Msukule wa Utumwani.
Hamza mara baada ya kusikia taarifa hio, mapigo ya moyo yalienda kasi mno kwa kuhisi tatizo ni kubwa.
“What position!”Hamza aliuliza haraka haraka na Black Fog alitoa majibu ya uelekeo na Hamza alikata simu palepale na haraka sana alifungua mlango wa gari na kuingia ndani.
“Hey! Nini kinaendelea?”Aliuliza Regina mara baada ya kuona sura ya Hamza ilivyokuwa siriasi ghafla tu baada ya kupokea simu.
“Kuna mtu anajaribu kumteka Irene , napaswa kuwahi kutoa msaada , Wife wewe ita usafiri wa Uber kukupeleka nyumbani”Aliongea Hamza.
Regina mara baada ya kusikia kauli hio , palepale aliingia ndani ya gari na kufunga mkanda.
“Wife , unafanya nini , naenda kumuokoa mtu!” Hamza alionekana kushangaa.
“Hata mimi pia nataka kwenda , haijalisihi ni hatari gani unaenda kukutana nayo , haijalishi ni wapi unaenda , usifikirie kuniacha nyuma”Aliongea Regina akiwa na macho yaliojaa usiriasi na ishara ya wasiwasi na woga,.
Hamza moyo wake ulitingishika , alijua mwanamke huyo alikuwa akihofia suala lingine la uhai na kifo kutokea , hivyo hakutaka kumuacha akienda mwenyewe.
Ingawa Hamza aliona haina haja , lakini kuokoa muda aliishia kutingisha kichwa na kuliwasha gari.
Alikanyaga pedeli ya spidi na kuingiza gari ndani ya barabara na kutoka ndugki kama chui alieachiwa kutoka katika kibanda chake na kufanya watu kushangaa na kuona labda Regina alikuwa akijutia kutoa hela nyingi na sasa ukichaa umemshika.
Tukio lilitokea eneo la Mikocheni kwa Warioba kwenye barabara kuu katikati kidogo ya bustani ya kuuzia miti na maua nje kidogo ya Kawe , ni eneo ambalo lilikuwa na miti mingi na hifadhi ya viwanja vya manispaa ya maendeleo ya jiji.
Mara nyingi eneo hilo lilikuwa halikosi watu ambao walikuwa wakielekea na kutoka Mwenge , lakini kutokana na muda pamoja na watu kujiandaa na sikukuu eneo hilo halikuwa na watu wengi.
Muda huo ndani ya eneo hilo kulikuwa na mapigano makali yaliokuwa yakiendelea, kulikuwa na watu kadhaa waliokuwa wakisogea kwenda mbele na kurudi nyuma kwa spidi kubwa , huku sauti za vishjindo na milio ya visu ikisikika.
“Clang , clang!!”
Visu viwili vilionekana kuzuia mashambulizi ya upanga mrefu. Mwanaume aliekinga shambulizi lile alijikuta akirudi nyuma na kukwepa shambulizi lingine kutoka kwa mtu mwingine.
Mwanaume wa umri wa makamo alionekana yeye peke yake akipambana na watu wanne waliovalia Mask nyeusi na mavazi ya rangi ya kijivu. Kwa kuangalia tu nguvu zao zilikuwa ndogo mmoja mmoja kulinganisha na mtu waliekuwa wakimshambulia , lakini kwasababu walikuwa wakishambulia kwa pamoja, walionekana kufanya bwana yule kupata wakati mgumu.
Na kilichomuongezea ugumu zaidi ni kwamba alipaswa pia kumlinda msichana mdogo ambae alikuwa akitetemeka pembeni yake kando ya mtaro.
Irene alikuwa katika hali ya woga kiasi kwamba mpaka machozi yalikuywa yakimtoka , huku mikono yake akiwa amekumbatia begi la madaftari akiwa anatoka kujisomea.
Katika maisha yake hakuwahi kutarajia ghafla tu akiwa katikati ya barabara atasogelewa na watu waliovalia kininja na kutaka kumteka, ilikuwa ni kama anaangalia filamu .
Ni kwa bahati nzuri tu mwanaume alievalia mavazi meusi alijitokeza na kumkinga kwa mbele na kumwambia asikimbie , kwani kuna uwezekano wa wengine mbele.
