Ndani ya jengo moja lefu lililopenezesha jiji katikati ya Posta , huku juu kabisa likiwa na maandishi ya JR Tower , katika Floor namba Ishirini na Mbili alionekana mwanume mwenye asili ya kisomali akiwa amesimama kwenye dirisha ambalo lilikuwa likimpa uwezo wa kuona Madhari ya Baharini , bwana huyu alikuwa katika lika la Ujana , mwenye nywele zake zilizompendezesha , hakuwa mfupi sana wala hakuwa mrefu sana , mwenye mwili wa saizi ya kati, na kwa haraka haraka ungejua bwana huyu alikuwa ni mtu wa kujipenda kutokana na mavazi ya gharama aliovaa .
Nyuma ya mgongo wake , kulikuwa na meza kubwa iliokuwa na tarakishi kubwa ya kampuni ya Apple , ikiwa inatoa mwanga hafifu huku ikionekana ilikuwa ikitumiwa na bwana huyu , huku mbele ya Tarakishi hii kulikuwa na Kibao kikubwa mfumo wa kioo kilichokuwa na jina lililosomeka CEO Abubakar Hamadi, JR Group Of Compenies.
Dakika chache za mwanaume huyu kusanifu mandhari ya nje , kama mtu ambaye alikuwa akitafuta dosari , hatimae mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na alionekana kijana mwenye nywele za Marasta akiingia na kumfanya bwana huyu atambue uwepo wa kuingia kwa mtu ofisini kwake.
“Boss nimafanikiwa kupata taarifa yake”Aliongea bwana huyu kwa heshima huku akisogelea Meza ya bei ghari iliokuwa hapo ofisni.
“Nipe ripoti”Aliongea CEO Abu huku akikalia kiti chake na kisha alipokea bahasha iliokuwa mikononi mwa Marasta na kisha aliifungua na kuanza kupitisha macho yake huku akizidi kushangazwa na kile anachokisoma.
“Una uhakika hii ripoti ni sahihi , haujaichanganya na ya mtu mwingine”
“Ni sahihi kabisa bosi , vyanzo vilivyonipatia hio taarifa ni vya kuaminika”Aliongea Marasta.
“Unaweza kwenda , lakini nataka mumfatilie huyu mtu na mnipe taarifa zote kwa kila anachokifanya”
“Sawa bosi”Alijibu na wakati huo huo simu ya mezani ilitoa mlio kuonesha inaita , alinyanyua mkonga huku akimpa ishara Marasta kuondoka.
“Boss kuna mgeni wako”Ilikuwa ni sauti ya katibu Muhtasi wake afahamikae kwa jina la Sarah.
“Sawa mruhusu”Aliongea Abu na ndani ya dakika chache mlango ulifunguliwa na mwanaume mzee alievalia suti yake ya aina ya Navy black , akiwa anapata sapoti kwenye mkongojo uliokuwa unang`aa kwa madini ya Shaba, mzee huyu licha ya kuonekana umri wake umeenda lakini Afya yake haikuwa mbaya sana.
“Mr Alex ! karibu sana”Aliongea Abuu kwa sauti ya kiheshima huku akinyanyuka na kumkaribisha mzee huyu na kwenda kukaa kwenye masofa ya gharama yaliokuwa ofisini hapo.
Mzee huyu alimwangalia Abuu kwa namna flani ya kukatishwa tamaa , na kisha aliketi huku akivuta pumzi.
“Ni ujinga gani unafanya Abuu mpaka kunifanya nije mwenyewe ofisini”Aliongea mzee huyu kwa ghadhabu huku Abu akionekana ni mwenye kujua kosa lake.
“Nisamehe sana baba, najua mpango wa awali ulifeli lakini naamini mpango B utafanikiwa”.
