Roma alitoka kazini muda wa tisa kamili na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani , baada ya kufika na kusalimiana na Bi Wema moja kwa moja aliingia kwenye chumba chake kwa aili ya kupumzika , huku akiwaza aende kiwanja gani cha bata , baada ya lisaa limoja la kupumzika , simu yake ilitoa mwanga kuashiria kuna ujumbe ulikuwa umeingia , aliichukua na kuutazama na kisha alitabasamu.
“Hey! Malkia Doris naona ushanimiss”.
“Acha kujishaua mwanaume , nimekutafuta kwani ninahitaji msaada wako , ila sio lazima kama hautonisadia”.
“Nipo tayari kufanya lolote kwa mrembo kama wewe na isitoshe ushawahi kunisaidia nina deni kwako”
“Kama unalijua hilo tuonane jioni saa moja The palm Hotel”.
“Nitafika hapo muda huo mrembo wala usiwaze”
“Sawa ila uje umevaa vizuri sasa , na pia kuwa makini na mkeo usimuage kama unakuja kwangu”Roma alitabasamu na ujumbe huo wa meseji na kisha kuweka simu pembeni na kuuchapa usingizi alikuja kuamka muda wa saa kumi na mbili na nusu , aliona ni muda mzuri wa yeye kujiandaa na ndani ya dakika kumi na tano alikuwa tayari yuko vizuri.
Alitoka na kumkuta Bi Wema akiangalia TV sebuleni .
“Bibi, Edna asharudi?”.
“Bado hajarudi , ila kanipigia simu saa kumi kuwa atachelewa ana miadi na mtu”Aliongea huku akiendelea kuangalia runinga na Roma Kuna kajiroho ka wivu kalimuingia na kujiuliza ni mtu gani Edna anamiadi nae pasipo yeye kujua , ila hakutaka kujali Zaidi , alikumbuka vyema ndoa yao sio kama ndoa za kawaida ni ndoa ya maigizo tu na hakukuwa na mapenzi katikati hivyo kila mtu alikuwa na mishe zake.
Alimuanga bi Wema kwamba anatoka na anaweza kurudi ama asirudi kabisa na kisha aliondoka , licha ya Roma kupotezea swala la Edna ila kama mwanaume kuna kitu kilichokuwa kinamuendesha katika moyo wake , hakujua sababu ni nini ila alikuwa na hasira mno.
Ndani ya dakika kumi aliingiza gari yake ndani sehemu ya geti la hoteli hio na kusimamisha gari na kumkabidhi funguo Valet(mtu anaehusika na kuegesha magari ndani taasisi, kampuni au hoteli) , alikaribishwa na ufahari wa hali ya juu wa hoteli hii.
“Waoh! Umependeza Roma”Aliongea Doris baada ya wawili hao kuonana sehemu ya kusubiria wageni , upande wa Doris alionekana kama Malaika , mavazi aliochagua kuvaa siku hio yalikuwa yamempendezesha mno huku uzuri wake ukizidi kumfanya kuonekna wa kipekee sana ndani ya eneo hilo.
“Umependeza pia mrembo, hakika wewe ni mzuri Doris”
“Haha.. Acha unafiki Roma mimi ni mzuri Zaidi ya mkeo?”Hapa ni kama swali hili lilimkosesha raha Roma kwani akikumbuka uzuri aliokuwa nao Edna sio wa kawaida na hata kwa Doris hakuwa akimfikia hata kidogo , ila sasa swala lililomkosesga raha ni kwamba mke wake muda huo hakujua ana miadi na mtu gani.
“Hehe.. nisikufiche mke wangu mzuri bhana ndio maana nimemuoa”Aliongea Roma na kumfanya Doris ajifanyishe kununa , lakini Roma alitabasamu.
“Kuna mtu nataka leo nikutambulishe kwake , naomba uigize kuwa mpenzi wangu kwa usiku wa leo”Aliongea Doris na Roma alijikuta akishangaa , inakuwaje mwanamke huyu akamchagua kwa kazi hio ilihali anajua kabisa ana mke , lakini pia kwanini amemchagua yeye , ila hakutaka kuwaza sana , alikubali kwani bidada huyo alikuwa akimkubali kwa roho yake nzuri , kitendo cha siku ile kumsaidia nauli bila ya kujuana kilikuwa na maana kabisa ndani ya ulimwengu wenye watu wenye roho mchanganyiko.
“Hata usijali mrembo , mimi kama ningeamua kuwa mwigizaji ningekuwa maarufu sana , maana nina kipaji cha kuigiza”Aliongea Roma na kumfanya Doris atabasamu.