Muda ule Irene akiwa hajui chakufanya kwa kutokujua aendelee kumwamini mtu aliemwambia asikimbie , ghafla tu alihisi mkono ukilishika bega lake kwa nyuma.
“Ahh!!”
Alijikuta akishituka kwa nguvu huku akigeuka nyuma mara mmoja.
Nyuna yake alionekana mwanaume asiemjua , mwanaume huyo sura yake ilikuwa imepauka sana , huku macho yake yakiwa yamesinyaa kwenda ndani. Alikuwa ni mweusi lakini mwenye nywele ndefu mno kama za kizungu zilizofungwa kwenda nyuma , akiwa katika mavazi ya joho.
“Miss Irene nifuate”Aliongea yule mwanaume kwa lugha ya kingereza, lakini sauti yake ilikuwa kali kuashiria ilikuwa kama ya mwanamke na sio ya mwanaume .
Irene alizidi kutetemeka mara baada ya kuona mtu huyo mwenye muonekano usio wa kawaida , pamoja na sauti yake isioendana na mwonekano.
“Wewe.. Wewe ni nani?”Aliuliza
“Mimi ni Msukule wa Utumwa , sina thamani ya kujulikana kwako”Aliongea.
“Msukule wa Utumwa! Irene alijikuta mwili ukishikwa na baridi mara baada ya kusikia jina hilo.
“Msukule wa Utumwa , maana yake nini?”
“Msukule wa Utumwa ni msukule wa utumwa , hakuona maelezo mengi”Aliongea kwa sauti ya kunong’oneza.
Irene alijikuta akichanganyikiwa zaidi na maneno yake.
“Kwanini mnataka kunikamata?”Aliuliza Irene kwa hofu.
“Msukule wa utumwa kazi yake ni kufuata maagizo ya mtumishi wake , hatuulizi sababu”
Bazo ambae alikuwa amezingirwa na wanaume wanne wakimshambulia , mara baada ya kugeuka aliweza kumuona Msukule wa utumwa na macho yake yalimtoka kwa mshituko.
Palepale alijikuta akipiga sarakasi mbili matatata sana huku siraha zikipita katika uso wake na ile anatua chini alikuwa amepunguza ukaribu wake na Irene.
“Ms Irene sogea karibu yangu”
Irene palepale alitaka kukimbia kumsogelea
Bazo , lakini ila anataka kufanya hivyo yule Msukule wa utumwa , alikuwa ameshajitokeza mbele yake na kumzibia njia.
Ilikuwa ni kwa spidi sana , kiasi kwamba hata Irene mwenyewe hakujua ni kwa namna gani mtu huyo aliweza ghafla tu kuwa mbele yake.
Yule Msukule wa utumwa hakujali mshangao wa Irene na aliishia kumwangalia Bazo kwa macho makali yenye chuki.
Bazo palepale alikumbwa na mlipuko wa nishati za mbingu na ardhi na kwa spidi ya hali ya juu aliruka sarakasi , akiwa ametanguliza kisu mbele na kumsogelea Msukule Wa Utumwa .
Msukule wa utumwa alisogea kama kivuli na kukwepa shambulizi la Bazo.
Lakini ni kama Bazo alishategemea shambulizi lake atalikwepa , vinginevyo asingeweza kujitokeza katika eneo hilo bila ya yeye kumuona. Hivyo lengo lake ni kumfikia Irene na kumpatia ulinzi.
Ilionekana kundi hilo la watu , walichotaka pekee ni kumteka Irene na sio kumuua. Hivyo kidogo hakuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama wake.
“Ms Irene kimbia upande wa kushoto kwako , endelea kukimbia na usisimame”Aliongea Bazo kwa nguvu.
Irene haraka sana alianza kukimbia kuelekea uelekeo alioelekezewa. Ingawa spidi yake ilikuwa ndogo sana , lakini alijitahidi kutumia nguvu zake zote kukimbia.
Yule Mtumwa mara baada ya kuona vile , alionekana kutokuwa na haraka na alimwangalia Bazo kwa sura ya kikauzu.
“Unaonekana hujui kikufaacho, nilitaka kufuata maagizo ya master na kutokuua , lakini ukithubutu kuzuia alichotaka Master . Usije kunilaumu mimi Msukule wa Utumwa kuwa mkatili”
Mara baada ya kumaliza kuongea , aliinua mkono wake juu kwa ishara na wale maninja wengine wanne walimuacha Bazo na kwenda kumzingira Irene.
