za kitanzania.
Lakini hata hivyo haikumpa shida , maana option zote mbili alikuwa akiweza kufanya , aidha kuitengeneza na kuirudisha katika mwonekano wake wa kawaida kama bima haitoshelezi au kununua nyingine. “Nitakusaidia , haina haja ya kuwa hivyo”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
Irene mara baada ya kusikia , Hamza angewezxa kumsaidia , alijikuta akishkwa na furaha.
“Hamza nilidhani utanifokea kabla ya kunisaidia . Kwa ujinga wangu naenda kukugharimu kiasi kikubwa cha pesa . Asante sana , naahidi nitakulipa kwa namna yoyote unayotaka”
Hamza aliishia kutabasamu kwa uchungu na kujiambia kwahio ashakuwa danga tayari.
“Hawa watu ni wakina nani?” Aliuliza Hamza akinyooshea kidole wasichana watatu na wanaume waliokuwa wamesimama kando ya gari ya Irene.
“Hawa dada walikuwa wakipita , huyu baba ni mlinzi ndani ya supermarket. Walikuja baada ya kuona nimegonga nguzo , kulikuwa na wengine wameondoka kabla ya kutokea”
“Hey! dada huyo ni mpenzi wako?”Aliuliza dada aliekuwa katika mavazi ya kiofisi.
Hamza mara baada ya kusikia Irene akiulizwa juu ya yeye kuwa Boyfriend ni kama hakupenda. “Ndio dada, unamuonaje ni handsome eh!”
Irene ni kama alikuwa ameamka katika hofu ya kugonga gari na sasa alikuwa akitaka kutamba na Hamza.
“Haha ! Kwa bahati mbaya sio aina ya chakula changu , kama mpenzi wangu anesikia nimegonga gari angenifokea mpaka basi. Lakini naona mpenzi wako hajakufokea zaidi ya kukumbatia na kukutuliza , Hakika una bahati”
Irene kusikia hivyo alijikuta akisikia sana raha , huku akimwangalia Hamza na macho ya kuridhika na yaliojaa mahaba.
Hamza muda huo alijua nini anachomaanisha, lakini ukweli ni kwamba hata kama ingekuwa ni mwanamke mwingine ambae angekuwa katika ajali asingewaza sana kuhusu gharama za gari zaidi ya kumsaidia kwanza kama alivyofanya kwa Irene.
Kwake yeye kufokea mwanamke na kumpiga ni kitu ambacho anaamini sio kwa ajili ya wanaume kufanya.
“Wewe Irene hebu acha kucheka , vipi ulishawasiliana na watu wa Bima?”
“Ndio nimetumia namba za kwenye gari na anasema anakuja”
Mara baada ya watu kutawanyika , fundi kutoka Bima alifika na kisha alianza kukagua na aliangalia kitambulisho cha gari na kuona kweli ilikuwa kwenye mfumo wao wa Bima.
“Huu mlango unapaswa kubadilishwa kabisa , hivyo itahitajika kuutoa kabisa. Hii ni ajali kubwa sana , mnapaswa kwanza kuwataarifu polisi waje wakague na kuwapatia ripoti ya uthibitisho”
“Ah! Si itakuwa hela nyingi sasa?”
“Ni kama milioni arobaini hivi kutokana na gari yenyewe “
“Nini! Mbona ghali hivyo?”
“Hii gari ipo chini ya bima ya kampuni yetu , kwanza unapaswa kuwasiliana na mmiliki wa gari na kisha hakikisheni mnapata uthibitisho kutoka polisi na ndio kampuni itaweza kufidia kila kitu”Aliongea na kisha alitoa maelekezo machache kidogo na kupanda pikipiki yake na kuondoka .
Hamza upande wake aliishia kukuna kichwa,alijiuliza kwanza ni nani ambae amempatia Irene gari ya kifahari namna hio kuendesha?.
Hata hivyo hakutaka kuwaza sana na palepale muda mfupi tu polsii wa barabarani walifika na mara baada ya kuona Irene ameharibu nguzo , walimwambia kwanza anapaswa kulipia nguzo na kisha aende polisi kuchukua ripoti.
Irene ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na utaratibu wa hatua nyingi namna hio na kichwa kilianza kumuuma, ni kwa bahati tu Hamza alikuwepo.
Hamza aliangalia gari hio na aliona bado ilikuwa ikiendesheka.
“Haina haja ya kwenda kucheza leo, nitakupeleka sehemu ukale kwanza na kesho nitakusaidia kufuata taratibu na kupata ripoti”Aliongea.
“Utanisaidia kweli?”
“Unatakja kufanya mwenyewe?”
