Roma aliendesha gari kama kichaa , uzuri ni kwamba barabarani hakukuwa na magari mengi , alitumia dakika chache tu kufika ndani ya Kibaha na kukunja kushoto barabara ya vumbi kama vile alikuwa akielekea Bagamoyo nyuma ya kiwanda cha kuunganisha magari na akasonga mbele.
Alikuja kusimamisha gari yake mita mia moja kutoka kilipokuwa kilipo kiwanda hiki cha kuunganisha magari na kisha alisimama huku akiangalia eneo ambalo watu hao walimwelekeza , bado hakuwa akiona nyumba yoyote hivyo alishindwa kusogea mbele, baada ya kusimamisha gari kwa dakika kama kumi hivi simu yake ilianza kuita.
“Mr Ramon tumehakikisha umekuja peke yako , unaweza kusogea mbele mita mia nne kutoka ulipo kisha kunja kulia utaona nyumba yenye geti jeusi na simamisha gari yako hapo”.
Roma bila ya kujiuliza , aliendesha gari na baada ya kusogea umbali unaotakiwa kama alivyokuwa amepewa maagizo , aliona barabara ya vumbi iliokuwa ikikunja kulia , alichukua Barbara hio na kusimamisha gari mara baada ya kuona ukuta mrefu ambao ulifanya usiweze kuona ndani ya ukuta huo ndani kuna nini , baada ya kushuka tu kwenye gari ni kama walikuwa wanamsubiri kwani kijana mmoja mwenye koti jeusi alievalia kofia ya chepelu alimyooshea Roma bastora na kumuingiza ndani ya jumba hili.
Roma aligundua kuwa hiii sio nyumba bali ni Godauni , kwani ndani hapa kulikuwa na magari yale ya kuchimbia barabara yakiwa katika hali ya uchakavu na baadhi ya mavyuma mengi makachakavu.
Walimwigiza kwenye jumba lililokuwa mbele ,upande wa kushoto huku vijana watatu wakionekana ndani ya eneo hilo wawili walikuwa na siraha za moto na mmoja aliekuwa anavuta sigara ndio hakuwa na siraha lakini alionekana kuwa ndio kiongozi , Roma alianza kuangalia mmoja mmoja kwa hasira.
“Edna yuko wapi ?”
“Tuliza wenge wewe fala”Aliongea huku akimsukumia ndani ya chumba na hapo ndipo alipomuaona Edna akiwa amefungwa kwenye kiti , kitendo cha Edna kumuona Roma ni kama vile hakukitarajia, Roma alimwangalia namna mwanamke huyo alivyokuwa ametawaliwa na machozi usoni na kumuonea huruma, lakini baada ya Roma kugeuka upande wa pili aliweza kumuona mtu mwingine na huyu alikuwa ni baba yake Edna wote wakiwa wamefungwa.
Mbele ya Edna kulikuwa na kijisturi ambacho kilikuwa na makaratasi na karamu , huku pembeni kuna jambazi mmoja aliekuwa amekaa kwenye matofari matatu yaliokuwa yamepangwa kwa ustadi.
Roma hakuweza kutambua sura hata moja , alisukumiwa na kwenda kufungwa karibu na baba yake Edna miguuni na mikononi kwenye kiti.
“Mnataka nini kwa Edna , nishakuja mfungueni sasa”
“Tushakuambia tuliza wenge, wewe hata haunathamani kwetu , umeitwa hapa kwa ajili ya kufa, na Edna ameletwa hapa kwa mpango mwingine”Roma hakuelewa kinacho endelea lakini alikuja kuelewa baada ya kuona bwana mmoja hivi aliekuwa amekalia tofali alikuwa akimlazimisha Edna kutia saini kwenye makaratasi yaliokuwa yapo mbele yake.
“Mrembo acha kutupotezea muda tia saini umuokoe baba yako , nitahesabu mpaka nne maana umetusumbua sana , usipo fanya kile tunachotaka hii itamuhusu baba yako”Aliongea bwana huyu huku akionekana hana hasira hata kidogo.
Edna alimwangalia baba yake na kisha kugeuza macho kwa Roma na kisha kuziangalia karatasi zilizokuwa mbele yake , karatasi zilizokuwa zikimtaka kutia saini ili kuruhusu asilimia sitini ya hisa za kampuni yake kwenda kwa mtu mwingine.