Palepale yule bwana Mtumwa alimsogelea Bazo akiwa katika umbo kama la nyoka. Bazo alitaka kwenda kumsaidia Irene , lakini kwa uwezo alioona kutoka kwa Mtumwa pamoja na kuzidiwa nguvu alijikuta hana jinsi.
Alijiambia mpango ni kummaliza kwanza huyo
Msukule wa Utumwa na kisha kwenda
kumsaidia Irene. Hivyo aliongeza uwezo wake katika kiwango cha juu sana katika kushambuliana na Msukule wa utumwa .
Wakati kila mmoja akimsogelea mwenzake , umbo la Msukule wa utumwa lilikuwa la ajabu mno kiasi kwamba lilitengeneza hali ya kumchanganya Bazo.
Bazo upande wake hakutaka kuingia katika mtefo wa mbinu hio na kwa kutumia kisu chake alisogea na kumltenga Msukule katika eneo alihisi ni shingo .Lakini katika hali ya kutotarajia , Msukule ule wa utumwa haujukwepa kabisa shambulizi lile na badala yake alidaka kisu kile na kilichosikiika ni sauti ya mvunujiko ilioambatana na cheche.
Bazo mara baada ya kuangalai kwa umakini , alijikuta akiwa katika mshangao , aligundua mkono wa Msukule wa Utumwa ulikuwa umetengenezwa na chuma. Mikono yake ilikuwa ni kama ya roboti , lakini umbo lake lilikuwa likitisha mno, ni kama vile ni kucha za Zimwi.
Alijikuta akijiuliza huyu ni binadamu au ni jini? Bazo alijawa na hofu lakini hakuacha kuendelea kushambulia. Alitumia mguu wake mmoja kurusha teke na kumlenga Msukule wa utumwa katika tumbo lake.
Msukule ule wala haukukwepa , na teke lile lilimpata kisawa sawa katika kiuno chake. Alionekana kupata maumivu kiasi cha kutoa mguno lakini haraka sana alitumia mkono wake wa kushoto na kushika paja la Bazo.
“Siiiii!!’
Surulali yake ilichanwa na zile kucha za chuma zilitoboa ngozi yake na kumpelekea maumivu makali.
Bazo alikuwa katika maumivu , alikuwa na bahati tu baada ya kuona kucha zile hazikuwa na sumu, vinginevyo angeweza kufa mara moja.
Lakini mara baada ya muda wa kupambana na huyo Msukule, Bazo aligundua , ijapokuwa alikuwa na kasi katika kushambulia , lakini uwezo wake haukuwa mbali sana na wake , ni kama walikuwa wakilingana ki uwezo, hivyo ingechukua muda mrefu sana mpaka mshindi kupatikana.
Ijapokuwa Bazo alitakiwa kumsaidia Irene kutoka kwa wale maninja wengine wanne , lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kumshinda kwanza Mskule wa utumwa.
Upande mwingine , Irene hakwenda mbali sana alikuwa ameshafikiwa na wale maninja wanne na kumzingira pande zote.
Msichana huyo alijua amekwisha kamatwa na watu hao na hana lingine la kufanya kujisaidia, lakini ile watu wale wanataka kumkamata, ghafla tu vivuli vya watu sita vilijitokeza kutoka pande zote za barabara.
Watu hao sita wenyewe walikuwa na mask za vilemba usoni , walionekana kama vile walikuwa maninja kwenye filamu za kihistoria za kituruki.
Irene alijikuta akipiga makelele , ila wale maninja wanne waliokuwa wakimfukuzia walishituka haraka na kuanza kushambuliana na wale watu sita wa mask nyeusi za vilemba, mara baada ya kuhisi nia yao mi kutaka kumuua Irene.
Ghafla tu pambano lilichukua sura mpya , huku Irene akishikwa na wale watekaji na kutupiwa pembeni kwenye majani kwanza kuruhusu pambano.
Bazo mara baada ya kusikia purukushani za mapigano zikitokea upande aliokimbilia Irene, alijikuta akishikwa na hali ya kuchanganyikiwa akijiuliza ni jambo gani lilikuwa likiendelea. Bila kujijua kitendo cha kushangaa alikuwa amempa nafasi adui na kumshambulia.
