Mchoro wa kesho yetu
Alikuwa ni Mama Wadeni wa kituo cha kulele watoto cha Morogoro ,Foot Academy, aliekuwa ameongozana na kundi la watoto. Pembeni yake kulikuwa na mwanaume mzee. Hamza alimjua ni moja ya wazee waliokuwa wakisaidia ndani ya kituo hicho. Hakumuona Mzee Hizza.
“Madam Wadeni!” Aliita Hamza kwa mshangao mara baada ya kumuona.
“Hamza! Kumbe na nyie mmekuja! Nilikuwa nikijiuliza kama ningewaona , ila matarajio yangu yamekuwa sahihi”Aliongea mwanamama huyo akiwa na mwonekano wa furaha huku akimwangalia Regina.
Upande wa Regina muda huo alikuwa akimwangalia msichana mdogo kibonge aliekuwa bize kulamba ice cream. Na msichana yule mdogo mara baada ya kumuona Regina alimtolea ulimi kwa ishara ya kumchokoza.
“Dada Mbahili”Aliongea yule msichana , walifahamiana na Regina kituoni alipoenda na Hamza na matukio yaliotokea ndio yalimfanya Regina kuonekana na msichana huyo kama dada mbahili.
Regina alichanua macho yake na ile anataka kubishana na huyo msichana aligundua alikuwa eneo la wazi na watu wengi walikuwa wakiwaangalia, hivyo aliishia kujifanyisha hakumsikia.
“Madam Wadeni , na nyie mmealikwa”Aliuliza Regina.
“Katibu wa Viwanda ndio katualika mara baada ya kuona michoro ya watoto. Amesema itaongeza uzito juu ya mchoro tuliowakilisha kupigwa mnada kama watoto watashiriki pia.Ndio maana nimekuja nao. Isitoshe huu ni mkutano wa mabosi, hivyo nimeona sio mbaya kama watakuwepo hapa kutoa shukrani zao”
“Mhmh! Mbona sijawahi kusikia huu utaratibu, nani kasema uwalete?”Aliongea Regina akiwa amekunja sura.Kawaida licha ya vitu mbalimbali kuletwa kupigwa mnada lakini watoto hawakushiriki kabisa zaidi ya viongozi wawakilishi pekee .
Lakini muda huo mwanaume mwenye kitambi mrefu kidogo alievalia suti nyeusi ya Armani alisogea akiwa na uso uliopambwa na tabasamu.
“Katibu Gondwe , wewe ndio umemwalika
Madam Waden na watoto kuhudhuria?”
“Kumbe bosi Regina unafahamiana na Waden wa Foot Academy! Ndio ni mimi niliewaalika”Alikubali bila shaka yoyote na kisha alimgeukia Wadeni.
“Wewe ndio ndio Madam Hizza! Mimi ni Khatibu Gondwe , ndio niliekutumia mwaliko”Aliongea Katibu akipeana mikono na Madam Wadeni huku akiwaangalia watoto kwa namna ya kuwahesabu.
“Mbona umekuja na watoto wachache sana?”
“Oh! Ndio , nimeona itapunguza usumbufu kudili nao wote , maana wengi ni watundu sana” Waziri kusikia vile alionekana kutoridhika.
“Wadeni upo siriasi kwelim niliposema uje na watoto nilimaanisha wengi hata kituo kizima. Kwanini kuwe na usumbufu. Hata hivyo sio mbaya , muda ushaenda sana hatuwezi kubadilisha”Aliongea na kisha palepale aligeuka na kuanza kuita baadhi ya watu ambao alionekana kutangulizana nao.
“Mzee Dochi , Mzee Filimbi sogeeni sasa ni muda wa kupata picha ya pamoja na watoto”
Wafanyabiashara kadhaa walisogea waliokuwa wakisalimiana na Regina mara baada ya kumuona.
Mara baada ya hapo waliita watu na kuwachukua wale watoto na kwenda kuwasimamisha katika mabango waliokuwa wameandaa . Mabango hayo yalikuwa na majina yao kama vile walikuwa wakihofia wasipoandika majina kuna mtu anaweza kutowatambua.
“Huyu Gondwe ni nani?”Aliuliza Hamza ambae hakuwa na uso mzuri kabisa.
Ilikuwa ni wazi kabisa watu hao wanawatumia hao watoto kujitafutia sifa na sio kwamba wapo na moyo wa dhati wa kuwasaidia.
