Regina aliekuwa na hali ya wasiwasi , dakika kadhaa zilizopita , aijikuta akikunja ngumi kwa hasira mara baada ya kuona jambo lile. Macho yake yalikuwa yamejaa ukauzu wakati akishuka kutoka kwenye gari.
Hamza alikubwa na hofu na haraka sana alitoa mkono wake kutoka kwa Irene na kujiweka pembeni , huku akitoa tabasamu la wasiwasi.”
“Wife nadhani haujafikiria vibaya..”Hamza aliongea kujitetea.
Irene kwa aibu alirudi nyuma ya Hamza huku akimwangalia Regina kwa hofu.
“Sister Reg..”
“Mimi sio dada yako” Regina alikaripia.
“Wife nipe nafasi nijielezee”
“Nina macho , sitaki maelezo yako. Yaani nimekuchukulia poa sana , imegeuka mwalimu na mwanafunzi mmeamua kutegana kwa michezo ya kuongopeana kutekwa. Eti Irene anataka kutekwa , kumbe kuja mpaka huku navuruga mipango yenu ya kimapenzi”
Hamza alijikuta akikosa neno , mara baada ya kuona Regina kuelewa vibaya na kutoona kweli kulikuwa na shida. Ila kwa mtu yoyote angefikiria hivyo , maana hakukuwa na ishara yoyote ya watekaji ndani ya eneo hilo na kubwa zaiudi ni kama magari yalikuwa yamezuiliwa kwa muda na sasa yalikuwa yakipita kwenye barabara hio na kufanya kila kitu kuonekana kawaida.
“Wife , sio kama unavyofikiria , ni kweli hali ilikuwa ya hatari sasa hivi . Nisikilize taratibu ni suala pia linalohusiana na wewe” Hamza aliona anapaswa angalau kumwelezea Regina juu ya suala ambalo Msukule wa utumwa aliongea.
Lakini Regina angewezaje kupata mudi ya kuendelea kumsikiliza.
“Hayo hayanihusu mimi , mnaweza kufanya mnavyotaka”
Mara baada ya kuongea hivyo , kwa hasira alirudi katika gari na kuligeuza na kuondoka.
Hamza aliishia tu kuganda katika eneo moja , huku akikuna kichwa chake na kisha palepale alilazimisha tabasamu na kumwangalia Irene. “Nitakurudisha nyumbani kwanza”
“Nimemkasirisha Sister Regina sana eh ?”
“Ana hasira na mimi sio wewe , usifikirie sana”aliongea Hamza.
“Hamza , nakupenda lakini sitaki kugombana na Da- Regina , nilidhania kwasababu una wanawake wengine hatojali ukiwa na mimi pia”Aliongea Irene.
Hamza alijua alichoongea Irene ni kweli , lakini kuhusu Regina hali ilikuwam imebadilika sana tokea wafahamiane. Safari ile ya kwenda Ulaya ilikuwa imebadilisha sehemu kubwa ya mahusiano yao na kuingia katika ubora mwingine kabisa.
Zamani Regina asingejali sana kwasababu ya aina ya kukutana kwao , lakini kipindi hicho moyo wa Regina ulikuwa umekomaa sana kimapenzi. Lakini pia ilikuwa ngumu kwa Hamza kusema Regina hakuwa na furaha kwasababu ya wivu , ilikuwa ni kuonyesha alikuwa akijali.
Lakini hata hivyo Hamza ilikuwa ngumu kwake kukata mawasililiano mara moja na kila mwanamke , hivyo alipanga taratibu kuwasiliana na Regina mpaka amuelewe .
Alijua mchakato huo ungekuwa na changamoto nyingi lakini Hamza aliamini kwa namna yoyote ataweza kufanikiwa.
“Irene , usiongee chochote tena , nitakupeleka kwanza nyumbani kwenu”Aliongea Hamza na palepale alitoa simu kuita taksi , lakini Irene alimzuia na kisha akanyoosha mkono nyuma kumuashiria Bazo aliekuwa akisogea taratibu taratibu kwa umbali.
“Yule mjomba wewe ndio uliemtuma kunilinda, si ndio? Ni bora yupo hapa. Wewe nenda kamtafute Sister Regina ana hasira na haitokuwa vizuri ukinipeleka nyumbani. Utamfanya awe na hasira zaidi”
“Si muda mchache tu mpaka kufika kwenu? Sina haja ya kujali sana nitawahi tu kurudi”Aliongea Hamza.
“Muda mchache! Wanawake wanajali huo muda mchache kuliko mwingi utakaompa. Wewe nenda , mimi niko sawa , maana watu wabaya wenyewe washakufa”
Hamza hakutaka kuendelea kumsikiliza Irene akimbembeleza maana hata yeye alikuwa na wasiwasi na Regina , hivyo hakuwa na jinsi na kumpa taarifa Bazo kumsindikiza Irene mpaka nyumbani.
