Bilioni kumi waliona ni hela nyingi sana na , ni ngumu kwa Regina kuwa na Cash ya kiasi chote hicho cha pesa , labda auze hisa za kampuni au kuuza vitu alivyokuwa akimiliki.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kama Regina angetumia bilioni kumi , maana yake asingebakiwa na hela binafsi , zaidi ya hisa za kampuni pekee ambazo ndio utajiri wake hukadiriwa .
Ijapokuwa ni kiasi ambacho anaweza kupata ndani ya muda wa mwaka mmoja tu , lakini bado kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa.
Hamza hata yeye aliona mwanamke huyo , alikuwa amekurupuka , ingawa alifurahi kuona kituo kinakwenda kupata kiasi kikubwa cha pesa , ila hakutaka mke wake kutumia nusu ya hela zake zote kwasababu alikuwa na hasira juu yake kwa kujihusisha na Yulia.
“Wife hakuna haja ya kutoa kiasi chote hicho. Yulia anatumia hela za familia yake , ila wewe unatumia za kwako ulizopata kwa jasho”Aliongea Hamza.
Regina aliishia kumpotezea Hamza na alimwangalia Yulia akiwa kimya tu.
Vimulimuli vya kamera vilikuwa vikimmulika Regina mfulululizo. Muda huo hakuna aliethubutu kuondoa kamera katika eneo Regina alilokaa.
Mshereheshaji nae , hakuwa na haraka ya kutangaza , alivuta pumzi nyingi na kumsubiria Yulia kuongea.
Yulia aliishia kusinyaza macho yake kwa muda, na mara baada ya kufikiria kwa sekunde kadhaa aliishia kushusha kibao chake chini huku akishusha pumzi.
Ingawa alikuwa na hela nyingi , lakini kama angetumia bilioni kumi , watu wa famili yake wasingekuwa na furaha nae. Hata kama ni kifamilia , kiasi hicho cha pesa kilikuwa kikubwa mno.
Msherehesjaji mara baada ya kuona hivyo , haraka sana alitangaza na kisha akagonga meza chini kuashiria mchoro umeuzwa.
Sauti nyingi za makofi zilisikika ukumbi mzima, licha baadhi ya watu kumuona Regina kama kichaa , lakini wengi walimpongeza kwa ujasiri wake.
Watu wengi walitegemea kwanzia kesho na sherehe zote za christmass na mwaka mpya , tukio la Regina lingekuwa mada ya moto itakayovuma.
Katibu Gondwe aliishia kuufyata huku macho yakiwa yamtemtoka , licha ya yeye pia kuwa mfanyabisahra , bilioni kumi ni hela zake zote za uendesjaji katika biashara zake. Na ule mpango wa kutumia picha kujipa promo ulifutika mara moja.
Baada ya mchoro kununuliwa kwa bilioni kumi , mnada uliofuata ulipooza ghafla. Hata tukio la Harambee hela iliokusanywa haifukifia hata nusu ya kiasi ambacho Regina ametoa.
Mwisho wa Mnada na Harambee , mshereheshaji alikubali ombi la wengi na kumwalika Regina juu ya steji kwa ajili ya kutoa neno ni kipi kimemsukuma mpaka kuamua kutoa kiasi chote hicho cha fedha?.
Hamza mwanzoni alijua mwanamke huyo asingekuwa tayari kupanda juu ya steji na kuongea , lakini ilikuwa nje ya matarajio yake mara baada ya kumuona Regina akisimama na kuanza kuzipiga hatua kusogelea steji.
Mwonekano wa Regina ulikuwa ni wa kikauzu na wa utulivu wa hali ya juu mara baada ya kupokea microphone.
“Najua...”Alianza, “Wengi wenu sasa hivi mnadhani labda nimekuwa kichaa kwa kufanya kitu ambacho naweza kujutia”
Ukumbi wote ulikuwa kimya , huku wengi wakiongea chini , ilikuwa kweli , watu wengi walijua Regina anafanya kitu ambacho angejutia baada ya kutoka hapo.