Hamza aliwachukulia Madam Wadeni , Mzee
Hizza na watoto wa kituo cha Morogoro kama familia yake , hivyo ilikuwa kawaida kutokuwa na furaha kwa kuona tukio hilo.
Mara baada ya kuona sura ya Hamza, Regina alijua tu lazima atakuwa amekasirika.
“Ni katibu mkuu wa wizara ya biashara na viwanda. Ni mfanya biashara mkubwa wa kuzalisha chuma”Aliongea Regina.
“Najua utakuwa umekasirika , lakini hakuna haja ya kulikuza hili suala kwani haitokuwa nzuri kwa watoto”
Hamza macho yake yalisinyaa , kama isingekuwa hakutaka kumtia wasiwasi Madam , angeshafanya jambo mpaka muda huo.
Mara baada ya watoto hao kupangwa vizuri mbele ya mabango , wafanyabiahsa wale walisogea wakiwa na matabasamu ya kutosha osoni na picha zikaanza kupigwa na waandishi wa habari ambao walionekana kabisa walikuwa wameandaliwa kwa kazi hio.
“Bosi Regina., unaonaje ukiungana na sisi. Haina haja ya kuwa na bango la kukutambulisha. Sura yako ni utambulisho tosha”Aliongea Gondwe.
“Haina haja”Aliongea Regina akitingisha kichwa.
Ukweli ukaribisho huo ulikuwa wa kinafiki tu na Gondwe na wenzake hawakutaka Regina ashiriki, kwasababnu walijua Regina akiwa sehemu ya picha hawatoonekana tena.
Muda huo sauti ya maringo na hatua za kimapozi zilisikika.
“Mbona kuna shamra shamra sana hapa?”
Alikuwa amevalia gauni refu lenye pasua la saizi na kikoti cha manyoya kilichomkaa vyema mwilini na kumfanya aonekane kama malkia.
Uvaaji wake uliop[itiliza ulivutia watu wengi , hata Regina ambae alikuwa na mwonekano wa kuvutia kidogo , alifunikwa na vazi hilo.
“Oh ! Bosi Yulia naona umefika na wewe muda mwafaka. Unaonaje ukiungana na sisi na kupiga picha kadhaa?”Aliongea Gondwe.
“Katibu Gondwe , huyo msichana mbele yako anavutia mno , naweza kumkumbatia”Aliongea Yulia.
Walipokuwa wamesimama katikati ya wanaume hawakuwa na furaha , sasa baada ya kumuona Yulia macho yao yalichanua.
“Dada Mkubwa wewe ni mrembo sana”Aliongea kifurushi.
Yulia kusikia hivyo alifurahi na kuinama chini na kumkumbatia.
“Kweli! Na wewe pia ni mrembo mno. Niambie jina lako ni nani?”
“Naitwa Esma Bando”
“Esma Bando! Jina limekukaa vizuri mno , ulivyonenepa kama kakifurushi”Aliongea Yulia huku akicheka.
“Ni Bando sio kifurushi”Aliongea Esma.
“Okey ! Esma Bando. Mimi dada yako mkubwa nitakupeleka kula vitu vitamu baada ya hapa”Aliongea Yulia akionyesha ukarimu.
“Sawa dada mkubwa”
“Waheshimiwa , huyu mtoto ni mdogo sana. Mimi naondoka nae”Aliongea Yulia.
Gondwe na wenzake walijifanyisha kutokumuelewa na kuendelea kutabasamu na kumuacha Yulia aondoke na Esma Bando .
Yulia akiwa amembeba Bando, alienda mpaka mbele ya Regina na Hamza, na kwa macho ya kichokozi alimwangalia Hamza.
“Naona umekuja nae? Nilijua hatokuambia” Hamza aliishia kutoa tabasamu la uchungu, ,ingekuwa vizuri kama asingeongea chochote.
Regina alimwangalia Hamza na mwonekano wa maswali ila hakuongea chochote.
“Esma kati ya mimi na huyu dada , nani mzuri?”Aliongea Yulia,
Esma alimwangalia Regina kwa macho yasiokuwa na hisia , haikueleweka Regina alimfanya nin Bando mpaka kumchukia.