“Hapana sipo tayari , nitailinda kampuni hata kwa kifo”
“Mojaaa.. , mbilii , tatuu.. nne”.
“Paaah!!”Ulilia mlio wa risasi uliomfanya Edna afumbe macho , kwani hakuwa tayari kushuhudia baba yake akipigwa risasi, jambo hili hata kwa Roma lilimshangaza sana , hakuamini kama Edna yupo tayari kumuona baba yake akifa ili tu alinde kampuni.
“Mamaa... isiiiii... nakufaa Edna ”Ilikuwa ni sauti ya mauimivu iliomtoka mzee Adebayo , kwani alikuwa amepigwa risasi ya paja na damu zilikuwa zikimtiririka.
“Risasi itakayofutia itatua kwenye kichwa cha baba yako , nadhani unatuona kama tunatania , weka sahihi yako pumbavuu”
“Edna wape wanachotaka wata.. niua baba yak..o”
Edna alimwangalia baba yake kwa uchungu huku akitoa machozi.
“Nisamehe baba sipo tayari kufanya kama wanavyotaka , watuue tu wote”Aliongea Edna na kuwafanya majambazi hawa kushangaa lakini sio majambazi tu hata Roma alikuwa akishangaa.
Roma japo yeye alionekana kufungwa lakini ni kama amepumzika kwani hakuwa na wasiwasi kabisa.
“ Kama ndio unavyotaka basi hatuna namna tutafanya kile ambacho unataka , na nakuambia baba yakoo atakufa lakini pia kusaini utasaini”Aliongea jambazi kiongozi na kisha alinyanyua bastora yake na kumlenga baba yake Edna , huku Edna akifumba kwa mara nyingine macho kwani hakuwa tayari kushuhudia kifo cha baba yake.
“Nitahesabu upya mpaka tatu , kama utashindwa kutia saini hizo karatasi basi sitakuwa na jinsi kukupa kile unachotaka.. moja , mbili ….. , tatu”Edna hakutia saini na jambazi liingiza kidole kwenye Triga..
“Stop nipo tayari kusaini ,.. nitasaini muacheni baba yangu”Aliongea Edna na kuwafanya majambazi hawa watabasamu na jambazi lile kiongozi lilimpa ishara jamaa aliekuwa karibu na Edna amsogezee karatasi.
Edna aliangalia karatasi zile huku akitoa machozi , alichukua kalamu huku akiwa anatetemeka mno , hakuamini anakwenda kuachia hisa asilimia Sitini na kubakiwa na asiliamia therethini tu za umiliki ndani ya kampuni yaie kitendo ambacho kitamfanya kukosa kauli ya mwisho ndani ya kampuni.
“Hapana ngoja nimuokoe baba , pesa zinatafutwa tu na hata mama atanielewa , huyu ni baba yangu siwezi kumuangalia akifa mbele yake sitokuwa na furaha”Aliwaza Edna
“Fanya haraka”Aliongea jambazi kiongozi na Edna aliangalia karatasi zile na kisha kama mtu alieghaili aliweka kalamu chini na kisha akanyanyua uso wake na kumwangalia Roma kwa huzuni.
“Kabla sijasaini nataka mnihakikishie jambo moja”Aliongea Edna
“Ongea”
“Mtamuachia mume wangu akiwa hai maana hahusiki kwa chochote katika hili”Wale majambazi waliangaliana na kisha kiongozi alitoa simu na kusogea pembeni , alionekana hakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya ombi la Edna.
Roma alishangazwa na maamuzi ya Edna na kujikuta kuna kitu flani kipya kiliingia ndani ya moyo wake juu ya mke wake huyu wa mkataba.
“Bosi anataka tumuahidi Roma awe huru”
“Acheni upumbavu , mdanganyeni tu akishasaini mpigeni Roma risasi sitaki huyo mwanaharamu aishi tumieni akili”Ilisikika sauti upande wa pili.
“Sawa bosi”
Jambazi kiongozi alirudi na kumwambia Edna kuwa wapo tayari kutii ombi lake , lakini kwa Edna hakuwa mpumbavu alikuwa anajua kabisa watu hao watamuua Roma akishafanya kile wanachotaka.