“Swala sio mpango A wala Mpango B ninachotaka kujua ni kwanini swala la Master linachelewa kufanikishwa, nimekupa uongozi wa kampuni yangu kwakuwa nilikuwa najua uwezo wako , kwanini swala dogo kama hili linashindikana”Abuu kimya , alionekana ni mwenye kutetemeka.
“Anza kuniambia ni kipi kilifanya mpango wako wa kwanza kushindwa na huo mpango wako B ukoje na kama mipango yote ni ya kijinga nitakufukuza na kumpa mtu mwingine wa kuongoza makampuni yangu , siwezi kuvumilia ujinga katika swala hili”.
Mzee Alex ni mmiliki wa makampuni ya JR yote yaliokuwa yametapakaa ndani na nje ya nchi, makampuni yake yalikuwa yakitoa huduma nyingi sana kuanzia Maradhi , Nguo na chakula.
Mzee Alex alikuwa ni moja ya matajiri wakubwa ndani na nje ya taifa la Tanzania na alikuwa ndio kiongozi mkuu wa makampuni haya akihudumu kwa muda mrefu kama mkurugenzi mtendani na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi , miaka miwili nyuma alistaafu katika nafasi yake ya ukurugenzi mtendaji na kumpa nafasi hio kijana wake aliemlea afahamikae kwa jina la Abubakari Hamadi , moja ya sababu kubwa ya kumpatia nafasi hio kijana huyo ni kutokana na kwamba Mzee huyu katika uzao wake hakuwahi kubahatika kuwa na mtoto wa kiume , kwani watoto wake wote wawili walikuwa ni wa kike , huku Abu akiwa ni mtoto aliemlea na kumchukulia kama mwanae , ukijumlisha uwezo mkubwa wa akili wa kijana Abuu na ukaribu wao , aliona anafaa kuongoza makampuni yake na ndio hapo alipomteua kuwa mrithi wake.
*****
Alijikuta akiwa ni mwenye kukasirika mara baada ya kusikia neno ‘kahaba’ likitoka katika kinywa cha mwanaume aliekuwa mbele yake , mwanaume ambae kwa muonekano wake hakuwa kitu mbele yake , moja ya hasira aliokuwa nayo si kutokana na yeye kuitwa kahaba na mwanaume huyu ila ni kutokna na kutokuwa kwake makini mpaka kujikuta akitolewa usichana wake alioutunza miaka mingi tokea ajitambue , licha ya kusumbuliwa na wanaume mbalimbali , wenye sifa tofauti kubwa na ndogo , lakini kosa dogo alilolifanya katika maisha yake la kuamini watu , lilimpelekea kuingia katika mikono ya mwanaume aliekuwa mbele yake , ambaye baada ya kumuangalia kwa muda aliona hana hadhi yoyote ya kuwa nae katika ulimwengu wa mapenzi.
“Naitwa Edna Adebayo na sio kahaba kama unavyonitambua”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake nyororo huku akimwangalia Roma kwa sura iliojaa kujiamini , kama vile hakukuwa na kitu kilichotokea kati yao.
“Kama sio kahaba wewe ni nani , au kwasababu upo kwenye mjengo kama huu wa gharama kubwa , kifupi wewe ni kahaba wa hadhi ya juu ambaye kapuku kama mimi nilikuotea na kukufaidi”Aliongea Roma na kuzidi kumchafua roho mwanamke huyu na kwa Roma ni kama alikuwa amekusudia kuongea hayo maneno ili kumsoma mwanamke huyu aliokuwa mbele yake , kwani kuna kitu tokea aingie hapo ndani na kumuona huyu mwanamke ashakigundua , hakuwa mjinga kiasi cha Rami kuona mwanamke anafahamika kwa jina la ‘Bossi’ kuwa kahaba kama alivyomdhania siku tatu zilizopita.
Lakini licha ya Roma kutamka maneno hayo kwa mwanadada huyu , alionekana ni mwenye kuzuia hasira zake zisitawale akili yake.