“Kufa!!”
Msukule wa utumwa mara baada ya kuona Bazo amefanya kosa , palepale alichanua makucha yake ya chuma na kumlenga kifuani kama vile ni kiumbe cha kishetani.
Bazo alijikuta akilaani ndani kwa ndani , lakini hata hivyo alikuwa amechelewa sana kushitukia shambulizi hilo, hivyo ikawa ngumu kwake kukwepa.
Ghafla tu kivuli cha mtu kilitokea katika maua na kumpiga kikumbo Msukule.
Msukule wa utumwa mara baada ya kugongwa na kitu kilichokuwa na spidi kali mpaka kushindwa kushituka alijikuta akifyatuliwa kama mpira huku akitema damu nyingi.
Mara baada ya kuona mwanaume akiwa amesimama mbele yake, Bazo alijikuta jasho la ubaridi likimvaa huku ishara ya tumaini ikimrudia.
“My – Prince!”
Mtu aliemsaidia alikuwa ni Hamza . Hamza alikuwa akiendesha na mara baada ya kuona amekaribia , aliona anapaswa kwanza kuona hali ilivyo kabla ya kusogeza gari karibu , hivyo alishuka na kumuacha Regina kuendelea kuendesha.
Ijapokuwa Hamza aliharakisha kuja mahali hapo , lakini hakufanikiwa kufika haraka , ilikuwa ni kwa bahati tu aliweza kufika kwa wakati na kuyaokoa maisha ya Bazo.
Hamza hakujali makelele ya Bazo na haraka sana aligeuka na kuangalia upande wa kushoto kwake , pambano kali lililokuwa likiendelea na haraka sana alikimbia upande huo.
Hamza alisogea kwa kasi , hakujali kabisa kundi la maninja hao waliokuwa katika levo ya mzunguko kamili wa mafunzo ya nishati , kwake aliwaona kama vifaranga na mbwa tu.
Mara baada ya kumpaisha mmoja na ngumi m wawili wengine aliwapiga na mateke na kufa hapo hapo.
Irene mara baada ya kumuona Hamza ghafla tu ametokea , alijikuta akiacha kulia na sura yake kupoa na kujishika magoti kwa kuhema kwa tabu.
Ilimchukua Hamza dakika moja tu kudhibiti karibia maninja wote , watatu wakiwa wamekufa na wengine kupoteza fahamu.
Hamza mara baada ya kumuona msichana huyo akiwa katika hali ya woga kiasi cha kutia huruma aliishia kumshika mkono kwa namna ya kumpoza.
“Okey! Upo salama sasa”
Irene hatimae alirudi katika akili yake na kujikuta akimkumbatia Hamza kwa nguvu huku akilia.
“Hamza kwanini umechelewa. Naogopa sana...” Upande wa Hamza ukweli ni kwamba hata yeye alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa , muda mfupi mara baada ya kuona hao maninja waliovalia mask wakipigana aliweza kugundua walikuwa na mafunzo yanayofanan, kama vile wametoka kambi moja.
“Hamza , hawa watu ni wakina nani , kwanini wanataka kuniteka? Kuna mtu nimemkosea au kuna mtu anataka kunichukua kwa nguvu kimapenzi kwasababu ya uzuri wangu?”
Hamza alishindwa kujizuia na kutabasamu , huku akjiambia kuna haja gani ya kujifikiria mzuri katika wakati kama huu.
“Unafikiria sana , wewe sio mzuri peke yako mchi hii, mpaka watu waagizwe kuja kukukamata”
“Oh...” Irene alijikuta akianza kufikiria kwanini jambo hilo limemtokea na mara baada ya kuwaza mtu aliemkosea jina moja tu ndio lilijitokeza kichwani mwake.
“Au ni Sister Regina amegundua kinachoendelea kati yetu ndio maana ametuma watu kunikamata..”
“Wewe hebu acha kufikiria ujinga, najua hawa watu wanatokea wapi , lakini sijui kwannini walitaka kukuteka na wengine walionekana kutaka kukuua”Aliongea Hamza.
Wakati Hamza akiongea aliweza kuona kulikuwa na baadhi ya maninja waliokuwa wakijivuta vuta kwa maumivu wakipanga kurotoka.