Hamza aliishia kuvuta pumzi na kuzishusha , hakutegemea Irene angeweza kumfikiria kuhusu hali yake. Alijiambia kadiri msichana huyu atakavyoendelea kuwa hivi ndio namna itakavyokuwa ngumu kwake kumpotezea.
Kwasababu kulikuwa na giza Hamza hakuona haja ya kuchukua taksi maana ingemchukua muda mrefu kuzunguka , hivyo ghafla tu alipotea.
Irene mara baada ya kuona Hamza amepotea ghafla tu katika macho yake , alijikuta akipatwa na mshangao, huku akipepesa kope zake mara nyingi .
“Uncle huyu Hamza ni nani , kwanini ana uwezo wa ajabu hivi?”Aliuliza na kumfanya Bazo kufikiria kidogo kabla ya kujibu.
“Ms Irene , jukumu langu pekee ni kukulinda” “Oh! Basi sawa , nilitamani kama ungeniambia kidogo kuhusu Hamza , ila haina shida unaweza kunisindikiza turudi , Tunapanda wote kwenye taksi?”Aliuliza Irene akiwa tayari alisharequest na gari ilikuwa ikisogea ueleko wake.
“Nitakulinda kwa siri”Aliongea na kisha palepale alirukia upande mwingine wa fensi na kupotea.
Irene macho yake yaliishia kuchanua, alijiambia licha ya kuona mambo mengi katika mitandao na kucheza magemu na kuangalia filamu , ila kuna mambo mengi ya kushangaza yaliopo katika uhalisia.
Ghafla tu ile hofu ya kutekwa ilipotea yote na alijihisi ni kama mwigizaji.
Wakati Irene akipata Taksi kurudi nyumbani , upande wa Hamza alikuwa akikata kona mitaa kuwahi kurudi nyumbani.
Ile anafika tu ndio na Regina pia alikuwa akiingiza gari gereji na kutoka kuingia ndani.
Regina mara baada ya kurudi tu nyumbani alitupa mkoba wake na kwenda moja kwa moja mpaka chumba cha kujisomea na kujifungia.
Hamza ni kama alivyotegemea na alipitia dirishani kwake na kurukia kwenye balkoni ya dirisha la chumba alichokuwepo Regina na kusimama nje ya kioo kilichokuwa kikimuonyesha kwa ndani.
Kama kawaida aliweka muonekano wa kujitilisha huruma huku akimwangalia Regina aliekuwa ndani kwa hisia nyingi.
Mwanzoni Regina hakumuona Hamza , lakini mara baada ya kuvimba akiwa amekaa kwenye kiti , hatimae aliweza kuona kivuli cha mtu na aligeuka ndio alipoweza kumuona Hamza alikuwa amesimama kwenye balkoni.
Hamza hakuongea chochote wala hakujitingisha , alikuwa akivuita subira Regina kumuona .
Macho yao yalikutana , Hamza alitoa tabasamu lakini hakuongea chochote na kuishia tu kumwangalia.
Upepo wa baharini ulikuwa mwingi nje, jiapokuwa ilikuwa ngumu kumwathiri Hamza , lakini kwa Regina alifikiria ulikuwa ukimwathiri .maana katika jicho la mapenzi hakumchukulia Hamza kama sio wa kawaida.
Lakini hata hivyo Regina alikuwa amechukia na alijifanyisha kutokujali na alijimiminia maji kwenye glasi na kisha alirudi kwenye kiti chake na kuendelea kujiweka bize na kazi .
Hamza hakuongea chochote , wala hakusogea , aliishia tu kusubiri na mwonekano wake wa ukimya.
Mara baada ya nusu saa kupita Regina alijikuta akigeuka na kugundua Hamza bado alikuwa amesimama , ijapokuwa alikuwa amechukia lakini hakujisikia vizuri.
Alijikuta akisimama na kusogelea mlango na kuufungua.
“Unafanya ninii wewe? Unadhani ni sahihi kujitilisha huruma ?”
Hamza alijivunia na mbinu yake kwa kuamini Regina lazima angemwonea huruma , lakini licha ya hivyo aliendelea kuweka sura ya kizembe.
“Wife najua nimekukosea , lakini nilijua usingeweza kunisikiliza , hivyo nikaona nisubiri mpaka utakapo poa , kama unataka kunipiga nipo tayari , kama unataka kunifokea nipo tayari. Siwezi kukukimbia hata siku moja”
“Hebu acha kujitilisha huruma na nenda kwenye chumba chako” Regina alishia kukunja ndita , mara baada ya kuona uvumilivu unamshinda , alijua kabisa Hamza anacheza na akili yake lakini moyo wake unajikuta tu kulainika.
“Siwezi kuondoka , mke wangu kama usiponisamehe sitoondoka hapa”
“Basi endelea kusimama hapo milele na usiondoke , mimi naondoka”
Regina mara baada ya kuongea aligeuka na kutoka nje ya chumba hicho na kushuka chini sebuleni.