“Naomba uketi , nina mazungumzo na wewe”Aliongea kwa sauti ya upole huku akitangulia kukaa yeye na Roma alitabasamu na kisha kuketi.
“Nimeitikia wito , naomba uende moja kwa moja kwa lile uliloniitia” Aliongea Roma na kumfanya mwanadada huyu agundue mwanaume aliekuwa mbele yake ni wa namna gani , kwani alitegemea kuona Roma kuwa katika hali ya uoga kama tu angegundua uwezo wa kipesa aliokuwa nao , lakini kila kitu kilimjibu kivingine , kwani kijana huyu alionekana kujiamini mno , jambo ambalo lilimfanya aone maamuzi alioyafanya nisahihi , alichukua glasi yake ya wine iliokuwa kwenye meza ya kioo na kisha alikunywa mara mbili na kisha akaweka chini kwa mapozi ya kike .
“Naomba unioe”Aliongea mwanadada huyu , huku akionekana ni mwenye kuanza kukosa ile hali ya kujiamini aliokuwa nayo mwanzo.
Kwa upande wa Roma ni kama mtu ambaye hakusikia vizuri maneno yaliomtoka mrembo huyu mwenye haiba ya upole , aliekuwa mbele yake.
“Inawezekana sijakusikia vizuri mrembo wangu my one night stand , naomba urudie kauli yako tafadhari”.
“Naomba unioe tafadhari , ndio jambo pekee nililokuitia mahali hapa , nitakulipa kiasi chochote cha fedha”Aliongea mwanadada huyu huku muda huu akiweka sura ambayo ni kama mtu aliekuwa akiongea na mfanya biashara mwingine swala la kibiashara.
“Unaonekana kuwa mpole , lakini pia unamuonekano wa kuwa na tabia nzuri , lakini wito wako na ombi lako linanifanya nikufikirie kivingine , labda unieleze vizuri ni kuelewe vinginevyo nakataa ombi lako , kwani ndoa sio kitu cha kuombwa na mwanamke kiholela kilichotokea baina yetu ni kosa langu na lako pia”Aliongea Roma huku akichukua Chupa ya wine na hakujali glasi iliokuwa mbele yake , yeye aigida karibia yote na kurudisha chini.
“Nataka unioe kwa mkataba wa miezi sita , baada ya hapo tutaachana kwa talaka na nitakulipa kiwango kizuri cha pesa , nafanya haya kwani kuna mwanaume ambaye baba yangu mzazi ananilazimisha kuolewa nae , mtu ambae simpendi”.
Kwanza Roma alishangaa , lakini pia swala hilo lilimpa ukakasi kwa wakati mmoja , aliona swala la baba yake Edna kumlazimisha kuolewa na mwaname mwingine ni swala ambalo linaweza kutatuliwa kwa kumkataa huyo mwanaume na si kutaka kuoelwa na mwanaume yoyote yule ilimradi tu kuepuka kuolewa na mwanume asiempenda.
“Nakataa , sitaki kujua mengi kuhusu wewe , lakini swala lako lipo nje ya uwezo wangu , siwezi kuoa mtu kwa ajili ya kujipatia pesa huku ni sawasawa na kuuza utu wangu dada, hili swala lako kuna njia nyingine za kulitatua”.
“Kaka wewe kama mwanaume unatakiwa kuwajibika kwa matendo yako , ulinitoa bar pasipo ruhusa yangu ukanipeleka mpaka geto kwako ukanitoa usichana wangu pasipo ridhaa yangu , lakini juu ya yote nikaacha kukufanya jambo baya kwani ulichofanya ni kinyume na Sheria , lakini leo hii ninakupa ofa ya kunioa tena kwa kukulipa halafu unakataa ,nina nguvu ya kukufanya uozee jera Zaidi ya miaka therathini”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti ya hasira.