“Bazo!”
Aliita Hamza na palepale Bazo alisogea na kuwazimisha maninja hao kwa mara nyingine.
“Atakaejaribu kusogea tu , anakufa”Aliongea Bazo kwa tahadhari huku akichezesha kisu chake mikononi.
Hamza mara baada ya kumtuliza Irene , alimwambia akae pembeni na kisha alisogelea wale watu na kuwaangalia kwa namna ya kuwachunguza.
“Mmetumwa na Mathias Huge si ndio”Aliuliza Hamza.
Swali la Hamza lilimfanya Bazo kushangaa.
Hakutarajia maninja hao walikuwa watu kutoka Binamu na staili zao za mapigano kuwa za watu wa Bondeni.
Maninja kadhaa ambao walikuwa na fahamu waliishia kuziba midomo yao wakionyesha hawakuwa kabisa na mpango wa kuongea.
“Hata kama msitake kuongea , najua mnapotokea kutokana na mbinu zenu za mapigano na nembo za mavazi yenu. Msipo nijibu moja kwa moja nitaamini mnatokea kisiwa cha Binamu, hivyo nitamuuliza Mathias mwenyewe anipe maelezo”Aliongea Hamza.
Muda huo , Msukule wa utumwa ambae alijeruhiwa na Hamza , alionekana kurejewa na nguvu na kusimama kusogea karibu.
“Mr Hamza , Master wangu hakuwa na nia ya kumdhuru kabisa Irene . Tulitumwa hapa kwa ajili ya kumlinda pekee na pia kumpeleka kisiwani kama mgeni”aliongea Msukule Mtumwa kwa sauti ya shida.
“Wewe ni towashi!?” Aliuliza Hamza akiwa amekunja sura.
Hamza alikuwa na uwezo wa kumjua bwana huyo kuna kitu hakipo sawa kupitia sauti yake na pia msisimko wa nishati yake ya mbingu na ardhi ilikuwa sio ya binadamu wa kawaida.
“Msukule wa Utumwa ni vijakazi wa familia ya Master Mathias Huge , Mtumwa ni mtumwa yaani msukule”Aliongea na Hamza macho yake yalionekana kuelewa kitu.
“Nishawahi kusikia watu wa Binamu wamekuwa na utaratibu wa kuasili wavulana Yatima kwa kuwakusanya duniani kote na kisha kuwakata sehemu zao za siri na ulimi , ili kuwawezesha kuvuna nishati za mbingu na ardhi kwa wepesi bila kuchanganywa. Sijawahi kuamini kama ni jambo la kweli, kumbe ndio nyie mnaofahamika kama Misukule ya utumwani”Aliongea Hamza.
“Kwasababu umesema wewe ni kijakazi wa familia ya Huge , kwanini amekuja kunichokoza , ilihali tayari ana madaraka yote ndani ya watu wa Bondeni na Binamu. Au amechaganyikiwa?” Aliongea Hamza
Msukule wa utumwa alijua hakuwa na uwezo wa kupambana na Hamza , hivyo aliishia kuvumilia Master wake akisimangwa.
“Mr Hamza , unapaswa kujiuliza kwanini hao wenye Mask za vilemba , walikuwa wakitaka kumuua Irene?”
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alisinyaza macho na kisha aliwageukia wale maninja.
“Hata mimi nilikuwa nikijiuliza , nyie si wote mnatokea sehemu moja, Kwanini wengine mpo hapa kwa ajili ya kuteka na wengine mpo kwa ajili ya kuua?”
“Mr Hamza , hao unaowaona wametokea familia ya Dosala”Aliongea Msukule wa utumwa kwa kumaanisha.
“”Watu wa familia ya Dosala! Unamaanisha wametumwa na Mzee Dosala na mwanae?” “Ndio , upo sahihi kabisa”Alijibu.
Hali ya wasiwasi , ilionekana katika macho ya Hamza.
Mzee Dosal aliemtaja alikuwa ni moja ya familia huko bondeni ya ukoo wa Dosa.
Dosa ni jina la ukoo na herufi mbili za mbele zilikuwa ni uwakilishi wa mzaliwa ,Kama ilivyo kwa babu yake Regina aliefahamika kwa jina la Dosam , sasa alikuwa na kaka yake wa damu aliefahamika kwa jina la Dosal licha ya mama kuwa tofauti.
