“Kama umesema kila kikombe kina kahawa , kuna utofauti gani. Halafu mbona sijawahi kuona hivyo vifungashio?”
“Ndio habari ya mjini kwasasa hivi mke wangu, ni kahawa iliotengenezwa hapa hapa nchini , lakini kutokana na upekee wake ndio maana inauzwa kwenye migahawa mingi ambayo ni francaised.Nashangaa mwanamke kama wewe huna habari , wakati ndani ya kampuni wafanyakazi wengi wameshikilia mkononi” “Kwahio unasema mimi ni mshamba au?” “Hapana, ninachomaanisha ni kwamba mke wangu wewe ni wa matawi sana , ndio maana ni ngumu kujua biadhaa mpya za aina hii”Aliongea Hamza kujitetea.
“Nitajaribu kila kimoja , kujua radha yake ilivyo”Aliongea Regina huku akichukua mrija kutoka katika vikombe vyote na kuanza kufyonza kidogo katika kila kimoja.,
“Nataka hiki chenye maziwa ya soya, unaweza kunywa hiko kingine”Aliongea Regina huku akishangazwa na utamu wa kinywaji hicho.
Hamza mara baada ya kuona namna ambavyo mwanamke huyo alivyokuwa na furaha akinywa kinywaji alichomletea alijihisi joto kwenye moyo wake na kujiambia alifanya vizuri kupiga stori kidogo na marafiki zake Eliza. Ndio waliompa taarifa juu ya utamu wa kinywaji hicho, namna kinavyoshangamsha akili na radha yake.
Regina aligundua , Hamza alikuwa akimwangalia muda wote na kumfanya uso wake kushikwa na joto kidogo.
“Mbona unaniangalia kiasi hicho?”
“Ni kwasababu mke wangu anaonekana kuwa mzuri sana. Si kinai kukuangalia”Aliongea Hamza huku akicheka.
“Na hizo sifa unazonipa hata sikuamini tena. Leo nimetoka vijipele kwenye uso wangu, naonekana mbaya”
“Wapi! Mbona hata sivioni?” Hamza kweli hakuweza kuona hivyo vipele Regina anavyoongelea.
“Na huo upofu wako , utaonaje?”Aliongea Regina huku akitingisha kichwa chake kwa kumsikitikia.
“Vipi , si ulisema unatoka na Irene ? Mtoko wenu umeendaje?”
Hamza alifikiria kwa sekunde kadhaa na aliona sio mbaya kama atamwambia Regina kilichotokea.
Regina mara baada ya kusikia Irene alipata ajali alipatwa na wasiwasi kidogo na kuuliza kama alikuwa sawa na mara baada ya kusikia ni gari pekee lililopata shida aliona kumbe sio suala kubwa.
“Wife hujawahi kukutana na bibi yake Irene. Inaonekana anakufahamu vizuri tu na kunifahamu hata mimi na wewe tuna mahusiano”
“Sijawahi kukutana nae wala kumsikia na hata bibi na shangazi sijawahi kusikia wakimzungumzia , labda hawakuongea chochote. Ila itakuwa kulikuwa na mahusiano. Ninachojua tu ni Mama yake Irene aliekuwa ni jirani yetu na mara nyingi alikuwa akiishi na ndugu wa upande wa kwao”
“Basi itakuwa kuna kitu tu hatujui , ila kimetokea zamani kidogo , isitoshe wote ni wazee “Aliongea Hamza.
“Kwanini unajali sana. Kama una shauku sana kwanini usimuulize Shangazi?”Aliongea Regina.
Hamza alifikiria kidogo , ila aliona haina haja ya kumuuliza shangazi , hivyo aliamua kupotezea.
“Wife sitaki kuendelea kukusumbua. Endelea kuwa bize”Aliongea Hamza , hakutaka kuonekana kuwa siriasi na suala hilo na kumfanya Regina ahisi tatizo.