Hamza alijua alishapewa nafasi , hivyo haraka sana aliingia ndani na kumfuata moja kwa moja mpaka jikoni.
Muda huo Shangazi alikuwa amekwisha kulala muda mrefu tu.
Regina akiwa jikoni alitoa baadhi ya vyakula kwenye friji , alionekana alipanga kula chakula cha usiku usiku , maana hakuwa amekula sana wakati akiwa kwenye mnada .
“Wife unapaswa kunywa na juisi , ngoja nikumiminie”aliongea Hamza akikimbilia freezer.
“Hapana, na usiku wote huu unataka kunilisha vitu vya barafu. Unataka kuniona nikiganda?”
Hamza aliona alikuwa sahihi na alihamia kwenye maji yasiokuwa na baridi sana na kutaka kumiminia lakini Regina alimzuia.
“Sitaki kunywa maji wala nini , hivyo hebu acha kuhangaika mbele yangu, nijibu swali moja tu , ni kwa umbali gani umefikia na Irene?”
Regina aliuliza huku akimwangalia Hamza na macho kama vile anatafuta uongo kutoka kwake.
Hamza aliishia kumeza mate mengi na kisha aliongea ukweli.
“Hatujafikia ile hatua”Aliongea.
Hamza kuongea hivyo alijikuta akijisifia kwa uwezo wake wa kujizuia katika matukio yote ambayo alikuwa amekwepa. Kwanzia kipindi ambacho hakuwa amefahamiana na Regina alisharuka zaidi ya mitego mitatu ya Irene , baada ya kufahamiana na Regina alisharuka mitego miwili. Kama asingekuwa mvumilivu , ingekuwa ngumu kuongea muda huo.
“Mzee Wake anajua kuhusu kinachoendelea kati yenu?”Regina aliuliza tena.
“Sidhani , vinginevyo angeshaniletea matatizo muda mrefu tu”Aliongea Hamza na tabasamu la wasiwasi.
“Unajua kabisa atakuja kukutafutia matatizo halafu unaendelea , wewe hujui Irene ndio kwanza anapaswa kuingia chuo?”
Hamza aliishia tu kutojibu chochote , ijapokuwa aliona sio suala kubwa sana kwa mtoto wa umri wa Irene kuwa na mahusiano , lakini alikuwa ni yeye mwenye mahusiano nae na kama Baba yake Irene akifahamu hilo na matarajio aliokuwa nayo kwa binti yake lazima ingekuwa habari nyingine.
“Unadhani yule mzee na jinsi alivyoweka nguvu zake zote katika kumlea Irene atakubali Au kwasababu ya cheo chako cha ufalme wa kuzimu unapanga kumlazimisha?”
“Mke wangu unafikiria mbali sana , kwanini nifanye yote hayo ya kutaka kumlazimisha. Si itakuwa na sawa na haramia anaeteka mwanamke kwa ajili ya kuwa mke wake baharini. Isitoshe kwanini nifanye hayo yote wakati nina mke mzuri hivi.. hehehe”
“Hebu acha kucheka hivyo, ki ufupi., ngoja nikwambie tu , bado sijafikiria namna ya kudili na Eliza na Dina lakini ushamwingiza Irene katika orodha , mtoto ambae hata chuo hajaanza? Ni msichana ambae bado ni mjinga wa vitu vingi, kwanini unashindwa kumzuia huyo bwana mdogo wako kisa tu anaonekana kuwa mzuri?”
Hamza alijikuta akijiangalia hapo chini yeye mwenyewe na kujiambia kama kweli siwezi kumzuia huyu bwana mdogo kwanini bado wewe ni bikra?.
“Wife naomba utulie , naelewa unachomaanisha “aliongea Hamza akiwa na tabasamu akipanga kwanza kutoka katika hio dhoruba kwanza.
Muda huo huo simu ya Hamza ilianza kuita na mara baada ya kutoa aliona ni Black Fog aliekuwa akipiga na alipokea haraka.
“Rhoda vipi hali?”
“Bro! I am sorry ..”
Hamza mara baada ya kusikia sauti ya Rhoda iliokuwa katika hali ya kitetemeshi moyo wake ulipiga kwa nguvu.
“Kuna kilichotokea tena?”
“Bazo alimsindikiza Irene mpaka nyumbani salama lakini mara baada ya kufika ... Bazo amefanikiwa kumuua adui lakini kuhusu Irene
...”
“Nini kimemtokea huyo msichana?”Aliuliza Hamza kwa sauti ya juu , macho yake tayari yalikuwa yakitema cheche.
Hali ilimuogopesha hata Regina na kumfanya akakamae huku akimwangalia Hamza.
Unadhani Hamza ndugu zake ni nani?,Nini kimempata Irene?
Comments