Baada ya kuingia kwenye Lift walikuja kutoka kwenye floo namba ishirni ,Floor ambayo ndani ya hoteli hii ilikuwa ikihudumia VVIP.
Roma alishangazwa na ulinzi wa ndani wa hili eneo , kwani kulikuwa na walinzi waliokuwa wamevalia suti wakionesha kuimalisha ulinzi , alishangaa ni mwanaume gani Doris alikuwa anaenda kumtambulisha kwake , lakini majibu yake yalijibiwa mara baada ya kuingia ndani ya chumba namba 700 na kukutana na mwanaume aliekuwa amevalia Suti huku akiwa anakunywa mvinyo.
Bwana huyu kwanza alionekana kuwa mtu mzima , kwani sura yake ilikuwa ishaanza kukunjamana , alikuwa mrefu wa wastani mweupe mwenye kipara kwa makadirio ya umri alionekana kuwa na umri kati ya 45 kuendelea.
“Mister Kijembe huyu ndio mwanaume ninaempenda na ninapanga kuolewa nae , hivyo naomba unielewe ninapokuambia swala la mimi na wewe kuwa wapenzi haliwezekani”Aliongea Doris mara baada ya kukaribishana na kukaa , huku huyu mzee muda wote macho yalikuwa kwa Roma.
“Huyu Doris ananitafutia matatizo huyu , mtu mwenywe anaonekana kuwa na mipesa mingi na walinzi kibao si nitakufa akipanga kuniua”Aliiwazia Roma lakini hakuonesha hofu yoyote jambo ambalo Lilimvutia sana Doris.
“Doris huyu ndio babu ulieniambia anakutaka na hataki kukuelewa?”
Mzee yule alitaka kutapika wine iliokuwa mdomoni kwake mara baada ya kusikia anaitwa babu, na Doris alishangazwa na ujasiri aliokuwa nao Roma kwani licha ya kutaka kumtumia katika mpango wake lakini alikuwa akihofia Roma atamwangusha lakini imekuwa kinyume na mategemeo yake kwani Roma alifanya kazi Zaidi ya alivyokuwa akitaka kazi ifanyike yaani too perfect.
“Mzee usinifikirie vibaya ila kwa umri wako na wetu sisi tunapaswa tukuite babu , sasa ni aibu kwa mtu mzima kama wewe kusumbua vijana wakati muda wako kwa hayo mambo ushaisha, mimi nakushauri achana tu na vijana na kwanzia sasa endelea kujikita Zaidi kwenye kumuomba Mungu maana kwa ninavyokuona siku zako sio nyingi hapa duniani angalau tubu dhambi uingie peponi”.
“Kijana Chunga maneno yako , mimi sio babu kuwa na heshima .. halafu Dorisi huyu kichaa umemtoa wapi asiekuwa na heshima hata kwa wakubwa”.
“Mr Kijembe nimempenda huyu na ukichaa wake hivyo lililonileta hapa lishaisha na nadhani kuanzia leo utakuwa mbali na mimi”Aliongea Doris na kuamka ili waondoke , lakini kabla hajapiga hatua mbili Roma alimvuta Doris na kutua katika kifua chake na katika hali ya kutokutegemea alimpiga kiss kitendo kilichomuacha Doris katika mshangao maana ilikuwa ghafla sana.
“Bebi una vijilipsi vizuri nashindwa kuvizoea kila siku nitaving`ata mimi”Aliongea Roma kwa kumtania na kumfanya Doris aone aibu za kike.
“Babu kwaheri nadhani utazingatia maneno yangu”Aliongea Roma na kisha wakatoka.
“Halafu Roma umevuka mpaka mimi nimekuambia uigize kuwa Boyfriend wangu sio kunikiss umenikera”
“Hehe muone sasa .. kwani maana ya maigizo ni nini Doris .. halafu mbona umekuwa mwekundu hivyo, usiniambie kwamba nimezipandisha hisia zako , aliongea huku akimsogelea Doris wakati wakiwa kwenye Lift na Doris alizidi kujibana kwenye ukuta wa Lift.
“Bebi unaonaje ikawa kweli”Baada ya kumfikia kuinamisha uso wake mbele ya Dorisi aliekuwa ameangalia chini kama mwanamke asiewahi kukisiwa.
Mlango ulifunguka haraka kiasi cha kumkera Roma , ila hakujali Zaidi , waliongozana mpaka nje.
“Unaonaje Doris tukienda sehemu kwa ajili ya chakula kabisa , mimi nishatoa maagizo kwamba nitachelewa hivyo siwezi kurudi kabla sijala”.
“Sawa hata mimi pia nimetoa maagizo hayo”.