“Katibu Gondwe naomba nikuulize swali , ukiachana na harakati zako za kisiasa, kama mfanyabiashara , umewezaje kupata hela zote ulizonazo?”
Watu wengi walishangaa , hawakutegemea Regina angemuuliza Katibu Gondwe swali lingine?.
Katibu Gondwe alikuwa kwenye mudi mbaya mno , kama sio Regina yeye ndio angekuwa star wa usiku huo. Mara baada ya kusikia swali kutoka kwa adui wa maendeleo yake aliishia kulazimisha tabasamu .
“Kama mjasirialmali nilijua ni nini wajibu wangu kwa jamii na pili uwezo ninao”
“Uongo!”
Regina alikataa waziwazi jibu la Katibu wa biashara na viwanda na kufanya matajiri wengi waliokuwa ndani ya eneo hilo kumshangaa. Ni kama hawakutegemea kama Regina angekataa jibu waziwazi..
Katibu Gondwe aliishia kutoa tu mdomo , huku akiwa na hali ya kukosa amani na kama mwanaume hakujua namna ya kurudisha jibu.
Hamza aliishia kuangaza macho yake kulia na kushoto na alijikuta akishagaa mara baada ya kuona uwezo wa mke wake kuongea mbele ya watu ulikuwa wa juu mno. Aliona watu wengi walikuwa kimya wakitaka kusikia kile anachokwenda kuongea.
Mara baada ya muda wa ukimya,kila mtu akiwa amemkazia macho kwa umakini , Regina aliendelea ;
“Nimekataa jibu lake kwasababu sio yeye tu ambae anaweza kupata hela , kuna watu wengi hapa wanaweza kutengeneza pesa , ndio maana mpo wengi mliokaa hapa, kila utakae muuliza atakuwa na jibu hilo hilo , hakuna ambae atakataa, hana uwezo wa kutengerneza hela. Kuwa na uwezo wa kutengeneza hela , sio kwasababu ya uwajibikaji wenu kwa jamii , sababu ambayo inawafanya kuwa na uwezo wa kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa ni kwasababu mnajisikia vizuri mkiwa na hela nyingi , hivyo mpo tayari kufanya chochote kuona mnahela nyingi, Kwenu hela ni kama madawa ya kulevya , hamna namna ya kujisikia vizuri pasipo kuwa na hela za kutosha”
Watu wengi walimsikiliza kwa umakini , wengi walikubaliana nae na wachache pia ambao hawakukubaliana nae walikuwepo.
“Bosi Regina yupo sahihi , sio uwezo wetu unaotufanya kuwa na pesa nyingi pekee bali ni tamaa zetu ndio zinatusukuma kutengeneza pesa nyingi , matajiri wanapenda kuona akaunti za benki zikizidi kuongezeka masifuri na hakuna kiasi ambacho wanaweza kusema hiki kinanitosha”Aliongea mmoja.
Aliamini matajiri kuwa na hela nyingi sio kwasababu ya uwezo pekee wa kuzitengeneza , bali kutokana na hela kwao kuwa sehemu ya furaha yao , wapo tayari kufanya lolote hata kama ni nje ya uwezo wao kuona wanaingiza hela.
Yanahitajika matamanio ya kuzipenda hela sana ndio kuweza kuzipata nyingi , kwani bila matamanio huwezi kwenda mbali kuzipata .
“Pengine wote mnashangaa , kama nimeweza kutengeneza kiasi chote hiki cha pesa kwa nguvu kubwa , kwanini nitumie kiasi kikubwa mara moja kutoa msaada ? Sababu ni moja tu kwangu , hela kwasasa hazinifurahishi.
Watu wengi walikunja sura , kama isingekuwa ni Regina anaetamka maneno hayo , hakuna ambae angeendelea kusikiliza.