“Nisindikize kwenda kwenye Harambee na Mnada kesho. Kama una nafasi”Aliongea Regina.
Hamza alionekana kushangaa. Alikuwa tayari alishasikia kuhusu mnada huo kutoka kwa Yulia na ndio sasa Regina anamwambia.
Sasa kwasababu mke wake amekwisha kuongea na kumwalika , hakuona sababu ya kukataa. “Sawa , kesho nitajianda vizuri kwa ajili ya kukusindikiza na kuhakikisha unajivunia kwenda na mimi mke wangu”Aliongera Hamza akiwa na tabasamu.
“Eh! The Manificient King of hell will accompany me to a small charity auction , I’ am flattered”Aliongea Regina kwa kingereza huku akimwangalia Hamza na mwonekano wa kichokozi.
Hamza aliishia kutoa pumzi ya kufarijika mara baada ya kumuona Regina yupo kwenye mudi ya kumtania , na aliona ni vizuri.
“Wife nimekuita ‘ Mke au Wife ‘ Kwa muda mrefu , kwanini sijawahi kukusikia ukiniita’ Hubby?” Hamza aliona achukulie fursa mudi nzuri ya Regina.
“Kwanini unalazimisha nikuite hivyo , kwani haitoshi tu mimi kukuita kwa jina lako. Mbona wenza wengi tu wanaitana kwa majina yao?” “Lakini natamani kusikia ukiniita hata mara moja
, sio lazima kila saa japo mara moja moja”
“Nataka nifanye kazi , unaweza kuondoka sasa”Aliongea Regina huku akikaa katika mkao wa ubize .
Hamza hakuwa na jinsi , aliona bado mwanamke huyo hakuwa karibu sana na yeye kimwili , hivyo aliona ngoja asubiri , wakati utafika tu .
*****
Siku iliofuata Hamza aliishia tu kuzunguka ndani ya kampuni na ilipotimu muda wa jioni jioni , Regina alimpigia simu.
“Wife mbona kama muda wa kwenda kwenye harambee bado?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuona bado ni mapema.
“Kuna sehemu nataka unisindikize kwenda kwanza , tukitoka huko tutaelekea moja kwa moja kwenye mnada”
“Tunaenda kukagua biashara zako?”
“Hapana”
Kipindi hicho , Black Fog alikuwa msaidizi rasmi wa karibu wa Regina na ndio aliehusika mara nyingi kutoka na Regina kukagua biashara zake.
“Kuna sehemu binafsi naenda na nadhani itakuwa vizuri tukienda pamoja”Aliongea Regina.
Ijapokuwa Hamza alikuwa katika hali ya kushgaa , lakini bado alikubali na kushuka kwenye maegesho ya magari na kuwasha gari na kumsubiri Regina .
Haikuchukua muda Regina alishuka kutoka ofisini kwake akiwa ameshikilia mifuko. Hamza mara tu baada ya kuona mifuko hio , alijua ni wapi Regina anaelekea.
Mara baada ya wawili hao kuingia kwenye gari ,
Hamza aliendesha gari moja kwa moja mpaka yalipo makazi ya famili ya Regina ya zamani. Maneo ya Msasani.
Regina alipanga kumpatia Lamla zawadi ambazo alitoka nazo Paris , ijapokuwa alikuwa amesahau kwa muda , ila baada ya kukumbuka n i kipindi cha sikukuu , aliona ndio apeleke.
Mara baada ya kufika , kulikuwa na mabadiliko kiasi , kutokana na kuwepo mtu anaeishi ndani ya jumba hilo kubwa , angalu halikuwa na hali ya upweke sana.
Tokea Lamla arudi ndani ya nyumba hio ,
Regina aliwasiliana na TDS( Taita Domestic Service) Kuacha kuendelea na huduma yao.Hivyo kila kitu kilikuwa chini ya Lamla.