“Dada Mkubwa wewe ni mrembo mno , kuliko huyu Dada mbahili”
“Wewe...” Regina mara baada ya kusikia hivyo, alijikuta akipandwa na hasira , na alichukia kuona hawezi kushindana na mtoto mdogo.
“Dada Mbahili! Regina umewafanya nini hawa watoto kiasi cha kuwafanya wasikupende ? Watoto hawana dhambi , hawawezi kudanganya.
Ila sio mbaya nadhani awamu hii nimekushinda” Yulia mara baada ya kuongea hivyo aliondoka na Bando kuelekea upande wa vioski.
“Namchukia huyu mwanaharamu”Aliongea Regina huku akipiga miguu yake chini.
Hamza alihisi kichwa chake kikianza kumuuma. Ilionekana mbele ya Yulia , Regina alionekana bado mdogo.
“Mbona na wewe huongei. Ni kweli yeye ni mrembo kuliko mimi?”Aliuliza Regina kwa hasira akimwangalia Hamza.
“Inawezekana vipi! Hakuna mwanamke kwenye dunia hii mrembo kumzidi mke wangu”
Regina licha ya kusikia kauli hio , alishindwa kuimeza hasira yake.
“Kama ningejua bora nisingekuja. Nimekasirika sana kumuona huyu mwanamke”Aliongea.
Muda huo Katibu Gondwe alimaliza kupiga picha na watoto wa kituo cha FOOT na hawakuwa wamealika hao tu wa Morogogo bali walikuwa wameita watoto wengine ambao pia walipiga nao picha.
Hamza kuona hayo yote , moyo wake ulijisikia vibaya. Lakini asingeweza kufanya chochote kutokana na mazingira yalivyo.
Mara baada ya Wadeni kumaliza , aliwachukua watoto na kumsogelea Hamza.
“Nini kimekutokea , mbona sura yako imekuwa mbaya hivyo ?”Aliuliza Madam.
“Hakuna tu”Alijibu Hamza kifupi.
“Mtoto mjinga. Unadhani sijui nini unafikiria. Lakini katika ulimwengu huu kuna vitu ambavyo mtu hawezi kukataa hata kama hapendi au hafurahishwi navyo. Ila hayo ni mambo ambayo unakubaliana nayo tu kwasababu ni ya kupita, haijalishi mabosi wanatuchukuliaje , ila ili mradi tuna hela ndani ya kituo chetu za kusaidia maisha ya watoto. Sioni haja ya kufikiria sana , si ndio malengo ya kituo ?”
Hamza na Regina mara baada ya kusikia maneno ya mwanamama huyo , walishangaa baada ya kuona kwamba Madam Wadeni alikuwa akijua unafiki wa matajiri hao , ila aliamua tu kukubaliana nao kwa ajili ya watoto.
“Madam ni mara chache sana kuwakubali watu , ila kwako nimetokea kukubali sana”Aliongea Regina na tabasamu.
“Regina haina haja ya kuwa siriasi hivyo , mimi na Hiza tayari ni wazee na hatuna muda mwingi wa kuendelea kuwasaidia hawa watoto. Ikitokea fursa ya kuwasaidia , kitu pekee ni kufanya kila linalowezekana kufanikisha. Ijapokuwa malengo yetu kwasasa ni kutafuta mtu ambae anaweza kurithi nafasi zetu”
“Madam Wadeni , kwani mna shida ya kiafya , nakumbuka hata mara ya mwisho Mzee Hizza alionekana kukonda sana na hata wewe pia unaonekana kunyongea”Aliongea Hamza.
“Ukiwa mzee ni kawaida kukonda. Bado nina afya nzuri tu, hata usiwe na wasiwasi”Aliongea akijaribu kumthibitishia Hamza alikuwa na Afya nzuri.
“Sijui , ila sidhani kama kutatokea viongozi wazuri wa kituo kama wewe na Baba Hizza. Unaonaje tukisaidia , itakuwa vizuri mkipata mrithi mapema na kustaafu”Aliongea Regina.
Hata Hamza alikuwa akifikiria hivyo hivyo , ila hakujua nani angefaa kuongoza kwa kurithi nafasi za Wazee hao.
Regina alisalimiana na baadhi ya watu aliofahamiana nao kabl ya tukio kuanza.
Muda mchache baadae Hamza na Regina walionyeshwa siti zao na kwenda kukaa mbele kabisa.