Nani asiefurahishwa na hela? Hizo si kauli za masikini pekee ,kauli maarufu ya sizitaki mbichi hizi?.
“Ni wangapi kati yenu mnakumbuka mara yenu ya kwanza kuingiza kiasi kukubwa cha fedha ni hisia za aina gani mlizopata, ni furaha gani mliojisikia?”
Aliuliza Regina huku yeye mwenyewe akiwa amenyoosha mkono juu. Matajiri wengi waliokuwa ndani ya eneo hilo walinyoosha mikono yao juu , wakiwa na hali ya kumbukumbu za nyuma.
Kwao kiasi kikubwa cha kwanza kutengeneza katika maisha yao , hisia waliozpata ndio zilikuwa za aina yake.
“Mimi bado ni mchanga , lakini najua fika baada ya miongo kadhaa nitakuwa kama mabosi wengi mliopo hapa. Nitakuwa ni mwenye kukumbuka siku nilioweza kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kwa mara ya kwanza. Hata hivyo je sasa hivi ni kama mwanzo , je mkiingiza kiasi kikubwa mnapatwa na hisia mlizopata wakati mkipata kiasi kikubwa cha pesa kwa mara ya kwanza? Jibu ni kwamba hamuwezi. Sasa hivi mnajua hata kama mpate hala nyingi hamuwezi kuwa na furaha wala kupata msisimko mliokuwa nao mlivyofanikiwa kwa mara ya kwanza”
“Sisi ni kama mashetani ambao ili tuishi lazima tule hela bila kukoma , ndio maana kila kukicha tunawaza kukusanya hela ambazo tayari zishakosa thamani kwetu. Na kadri tunavyokula hela ndio njaa zinavozidi kutushika na kuona labda kiasi fulani kitanifanya kuwa na furaha , hivyo ngoja nijitahidi. Tunaishia kununua , Private jet , maboti ya kifahari , makasri na mengineyo lakini licha ya hivyo kila kitu kinakuwa kawaida. Hatimae tunaanza kufa ganzi , tunapatwa na homa ya ajabu inayoitwa kutoridhika”
Matajiri wengi walikuwa na hali zisizoelezeka katika nyuso zao. Ilikuwa kweili , zamani kupata bilioni kuliwafanya kuwa na furaha , lakini kipindi hicho kupata bilioni haikuwafanya kuwa na furaha , walitaka mabilioni na hata wakipata hayo mabilioni wanajikuta hawaridhiki na watakaka zaidi na zaidi , mwisho wa siku sio kutafuta hela tena bali ni ugonjwa wa kutoridhika ndio unaowasumbua.
“Bosi Regina hizo ni athari za kuwa tajiri , kila jambo lina faida na hasara zake”Aliongea mmoja wa wafanyabiashara.
“Kama unahisi hela ni ushetani , kwanini usitoe zote msaada kanisani au msikitini?” Aliuliza mwingine.
“Mnapaswa kuniuliza kwanini nimetoa bilioni kumi kama msaada , jibu ni hili nasijisikia vizuri sana hapa. Kabla sijawaza kutoa msaada wa bilioni kumi sikuwaza kabisa nitapata hisia kama ninazopitia sasa hivi , ni hisia zile zile nilizopata baada ya kupata kiasi kikubwa cha pesa kwa mara ya kwanza. Kutumia hela bila ya kufikiria ni kiasi gani utapata , ni dawa nzuri ya ugonjwa mliokuwa nao matajiri. Imenifanya sasa hivi nijue ni nini nakitaka na sio pepo wa hela anachokitaka kwangu. Kutoa ndio njia pekee ya kulimiliki pepo la njaa ya hela na sio pepo la hela kukumiliki. Ninachokitaka mimi ni umiliki , sitaki hela nataka kuyamiliki maisha yangu”
Regina mara baada ya kutamka kauli ya mwisho kwa nguvu , matajiri wengi walikumbwa na bumbuwazi. Wote walionekana kuathirika na maneno ya Regina kama vile alikuwa akiwahubiria.