“Kama mpo tayari nataka mumfungue yeye na baba yangu waondoke na mimi ndipo nitasaini.. siwezi kuwaamini”Aliongea na wakaangaliana lakini awamu hii kiongozi aliona afanye maamuzi bila ya kumshirikisha bosi wake, alimpa ishara jamaa aliekuwa ameshikilia bastora amfungue miguu Roma na baba yake Edna kisha awatoe nje.
“Wakishafika mbali na nikithibitisha wako mbali nitasaini Roma naomba umepeleke baba hospitalini ukitoka”
“Sawa Mke wangu nitafanya hivyo na Asante kwa kunipenda Mumeo”Huku akimkonyeza
Baada ya majambazi kukubaliana na matakwa ya Edna jambazi mmoja aliekuwa na bastora alimsindikiza baba yake Edna na Roma nje , baba yake Edna alikuwa aivuja damu japo sio sana , alikuwa akijikaza kwa maumivu.
Majambazi waliobaki baada ya kutoka walisubiria simu ya Roma iwapigie ili kumthibitishia Edna kama ashafika mbali na yuko salama lakini walikuja kushituka baada ya mwili kutua ndani ya chumba hiki walichokuwepo kwa nguvu kiasi kwamba kutoa mlio , baada ya wao wote kuangalia kwa umakini ndipo walipogundua ni mwili wa mwenzao.
“Kioba!”Aliiita jambazi mkuu kwa hamaki na ile anainua macho alimuona Roma akiingia , tena awamu hii alikuwa akijiamini kiasi kwamba utadhani yeye ndio aliewaagiza hao vijana, Mwenzao alikuwa tayari ashakufa tena kifo chake kilionekana kuwa cha kikatili mno kwani shingo ilikuwa imelegea sana.
“Katika maisha yangu nina sheriia tatu ambazo nimeziweka kwa mtu yoyote kutozivuka , moja sipendi kutishiwa Amani , pili sipendi watu wanaotumia ngao watu wengine kutimiza mambo yao, tatu kwangu neno Onyo ni mara moja ukirudia ni kifo na nyie makossa yote mnayo”Aliongea Roma kwa sauti ya upole kabisa na hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo na isitoshe hakuwa na siraha ila jambazi mmoja alikuwa na siraha.
“Mpige risasi unasubiri nini?”Aliongea jambazi yule kwa pupa na yule mwingine akainua Risasi ili kumpiga Roma , lakini kufumba macho na kufumbua , Roma tayari alikuwa ashamfikia na kilichosikika ilikuwa ni
“Crak’
“Mamaaa.. nakufaaa”
Ulikuwa mlio wa mvunjiko wa mfupa wa mkono uliokuwa umeshika Bastora lakini Roma hakuishia hapo tu alimshika shingo na kichwa na kukizungusha na mifupa yote ya shingoni ikakatika huku kichwa kikigeukia mgongo kitendo ambacho kilimfanya hadi Edna afumbe macho , kwani alishuhuidia Roma akiua kikatili mno mambo ambayo hakuwahi kuwaza atayaona laivu.
Jambazi mwingine baada ya kuona mambo sio kama alivyodhania , alikimbilia chuma na kulinyanyua huku akimtishia nalo Roma , na kwa Roma wala hakujali kwani alizidi kumsogelea huku jambazi hili lilikianza kutetemeka , kwani hakuwahi kukutana na aina ya mtu ambaye alikuwa akiua kama anaua kuku tema kikatili kwa namna alivyoshuhudia.
“Huyu sio mtu , ni shetani inabidi nipate upenyo wa kukimbia”Liliwwaza Jambazi hili
Jambazi alimrushia Roma lile Chuma lakini Roma alilikwepa halafu akalidaka na kulivuta kwa nguvu kitedo ambacho Jambazi alivutwa nalo kwani alikuwa amelishikilia kwa nguvu na baada ya kumsogelea Roma alipigwa teke la mguuni lililomfanya kuhisi maumivu makali mno na kutoa ukulele.
“Leo utaniambia bosi wako ni nani, aliekutuma kumteka mke wangu”Aliongea Roma huku macho yake yakionekana sio ya kawaida hata sauti yake pia sio ile iliokuwa ikizoeleka , aliongea kama roboti.
Alimshika yule jambazi na kama vile anavunja paja la kuku alimshika mguu kwenye Goti na kulipindisha kiasi ambacho mguu ule ulitoa sauti kubwa ya viungio kupishana na mguu ule kugeukia mbele.