Haikueleweka nini kilitokea baina ya wawili hawa hapo katikati ila ndani ya saa tatu za usiku walionekana kuwa ndani ya chumba cha hoteli moja iliokuwa ikipatikana ndani ya meneo ya Ubungo , hawakuwa tena wale wanaogiza ila wakati huu Doris alikuwa akitoa miguno ya kimahaba huku Roma akiwa ni mwenye kushusha viuno kama hana akili nzuri.
Baada ya lisaa limoja la Roma kumpindua mwanadada Doris huku mrembo huyu akifunga magori yasiokuwa na idadi kitu ambacho hakuwahi kufikia , Roma alihema kama mbwa aliekuwa akifukuzwa.
“Wewe na CEO mna ukaribu gani , maana nimewaona leo mkiongea kama marafiki?”
“Mh! Usiniambie na CEO na yeye unamtaka?”
“Yaani wewe , mbona unafikiria sana , mimi nimeuliza tu mrembo”
“Tumefahamiana muda tu , tokea kipindi hajawa CEO tuna urafiki wa Zaidi ya mika mitatu sasa”
“Nilijua mnafahamiana kikazi tu , kumbe mpo deep kiasi hiko?”
“Sio sana , ila naweza kusema mimi ni rafiki pekee wa Edna nje ya familia yake kwa hapa Tanzania”.
“Unamaanisha nini , unataka uniambie CEO mrembo kama yule hana marafiki , vipi kuhusu mume wake”
“Kuhusu marafiki kwakweli Edna hana , sifa yake yule ni mkimya sana na ni ngumu sana kutengneza marafiki , kuhusu mume kusema ukweli Edna amekuwa mgumu sana kunieleza mahusiano yake japo aliniambia hivi juzi kuwa ameshapata mume na anaishi nae na wala hajawahi kuniweka wazi kuhusu huyo mwanaume nimfahamu”Aliongea Edna lakini wakati wanaendelea na stori huku wakiwa uchi simu ya Roma ilianza kuita mfululizo na alishangaa maana hakuwa na watu waliokuwa wakimpigia mara kwa mara baada ya kuangalia jina alikuta ni Bi Wema , alishangaa na akaona huenda kuna tatizo.
“Roma uko uk.. wapi jamani Edna katekwa Romaa”
“Nini Bibi hebu niambie nini kimetokea”.
“Kuna watu wamenipigia wanasema Edna wamemteka na wanakutafuta wewe , nimewapa namba yako jamanii mimi nafanya nini ,… Edna Mugnu wangu ..”
“Bi Wema tuliza presha kila kitu kitakuwa sawa , ilimradi umesema wananitaka mimi basi jua Edna hatopata shida yoyote ile na swala hili usimwabie mtu yoyote nitalishughulikia mimi mwenywewe”Aliognea Roma na kukata simu , lakini ile anakata tu namba nyingine iliokuwa kweye mfumo wa Private numbe iliianza kupiga na Roma alipokea.
“Mr Roma tupo na mkeo na unachotakiwa kufanya ni kuja sehemu tutakayokuambia bila kutaarifu polisi au mtu yoyote yule , ukifanya ujinga wowote jua utaletewa Edna akiwa hayati”.
“Okey niambieni mko sehemu gani na nitafika mimi mwenywe”.
Roma aliambiwa eneo husika na kisha alimwangalia Dorisi aliekuwa akimwangalia kwa mshangao.
“Kuna nini Roma?”
“Mke wangu katekwa na natakiwa kwenda kumuokoa kwani watekaji wananitaka mimi”
“Nini .. usiende Roma mpenzi watakuua”
“Dorisi tutaonana , lazima nimuokoe mke wangu kwa namna yoyote ile hata kama kifo kitanihusu”Aliongea Roma na kuvaa nguo zake na kutoka akimuacha Dorisi katika hali ya wasiwasi.
****
Upande mwingine nje ya hoteli ya The Palm alionekan Mr Kijembe akitoka akiwa na walinzi wake na kuingia kwenye gari na kisha kuondoka ndani ya eneo hilo , muda mfupi baadae gari zile tatu mbili zikiwa na walinzi na moja ya katikati ikiwa na Mr kijembe ziliingia katika lango la Ikulu ya Dar es Salaam .
Baada ya kuingia Mr kijembe aliingiea kwenye chumba ndani ya jumba hili la ikulu , chumba ambacho kilionekana kuwa kama hospitali.
Baada ya kuingia ndani ya chumba hiki bwana mmoja aliekuwa amevalia gloves aliandaa vifaa flani hivi , huku Mr Kijembe akiwa amekaa kwenye kiti na bwana yule alimsogelea na kuanza kubabua ngozi kwenye sura na ndani ya dakika chache tu sura mpya ya mtu anaefahamika kwa watanzania wote ilionekana na huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Raisi Senga Kweka.