Irene kusikia hivyo alimkumbatia Hamza na kumbusu shavuni , bila ya kujali barabara hio ilikuwa na watu waliokuwa wakipita.
“Hamza unanijali mno. Nina furaha kubwa kuwa na boyfriend kama wewe”Aliongea Irene na kumfanya Hamza kuishia kucheka tu.
“Sijui kwanini , ila nashindwa tu kukukasirikia, hebu twende kwanza ukale”
“Hehe , si kwasababu unanipenda sana ndio maana”
Hamza aliishia kujiuliza au ni kwe,i ametokea kumpenda huyo msichana ndio maana hakasirishwi na matendo yake.
Mbona kama namchukulia tu kama mdogo wangu?.
Hamza alimchukua Irene kwenda kula na baada ya chakula alimpeleka nyumbani kwao. Licha ya kwamba gari ilikuwa imeharibika ubavuni , lakini iliendesheka vizuri tu.
Mara baada ya kufika Masaki anapoishi Irene na kuingiza gari ndani ya geti,mlango ulifunguliwa na mwanamke alieonekana kujipenda na alishangaa baada ya kuona gari ya Irene ilikuwa imepondeka na kumfanya kuwa na wasiwasi. “Nini kimetokea! Irene kwanini gari yako imehariibika , ulipata ajali?”
Ile anasogelea ile gari kwa kuizunguka ndio muda ule Hamza alishuka kutoka kwenye gari. Mwanamke yule mara baada ya kumuona Hamza alikunja ndita., huku macho yake yakionyesha hali ya mshangao.
Hamza hakuwa mgeni na sura ya mwanamke huyo , hio ni kwasababu kipindi alichokuwa akija kumfundisha Irene alishawahi kuona picha yake , alikuwa ni bibi yake Irene upande wa baba . Ilionekana baada ya baba yake Irene kuachana na mke wake alimwita mama yake kuishi na mjukuu wake.
“Shikamoo Madam! Nimefurahi kukuona kwa mara ya kwanza”Aliongea Hamza.
Irene upande wake haraka haraka alikimbia na kwenda kumshikilia mkono bibi yake huku akianza kumbembeleza.
“Bibi naomba usije kumwambia baba , akijua nimepata ajali hatoniruhusu tena kuendesha gari. Bibi nakuomba tafadhari”
Lakini sasa bibi huyo hakuonekana kumjali kabisa Irene na badala yake macho yake yalikuwa kwa Hamza , akimwangalia kwa namna ya wasiwasi.
“Irene , kwanini umekuja na huyu mwanaume” Irene alishangazwa na swali lile.
“Bibi Hamza ni tafiki yangu , alikuwa ndio mwalimu wangu mama alienitafutia”Aliongea
Hamza mwanzoni alishikwa na wasiwasi kidogo kwa kudhania Irene angesema yeye ni mpenzi wake. Hakutegemea Irene angeficha anavyomchukulia.
Ilionekana msichana huyo sio kwamba hakuwa akiogopa , bali alikuwa akimhofia mno bibi yake.
“Rafiki! Kwanzia leo huruhusiwi kukutana nae tena , huruhusiwi kuwa na urafiki na mtu kama huyu?”Aliongea huyo mwanamke wa makadirio ya miaka sabini kwa usiriasi mkubwa.
“Bibi! Kwanini ? Sisi ni matafiki tu, kwanini siruhusiwi kuwa nae kama rafiki”Aliongea Irene.
“Unasema unataka sababu? Wewe hujui huyu ni mume wa mtu? Wewe ni msichana na yeye ni mwanaume , kwanini kuwe na urafiki kati yenu. Ukiendelea kuwa hivi unadhani ni mwanaume gani wa maana kutoka familia nzuri atakutaka kukuoa hapo baadae?”
Hamza alifikiria maneno hayo na kuona alichoongea bibi huyo kilikuwa na mantiki. Lakini kwa wakati mmoja kwasababu ya kulindwa kuja kuolewa na familia nzuri kuzuiwa kutokuwa na marafiki si sawa .
Lakini hata hivyo kuna kitu ambacho Hamza alikigundua , pengine mwanzoni hakukijua , alionekana bibi huyu alikuwa na ukaribu zaidi na familia ya Regina mpaka kumjua mara moja tu kuwa alikuwa ameoa. Alikumbuka Regina alimfahamu Irene tokea akiwa mdogo kwasababu ya ujirani , hata kwa Prisila pia.Lakini muitikio wa bibi huyo kwa kuonekana na Irene haukuwa wa kawaida, alionekana kama mtu mwenye hofu.