Lamla alizoea kuishi maisha ya kifahari tokea akiwa mdogo , lakini mara baada ya kupitia magumu , alionekana mdogo mdogo kuanza kuyakubali maisha yake mapya.
Wawili hao mara baada ya kushuka kwenye gari , waliweza kumuona Lamla akitoka nje akiwa ameshikilia boksi kubwa la glasi au kioo.
Alikuwa amevalia Aproni na ndala miguuni. Nywele zake alikuwa amezifunga kwa kurudisha nyuma. Kama vile alikuwa bize kufanya kazi za nyumbani.
Katika lile boksi la glasi , kulikuwa na Kasa aliekuwa amelala kivivu ndani yake.
Mara baada ya kumuona Hamza na Regina , Lamla alionekana kuganda kidogo , alionekana kuwa na wasiwasi , lakini kulikuwa na hali ya furaha kwenye macho yake.
“Regina , Hamza , karibuni”Aliongea
Regina mara baada ya kuona kasa yule mdogo alionekana kushangaa.
“Unamlea huyo Kasa?”
“Ndio! Naboreka kuwa mwenyewe , sijawahi kufuga kitu chochote hapo kabla , lakini mara baada ya kusikia Kasa ni mwepesi kufuga na anaweza kuniondolea upweke . ndio maana nikamnunua kwa baba mmoja aliekuwa akiwasambaza. Nimeambiwa niwe namtoa juani kila siku ili mgogo wake kumulikwa na jua”
Regina mara baada ya kusikia , hivyo alijikuta akigeuka na kukagua mazingiraya nyumba na aliweza kuona mimea mingi ikiwa imepandwa. “Hayo maua wewe ndio umepanda?”
“Ndio, sipo sana bize ndio maana nikaona pia nipande pande maua”Aliongea na kumfanya Regina kutabasamu.
‘Vipi , umegundua sasa kazi nyingi ni ngumu kuliko ulivyokuwa ukifikiria?”
“Ni kweli! Sasa hivi kadri ninavyofikiria , najiona kweli sikuwa mtu mzuri”Aliongea huku uso wake ukiwa umejaa huzuni.
Regina alichukua ile mifuko chini na kisha alimpa ishara Lamla kupokea.
“Nimekuletea hizi. Nilienda Paris nikaona sio mbaya nikikuletea zawadi. Kuhusu mifuko mingine miwili niliokuja nayo , haijapata mtu , nimeona nikuletee pia”
Hamza mara baada ya kusikia maneno ya Regina kidogo tu atoe kicheko, Yaani Regina kanunua mikoba yote hio kwa ajili yake , halafu muda huo anaigeuza kama vile ni kweli imekosa mtu.Alimfikiria Regina ila hakupata picha kamili.
Lamla hakuwa mjinga , mara baada ya kuoina mifuko hio ya Zawadi , alijikuta akipanua mdomo kwa mshangao na sekunde chache mbele macho yake yaligeuka na kuwa mekundu.
“Regina kweli umeniletea hizi zawadi kwa ajili yangu?”
“Ndio , kama hutozipenda unaweza kuzitupa tu, isitoshe sina pakuziweka”Aliongea Regina bila ya hisia nyingi .
“Nazipenda , nina uhakika nitazipenda”Aliongea Lamla huku akitingisha kichwa kwa hamasa kubwa na kupokea.
“Karibuni ndani , mpate hata kinywaji chochote , sio vizuri kusimama nje wakati hapa ni nyumbani”Aliongea.
“Asante , ila kwasasa hapana , kuna sehemu tunawahi”Aliongea Regina.
Mara baada ya kumsikia Regina akiongea hivyo , Lamla alishikwa na hali ya kusikitika kidogo , lakini aliificha na kicheko .
“Basi hata siku nyingine , najua mpo bize , siku ukipata nafasi njoo nitakuandalia chochote”
Regina aligeuka na kujiandaa kuingia ndani ya gari , lakini kabla hata hajapiga hatua , Lamla aliita .
