Reader Settings

Ilikuwa ni muda wa asubuhi  ya saa mbili Roma alionekana akiendesha gari kwa spidi akielekea maeneo ya Mbagala , baada ya kuupiga mwendo kwa madakika kadhaa alikuwa mbele kabisa  ya nyumba ya  Rose , alipiga honi na mlinzi alifungua na Roma akaingia ndani na kwenda kugesha gari , baada ya kutoka aliingia ndani ya jumba hili ambalo lilikuwa kimya mno kwani Rose alikuwa akiishi yeye peke yake.

“Bebi karibu”Aliongea Rose huku akiwa ni mwenye mshangao mkubwa sana  kumuona Roma asubuhi asubuhi , alihisi kuna tatizo.

“Asante , nimekuja nina mazungumzo na wewwe ya muhimu sana”Aliongea Roma na kumfanya Rose ashangae huku akivua aproni  na kuiweka kwenye sofa kwani alikuwa jikoni na alionekana alikuwa akiandaa kifungua kinywa.

“Kuna nini mpenzi ,kuna kilichotokea?”.

Roma alitoa cheni flani hivi yenye  kidani cha  kichwa cha Tembo  na kumrushia Rose na akakiokota.

“Umeitoa wapi hii Roma? .. hiki ni kidani kinachowakilisha  kundi langu”

“Vijana wako jana wamehusika kumteka  mke wangu na nimewaua wote”Aliongea Roma na kumfanya  Rose ashangae.

“Usijifanye hujui hili jambo Rose ?”

“Bebi Calm Down sijui chochote juu  ya hili swala na sijatoa  ruhusa yoyote , itakuwa ni Ramso”

“Kama hujui swala kama hili naamini  hauko makini na kundi lako na wanafanya mambo ya kiholela kuhatarisha maisha ya jamii ,Rose sipo radhi kuona mtu yoyote ndani ya familia yangu anaguswa  na mtu yoyote yule na nipo tayari kuua  , hivyo naomba uwaweke vijana wako under control”Aliongea  Roma  na kisha kukaa chini ya sofa.

“Baby Am sorry”.

“Usijali nishakusamehe kipenzi , ila hakikisha maswala kama haya hayajitokezi hususani kwenye familia yangu”

Roma aliandaliwa chai na mchepuko wake Rose  na baada ya kushiba waliagana na yeye akaondoka huku akielekea kazini.

Baada ya Roma kuondoka Rose alijiandaa na kutoka kisha akaelekea ofisni kwake.

“Zonga mpigie simu Ramso  sasa hivi” afike ofisini kwangu”

“Sawa madam”

Baada ya madakika kadhaa Ramso aliingia  na alionekana kuwa na wasiwasi sana kwani  macho yake yalionesha, huku  jasho likiwa linamtoka,Rose macho yalikuwa yamebadilika hakuwa yule mrembo anaeonekana kuwa mpole ila huyu alionekana kuwa katili.

Aliinuka kwenye kiti chake na kisha alimsogelea  Ramso  huku mkononi akiwa na kisu kikali kinachowakawaka kwa kung`aa  ,, kisu aina ya Sime kama zile za wamasai huku kikiwa na alama ya Tembo katikati.

Ilikuwa ni kitendo cha fasta sana Ramso alitoa mguno wa maumivu baada ya kuchomwa na lile bisu kwenye paja  la mguu wa kulia damu kuanza kutoka mfululizo .

“Hio ndio adhabu yako ya kufanya  mambo bila ruhusa yangu”Aliongea Rose na akakivuta kisu kile na Ramso akadondoka chini  kwa maumivu huku Rose akifuta damu kwenye kisu chake  na kitambaa cheupe na kukitupia kwenye Dustbin.

“Anza kunieleza kwanzia mwanzo nini kilitokea”Aliongea huku akionekana sio mwenye utani hata kidogo.

“Nisamehe madam sitorudia tena”

“Achana na msamaha wako wa kipuuzi nieleze nini kilichotokea mpaka ukaenda kumgusa  mke wa Roma”

Ramso alieleza kwa wasiwasi  namna hali  alivyofuatwa na marasta na kutaka atoe vijana kwa kazi alioiita maalumu kwa malipo makubwa.

“Nitamaa ya pesa tu boss nisamehe”.