“Bibi Hapana! Hamza ni mtu muhimu sana kwangu . Mimi sitokusikiliza’
“Ninaenda kuongea na baba yako kuhusu hili na yeye ndio atadili na wewe! Tumekuharibu sana kwa kukudekeza. Angalia sasa marafiki uliokuwa nao?”
Aliongea na kisha bibi yule alimwangalia Hamza kwa macho mabaya.
‘Inakuwaje mwanaume umeoa , halafu unacheza na mjukuu wangu kama hivi. Hebu ondoka na usije kumsogelea tena. Kwa ajili ya Irene ngoja niishie hapa. Siku nyingine nikikuona na mujukuu wangu sitosita kumpigia simu bosi Regina”
“Kumpigia simu! Bibi mimi najuana na Regina na tulishwahi kula chakula pamoja. Siwezi kuogopa hata ukimwambia”Aliongea Irene kwa ubishi.
“Nini! Wewe .. umekutana na Regina ? Ni kwa muda gani tokea ukutane nae?”
“Nimekutana nae na ananifahamu tokea nikiwa mdogo”
“Alikwambia nini na kwanini mkutane kwa ajili ya chakula?”Aliuliza bibi kwa wasiwasi na hali ya mchecheto kidogo.
“Bibi kwanini upo hivyo leo? Najuana na Hamza ndio maana nimekuja kufahamiana na Sister Regina. Kwani kuna tatizo mpaka kutaka kujua ni lini nimekutana nae?”
Bibi yake Irene alikuwa na sura yenye hali ya kupaniki na mara baada ya kufikiria kwa sekunde kadhaa aliongea;
“Nakuonya kwanzia sasa , hupaswi kusogelea ndoa ya watu . Ukiendelea nitakufungia na hutoenda shule na hata chuo tutakupeleka nje ya nchi’
“Bibi....!!’
Irene kusikia hivyo machozi nayo hayakuwa mbali na kuishia kumwangalia bibi yake kwa hasira pekee. Hakutegemea bibi yake angemwadhibu kwa staili hio , kisa tu kuwa na ukaribu na Hamza.
“Bibi umeenda sana mbali , si kila siku unasema unanipenda sana. Wewe hunipendi tena na nakuchukia”
Mara baada ya kuongea aliikimbilia nje ya geti. “Wewe Irene unaenda wapi? Sijamaliza rudi hapa” Aliongea huku akionekana kuzidi kuwa na wasiwasi.
Hamza aliishia tu kupumua kwa nguvu na hakuongea chochote kwasababu hakujua uadui wa bibi yake Irene na yeye umetokea wapi.
“Bibi ngoja nikamlete”Aliongea Hamza na kisha alikimbilia nje kwenda kumleta Irene kabla hajaenda mbali.
“Irene hebu acha kukimbia”Aliongea Hamza wakati akimshika mkono Irene na kumfanya asimame na kumkumbatia Hamza.
“Hamza kwanini bibi anakuchukia sana?”
“Acha kwanza kulia. Wewe huoni hili sio kawaida ?”
“Sio kawaida?!” Aliuliza kwa mshangao kidogo huku akimwangalia Hamza.
“Ndio! Bibi yako anaonekana kufahamiana na familia ya mke wangu na kwa mwonekano wake wa leo ni kama kuna kitu ambacho kilitokea baina ya familia hizi mbili”
Hamza aliona hata kama ameoa , kumleta Irene nyumbani na kujitambulisha kama rafiki yake , haikuwa sababu ya kutosha kwa bibi yule kuonyesha hali ya kumchukia katika macho yake na kupaniki kwa wakati mmoja.
“Kuna kitu kilichotokea? Itakuwa ni kitu gani?”
“Hata mimi sijui . Ila hisia zangu zinaniambia kuna kitu kinaendelea”
“Hata mimi nashangaa. Sio mara yangu ya kwanza kumtambuslisha bibi marafiki zangu, na bibi ndio anaenipenda sana na kunijali kuliko hata ya mama. Nimeshangaa leo ni mara yake ya kwanza kunikasirikia namna ile kisa wewe”Aliongea Irene.
“Basi kutakuwa na sababu , kwanini bibi yako amekuwa hivi. Hivyo hebu acha kulia na kisha urudi nyumbani . unadhani kama bibi yako hakupendi ana mjukuu gani mwingine wa kumpenda? Nenda nyumbani na hakikisha haubishani na bibi yako , muache atulie kwanza. Tukishapata sababu kwanini amekasirika sana ndio tutajua namna ya kudili na tatizo”
“Hamza naona kabisa mwanzo ulikuwa una sita sita , ila sasa hivi unanichukulia kabisa kama mpenzi wako. Angalia unavyonishika sura yangu?””