Haikuchukua muda mrefu pia , viongozi kadhaa wa serikali walipanda juktwaani na kutoa hotuba fupi ambayo ilikuwa ndio kama ufunguzi wa tukio hilo la mnada na harambee.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni mnada kwanza na kisha ndio harambee ingefuatia.
Na haraka haraka ili kuokoa muda , mtu wa kuongoza mnada alikaribishwa na rasmi mnada ukaanza.
Kitu cha kwanza kupigwa mnada , ni mchoro kutoka katika moja ya kituo cha kulelea Yatima kilichopatikana Mkoani Tanga Wilaya ya Lushoto milimani.
Kulikuwa na kila aina ya vitu , iwe michoro , vifaa vya kuchomga na vitu vingine vingi vya kisanii , lakini hata hivyo, vitu hivyo havikuwa na thamani sana, isitoshe ufundi uliotumika haukuwa ule mkubwa. Ila matajiri walivinunua kwa hela nyingi zisizopungua laki nne.
Ilivyofikia zamu ya watoto wa kituo cha Foot , wakiongozwa na wadeni wao , waliweza kutoa karatasi kubwa kabisa iliokuwa imekunjwa kunjwa na mara baada ya kufunguliwa, kulionekana michoro ya aina nyingi katika karatasi hio ya pamoja . Moja ikiwa ni maua , michoro mingine ilikuwa majengo na nk. Ilionyesha dhahiri watoto walishirikiana kuchora mchoro mmoja. Na kisha kuupatia jina la Mchoro wa Kesho yetu.
Mshereheshaji wakati wa kuutolea maelezo mchoro huo , alimpa nafasi pia Madam Wadeni kusimama , huku akisema hela zote zitakazopatikana katika mchoro huo zitaenda moja kwa moja katika kituo chake bila ya kupunguzwa hata kidogo.
“Bei ya kuanzia ya huu mchoro ni laki moja , kila mtu anapaswa kuongeza elfu hamsini kila anapotaja bei”Aliongea.
“Nitauchukua kwa milioni kumi”Aliinua kibao Katibu Gondwe.
Kununua mchoro huo kwa milioni kumi , licha ya kutokuwa na thamani , ilionekana kiasi kingi cha pesa. Na watu wengi walimpongeza kwa kupandisha bei haraka mpaka kufikia milioni kumi.
“Watoto ni taifa la kesho , siwezi kuwasaidia watoto wote kwa hiki kiasi kidogo , kitu pekee ninachoweza kufanya ni kuonyesha ukunjufu wangu wa moyo , hivyo msinipongeze sana , mimi Gondwe ni suala dogo sana hili kwangu”Aliongea akiwa amesimama .
Kutokana na alichofanya , watu wengi waliona aibu kushindana nae , isitoshe walifahamu ndio aliewaalika watoto wa kituo cha Foot kutoka mbali morogvoro huko , hivyo alihitaji nafasi ya kujionyesha. Hivyo mabosi waliona haina haja ya kufanya mambo kuwa magumu kwake.
Isitoshe mchoro huo ulikuwa ni kama takataka tu baada ya kuununua , hata kama ungeuzwa kwa elfu kumi usingekuwa na thamani hio. Hivyo hakuna alieuhitaji.
Mara baada ya Katibu Gondwe kuongea hivyo, palepale alitembea na kumsogelea Madam Wadeni na kupeana nae mkono huku akiwapa nafasi waandshi wa habari kupiga picha.
Madam Wadeni hakuona shida , alionyesha ushirikiano na alienda mbali kutoa shukrani zake nyingi kwa niaba ya watoto.
Mara baada ya kuona tukio hilo na matendo yanayoendelea , Hamza alishindwa kabisa kuzikabili hasira zake na kuishia kucheka kikauzu na kuongea kwa sauti;
“Baada ya kupiga picha zote hizo , unatoa hela ndogo hivyo ?”
Ingawa sauti yake haikuwa kubwa sana , lakini ilitosha watu wengi kuisikia ndani ya ukumbi huo uliokuwa tulivu.
Isitoshe pia mwanaume ambae ameambatana na Regina , alikuwa ni sehemu ya macho ya watu wengi na walitamani kujua ni nani haswa , lakini hawakuweza kuuliza.
Katibu mara baada ya kusikia kauli ya Hamza , mwonekano wake ulikakamaa na aliishia tu kutoa tabasamu kuficha hasira yake.