Sasa ni sawa na kusema Dosal ni babu yake Regina na inasemekana hakuwa na uwezo wowote wa nishati za mbingu na ardhi na alitegemea nguvu ya nje , yaani konekshni kutoka mataifa yenye nguvu kwa ajili ya kuwa na nguvu ndani ya kitengo cha Binamu na Bondeni.
Mtoto wake Dosal , alikuwa ndio yule Mzee Suwi aliejaribu kumpokonya Regina pete , wakati wa msiba wa bibi yake, lakini Suwi yeye alikuwa ni mtoto wa kuasiliwa , hivyo hakuwa na damu sawa na ya familia ya Regina, hivyo ni sawa na ksuema kizazi kipya cha damu ya Dosa kilichobakia alikuwa ni Regina peke yake.
Hayo yote Hamza aliyafahamu na alijiuliza , kama ni hivyo kwanini Mzee huyo kutuma watu kuja kumuua Irene , kuna uhusiano gani ama siri gani ambayo imefanya maamuzi hayo yafanyike kwa maninja kutumwa kumuua Irene?.
Hamza muda ule alijikuta akishiindwa kujizuia na kukumbuka chuki ambayo bibi yake Irene alionyesha mara baada ya kuonekana na yeye. Alijiuliza au chuki ile ilikuwa na uhusiano na suala kama hilo?.
Hamza hakuwa na majibu ya kutosha na alijiona ajipe muda kujua sakata hilo kwa undani.
“Kwanini Mzee Dosal akatuma mtu kwa ajili ya kumuua Irene?”Aliuliza Hamza.
Irene aliekuwa akisikiliza , alijikuta akichanganyikiwa pia , licha ya kwamba hakuwa akielewa chochote kinachoendelea , lakini alitaka kujua kwanini watu hao walitaka kumteka na wengine walitaka kumuua.
“Mimi ni Mskule tu maana yake sijui kitu”aliongea.
“Hujui au hutaki kuongea?”Aliuliza Hamza.
“Sijui. Hata kama Mr Hamza umpige huyu Msulule wa Utumwa mpaka kifo chake , hawezi kujua kitu”
Hamza hakuwa na nia nyingine tena , alimpa ishara Bazo na palepale aligeuka na kumkumbatia Irene kwa mbele na kufanya macho yake kuwa kifuani mwake, ili asione kinachoendelea .
Irene hakujua kwanini mwanaume huyo ghafla tu alimkumbatia kwa mbele. Lakini ndani ya sekunde aliweza kusikia ukulele kutoka mbele yake.
Mara baada ya muda, Hamza alimwachia Irene na kuondoka eneo hilo akiwa amemshika mkono .
Irene alijikuta akishindwa kujizuia na kugeuza kichwa chake kuangalia kinachoendelea na alijikuta uso wake ukifubaa mara baada ya kumuona Bazo alikuwa amemuua yule Msukule wa utumwa na wale wengine ambao walikuwa hai na sasa alikuwa akiwaondoa barabarani na kuwatupia kwenye kiwanja kilichozungushiwa ukuta.
“Usiwe muoga , kwasababu ushapitia hili kwa mara ya kwanza , basi ni hakika utapitia tena hali kama hii baadae..”Aliongea Hamza wakati akimwangalia msichana huyo na tabasamu.
“Ila nitakulinda bure kabisa bila ya kunipa hela hata kidogo.”
Irene alijikuta ujasiri ukimvaa mara baada ya kusikia maneno ya Hamza na hatimae kutulia.Alijikuta akijibana kwenye mwili wa Hamza kimahaba na kumnong’oneza. “Hutaki nikulipe kwasababu unajua naweza kukulipa kwa staili nyingine”
Hamza alihisi kitu laini na cha kuchoma choma kikigusa mkono wake , na kujiambia huyu mtoto alikuwa amefanikiwa kuwa na mtaji mkubwa kifuani kwake.
Ile Hamza anataka kuongea neno , ghafla tu gari lilitokea katika makutano ya barabara ya kuingia Kawe na Mikochen B na kumulikwa na tochi.
Regina akiwa kwenye gari aliweza kumuona Hamza na Irene namna walivyokuwa wameshikana na kutembea , walionekana kuwa wapenzi kabisa.
Comments