“Nakubari kosa langu Dada na nipo tayari kwa ajili ya adhabu nitakayopewa , lakini swala la mimi kuuza utu wangu kwako ni swala ambalo haliwezekani”Aliongea Roma kwa hasira huku akinyanyuka akitaka kuondoka .
“Ukipiga hatua mbili kutoka nje ya mlango najitosa nje ya hili jengo , siwezi kuishi kwa aibu ya kubakwa na mwanaume kwenye maisha yangu na nakuapia dunia nzima itajua kuwa ulinibaka na sidhani kama utakua kuishi kwa Amani, na namna pekee ni kukubali ombi langu”Aliongea mwanadada huyu ila Roma hakugeuka aliendelea kutembea kuelekea mlangoni , lakini ile anataka kushika kitasa , alisikia mlango wa dirisha nyuma yake ukifunguliwa , aligeuka nyuma na kumuona Edna akimaanisha kile ambacho anataka kufanya .
Roma alijikuta akipigwa kama na radi kwenye kichwa chake na kuchuchumaa chini kwa maumivu ya kichwa , huku picha mbalimbali za maisha yake ya nyuma zikipita kwa kasi ,mboni za macho yake zilibadilika ghafla nakuwa za kijani na ndani ya sekunde kadhaa tu kwa tukio ambalo halikueleweka lilifanyika vipi alikuwa amembeba juu mrembo Edna huku akimrudisha kwenye sofa , kitendo hicho hata kwa mrembo huyu ambae machozi yalijaza mboni za macho yake alishangazwa na kitendo hiko.
“Sipo tayari kuona mwanamke wa pili anapoteza uhai kwa ajili yangu”Aliongea Roma kwa sauti nzito baada ya kumkalisha Mrembo Edna kwenye sofa.
“Kwa hio umekubali kunioa?”
“Sina jinsi”Aliongea Roma huku akifungua chupa nyingine ya Wine na kuigida kama maji.
Edna hakujali tabia ya Roma alitoa bahasha kwenye mkoba wake na kisha alichomoa karatasi yenye mkataba wa ndoa na kisha akampatia Roma na karamu, na Roma baada ya kupokea karatasi ile , wala hakutaka kuangalia ni kipi kipo ndani ya hio karatasi , aliweka sahihi yake sehemu husika.
“Mbona husomi mkataba kwanza?
“Sina haja ya kusoma , kwani nishajua kilichopo kwenye huu mkataba”
“Kama nini”
“Kama vile kuweka umbali katikati yetu , kutogusana na mengineo mengi”
“Ni kweli , lakini pamoja ya hayo sheria kubwa ni juu ya ndoa yetu kuwa siri baina yetu”Aliongea Mrembo Edna.
“Nini kinafuata baada ya hapa?”
“Tutaenda Bomani kwa ajili ya kusajili ndoa yetu na kuwa mke na mume kihalali , lakini kabla ya hayo inabidi ubadilishe mavazi na uoge utakate”Aliongea mwanadada huyu na kisha alitoa simu yake na kutoa maagizo na ndani ya sekunde chache tu Suzzane aliingia akiwa na suti ,viatu na makorokoro mengine na Roma alienda kuoga na alitumia muda mchache sana kuoga na kuvaa nguvo ambazo aliletewa na Suzzane.
Roma alikuwa amependeza mno na suti yake ya rangi ya blue , suti ya bei ghali ambayo ilimbadilisha kwa asilimia kubwa muonekano wake na kuwa na muonekano wa kipedeshee.
Baada ya kutoka kwenye chumba hiki cha kubadilishia nguo , waliokuwa ndani ya chumba hiko ni kama wamemsahau kama fukara , licha ya Roma kuwa na sura ya kawaida sana ambayo haikuwa kama ya mahadsome boy wa mjini lakini Suti aliokuwa amevaa ilimpendezesha na kumbadilisha.