“Ole wako lijirudie, siku nyingine hiki kisu kitaingia kwenye koo lako unaweza kwenda”

“Asante bosi kwa  kunisamehe niakutii kwanzia sasa”Aliongea Ramso na kisha alitoka.

Rose alirudi kwenye tarakishi yake na kisha aliwasha na kuandika jina la Edna Kwenye mtandao wa Google na kisha  maelezo kutoka Wikipedia yalitokea na kuanza  kuyasoma.

“Edna  Adebayoo  mwanamke wa kwanza kutoka  Tanzania na Afrika  na  kuingia kwenye Top 20 ya wanawake  matajiri duniani , anatajwa kuwa mwanamke mwenye ushawishi mkubwa katika medani za kibiashara ndani ya Afrika,utajiri wa Edna ni Dola bilioni tano za kimarekani akishika nafasi ya kumi  duniani  kama matajiri wenye umri mdogo.”.

Rose alisoma taarifa hio na kujikuta akivuta pumzi , ndio alikuwa anafahamu sasa mke ambae Roma alikuwa amemuoa , aliona  hana nafasi ya kuweza kushindana na mrembo Edna kwani alikuwa amemzidi kila kitu.

“Sina ninachomzidi ,  ninatakiwa kuridhika na nafasi niliokuwa nayo kwenye  maisha ya Roma”Aliiwazia Rose  huku akimuangalia mrembo Edna picha yake ikimuonesha kupokea tuzo kama  moja ya CEO wanawake waliokuwa wamefanya vizuri katika maswala ya uongoz ndani ya kampuni.

“Nilijua tu Roma sio wa kawaida  na ndiio maana nimetokea kumpenda , kwa jinsi alivyoniokoa kutoka kwa wale watu waliotumwa na baba yangu inanifikirisha mpaka sasa  na kutaka kumjua Zaidi na Zaidi”

****

Wakati hayo yakiendelea upande wa hospitali ya Aghakani katika wodi ambayo ilikuwa ikitumika kuhudumia wagonjwa wenye hadhi ya juu yaani VIP  alionekana Abuu akiingia ndani ya  wodi hii huku akiwa ametangulizana na  wasaidizi wake , bwana huyu alionekana hakuwa na furaha hata kidogo katika uso wake.

Baada ya kuingia ndani ya wodi aliokuwa amelazwa mzee Adebayo alimsalimia na kisha alikaaa kwenye kiti, huku mzee huyu akimwangalia kijana huyu kwa wasiwasi.

“Abu yule mtu ni katili sijawahi pata  ona , inakuwaje binadamu anaua bila ya kuwa na wasiwasi hata kidogo”Aliongea mzee huyu  kwa pupa.

Na baada ya kuona huyu mzee anaropoka aliwaruhusu walinzi wake na wahudumu watoke nje ili kubaki na mzee kwa  ajili ya meongezi.

“Nini kimetokea mzee?”.

“Nikama unavyo ona Abu, yule kijana sio wa mchezo ni katili na muuaji amenifanya kuwa kilema wa maisha”Aliongea kwa hali ya simanzi.

“Hata kama ni mkatili vipi mzee , siwezi kuruhusu aendelea kuwa na Edna ilihali nimefight kwa ajili yake kwa muda mrefu”.

“Hata mimi sijakata tamaa Abuu , lazima yule mwanaharamu nimkamate na kumrudishia haya  alionifanyia , ila nakutahadharisha tu kwamba yule kijana sio wa kawaida na tunapaswa kuwa makini”Abuu baada ya kuona hana  la kufanya hapo ndani aliaga  na kuondoka huku akiwa ni mwenye mawazo , alikuwa akiwaza ni namna gani ya kumdhibiti Roma , hata yeye alikuwa ashajua Roma hakuwa mtu wa kawaida , kwani alikumbuka siku aliyokwidwa na mwanaume huyo na kuning`inia hewani.

Wakati akiwa anatoka simu yake ilitoa mlio na kuonesha ilikuwa inaita  , baada ya kuona jina la mpigaji alisimama na kisha akapokea.

“ Ndio baba!”

“Sawa nakuja”.

Abuu alliongeza mwendo  na kisha alitoka ndani ya hospitali  na ndani ya madakika kadhaa alikuwa ndani ya eneo walilokuwa wakiishi  matajiri Masaki.

