Nadharia ya Kijasusi: Fumbo la Mlinzi wa Baa Aliyekuwa na Akili Kuliko Albert Einstein
Wakuu, salamu.
Mifumo ya elimu duniani haikutengenezwa ili kugundua akili; ilitengenezwa ili kuzalisha wafanyakazi wanaotii amri.
Ukitaka kuona jinsi dunia inavyoweza kumpita na kumdhau mtu mwenye akili kuliko wote, mwangalie mtu anayeitwa Christopher Langan.
Kwa miaka miwili, ulimwengu unaamini kuwa watu wenye akili zaidi wako Harvard, NASA, au Wall Street wakiwa wamevaa suti. Hiyo ni picha ya kufikirika. Mtu mwenye IQ kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya kisasa—iliyofikia kati ya 195 na 210 (wakati Einstein alikuwa na 160 tu)—hakatizi kwenye korido za vyuo vikuu.
Alikuwa anasimama mlangoni mwa baa chafu usiku akisukuma walevi.
Christopher Langan hakuthaminiwa kwa sababu mifumo ya kijamii haipendi watu wenye akili wanaotoka kwenye umasikini uliokithiri. Wanawataka wawe watumwa wa jembe au walinzi wa milango.
Langan alizaliwa Marekani katikati ya umasikini wa kutupa. Alilelewa na baba wa kambo aliyekuwa anampiga kila siku.
Lakini akiwa na umri wa miaka minne tu, alijifunza kusoma mwenyewe bila mwalimu. Alipofika sekondari, alikuwa anajifundisha mwenyewe hesabu za juu kabisa za chuo kikuu, fizikia ya kweli, na falsafa. Kwenye mtihani mkuu wa SAT wa kuingia chuo kikuu nchini Marekani, Langan alipata alama 100% za ushindi, licha ya kwamba alilala katikati ya mtihani ule kwa uchovu.
Alipojiunga na chuo kikuu cha Montana, mtego wa mfumo ukamkamata. Mama yake alisahau kujaza fomu moja tu ya kupata mkopo wa masomo. Chuo kikasema: "Kama huna pesa, ondoka." Langan alijaribu kuwaeleza wakuu wa chuo kuwa yeye ni tofauti, ana uwezo mkubwa, lakini wakafunga milango. Mifumo iliona karatasi ya fomu ina thamani kuliko ubongo wake.
Langan aliondoka chuo na kurudi mtaani. Kwa miaka 20 iliyofuata, mtu huyu mwenye uwezo wa kutatua mafumbo makubwa zaidi ya ulimwengu alifanya kazi kama kibarua wa ujenzi, mbeba mbao, na mlinzi wa baa.
Wakati akisimama mlangoni kuzuia wahuni wasivunje chupa, kichwani mwake alikuwa anasuka nadharia mpya kabisa ya jinsi ulimwengu ulivyoumbwa na jinsi hisabati inavyoweza kuthibitisha uwepo wa Mungu.
Matajiri na wasomi vya vyuo vikuu walipogundua uwepo yake miaka ya baadaye kupitia vipimo vya IQ, walijaribu kumkaribisha. Lakini Langan aliwakataa. Aligundua mapema sana kuwa wasomi wengi hawataki ukweli; wanachotaka ni kulinda vyeo vyao na mikataba ya fedha ya makampuni makubwa.
Wajinga wanapima akili ya mtu kwa kuangalia kiwango cha cheti cha chuo au suti aliyovaa, lakini mifumo inajua ukweli: ubongo mkali zaidi duniani ulikuwa unashika jembe shambani na kulinda baa.
Fumbo la Christopher Langan: Ubongo Hatari Zaidi Duniani Aliyeshindwa na Karatasi ya Fomu ya Chuo
Tabea singano · Dakika 2 za kusoma ·