“Regina!”
“Ndio , kuna unachotaka kuongea?”Aliuliza Regina bila kugeuka na muda huo alionekana Lamla akijing’ata ng’ata.
“Najua ninachoweza kusema sasa hivi kinaweza kisiwe na maana , lakini bado nataka kukuambia , Samahani”
Regina mara baada ya kusikia kauli hio, alitetemeka kidogo.
“Ulishaniambia hivyo mara ya mwisho”Aliongea Regina.
“Ndio. Lakini nataka kuongea kitu chochote kwako leo . Asante sana , nakushukuru sana. Najua hakuna kitu naweza kukufanyia katika haya maisha , lakini kama pepo ipo natamani kuja kuwa mama kwako. Moja ya kitu ninachojutia mpaka sasa , ni tokea siku niliokuona sijawahi kukujali kabisa.”
Regina aliishia kukunja ngumi kidogo na kisha kuiachia na akavuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Siku ya Christmass , njoo Kigamboni nyumbni , nadhani haitokuwa vizuri kumhangaisha shangazi kuja mpaka huku”Aliongea
Lamla alijikuta akishangaa , kama vile alikuwa amesikia vibaya na kujikuta akiuliza kama Regina anamaanisha.
‘Ni kweli naweza kuja?”
“Usifikirie vibaya , sitaki tu kumuona shangazi akichoka kuja mpaka huku. Pia itakuwa vizuri kama utakuwepo na kumsaidia saidia”Aliongea Regina.
“Naelewa , hata usiwe na wasiwasi , hakika nitakuija na kumsaidia na maandalizi”Aliongea Lamla huku akiitikia kwa furaha.
Mpakla hapo Regina hakuingia kwenye gari haraka na Lamla hakujua nini cha kuongea , kila mmoja alionekana kuwa katika hali ya kutafakari.
Hamza aliishia kunyamaza kwa sekunde kadhaa na kisha aliishia kusugua pua yake akihisi hali ya hewa kidogo imekuwa nzito.
Alijikuta akiangaza macho yake na kumshangaa yule kasa aliekuwa kwenye boksi akipigwa na jua.
“Huyu mbona ni kasa mweusi?!”
Lamla alijikuta akikurupushwa kutoka kwenye mawazo mara baada ya kusikkia sauti ya Hamza.
“Kuna shida kwani ? Mimi nilikutana na mzee wakati nikitoka sokoni ndio akaniambia anamuuza , nilivyoona ni mzuri nikamnunua”
“Kuna shida kwani akiwa mweusi?”aliuliza Regina.
“Huyu ni Kobe mweusi , ni jamii ya kobe ambao ni adimu sana. Nadhani huyo baba aliekuuzia alimpata kwenye mabonde ya maji ndani ndani huko porini , ila aina hii ya Kasa wanalindwa mno kutokana na kuadimika kwake”Aliongea Hamza.
Regina alishindwa kujizuia na kumwangalia huyo kasa , alionekana kulala kivivu vivu na macho yake ya rangi ya kijani , ukweli ni kwamba alionekana kuwa wa kijani ambae anaelekewa kuwa mweusi .
“Kwahio unataka kusema nini? Kwamba ampeleke katika idara ya hifadhi wanyama au”Aliuliza Regina.
“Haina haja , kwasababu unamlea basi endelea kumlea”Aliongea Hamza na kisha kumwangalia Lamla kwa macho ya udadisi.
“Kama unataka kuwa mama bora , sio mbaya kuanza kulea kobe”Aliongea na kumfanya Lamla kuwa na macho yaliojaa shukrani. “Asante sana, nitafanya hivyo”
Hamza na Regina waliingia kwenye gari yao na kisha walianza safari ya kuelekea kwenye Harambee na mnada.
Wakiwa njiani , Hamza alishindwa kujizuia kumwangalia Regina mara kwa mara na kuwa na tabasamu.