“Wewe ni mshirika wa Mkurugenzi Regina sio. Inaonekana una maoni mengi kuhusu mimi , naweza kujua jina lako na cheo chako kama hutojali”Aliongea.
“Mimi sio Mdoshi kama wewe, kazi yangu ni ya ulinzi tu “Aliongea Hamza.
“Nini!” Mara baada ya kusikia Hamza alikuwa ni mlinzi tu halafu anajaribu kuongea ongea alijikuta akikunja uso kwa hasira.
“Yaani mlinzi tu halafu unathubutu kukejeli ukarimu wangu ? Bosi Regina ni tabia gani hii ya mtu uliekuja nae?”
“Hujamuelewa tu alichomaanisha , anasema punguza ubahili”
“Wewe..” Katibu ghafla tu alikosa usemi na kufanya watu waliosikia kauli hio kushindwa kujizuia na kuachia kicheko.
Regina alimwangalia Regina kwa sekunde kadhaa na kisha aliinua kibao chake juu.
“Nitaununua kwa milioni mia moja”
“Haaa!!”
Wimbi kubwa la mmako lilisambaa karibia ukumbi mzima , mara baada ya kusikia kauli ya Regina . Hata mwendesha mnada mwenyewe alijikuta akishangaaa na kudhania , labda amesikia vibaya.
“Samahani! Mkurugenzi Regina , unamaanisha milioni mia moja?”Aliuliza kupata uthibitisho.
“Ndio” Regina aliitikia.
Hamza aliishia kumwangalia mke wake na kujiambia huyu msichana anaelewa kauli ya mke anapaswa kumfuata mume. Kiasi hicho cha pesa kilikuwa kikubwa kulinganisha na milioni kumi aliotoa Katibu na kumkomesha kabisa.
Mwendesha mnada alijifikiria mwenyewe na kujiambia kama mchoro huo unaweza kuuzwa kwa milioni mia moja , si jiwe la rangi tu kando ya barabara linaweza kugeuka almasi na kuuzwa kwa bilioni?.
Waandishi wa habari waliokuwa ndani ya eneo hilo walimmulika Regina na picha za kutosha na hawakumjali tena Katibu Gondwe. Kwenye vihwa vyao walikuwa wakijiambia , hio ni taarifa kubwa kesho kwenye vyombo vya habari.
Katibu Gondwe alikuwa na hasira kiasi kwamba uso wake mweupe uligeuka kuwa mwekundu, ilikuwa ngumu kwake kutoa zaidi ya milioni mia kununua uchafu unaoitwa mchoro kwa ajili ya kushindana na Regina.
“Milioni mia , kwa mara ya kwanza , milioni mia kwa mara ya pili...”
Ile watu walipodhani , Regina anakwenda kuutwaa mchoro kwa kiasi cha milioni mia moja , sauti nyingine kutoka nyuma ilisikika.
“Milioni mia mbili!”
Yulia na sauti yake ya maringo aliongea . Hali ya msisimko ilipaishwa zaidi na kauli ya Yulia Sio kwamba hakukuwa na matajiri wakuweza kutoa kiasi hicho cha pesa ndani ya eneo hilo , kulikuwa na matajiri wakubwa tu kama Tajiri Salim , Tajiri Bilali, Tajiri Rost na wengine. Licha ya kwamba wengi wao walikuwa wakitoa misaada kwa watu wenye uhitaji , lakini ni wachache waliokuwa na moyo wa kutoa zaidi ya milioni mia mbili kwa pamoja.
Kingine hakuna ambae alikuwa tayari kushindana na mrembo Regina ambae alikuwa ni kama malaika wa biashara ndani ya Tanzania? Waliona haina haja ya kushindana na mwanamke huyo.
Umati huo ulishindwa kujua nini kinaendelea , ukweli ni kwamba Katibu Gondwe ambae alipanga kuchukulia mnada huo kama sehemu ya kujitangaza katika mbio zake za kuwania Ukurugenzi wa shirika la misaada dunani ukanda wa Afrika , hakujua cha kuongea tena , kwani alifunikwa na akafunikwa tena.