Hamza palepale alishituka , kumbe alikuwa akionyesha mahaba kwa Irene bila ya kujijua.
“Hehe huna haja ya kuwa na hofu , nilijua tu msichana mrembo kama mimi huwezi kuacha kunipenda”AliongeaIrene huku akimkumbatia Hamza.
Hamza aliishia tu kulaumu tamaa zake , ukweli hakujua ni tamaa au nini .
Baada ya dakika chache za kumtuliza Irene hatimae alimrudisha nyumbani na kisha alitumia usafiri wa bolt kurudi nyumbani. Hamza kabla hajakaribia nyumbani , alikumbuka , hakuwa amenumnunulia Regina zawadi yoyote , hivyo aliomba kushushwa na kisha moja kwa moja alienda katika moja ya mgahawa na kuchukua kahawa ya maziwa ya kawaida na ya soya.
Mara baada ya kufika nyumbani , Shangazi alikuwa amekaa kwenye masofa living room na alikuwa akingalia Tv, alikuwa deep katika tamthilia hio kiasi kwamba alikuwa hadi akifuta machozi.
Mara baada ya kumuona Hamza amerudi, na kumuona akiwa na machozi alishikwa na aibu kidogo na kujibaraguza .
“Hamza , mbona leo umerudi mapema sana?” “Nimerudi baada ya chakula. Vipi Regina amesharudi ?”
“Ndio , baada ya kula ameenda kwenye chumba chake kwa ajili ya kuendelea na kazi”
Hamza aliishia kutabasamu na kisha
alizipandisha ngazi kuelekea katika chumba cha Regina na kugonga mlango , lakini aliishia katikati mara baada ya kumsikia Regina alikuwa akiongea na simu , hivyo aliingia moja kwa moja.
Regina alikuwa bize mno , mbele yake kulikuwa na furushi la makaratasi , huku akionekana alikuwa akipokea maelekezo kupitia simu kuelewa baadhi ya vipengele. Na mara baada ya kumuona Hamza akiingia aliishia tu kumwangalia na kumalizia kuongea na simu. “Vipi naona leo umerudi mapema ?”
“Ndio mke wangu. Nimekuletea kahawa ya aina mbili , kikombe cha kulia ni kahawa ya maziwa na ya kushoto kwangu ni ya soya, vipi unataka ipi hapa?”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
******
“Vipi mbona unaonekana kuwa na furaha sana?” Ilikuwa ni sauti ya Kanali Dastani kwenda kwa mwanamke alievalia nguo ya kulalia ya kitambaa cha hariri , katika moja ya hoteli ya kifaharai iliokuwa katikati ya jiji .
Mwanamke huyo alionekana alikuwa akiongea na simu na ilikuwa ni kama amepokea taarifa nzuri .
“Nilikuambia ilikuwa chaguo zuri kumtumia Irene”Aliongea huku akisogea kimadaha na kwenda kukaa kitandani .
“Unamaanisha nini?”
“Sikutegemea. Ila inaonekana mpango wetu umeenda haraka zaidi kuliko nilivyotarajia. Nimepokea simu Irene kaiharibu gari yangu”Aliongea.
“Tresha nina wasiwasi na matendo yako , ya kwanza ilikuwa Alex na sasa unataka kuwa karibu na huyu Hamza. Sioni faida yoyote”
“Dastani shida inayokusumbua naijua, unasumbuliwa na wivu , unadhani kwasababu Yulia katokea kumpenda huyu Hamza , hata mimi nitahadaika na kutoka nje ya mipango ya kazi. Kama ndio unachowaza kuwa na amani. Isitoshe hii ndio nakusaidia wewe. Sidhani unaweza kufanikisha mpango wa Yasin bila msaada wangu”Aliongea huku akiwa na hali ya kujivunia kwenye uso wake.
“Unafikiria mbali. Ninachotaka mimi ni umakini juu ya mipango yetu , unaona kilichomtokea mzee Mgweno. Sasa hivi Malibu macho yote yanamchunguza kwa kushirikiana na Sinagogu. Kosa kidogo tu na sisi tutaingia kwenye rada za jeshi”
“Pole yake Aunt Rehema . Namsikitikia kwa kile kilichomkuta ma kumuunganisha Mgweno”Aliongea.
“Licha ya Rehema kuwa na msaada mkubwa na kukufikisha hapo ulipo , lakini sioni huzuni kabisa katika macho yako”Aliongea Dastani huku akiwa na kejeli kwenye uso wake.