Baada ya masaa kadhaa ,Roma akiwa ameongozana na Mrembo Edna walitoka kwenye gari ya gharama sana ana ya Mercedenz Benz toleo jipya na kuingia ndani ya jengo la Bomani , na haikuwachukiua muda Mrefu kila mmoja alisaini cheti cha ndoa na kisha walipiga picha ya uthibitisho na kuwa mke na mume halali.
“My wife mrembo … Mungu kweli ananipenda siamini kama nimepata mke mrembo kama wewe”Roma alianza utani wake pasipo kumzingatia Mrembo Edna huku akijifanya kumsogelea kwa ajili ya kumkumbatia , lakini aliishia kukatwa jicho na kupigwa kikumbo na mwanadada huyu.
Waliingia kwenye gari huku dereva akiwa mrembo huyu na ndani ya madakika kadhaa ya barabarani gari ilikuja kusimama kwenye geti lenye ukuta mkubwa maeneo ya ushuani Osterbay na baada ya dakika chache geti lile lilifunguliwa na mlinzi na kisha Edna aliingiza gari na kwenda kulipaki katika eneo husika na kisha alishuka kwenye gari.
Lilikuwa ni jumba la kifahari mno lililokuwa mbele yao , Roma alishangazwa na mandhari mazuri ya jumba hili , na kwa harakaharaka aliona mtu anaeishi kwenye hii nyumba alikuwa mtu mwenye ukwasi mkubwa wa pesa.
“Hapa ni nyumbani kwa baba yangu na tumekuja hapa kujitambilisha kwake , hivyo tujitahidi kuonekana kama wanandoa kweli”.
“Unaongea kama vile sisi sio wanandoa, tunahistoria ndefu kabla hatujafanya maamuzi ya kufunga ndoa mke wangu , au ushasahau kuwa mimi ndio niliokuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi, my babe Edna acha zako bhna”Huku akimshika mkono na kumvuta kifuani , swala ambalo juu kabisa ya gorofa ya nyumba hii alionekana mzee akishuhudia kitendo kinachofanyika , Edna alitaka kujinasua kwenye mikono ya Roma , lakini Roma alimpa ishara kwamba baba yake yupo juu ya ghorofa anawaangalia na yeye aliangaza macho yake juu na kuona kivuli cha mtu kikitokomea kwenye Balcony.
“Kwenye wanaume wote ambao nishawahi kukutana nao sijawahi kuwaza nitakutana na mwanaume ambae huna aibu kama wewe”.Aliongea Edna kwa hasira huku akitangulia kwenda mbele na kumfanya Roma atoe tabasamu la kifedhuli na kumfata.
“Baba , nimekuja kumtambulisha mume wangu , sitaki tena kusikia juu ya kuolewa na mwanaume mwingine . nampenda Roma na nitaishi nae mpaka kifo kitakapotutenganisha maana tunapendana “Huku akimwegamia Roma ambaye alikuwa ni mwenye tabasamu zito huku akimwangalia mwanaume alikuwa mbele yake kwenye sebule hii kubwa iliojaa thamani za bei ghali.
“Mzee kama alivvyosema bebi wangu hapa , mke wangu kipenzi , nyongo mkalia ini , nimekuja kujitambulisha , na naomba unisamehe kwa kuja tukiwa mke na mume , kwa majina naitwa Roma Ramoni ni mwenyeji wa hili jiji , kazi yangu ni kubeba mizigo soko la Mbagala Rangi tatu”Aliongea Roma na kumfanya mzee huyu aanze kuhema kwa taabu , huku Edna akiwa ni mwenye kushangaa namna ambavyo Roma alikuwa akijiamini na kukosa aibu.
“Unasemaje wewe , kikaragosi .. Ednaa..!! ni laana gani unaniletea ndani ya familia yangu??”Aliongea mzee huyu huku akikaa na kuanza kuhema kwa taabu , lakini wawili hawa hawakuwa ni wenye kujali.
Comments