Mwanzoni aliona ni sawa kwa mwanamke kauzu kama Regina kushindana nae maana alishazoea kama mfanyabiashara , lakini mpaka Yulia , Mwenyekiti wa makampuni ya Prima
Wanyika. Nani wa kuthubutu kushindana nae , ilihali hata cheo chake kilitokana na koneksheni na familia hio .
Katibu huyo aliishia kutoa tabasamu la wasiwasi na kisha bila ya kupenda alijikalisha chini na kutulia. Ilionekana dhahiri hakutaka kuendelea kutaja bei.
Hamza upande wake alihisi kuna kitu hakipo sawa na ilikuwa ni kweli , kwani mara baada ya kumwangalia Regina , macho ya mwanamke huyo yalikuwa na hali ya ukauzu usiokuwa wa kawaida.
Upande mwingine Yulia alikuwa akijisikia raha, alimwangalia Regina na tabasamu la kejeli, lililojaa uchokozi.
“Milioni mia tatu” Regina aliinua kibao kwa mara nyingine na kuongea.
Kwa mara nyingine hadhira ilishikwa na mshituko. Mwendesha mnada kidogo tu azimie.
Katibu Gondwe aliishia kutoa kitambaa tu na kujifuta jasho. Hakutaka kuongea neno na aliishia kujiuliza ni watu gani hawa?.
Alikuwa akifikiria fikiria kutoa kiasi kikuibwa cha pesa , maana aliona kama angekosa mchoro huo , ingekuwa ngumu kwake kujitangaza na picha alizochukua.
“Milioni mia tatu kwa mara ya kwanza..”
Bila ya kusubiri mwendesha mnada kuongea kwa mara ya pili , Yulia aliinua mkono wake tena.
“Bilioni moja”
Kwa namna ambavyo Yulia alitamka neno , Bilioni moja ni kama alikuwa kwenye duka la mangi na ananunua pakti ya sigara.
Matajiri wenye asili ya kihindi na kiarabu waliokuwa ndani ya eneo hilo , walijikuta pia wakishikwa na butwaa.
Bilioni moja. Kwao waliona ni kubwa sana na ingefanya mambo mengi ya kuendeleza biashara zao. Baadhi ya wajasiriamali waliokuwa na mitaji chini ya bilioni moja sura ziliwashuka , ilikuwa hela nyingi sana.
“F*ck! Naota au , ni kweli Yulia katangaza kutoa bilioni moja kwa ajili ya ule mchoro?”
“Kwenye maisha yangu yote ni bwana mdogo ndani ya suruali yangu anaeweza kutema bilioni moja pekee”
“Hahahah..”
Kundi hilo la watu waliishia kucheka na kushangaa. Lakini kwa wakati mmoja walimuone wivu Wadeni kwa kuwa na bahati namna hio kwenye usiku huo wa mnada.
Upande wa Madam Wadeni , alitaka kuzimia. Licha ya kwamba kituo chake kishapokea msaada mkubwa , lakini bilioni moja ilikuwa hela nyingi sana.
Hamza hakujali ni kiasi gani Yulia anatumia, jambo kubwa hapo ni kwamba Regina alikuwa akitaka kupasuka kwa sababu ya Yulia.
Regina aliishia kugeuza kichwa chake na kumangalia Yulia na kisha palepale alikunja ngumi na kuinua mkono wake juu.
“Bilioni kumi”
“Pwaah!”
Waliokuwa wakinywa vinywaji kidogo kidogo , walijikuta wakitema chini kama vile vinywaji vimekuwa vichungu ghafla mara baada ya kusikia kauli ya Regina.
Eneo lote lilipatwa na hali ya ukimya ghafla , matajiri waliokuwa ndani ya eneo hilo , ghafla tu walijikuta mikono yao ikianza kuwatetemeka. Hawajawahi kuona mnada kichaa wa namna hio ukitokea ndani ya ardhi ya Tanzania.
Tena kwa kununua mchoro ambao haukuwa na thamani yoyote , lakini ghafla tu unafikia thamani ya bilioni kumi.
Yulia alijikuta akikunja sura , huku akimwangalia Regina na mshangao
“Bosi Regina , usiwe na haraka , bilioni kumi ni hela nyingi sana..”
“Kweli kabisa , haina haja ya kushindana na
Yulia , utajiri wao ni wa kifamilia”
Baadhi ya wajasiriamali waandamizi , waliokuwa na mahusiano mazuri na Regina walijaribu kumtuliza atengue kauli.
Comments