“Mamaaaa.. nakufaaa….”Ulikuwa ni ukululele wa aina yake
“Sema nani kawatuma la sivyo naendelea na mguu wa pili?”
“Nasema .. nasemaa”
“Okey ! nadhani uanze kuaongea sasa”
“Alietutuma ni Jose na Baba yake Edna”.Roma ni kama hakuwa ameelewa vizuri .
“Ongea vizuri ueleweke au unataka niendelee..”
“Huyu mzee eliekuwepo hapa na Jamaa anaefahamika kwa ina la Jose ndio alietuagiza , ila huyo Jose anasema pia ana bosi wake alietoa kazi hio”Baada ya kuongea vile lile Jamaa ni kama Edna hakuwa akimuamini , alinyanyua karatasi zilizokuwa mbele yake na kuzisoma na alijikuta akiishiwa nguvu mara baada ya kuona karatasi hizo zilikuwa na jina la baba yake , inamaana muda wote alitakiwa kusaini ili kuruhusu hisa ziende kwa baba yake.
Roma aliona maelezo hayo yanajitosheleza , alichukua lile chuma na bila hata ya huruma , alimchoma nalo Shingoni kiasi cha kufanya Damu imrukie na kumchafua kwenye nguo mpaka usoni Roma aligusa ile damu usoni na kisha kuinusa.
“Mwamba ana damu inanuka vibaya huyu” Aliwaza
Na huo ukawa ndio mwisho wa majambazi yote matatu yaliokufa kikatili mno na kwa mtu yoyote angeshuhudia maiti hizo hakika angeishia kusema Roma ni Shetani..
Lakini wakati anamaliza mara mlango ulisukumwa na mtu anaechehemea huku akiwa na bastora mkononi na huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni baba yake Edna.
“Edna Saini hizo karatasi kabla sijaachia Risasi”Aliongea mzee huyu huku akionekana ni mwenye kuvumilia maumivu kwani hadi mikono ilikuwa ikimtetemeaka.
“Baba .. siamini kama unaweza kwenda mbali kiasi hiki….”
“Kimya mpumbavu wewe mimii sio baba yako , saini karatasi hizo kabla sijakutandika risasi ya kichwa na huyu muaaji mwenzako hapa”Aliongea huku Roma akimwangalia mzee huyu na kisha akatabasamu.
“Mzee bora ungekimbia baada ya mimi kukuacha kule nje , ila nimekupa nafasi ili hali najua ulikuwa kwenye huu mpango ila ukajileta mwenywe hivyo sina budi ya kukupeleka kuzimu”Aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae kuona Roma alikuwa ashajua kuwa baba yake alikuwa akihusika , alishangazwa na uwezo wa Roma na kujiuliza maswali mengi.
Baba yake Edna alimwangalia Roma na kisha akaangalia namna Roma alivyoweka mguu wake kwenye kichwa cha jambazi linalovuja damu shingoni na kutikisika kama kuku bila wasiwasi kama vile kaweka mguu kwenye tofali , mzee huyu alijikuta mwili wake ukipatwa na ubaridi ambao hakuelewa alijiuliza huyu matu ni binadamu au mnyama.
“Baba naomba uweke hio siraha chini nitaacha hili lipite ,, licha ya kwamba sitokuja kusahau”
“Tulia Edna .. mmeninyanyasa sana wewe na mama yako kiasi cha kunifanya nionekane mwanaume bwege ndani ya macho ya walimwengu , leo nalipiza maumivu mlionisababishia kwa miaka mingi”Aliongea huyu mzee na hakuwaza tena alivuta triga yake kwa dhumuni la kuua , lakini kabla hajatimiza azima yake alijikuta akipigwa na chuma mikononi na Siraha ile kwenda chini.
“Kitendo cha kurudi hapa ndani umejitafutia kifo chako”Aliongea Roma na kumpiga teke sehemu iliokuwa na Jeraha na kumfanya mzee huyu apige yowe , lakini Roma hakuishia hapo tu , alimkanyaga kwenye kigoti cha mguu na kusababisha mfupa wa mguu uvunjike , yote hayo aliokuwa akiyafanya hakumuwazia Edna alikuwa kwenye hali gani.