“Vizuri! Umeongea vyema”
Haikujulikana ni nani alieongea wa kwanza , lakini ghafla tu watu waliunga mkono na makofi mengi yalisikika.
“Shenzi! Hata mimi pia ngoja nitoe kiasi kikubwa cha pesa kujitia hasara , kufikiria tu kutoa bilioni kadhaa nahisi mwili kunisisimka”Mmoja aliongea.
“Ndio kabisa , msisimko wake unaonekana kuwa mzuri zaidi kuliko kununua boti ya kifahari” Matajiri wengi walionekana hisia zao kuamka , waliona pengine wakitumia hela zao nyingi kutoa msaada wanaweza kuipata furaha ambao wameikosa kwa muda mrefu licha ya kununua vitu vingi vya kifahari.
Regina alishuka nje ya steji , akipongezwa na makofi mengi sana mpaka alipoirudia siti yake.
“Wifey! Kwahio kumbe uwezo wako wa kuongea mbele ya watu ni mkubwa hivi.Nilijua huwezi kuongea neno hata moja mbele ya kadamnasi ya watu”Aliongea Hamza.
“Kama sijui kuongea mbele ya watu , nawezaje kuwasiliana na wafanyakazi wangu. Usiniambie kwenye vikao naenda tu kukaa kimya?”
Hamza alikuwa akijua Regina alikuwa na confidence ya kutosha kuongea mbele za watu , ni hivyo tu alikuwa akitafuta namna ya kumsifia.
“Lakini mke wangu , unapanga kweli kutumia bilioni kumi kwa ajili ya kutoa msaada? Mbona ni kama hela nyingi sana , umemfanya hata Madam Wadeni kuchanganyikiwa”
Bila ya kusubiri Regina kujibu , Yulia alisogea.
Hamza alikuwa na wasiwasi ni kauli gani mwanamke huyo anakwenda kuongea.
“Regina nimekubali kushindwa leo , hotuba yako iliokuwa ni yenye kugusa sana” “Asante”Alijiibu kavu.
Yulia aliishia kumwangalia Hamza na mwonekano wa kichokozi.
“Kesho kutwa naelekea nyumbani kusherehekea sikukuu ya Christmas na mwaka mpya.Unapaswa kutafuta muda wa kuonanakabla sijaondoka”Aliongea
Hamza mara baada ya kusikia sentensi hio , miguu ilimlegea na alitamani kumpiga Yulia kibao cha makalioni. Kuongea hivyo kama sio kumtafutia matatizo ni nini?.
Lakini Yulia alikuwa ashaondoka baada ya kurusha bomu na kumuacha yeye na Regina pekee. Aliangaliwa na jicho sio la kawaida.
“Wife sio kama unavyodhania , ameongea vile kwa ajili ya kutaka tu kutugombanisha , usimsikilize kabisa”
“Unapaswa kumuwahi , amekuwambia anarudi nyumbani kwao?”Aliongea Regina na kisha palepale alitembea kumsogelea Wadeni.
Madam Wadeni alikuwa bado katika hali ya kiwewe , Bilioni kumi za haraka haraka alijihisi ni kama anaota hela zinamdondokea kutoka juu angani.
“Mkurugenzi Regina , nashindwa kujua ni kwa namna gani nikushukuru kwa ukarimu wako. Natamani kupiga magoti na kushukuru kwa niaba ya watoto na wafanyakazi wote wa kituo”
“Madam! Huna haja ya kuwa hivyo ,. Ni kama nilivyosema , nimetoa kiasi hiki cha pesa kwa ajili yangu binafsi kujisikia furaha.Umefanya mambo mengi mzuri kulinganisha na mimi kwenye maisha yako”Aliongea Regina.