Baada ya kufika nje ya geti kubwa alifunguliwa na kuingiza gari ndani na kisha aliliegesha na kuingia sebule ndani ya jumba hili ambalo lilionekana lilikuwa la kifahari , baada ya kuingia mtu wa kwanza kumuona ni msichana mmoja mrembo aliekuwa amejiachia kihasara hasara akiwa na simu yake kubwa akionekana ni mwenye kuchat eneo la Sebuleni..

“Queen  mzee yuko wapi?”

“Kwenye ofisi yake”Aliongea mwanadada huyu pasipo ya kugeuka , alionekna kuwa ni wale wanawake waliokuwa na maringo. Ila Abuu hakujali alipandisha ngazi kuelekea juu  na ndani ya dakika chache alikuwa ndani ya ofisi iliokuwa kubwa , huku ikiwa na mavitabu mengi na makabrasha mbalimbali , huku mbele yake kukiwa na masofa na meza kubwa iliokuwa na tarakishi kubwa ya kampuni ya Apple , huku nyuma ya tarakishi hio akiwa mzee Alex

Baada ya mzee huyu kumuona Abuu amefika alitoka alipokuwa amekaa na kisha alimsogelea Alex na kisha alimramba kibao.

“Abuu mbona siku hizi umekuwa na uwezo  mdogo wa kufikiria”

“Nisamehe baba , ni kwamba sikuwa na taarifa sahihi zinazomuhusu Roma  na ndio maana mpango wangu umefeli”

“Acha sababu zako za kipuuzi , unajua ni vitisho gani napokea kutoka kwa The Doni , kwanini hili swala unalifanya lichikue muda mrefu hivi”Abuu hakuwa na majibu , alifokewa mno.

“Nakupa siku kumi kwanzia leo  swala hili uwe ushalifanyia kazi , sitaki uzembe tena ukishindwa  nakutoa kwenye nafasi yako”Aliongea mzee huyu  kwa hasira na Abuu alitoka huku hasira juu ya Roma zikiongezeka Zaidi.

“Roma nitakuua kwa nmna yoyote ile hata kwa kukodi watu kutoka nje ya nchin siwezi kudhaliliska kiasi hiki” .

Baada ya kutoka ndani ya jumba hili moja kwa moja alipanga kwenda  ofisini kuendelea na kazi huku akiendelea kufikiria namna ya kumdhibiti Roma na hatimae  Edna , dakika chache alikuwa nje ya ofisi yake  huku katibu muhtasi akimwangalia kwa wasiwasi.

“Kuna nini?”

“Mgeni”Alijibu na kufungua mlango na kisha akaingia na kumkuta mgeni akiwa  amekaa kwenye kiti chake cha mzunguko akiwa hana habari, na mgeni huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Roma .

Abuu alimtazama Roma kwa hasira kali mbo na alitamani awe na siraha ammalize pale pale  , lakini siraha hio hakuwa nayo.

“Nani kakuruhusu kuingia kwenye ofisi yangu bila ruhusa”

“Nimejiruhusu mwenyewe kwani vipi?”

“Kuwa na heshima kwenye ofisi za watu bwana , toka kwenye kiti changu”

“Ninatoka lakini leo nimekuja kukupa onyo kwa mara nyingine ya pili  na  unabahati sana  kwani huwaga sitoagi  onyo mara mbili , mimi sheria yangu ni onyo mara moja ukirudia  ni kifo , sasa nakuambia hivi mimi Roma Ramoni ikitokea  siku muda na saa yoyote umemsumbua  Edna mke wangu, anza ktubu dhambi mapema  angalau nikikupelekka kwa father God uingine peponi”Aliongea  na kisha akanyanyuka na alivyomfikia Abuu alipiga teke  lililomfanya abuu atoe kulele maana ni kama amegongwa na chuma.

“Hakikisha unatii hiki nilichokuambia siku ya leo , ukifanya ujinga nitahakikisha unafia kwenye hiko kiti”

Roma alifungua mlango na kisha kutoka nje lakini ile anakaribia  mapokezi uso kwa uso na Edna aliekuwa anaonekana kama vile hakijatokea kitu  jana yake kwani alikuwa na uso ule ule wa kikauzu na mwendo wa kujiamini akiwa ametangulizana na Sekretari wake.

“Huyu mwanamke ni ngangari bwana” Aliwaza Roma

Previoua Next