Roma alimvunja mzee Adebayo miguu yote na hapo ndipo alipomgeukia Edna ambaye muda wote alikuwa kwenye mshituko kiasi kwamba hakuwa hata akiongea kwani alikua ni kama mtu aliekuwa amezimia huku anaangalia , ile Roma anamfungua Kamba Edna alizimia palepale.
Baada ya lisaa limoja Roma alifika Kigamboni na kumtoa Edna kwenye gari na kuingia nae ndani huku Bi Wema akiwa kwenye mshangao kwani alimuona Wema akiwa na damu mwili mzima.
“Nini kimetokea Roma?”Aliuliza bibi huyu huku akionekana ni mwenye wasiwasi.
“Kuna wapuuzi wanajifanya wajanja , wamemteka mke wangu na mimi nimelipiza kwa kuwaua”Bi Wema macho yalimtoka.
“Umesema umewaua?”
“Ndio wamekufa , mwingine ni baba yake Edna nimemvunja miguu ili akampe taarifa anaeshirikiana nae”Huku akimpandisha Edna juu kweye chumba chake akifuatiwa na Bi Wema .
Roma ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia kwenye chumba hiki cha mke wake , kilikuwa ni chumba kikubwa kilichokuwa kinapendeza sana kuitwa chumba cha mwanamke CEO mkubwa ndani ya ulimwengu wa wafanya biashara duniani.
“Bibi atazinduka huyu baada ya muda alikuwa kwenye mshituko”
“Unajuaje Roma wakati mtu yupo mahututi tumepeleke hospitalini”.
“Haina haja Bi Wema, Atazinduka”Aliongea Roma na kisha akatoka akimuacha bibi huyu kwenye mawazo , hakuweza kujua Roma ni mtu wa namna gani kwani alionekana kujiamini mno.
Baada ya kutoka ndani ya chumba chake aliingia bafuni na kuoga na baada ya kumaliza alichukua simu yake na kumpigia Doris na kumwambia ashamuokoa mke wake na yeye yuko salama baada ya kukata simu alitafuta namba ya Rose.
****
Ilikuwa ni muda wa usiku saa tisa kamili ndani ya chumba kikubwa anacholala mheshimiwa Rais Senga , akiwa amepumzika na mke wake mara simu yake kubwa ya I phone ilianza kuita mfuliulizo kiasi cha kumuamsha na kushangaa ni nani anampigia muda huo kwani sio kawaida yake , na mara nyingi akipokea simu usiku sana huwa ni za dharula na kuna tatizo kubwa ambalo wasaidizi wake wameshindwa kulitolea maamuzi, aliangalia jina la mpigaji na kujikuta usingizi ukimuishia jina kwenye kioo lilionekana limeandikwa Senior(Mkubwa kazini).
“Mheshimiwa kuna nini? , maana sio kawaida kunipigia muda huu”.
“Senga ulinihakikisha kuwa Edna atakuwa salama ndani ya taifa lako , lakini nini hiki kinaendelea ndani ya nchi yako”
“Naomba upunguze jazba Senior nini tatizo?”
“Vijana wangu wamenitumia ripoti kwamba Edna alitekwa”
“Nini..!! , unahakika na hio taarifa Senior?”
“Nina uhakika na vijana wangu wangu Senga , nimewapa kazi hio moja tu ya kumlinda Edna kwa siri”
“Vipi hali ya Edna kwa sasa??”.
“Ni bahati kwamba sasa hivi ana mume , kwa hilo namsifia sana , yule mtoto ana akili sana kachagua mume bora”
“Unamaanisha Roma ni mume bora kwa Edna?”.
“Ndio Senga mchunge sana huyo kijana sio mtu wa mchezo mchezo na ni mtu katili kuwahi kutokea katika huu ulimwengu hakikisha unakuwa upande mzuri na yeye kukusaidia kwenye mpango wako, mimi yangu ni hayo tu na nikwambie Senga haupo makini kabisa Edna anatekwa huna habari , mimi niliopo ng`ambo ya pili ya nchi yako nimepata taarifa kabla yako , nimekasirishwa sana na jambo hili ,Usiku mwema nadhanni tutaongea Zaidi juu ya mipano yetu siku tukionana”Aliongea Senior na kisha kukata simu.
“Who is this Guy?”Alijiuliza mheshimiwa Senga huku akiwa ni mwenye kushangaa Senior anamfahamu Roma.
“ My guess was right he is not normal , there is more hidden info about him , I have to dive deep to discover more details”
Comments