“Hili sio jambo dogo kabisa , ukweli nikwambie tu. Sijawahi kuwaza tutakuja kupata kiasi kikubwa cha pesa namna hii kwa ajili ya kituo. Nashindwa hata kujua ni kwa namna gani tunakwenda kuzitumia. Isitoshe wewe na Hamza ni mume na mke naona ni kama nachukua hela za familia”
“Madam kama unahisi kutuo hakihitaji kiasi chote hicho cha pesa , zinaweza kugeuzwa za kitaasisi ili kufikia watu wengi zaidi , nchi yetu ina yatima kibao ambao wanahitaji misaada”
Madam Wadeni mara baada ya kusikia kauli hio ya Regina , alijikuta akishangaa , kama vile alikuwa akifikiria juu ya suala hilo.
“Madam hili ni wazo zuri kweli , unaweza kukaa chini na Mzee Hizza mkajadiliana. Kama kweli mtaunda Foundtadion, itawasaidia kuwekeza hizi hela kibiashara na kuziongeza zaidi na faida inayopatikana itaendelea kusaidia wenye mahitaji. Si ndio wife?”
Hamza alitaka kumuunga mkoo Regina , ili kuwa na furaha , lakini ilikuwa ni kwa bahati mbaya mwanamke huyo alikuwa amekasirishwa na Yulia, hivyo aliaga na kuondoka bila ya kujibu.
“Madam sisi tunakuacha , usifikirie sana kuhusu ukubwa wa kiasi cha pesa , hela inatatua shida nyingi. Kama kituo mnaweza kukaa chini na kufikiria namna ya kuzitumia mtakavyooona inafaa”Aliongea Hamza na kumfanya Madam kutabasamu.
“Namuona Regina anaonekana kuwa na hasira. Ingawa sio sahihi kujua nini sababu , lakini nakushauri kwenda kumbembeleza. Wanawake hawawezi kustahimili kubembelezwa na wanaume wanaowapenda”
Hamza alitingisha kichwa na kisha kumfuata Regina nje.
Ile Hamza anafika nje , wakati Regina akiwa amefikia gari na yeye pia , Regina aligeuka na kumwangalia kwa mshangao.
“Unaenda wapi?”
“Wife si tunaenda nyumbani?”
“Nenda kamtafute Yulia, kwanini unataka kwenda nyumbani na mimi ?”Aliongea Regina bila ya kuonyesha furaha.
“Wife alichoongea Yulia ilikuwa makusudi ya kukufanya uwe hivi , ukiendelea kuwa na hasira utamfanya afurahi”
“Basi mpigie sasa hivi mbele yangu na umwambie huwezi kuonana nae tena na akusahau”Aliongea Regina akiwa na uso wa kikauzu.
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio , mwili wake ulikakamaa na kujiambia yote hayo yalikuwa makosa ya Yulia. Ukweli Regina hakuwa na haja ya kwenda mbali hivyo , lakini uchokozi wa Yulia wa siku hio , ulienda mbali sana. Lakini hata hivyo ingekuwa ngumu Hamza kusikiliza kauli ya Regina na kumpigia kweli simu na kumwambia h awezi kuonana nae tena.
Muda huo huo Hamza akifikiria cha kuongea , simu yake ilianza kuita na haraka haraka aliitoa mfukoni na kuangalia nani anampigia na alikuta ni Black Fog.
“Rhoda vipi! Kuna taitzo?”
“Bro Bazo amezingirwa na watu waliovalia Mask. Inaonekana kuna mtu amepanga kumteka Irene “Aliongea Black Fog.
Bazo ni moja ya maninja wa Baffodil ambao walipewa kazi ya kuml;inda Irene kwa siri na kwa umakini wa juu.
Kama lisingekuwa suala kubwa , Bazo asingechukua hatua ya kupiga simu na kuomba msaada. Hata pale Irene alipopata ajali, Bazo hakuchukua hatua kwasbabu halikuwa suala kubwa sana. Labda tu Irene yupo katika hatari kubwa.
Nani anachokoza nyuki?
Comments