“Unataka nitoe kilio , ndio uione huzuni katika macho yangu , sikatai Rehema ndio alienifanyia koneksheni mpaka kufahamiana na wakubwa , lakini hio haiondoi ukweli kwamba nimefika hapa kwa juhudi zangu , ndio maana mimi nipo hai , lakini yeye alishatangulia mbele za haki”
“Tukiachana na hayo , vipi kwanza hili suala la
Alex. Una uhakika hajui chochote?”
“Nishakwambia hajui chochote , ndio maana nimemwachia huru. Alex anatumika tu , lakini suala la malighafi zinazowekwa katika vyungu hahusiki kabisa , yeye ni msambazaji na vyungu anavyopelekea wateja vinatengenezwa sehemu nyingine kabisa. Mwanzoni nilidhani ni suala lenye muunganiko wa moja kwa moja na watu wa Binamu , lakini sivyo. Kuna uwezekano Jasusi Alonzo ni Decoy”
“Decoy! Unamaanisha nini?”
“Wakati ulipokuwa Ufaransa nilikuwa nikifuatilia hili suala kwa umakini mkubwa . Alonzo anapokea maagizo chini ya watu wa kanisa la Wabrazili , lakini katika moja ya kumfuatilia , nimegudua pia yupo chini ya Taasisi ya Haliz Foundation”
“Haliz Foundation na kanisa la Wabrazili! Unataka kusema nini?”Aliongea Kanali huku akihisi kama kuna kitu kinakuja kwenye akili yake.
“Kuna uwezekano wa muunganiko kati ya taasisi ya Haliz Foundtation na vyungu , lakini vilevile kuna uwezekano wa Haliz kuwa na mahusiano ya karibu na makanisa ya Wabtazili na kama ni hivyo basi moja kwa moja Kanisa la Wabrazil lipo chini ya wasinagogu
“Na kama kanisa la Wabrazil lipo chini ya Wasinagogu maana yake , Wabtazil wanajua moja kwa moja suala la vyungu lipo vipi na Alonzo kuonekana kama analifuatilia hili suala ni kama chambo tu kufunika kile kinachoendelea”Alimalizia kanali.
‘Ndio maana nikasema Alonzo anaweza kuwa Decoy Agent. Hili ni suala ambalo hatuna uhakika nalo kwasasa kutokana na mkanganyiko wa matukuo yaliotukia hivi karibuni . Ingekuwa rahisi kwetu kama Rehema angerudi Tanzania . Sasa hivi lipo juu yako Dastani kulitafutia ufumbuzi”Aliongea Tresha.
“Ufumbuzi! Unamaanisha unataka niwe mrithi wa nafasi ya Rehema?”
“Unadhani isipokuwa wewe , atakuwa nani? Kama huwezi kufanya mwenyewe wasiliana na umoja wako wa Black Trinity waamshe jasusi wao ndani ya kitengo, Sidhani kama wanakosa Sleep Agent ndani ya Malibu”
“Hapana , siwezi kuwasiliana na umoja kwasasa. Ni mapema mno, kwasasa ulinzi ni mkubwa sana ndani ya kitengo na kila mwanachama anafuatiliwa”Aliongea na Tresha alimwangalia usoni kwa sekunde kadhaa na kisha akapotezea.
‘Vipi kuhusu faili umefanikiwa , Au safari ya Ufaransa imekuwa bure?”
“Upo mwanga tu , mbinu yangu niliotumia imelipa kwa kiasi flani , lakini sina wasiwasi kwasasa. Nishapata shabaha nyingine’
“Shabaha nyingine! Unamaanisha nani?”
“Mdogo wake Dina , kutoka upande wa familia ya babu yake. Inaonekana bado ana kinyongo na Dina kuwa kiongozi na sio yeye. Ninavyosema sasa hivi wapo hapa Tanzania. Ni mimi tu kupanga mipango yangu ya namna ya kumuingia
, ni rahisi kupata hili faili.”
“Ukifanikiwa nina uhakika utajiweka katika nafashi muhimu sana ndani ya circle ya Eliasi.
Kulia yupo Yasin , kushoto yupo Eliasi. Tukifanikiwa kumwangusha Yulia na kumpandisha Yasin . Mipango yetu yote itanyooka”
“Kwa Yulia sio kirahisi sana. Uwepo wa Hamza ndio changamoto. Licha ya hila nyingi kuchezwa afie Ufaransa lakini imekuwa tofauti. Yule mtu ni hatari sana”
“Hamza niachie mimi. Udhaifu wake upo kwa wanawake na hao hao watakuwa anguko lake”Aliongea Tresha huku akisimama na kujizungusha zungusha kwenye kioo.
Comments