Regina alikuwa akimwona kila saa na alikuwa kimya , ila alishindwa kuvumilia mara baada ya kuona Hamza anazidi.
“Unamwangalia nani na kutabasamu?”
“Hamna tu , ni kwamba nashindwa kujizuia na kuona mke wangu anazidi kupendeza kila saa ninavyomwangalia, hivyo nashindwa kujishikilia na kukuangalia mara kwa mara”
“Mh! Lazima utakuwa unanikejeli ndani kwa ndani?”
“Kwanini nikukejeli?”Hamza alishangaa. “Unaijua sababu mwenyewe ya kunikejeli , huna haja ya kujifanyisha”
“Wife m ukweli ni kwamba hata sijali kama umemsamehe Lamla au unaendelea kumchukia , ila ukweli nimetokea kukubali moyo wako , kama ingekuwa ni mimi, nisingeweza kufanya hivyo”Aliongea Hamza.
“Kweli!” Aliuliza Regina huku akionyesha hali ya mshangao kiasi katika macho yake.
“Unadhani naweza kukudanganya. Nimekuwa mbwa?”
“Wewe ni jibwa kabisa”
“Basi wewe ni kajimbwa kadogo”
“Mimi sio mbwa. Shenzi!”
“Haha, mke wangu unavyonukia ni kama vile vimbwa vya kijerumani” Regina kusikia hivyo alijikuta akikasirika na kugeuza kichwa chake pembeni.
“Sitaki kuongea na wewe tena”
Ilikuwa utani tu , hivyo Hamza asingeendelea kumwambia alikuwa mbwa.
Hamza mara baada ya kuishi na mwanamke huyo kwa muda mrefu kidogo , aligundua alikuwa akijali sana mwonekano wake , hivyo hakufurahishwa na utani wa kuambiwa alikuwa mbwa wa kijerumani.
Mara baada ya kufika katika jengo ambalo mnada na harambee ya kusaidia watu,wawili hao walishuka nje ya gari na waliweza kuona kulikuwa na magari mengi zaidi ya mia yaliokuwa ni ya kifahari. Kusanyiko hilo la Harambee lilionyesha ukubwa wake kwa namna lilivyokusanya watu wazito ndani ya jiji la Dar.
Eneo la nje la kuingilai kulikuwa kumepambwa sana, asilimia kubwa ya mapambo yalikuwa ni yale ya kukaribisha mwaka mpya.
Kwasababu ilikuwa ni Harambee na Mnada watu wengi walivalia kawaida.
Mwonekno wa Regina ulivutia watu wengi. Wasifu wa mwanamke mrembo na tajiri , ilikuwa ni moja ya sifa kubwa iliombeba Regina.
Watu walijaribu kumsogelea Regina kuongea nae , lakini kama kawaida ya Regina hakujisumbua kuendeleza maongezi muda mrefu zaiid ya salamu pekee tema ile ya kujivuta.
Lakini hata kama Regina alionekana kuwapotezea watu hao , hakuna ambae angekasirika , isitoshe ukauzu wa Regina ndio ulifanya watu wengi kutamani kupata fursa ya kumsogelea na angalu kuongea nae kwa muda mrefu na kwenda kujisifia.
Hamza alishindwa kujizuia na kujihisi kujivunia katika moyo wake , katika macho ya wengine , mwanamke kauzu kama huyo ambae ni ngumu hata kuanzisha nae maongezi , alikuwa ndio mke wake. Ingawa nafasi yake kama mume kwa Regina haikuwa imefahamika kwa watu wengi lakini Hamza alijihisi kidume kweli.
Ile wawili hao wanakaribia kuingia katika mlango wa ukumbi , kundi dogo la watu lilionekana na kumvutia Hamza macho.
Alikuwa ni mwanaume na mwanamke wazee hivyi ambao wameongozana na watoto wadogo na walionekana ndio wanafika.
Comments