“Kabwe nipe taarifa zinazomhusu Roma sasa hivi unikute kwenye ofisi yangu”Sawa mheshimiwa.
Baada ya mheshimiwa Senga kuingia ndani ya ofisi yake alionekana kuwa ni mwenye hasira sana, hakutarajia kama atakuja kudharauliwa na kijana mdogo kama Roma katika maisha yake , alikuwa ni mwenye hasira sana .
“Nadhani hanijui vizuri huyu , yeye ni nani mpaka aharibu mipango yangu , Dorisi kwangu ndio kila kitu juu ya kutimiza mpango wangu”Alijiwazia mzee huyu na kushituliwa na mlango uliokuwa unagongwa na akaingia Kabwe Mlinzi mkuu wa kujitegemea wa Raisi Senga.
“Umepata nini mapema hivyo?”.
“Taarifa niliopata mheshimiwa juu ya Roma ni kwamba jina lake kamili anaitwa Roma Ramoni alifika ndani ya jiji la Dar Es salaam miezi sita iliopita , ni mhitimu kutoka chuo cha Harvad akichukua masomo ya uongozi wa biashara , siku chche zilizopita alifunga ndoa na CEO Edna”
“Unamaanisha Edna na Roma ni wanandoa , wamefunga hio ndoa lini na mbona hii taarifa sina Kabwe”.
“Mheshimiwa nilikuwa naandaa taarifa kwa ajili ya kukupatia na kilichonichelewesha ni ugumu wa taarifa zilizokuwa zikimuhusu Roma”Aliongea Kabwe
“Kabwe unatakiwa kuelewa kuwa Edna ni muhimu sana kwangu katika mipango yangu zidi ya The Doni na taarifa yoyote inayomuhusu lazima inifikie sawa ?”
“Sawa mheshimiwa”.
“Kuna taarifa nyingine kumuhusu huyu Roma maana siamini kama mtu kama yeye kumuoa Edna bila ya kuwa na sababu lakini pia wakati huo huo kuwa na mahusiano na Dorisi”
“Taarifa nyingine nimeweza kupita kutoka kwa kampuni ya Vexto inaonesha Roma anauwezo wa kuzungumza lugha ishirini na mbili”
“Nini!!?, lugha ishirini na mbili na mnamuona mtu huyo wa kawaida , kuna taarifa kubwa inayomuhusu huyu mtu nataka hio sio hii feki ya kusomea chuo cha Harvad”Aliongea Mheshimiw Senga huku akiwa ni mwenye kushangaa , alijua mtu wa kawaida hawezi kuwa na uwezo wa kuongea lugha nyingi kiasi hicho , kuna hisia mbaya zilikuwa zikimwandama.
“Anaweza kuwa mtu hatari kwa Edna huyu , huenda ni mpango wa The Doni Edna kuolewa na huyu Roma” Aliwaza mhesimiwa.
“Kabwe fuatilia taarifa za huyu mtu kwanzia wazazi wake na kila kitu kinachomuhusu , anaweza akawa hatari kwa Edna hivyo swala hili linapaswa kufanyika haraka”
“Sawa Mheshimiwa , lakini bipi kuhusu Doris?”
“Doris pia ni wa muhimu lakini kazi hio nitampa Kiga , lazima nimuweke Doris karibu kama ninataka kupata taarifa zote zinazomuhusu baba yake The Doni”Aliongea Raisi huku akikaa kwani muda wote alikuwa akizunguka zunguka.
“The Doni anajifanya mjanja sana kujificha , ila asichojua ni kwamba nina taarifa zote na uthibitisho wa Doris kuwa mtoto wake na kupitia yeye nitampata tu , hawezi akaniendesha kama gari bovu mimi huku wananchi wakiniita Raisi”
Mheshimiwa Raisi alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu na kuogopa kwa wakati mmoja , kuchelewa kwa taarifa ya ndoa ya Edna kumfikia yeye aliona ni swala ambalo linaweza kumuweka Edna matatizoni alishangazwa sana na Edna kuoelewa na mtu anaeweza kuzungumza lugha ishirini na mbili bila yeye kujua , aliona usalama wa taifa walikuwa hawafanyi kazi yao kwani hio ilikuwa ni taarifa kubwa sana na ilitakiwa kufatiliwa.
“Hapana swala hili pia lazima nilifanyie kazi , licha ya Vexto kuwa kiini cha mipango yetu lakini Edna hatakiwi kudhurika hata kidogo , mkataba wa siri niliosaini baina yangu na mama yake utakuja kunifunga baadae”
Comments